Ukate miti milioni mbili halafu umuombe Mungu akuletee mvua? Serious?

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,025
Wakati tunatangaza kuharibu miti zaidi millioni mbili tulimuomba Mungu? Au wenzetu hamjui umuhimu wa miti?

Haya mlipanda miti mingapi? Leo hii mnataka kufunga eti Mungu alete mvua, you guys! Mko Sawa kweli?

Tusimdhibaki Mungu ana kazi za msingi sana kuliko hii, yaani tukate miti kwa mbwembwe vile kisa mnajenga bwawa? Liko wapi? Mtalijaza mikojo Wallah.

Anyway, CCM hoyeeee, mitano tena

=====

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme Tanzania

16 Mei 2018

Ukataji wa miti zaidi ya milioni 2 ni maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha umeme wa megawati
2,100

Serikali ya Tanzania inajiandaa kukata miti eneo la ukubwa wa asilimia tatu ya hifadhi ya taifa Selous.

Mapema asubuhi ya Jumatano, serikali ilipokea maombi ya zabuni ya kukata miti hiyo kutoka kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi yaliyoonyesha nia ya kutekeleza mradi huo wa kukata miti.

Serikali inasema ukataji huu wa miti zaidi ya milioni 2 ni maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha umeme wa megawati 2,100 utakaojengwa ndani ya hifadhi hiyo.

Hatua hii inaongeza ukosoaji dhidi ya serikali kutoka kwa wanaharakati wa mazingira ambao tangu serikali kutangaza nia ya kujenga mradi huo wa umeme, wamekuwa wakipinga mradi huo kuwa ni hatari kwa wanyama pori na viumbe wengine waishio katika hifadhi hiyo ya Selous, ambayo inatambuliwa pia kama urithi wa dunia.

Wanamazingira watoa tahadhari kuhusu mpango wa serikali

Ni wazi kwamba serikali ya Tanzania imedhamiria kuendelea na mradi huu wa kufua umeme, huku kukiwa na ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa mazingira, ambao wanaelezea wasiwasi wao kuhusiana na athari za hali ya mfumo wa kiikolojia ndani ya hifadhi ya Selous.

Hata hivyo hivi karibuni kuhusu mradi huo Rais John Magufuli aliweka wazi kwamba, serikali yake haitakwamishwa na ukosoaji wa aina yoyote ya kimazingira katika kutekeleza mradi huu mkubwa wa umeme.

Rais alisistiza kuwa wakati serikali yake inatekeleza sera ya viwanda,mradi huu wa umeme,ni muhimu zaidi kufikia malengo hayo.

Mtendaji mkuu wa wakala wa misitu Tanzania Profesa Dosantos Silayo ameiambia BBC sababu za kuuzwa kwa miti itakayo katwa kwenye hifadhi hiyo kupisha mradi huo.

''Sasa serikali imeona si vizuri kuiondoa miti katika hali ya kuiharibu inaweza kuwa na thamani, serikali imeamua kuitoa kwa utaratibu ambao utaiwezesha iuzwe kwenye makampuni mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kutengeneza samani ndani na nje ya nchi, hii si biashara, na kwa kweli haijawa nia ya serikali kufanya uharibifu kwenye hifadhi zake''.

Hata hivyo Mwanasheria wa mazingira Dokta Rugemeleza Nshala amezungumzia ni hatua gani za muhimu kuzingatiwa katika utekelezwaji wa mradi huo.

''Ni kitu ambacho kinapaswa kitekelezwe kwa umakini mkubwa kwa sababu eneo la hifadhi na bado lile eneo wanalotaka kukata miti bado halijatolewa kutoka eneo la hifadhi na ni eneo ambalo ni la urithi la dunia.Umeme unahitajika na mazingira yanahitajika.mazingira yakiharibika hasara ni kubwa zaidi''.

Kwa sasa Tanzania inayokadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 50,inazalisha kiasi cha megawati 1400 tu za umeme kiwango ambacho hakikidhi mahitaji ya nishati ya umeme ya nchi.

Mradi huu mkubwa wa umeme unatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati zaidi ya 2000 za umeme ili kuimarisha mahitaji halisi ya umeme.

Chanzo: BBC
 
Mbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:

Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana

Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai.

The choice is yours
 
Mbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:

Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana

Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai....

The choice is yours
Bwawa limejengwa, je ina maana mvua haitanyesha milele?
 
Mbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:

Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana

Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai....

The choice is yours
Wallahi hii kesi ya ugaidi siyo ya kweli na haina maslahi yoyote kwa taifa la tanzania zaidi ni kujidhalilisha tu! Nasema mama embu wafute kazi wote waliokudanganya tuanze upya watu wanasema na itawezekana mvua zisinyeshe kwa ajili ya utawala onevu
 
Mbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:

Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana

Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai.

The choice is yours
Viongoz wa din wanaombea MVUA mdomon Huku moyon wanaombea MBOWE AWASHINDE MADHALIMU
 
Wakati tunatangaza kuharibu miti zaidi million mbili tulimuomba Mungu?? Au wenzetu hamjui umuhimu wa miti?

Haya mlipanda miti mingapi?? Leo hii mnataka kufunga eti Mungu alete mvua....you guys! Mko Sawa kweli??

Tusimdhibaki Mungu ana kazi za msingi sana kuliko hii, yaani tukate miti kwa mbwembwe vile kisa mnajenga bwawa? Liko wapi? Mtalijaza mikojo Wallah.

Anyway, CCM.hoyeeee, mitano tena

View attachment 2015760
Hujitambui wala hujielewi mtoa uzi
 
Mbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:

Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana

Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai....

The choice is yours
Kunyoa ama kusuka mchicha
 
Back
Top Bottom