Ukatili kwa watoto: Kichanga chaokotwa kwenye shimo, chafariki muda mchache baada ya kuokolewa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,923
10,458
DSC00138.JPG

Mwili wa kichanga ukiwa umefunikwa baada ya kufariki.

DSC00139.JPG

Shimbo ambalo kichanga kilikutwa.

WIMBI la wanawake mkoani Mbeya kujifungua watoto na kisha kuwatupa na wengine kutoa mimba limezidi kushika kasi na kukithiri baada ya vitendo hivyo kuripotiwa na vichanga kuokotwa kwenye mashimo na mitoni.


Kukithiri kwa vitendo ni baada ya leo Wananchi wa Mtaa wa Mwambenja kata ya Iganzo jijini Mbeya kugundua kutupwa kwa mtoto anayesemekana kuwa na umri usiozidi siku moja jinsia ya kike katika shimo la choo kisichotumika.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa huo, aliyefahamika kwa jina la Lukasi Mwakalonge, alisema alipewa taarifa na wananchi wake mchana na kuambiwa kuna katoto kametupwa shimoni na bado ni kazima hali iliyomlazimu kutoa taarifa katika Jeshi la Polisi.

Alisema baada ya kufika eneo la tukio na kugundua kuwa mtoto bado yuko hai wakaamua kumtoa ndani ya shimo huku wakisubiri jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zaidi lakini akawa amepoteza maisha muda mfupi baada ya kutolewa ndani ya shimo.

Hata hivyo jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, vitendo hivyo vya wanawake kutupa watoto kabla na baada ya kujifungia bado vinazidi kutokea hapa nchini ingawa hakuna takwimu sahihi za wanawake waliopatikana na hatia kwa makosa kama hayo.

Credit: Mbeya yetu
 
R.i.p mtoto,unaenda kukutana na nasra pamoja na denic.

Waliowaleta duniani ndio waliowatesa na kuwatoa uhai wao.
 
Hivi kama hutaki kuzaa kwa nini usikinyofoe kizazi? ?hua najiuliza hivii hawaumwi uchungu""?mtu unaanzaje anzaje kutupa mtoto uliekaa nae tumboni miezi 9 ? Kama shida zipo tu hua haziishii hawa wanawake wanaotupa watoto serikali iwachukulie hatua kali ni wauaji
Inauma sana jamanii
 
R.i.p mtoto,unaenda kukutana na nasra pamoja na denic.

Waliowaleta duniani ndio waliowatesa na kuwatoa uhai wao.
Inasikitisha sana,ni watoto wangapi Tanzania na duniani kote wanakutana na mambo haya ya kinyama,tunaowajuwa na tusiowajuwa.
 
Mtaani mtu akiwa na mimba anajulikana..kwanini wakimuona tumbo halipo tena na mtoto hana wasimfatilie mhusika?

Yaani hawa watoto wanaotupa wangeniletea tu mimi nilee,Mtoto anavyokuwa na uzito af unatupa??Kama matatizo ya uchumi unayajua kwanini ukubali kuzaa?utasingiza bahati mbaya,wache mtoto aishi utalea vipi utajua tu mbeleni.
Wengine wakikataliwa na so called mpenzi,wanaona suruhisho ni hilo...walah mnazikataa neema na barakaa za Mungu,na bahati haiji mara mbili..
 
Ili tatizo limekithiri sana hivi kana hutaki mtoto kwa nini usijuzue kuzaa ??? Kuna njia kibao za kuzui kupata mimba ....kwa nini usizuie?
Hakuna mimba ya bahati mbaya ni uzembe na roho ya uuaji tu
Nakereka mimi basiii tu!!
 
Natamani ningekuwa baba wa hako katoto kwa sababu kangebahatika kuwa na maisha mazuri sana yaliyojaa upendo usio na kikomo.
 
Dhambi hii itawatafuna.....Damu ya mtoto huyo itawalilia na kuwanyima kicheko na tabasamu la mtoto huyo.
R.I.P. Uncle Wangu.
 
Jamani wanawake 2mekuwa na roho za kikatili sn sn sn.....kuna anaye tafuta mtt mchn na ucku lkn hapati mwngn anapewa hyo neema ya kupata mtt alafu anam2pa....mungu a2rehemu wanawake.....R.I.P mtt...
 
Oooh God leo tena!! Jana kaliokotwa kengine huko kawe, watoto walikuwa wanacheza mpira ukaangukia kwenye plastic bag yenye mtoto, tena mama alivyokatili alimfunga mdomo kwaplasta...
Imenifanya nisilale hii picha
 
Hizi kesi zinazidi kila leo hadi inatia simanzi kwa kweli.

Sijui haya mashetani watu huwa hayajui nini kitakachofuata baada ya kungonoka?!

Wangeanzishiwa sheria kali labda wangepunguza huu unyama tunaouona kila siku.
 
Back
Top Bottom