Ukatili Huu; Apigwa kikatili na mume kisa ndama kufariki

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
458
170
Nimeisoma hii habari imeniacha hoi!, ukatili kama huu sijui utaisha lini Tanzania, inasikitisha sana na wala haijapewa uzito unaostahili kwenye vyombo vyetu vya habari!!!:angry:

"....Aliporudi tu kutoka katika pombe zake kitu cha kwanza kuniuliza ilikuwa ni wapi alipo ng’ombe wake, nikamwambia amekufa, akaanza kutukana na kisha akaenda nje kuleta kamba akanifunga
miguu,mikono na shingo na kufunga kwenye tendegu la kitanda na kuanza kunipiga kwa fimbo huku akidai ndama wake..."

"....Baada ya kunipiga alienda kwa wake zake wengine kwani mimi ni mke wa tano, nikabaki ndani na kichanga na wanangu wengine ingawa bado wadogo walikuwa wananisaidia kwa shida," anaeleza Sarah.

....Mwanamke huyo anasema kuwa aliendelea kutaabika ndani na vidonda vikaanza kuoza na kutoa harufu kwani hakuwa na uwezo hata wa kunyanyuka kwani msaada alioupata ni kutoka kwa watoto wake wadogo....
Habari kamili hii:
Mwanamke apigwa kikatili na mume kisa ndama kufariki
 
Mbona ni kawaida kwa watu wa kanda ile? Ila kwa kweli inatia huruma sana, serikali ingejaribu kukomesha unyama kama huu! Na pia wanaume waachane na mila potofu kama hizi. Yaani mwanamke azae, alee watoto wake na pia alee ng'ombe. Mwanamume kazi yake ni kutembelea wake tu hakuna analofanya lolote zaidi ya kuwapa mimba tu wanawake,

Huu ni unyanya saji wa hali ya juu kwa wanawake. Nampa pole mwathirika wa tukio, ila mhusika afikishwe kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho na kwa wengine.
 
Nimeisoma hii habari imeniacha hoi!, ukatili kama huu sijui utaisha lini Tanzania, inasikitisha sana na wala haijapewa uzito unaostahili kwenye vyombo vyetu vya habari!!!:angry:

"....Aliporudi tu kutoka katika pombe zake kitu cha kwanza kuniuliza ilikuwa ni wapi alipo ng'ombe wake, nikamwambia amekufa, akaanza kutukana na kisha akaenda nje kuleta kamba akanifunga
miguu,mikono na shingo na kufunga kwenye tendegu la kitanda na kuanza kunipiga kwa fimbo huku akidai ndama wake..."

"....Baada ya kunipiga alienda kwa wake zake wengine kwani mimi ni mke wa tano, nikabaki ndani na kichanga na wanangu wengine ingawa bado wadogo walikuwa wananisaidia kwa shida," anaeleza Sarah.

....Mwanamke huyo anasema kuwa aliendelea kutaabika ndani na vidonda vikaanza kuoza na kutoa harufu kwani hakuwa na uwezo hata wa kunyanyuka kwani msaada alioupata ni kutoka kwa watoto wake wadogo....
Habari kamili hii:
Mwanamke apigwa kikatili na mume kisa ndama kufariki

heri mimi sio wa kanda ile.....maana ukatili na unyanyasaji kama huu hata shetwan hapendi.
 
Back
Top Bottom