Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,550
- 729,445
Ni dhana mpya iliyoibuka kwa kasi miaka ya tisini mwishoni, wakajitokeza madaktari makanjanja wakata vimeo huko mitaani na uswazi, sasa hivi ni kitu cha kawaida kabisa kuna watu wanaendesha maisha yao kwa kukata vimeo kukata vimeo hakuna tofauti sana na kukeketa, tofauti yake kubwa ni midomo tuu
Binafsi sijawahi kuona kwenye hospitali zetu hizi kukiwa na huduma maalum ya kukata vimeo, hii iko huko vichochoroni kwa akina kajamba nani na serikali yetu imelala usingizi wa pono huku watoto wetu wakiathirika
Kimsimgi hicho kinachoitwa kimeo ni kiungo kimoja muhimu sana kwenye mwilini hasa kwenye mfumo wa hewa kwa jina lingine huitwa kidaka tonge, hiki ndicho kiungo ndani ya koo ambacho huziba njia ya hewa inayoelekea puani pindi chakula kinapopita kooni , na pia hutumika kama sensor ya chochote kinachopanda toka tumboni (kwa muktadha huu minyoo) kesi zote za kupaliwa huhusika na hiki kiungo
Kwanini watu hukatwa kimeo?
Kiafya mwanadamu anatakiwa kunywa dawa ya minyoo kila baada ya siku 90 (miezi mitatu) hii ni kutokana na vitu mbalimbali anavyokula na kunywa ambavyo vina vimelea vya minyoo...minyoo huzaliana na kumea tumboni baada ya miezi mitatu na hivyo kusababisha kichefuchefu kutapika na kupaliwa
Watoto wengi uswahilini hupata maambukizi ya minyoo kwa urahisi kutokana na mazingira wanaoishi na wazazi/walezi hawalipi hili kipaumbele minyoo inapokomaa tumboni hufanya ziara mwilini na kujikuta kuja mpaka kwenye koo, hapa mtoto lazima atapaliwa na kukohoa kikohozi kikatuletea hata kutapika kulingana na mechanism iliyopo
Mzazi/mlezi kwa kukosa elimu sahihi hudhani mtoto ana kimeo na kumtafuta mtaalamu mkata vimeo, huyu mtaalamu bandia anachofanya ni kukata sensor inayosumbua na mtoto kukoma kukohoa kupaliwa na kutapika, hii si sawa na kumpelekea fundi gari yenye shida ya check engine kisha akachomoa sensor husika...hapa hajatatua tatizo
Kitu kibaya ni kwamba siku hizi hizi dawa za minyoo zinasaga na hazikuonyeshi minyoo yako zamani zile tulikuwa na dawa ya anteper, hii ni kiboko kama una minyoo ukishainywa huendi kujisaidia chooni bali mahali ambapo utaona mzigo utakaotoka tumboni mara nyingi ilikuwa inatoka minyoo tupu
Jiulize kwanini wanaougua kimeo ni watoto wa fukara?
===Tafakari! Chukua hatua===!!!