Ukatili hujibiwa kwa sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukatili hujibiwa kwa sheria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 25, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  KIJANA Lillah Hussein (24), amehujumiwa kikatili na hatimaye amefariki dunia. Ni chini ya wiki moja tangu alipotendewa unyama usiomithilika. Alikamatwa, akatishwa, akapigwa na baadaye, kama vile mateso hayo hayakutosha, akateketezwa kwa moto baada ya kuvikwa tairi la gari na kumwagiwa petroli.

  Hayo yamemkuta alipokamatwa ndani ya hoteli ya South Beach Resort iliyoko Kigamboni, Dar es Salaam. Hii ni hoteli yenye historia ya uhusiano mbaya kati ya wamiliki na wenyeji wa maeneo yanayoizunguka.

  Hata kama alitenda kosa lolote, Lillah hakustahili kukatiliwa kiasi hicho. Bali alipaswa kukabidhiwa vyombo vya sheria kwa hatua zinazofaa kisheria.

  Sasa Lillah ni marehemu. Ungetarajia katika nchi ambayo viongozi wake wanajinasibu kwa kuendesha mambo chini ya misingi ya sheria, mtiririko wa sheria ukatumika kushughulikia watuhumiwa.

  Kulingana na mazingira yaliyokwishajionesha mwanzoni tu mwa tukio, ni dhahiri tunaona jitihada za kutaka kupinda haki na ikiwezekana kuizuia isitendeke.

  Nyaraka zilizotufikia zinaonesha watuhumiwa wamefunguliwa mashitaka mepesi ya "kujeruhi" na "shambulio." Baada ya kusomewa mashitaka hayo, wamepewa dhamana na kwa sasa wako nje.

  Dhamana hiyo ni kinyume na maombi ya waendesha mashitaka waliopendelea dhamana isitolewe kwa kuwa mtu aliyejeruhiwa ameshafariki dunia na majeraha aliyopata yanachukuliwa kuwa chanzo kikuu cha kifo chake.

  Tunazo taarifa kuwa tangu watuhumiwa walipokamatwa, wakuu wa Polisi Temeke, wamekuwa wakipokea simu za baadhi ya viongozi waandamizi serikalini kufuatilia.

  Viongozi wanaopiga simu wanaulizia na kutaraji mambo yaende harakaharaka na ikibidi wawekezaji wanaowapenda kama roho zao, wabaki nje.

  Hivi ni vitendo vibaya visivyopaswa kutokea nchini. Kumfuatilia mtuhumiwa aliyehujumu raia na mfuatiliaji akawa anajitahidi kuzuia haki kutendeka, ni kukaribisha ufisadi katika jukumu muhimu kijamii la utoaji wa haki.

  Tunataka kuamini harakati za viongozi hao ambao tunawafuatilia ili kuwafichua, ndizo zilizotetemesha Polisi hata kufungua mashitaka mepesi kwa watuhumiwa wakati wakijua fika kuwa waliyemkatili, ameshafariki dunia.

  Viongozi wanaohusika wana haki ya kuonea huruma wawekezaji lakini lazima waheshimu sheria. Ni vema wakatambua machungu waliyonayo ndugu na jamaa za marehemu.

  Hebu wangechukulia tukio hilo kama limemkumba ndugu yao, wangejisikiaje? Wangetulia, wakakaa na kufunga midomo yao?

  Hapana shaka wangeonekana makatili vilevile kama wale waliomjeruhi Lillah na kumsababishia kifo angali kijana mbichi.

  Tunasema huruma za viongozi kwa wawekezaji zisipitilize mipaka ya sheria za nchi. Tunahimiza watuhumiwa wafunguliwe mashitaka yanayofanana na uzito wa kile kilichotendeka na matokeo ya kitendo hicho.

  mwanahalisi
  [​IMG]
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hii serikali bana,yaani wawekezaji wanauwa na bado wana pewa nafasi ya kutetewa? hivi hii nchi wapi tunaelekea? jamani tuamke ikiwezekana tulipize kisasi haiwezekani kijana mwezetu achomwe moto na wawekezaji wanaotetewa na serikali then tunakaa kimya,leo kwake kesho kwetu,tusitegemee serikalii kufanya maamuzi mema juu yetu,nguvu ya umma itumike,
  inauma sana
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Loh!Kweli binadamu tuna roho za ajabu!Hamna kosa linalohalalisha kumchoma binadamu mwingine moto!Shame on them...Mungu na awalaani!
   
 4. Mpiga Nyoka

  Mpiga Nyoka JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Am ashamed kuongozwa na vipofu lkn siku zao zinahesabika. Hao wanaowaita wawekezaji ipo ziku tutawachuna ngozi we waache wadanganywe na hao mafisadi. Tusikubali mTz mwenzetu afe bure kwa maslahi ya mafisadi na wawekezaji... LAZIMA HAKI ITENDEKE.
   
 5. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  lol huyo chapati cjui chipata nilifafanya kazi kwake ilikuwa noma kwanza ugali haragwe mwaa.....mwiii na unyanyasaji wa kutosha wahindi anawakusanya mule ndani anawadhalilisha atakavyo kumtwnga general meneja wake makofi hadharani ni kawaida tuuu,haajiri mtu yani ni kama laana manake acheni tuuu!mie nlitimka bila kuchukua hata salariooo!!!!
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  lol huyo chapati cjui chipata nilifafanya kazi kwake ilikuwa noma kwanza ugali haragwe mwaa.....mwiii na unyanyasaji wa kutosha wahindi anawakusanya mule ndani anawadhalilisha atakavyo kumtwnga general meneja wake makofi hadharani ni kawaida tuuu,haajiri mtu yani ni kama laana, acheni tuuu!mie nlitimka bila kuchukua hata salariooo!!!!mungu amelipa!lakini pia nna mashaka km sheria itapita pande hzo huyo jamaa haaa!!!acha tuu
   
Loading...