Ukatili kwa watoto wetu mpaka lini?

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,350
2,000
Habari wanajamvi,

Vitendo Vya Ukatili Kwa Watoto Vmekuwa Ni Jambo La Kawaida Siku Hizi.

Mtoto John William Wa Miaka 4, Huko Geita,amefariki Dunia Baada Ya kupata Kipigo Kwa Kuchelewa Kumfungulia Mlango Baba yake Aliporudi Usiku
Mtoto Huyo,Alicharazwa Viboko Mwili Mzima,Akapigwa Mangumi Na Mateke.

Akapewa Adhabu Ya Kuzunguka Nyumba Yao Usiku Huo Mara Kadhaa Na Kisha Kupakwa Pilipili Machoni Ambapo Adhabu Hizo Zilipelekea Mtoto Huyo Kupoteza Maisha.

Source: The Citizen 26

My take;

Hivi Katika Hali Ya Kawaida Mtoto Wa Miaka 4 Ni Wa Kumfungulia Mtu Mlango Usiku Wa 8?

Jaman Ifike Mahali Tuwe Walinzi Wa Hawa Watoto Wanaumizwa Na Kuathiriwa Kisaikolojia Na Hawa Wazazi Wapuuzi,mda Huo Unakuta Hilo Zee Limelewa Anakuja Kumtesa Mtoto Kiasi Hichi!

Ukiona Mtoto Wa Jirani Yako Anapata Mateso Kama Haya Ni Bora Kumshtaki,mi Wakwangua Akiwa Na 4 Years Nadhani Bado Atakuwa Anabebwa Mgongoni.

Hainiingii Akilini Ndo Mfungua Mlango Usiku Huo Ambapo Watoto Wenzake Wanakuwa Usingzini Wanaota Ndoto Jamani Inauma Sana Kuwakatisha Watoto Maisha.
=====================================
Geita. Simanzi, vilio na majonzi vilitawala Kijiji cha Misiri, Kata ya Bugarama, wilayani Geita, kutokana na tukio la kifo cha mtoto, John Wiliam (4) aliyefariki baada ya kupewa adhabu na baba yake mzazi.

Ilidaiwa kwamba mtoto huyo alifariki baada ya kuchapwa fimbo mwili mzima, kupigwa ngumi na mateke, kisha kupewa adhabu ya kukimbia riadha kuzunguka nyumba yao usiku wa manane.

Baada ya kumalizika kwa adhabu hiyo alipakwa pilipili machoni na makalio hali iliyosababisha mtoto huyo kuzidiwa na kupoteza maisha juzi jioni.

Baba wa mtoto huyo, William Kibyala (40), anadaiwa kufanya ukatili huo baada ya kumtuhumu mtoto wake huyo kukataa kumfungulia mlango wakati alipotoka matembezini usiku wa manane.

Tukio hilo lilitokea Mei 23, mwaka huu saa 10 jioni, siku moja baada ya baba huyo kufika nyumbani usiku akitoka katika matembezi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alisema baba wa mtoto huyo alikamatwa muda mfupi baada ya tukio hilo.

"Baba wa mtoto huyu aligonga mlango ili afunguliwe, lakini kutokana na usingizi, mtoto huyo hakuamka kufungua mlango," alisema Konyo na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Misiri, Someke Mhangwa alisema: "Ni uamuzi wa mahakama, lakini tunataka akipatikana na hatia apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

"Baada ya kupata taarifa za tukio hili, nilifika nyumbani kwa baba wa mtoto huyo na kukuta mtoto wake akiwa amefariki, huku mwili wake ukiwa umevimba pamoja na kuwa na majeraha sehemu mbalimbali."

Alisema kutokana na kupata taarifa hizo mapema aliwasiliana na Polisi Wilaya ya Geita ambao walifika eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa.

Baadhi ya watoto wa familia hiyo, walisema si mara ya kwanza kwa baba yao kumtesa John na kwamba alikuwa akimnyima chakula.

Mmoja wa watoto hao, Shija William alisema mdogo wao alikuwa akipewa adhabu hiyo kwa madai kwamba mama yao alimbambikia mtoto huyo na hakuwa wake.

"Baba alikuwa anasema kwamba mdogo wetu si mtoto wake na kwamba mama alimsingizia kuwa ni mwanaye wakati siyo kweli,'' alisema William.


Chanzo: http://www.fikrapevu.com/ukatili-ba...oni-amchapa-viboko-ngumi-na-mateke-hadi-kufa/
 

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,020
1,250
Jamani wandugu tukumbuke kwamba kuna sababu kubwa inayosababisha ukatili huu kutesa watoto kutokea.
1.Kufunjika kwa ndoa(hii hupelekea mtoto kupata malezi yasio na uhakika wa upendo toka kwa mzazi mmoja tu.

2.Kufariki kwa wazazi(hii hupelekea mtoto kulelewa na ndugu au jamaa wengi wao wasio na huruma na mapenzi kwa mtoto.

#Tujitahidi kuzitunza na tudumu ktk ndoa zetu na pale penye dosari ni vyema tujirekebisha kwa faida ya malezi kwa watoto wetu.
#Pia tuwe na mioyo ya upendo kwa watoto tunaowalea waliotokana na kufariki kwa wazazi wao.
 

Jonathan Kiula

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
315
225
Nadhani watu tunatofautiana sana tena sana kama vile mbingu zinavyotofautiana na dunia maana haya mambo nikiyasikia najiuliza sana kama hawa wanaofanya haya ni watu wa kawaida, majuzi yule mama wa Morogoro na mume wake walivyomtesa mtoto wa dada yake(mwenye umri wa miaka minne) kwa kumfungia ndani mpaka mtoto akadhoofika kiasi kile sasa linakuja hili la huyu wa Geita dah! Nasikitika sana kuona ukatili kama huu ukifanyika kwa watoto ambao wanahitaji kuonyeshwa upendo mkubwa sana kweli nasikitika sana na huzuni kunijaa sana moyoni kwa matukio kama haya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom