Ukatili! Mke amuua Mumewe kwa kumpiga na kikombe kichwani huko Mburahati..!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
SHETANI anazidi kuuatamia ulimwengu! Mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Farida mkazi wa Mburahati jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kumuua mumewe aliyetajwa kwa jina la Amos Joseph kwa kumpiga kwa kukombe kichwani, Ijumaa linaidondosha kama ilivyo.
Amos Joseph enzi za uhai wake.

Akisimulia mbele ya gazeti hili mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.
Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.
Mtuhumumiwa wa mauaji, Farida.
“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu nikidhani ameumia kidogo, kwa sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana mara kwa mara na tulishawaonya. Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na shughuli zangu.
“Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija.
Dada wa marehemu Amos.
Dada mwingine wa marehemu aliyejulikana kwa jila la Christina, alisema yeye aliwahi kufika nyumbani kwa Farida na kumkuta kaka yake akiwa amelala chali huku damu zikimvuja, muda mfupi polisi waliwasili na kufanya taratibu zote muhimu.
Marehemu Amoni alizikwa siku chache baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.
Dada wa marehemu.
Gazeti hili linaipa pole familia ya marehemu na linamuomba Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu Amosi-Amin.
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,889
2,000
Kuna watu wanafikiri watapigana kila siku na wataendelea kubaki salama.

Kufikia kupigana ni kushindwana na inabidi mmoja achukue uamuzi wa kumuacha mwenzie lasivyo kila leo watu wataendelea kuuwana.

Hivi ni vifo vya kujitakia kabisa.
 

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,759
2,000
Watu wengine wana roho za ajabu!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
909
500
mhhhhh hatariiii ..nilishazoea kusika wadada wanauliwa na weza wao leo upepo umegeuka...R.I.P.tangulia wengine tutafata.sis tu mavumbi na mavumbin tutalud. bwana alitoa na bwana ametwa jina lake lihimidiwe.
 

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,314
2,000
Dah......atakuwa alimpiga na bilauri au kikombe gani ambacho kinatoa uhai.......?...tuchague aina za vikombe vya kuweka ndani jamani.......RIP Amos....
 

marejesho

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
6,642
2,000
Kuna watu wanafikiri watapigana kila siku na wataendelea kubaki salama.

Kufikia kupigana ni kushindwana na inabidi mmoja achukue uamuzi wa kumuacha mwenzie lasivyo kila leo watu wataendelea kuuwana.

Hivi ni vifo vya kujitakia kabisa.

Na mimi nimejiuliza swali hilo hilo...kwani kulikuwa na ulazima ndoa hiyo kuendelea? Watu wanavunjwa mikono, miguu na bado wapo tu..
Juzi juzi hapa mwingine alinyofolewa korodani zake...
Ifike mahali watu wafanye maamuzi magumu kuepusha vifo
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,853
1,250
Dah......atakuwa alimpiga na bilauri au kikombe gani ambacho kinatoa uhai.......?...tuchague aina za vikombe vya kuweka ndani jamani.......RIP Amos....

ndio maana mimi nimenunua vya plastiki tu.
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,412
2,000
Taarifa ya kutoka ukerewe, ROSE KIWELW 29 AMEUWAWA NA MPENZI WAKE KWA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO, DAMU ILIVUJA HADI MAUTI YAKE. KISA WIVU WA MAPENZI. NJEMBA IMEKAMATWA
 

marejesho

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
6,642
2,000
Taarifa ya kutoka ukerewe, ROSE KIWELW 29 AMEUWAWA NA MPENZI WAKE KWA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO, DAMU ILIVUJA HADI MAUTI YAKE. KISA WIVU WA MAPENZI. NJEMBA IMEKAMATWA


Yale yale...

Sasa huyu njema hajasikia kwamba kuchapiwa ni siri ya ndani?
Ona sasa mapenzi yamemsababishia kwenda lock up...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom