Ukata wa fedha warudisha nidhamu ya madada, hata kwenye daladala, treni wanatongozeka

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF Umuhofia kwenu,

Leo nimeona nilete hili la asante Magufuli. Vijana inabidi tulipongeze kwani tumepata ngekewa ya kuwapata mademu wazuri ambao hapo awali walipotea kabisaa kwa sababu ya kutekwa na vibabu kimahaba.

Wengi wao waliwaza sana kupewa vijumba, magari hata kupangishiwa nyumba mzima ilimradi tu aonekane mdada wa mjini. Hivi sasa vibabu vingi vimetemwa utawala Magu, na vingine kubanwa kabisa, no safari , no fedha za ovyoovyo.

Hivyo basi wadada wengi ambao ulikuwa ukiwapa Hi wanakuangalia kwa jicho baya au ukirogwa ukakutana na demu ambaye bado anachati na kibabu ukamemesha, anasimamisha Inote /Pad yake ya mchina na kukuangalia jicho baya utafikiri umeua mtu, hivi sasa wapo wengi wamepaki magari, wengine kurudisha nyumba, wamebadilisha sauti zao zimekuwa za upole sana.

Konda akipita kukusanya chake wanatoa jicho la upendo waone kama watalipiwa. Jamani Magu mwema aisee, sasa hivi tunapata videmu vizuri wakati tulikuwa tunadhani wameumbiwa wenye nacho. Sasa hivi kesi nyingi kwa wakina mama zitapungua na watoto wa ndoa ndondo wataisha.
 
Kaah yaani nijipendekeze kwa nauli ya daladala 400???? Hapana aiseeeh bora nisotee hadi upepo utulie.
si unakuwa na hali ya kujiweka kutongozeka, baada ya kulipiwa kanauli si inabidi salamu zianzie hapo, njemba si inaanza kujitutumua hadi inakushusha kwenye daladala na kukubadilisha ulipokuwa unaelekea.
 
Kwa hiyo hiyo 400 ya nauli ya daladala????
 
si ndio mwanzo, si kwamba hauna kabisa madem wengi hawapendi kutoa wanapenda kutolewa tu, alafu ndio uwatwae
Hizo hela za mihogo ndiyo zimfanye mtu ashushe hadhi yake basi huyo demu atakuwa mbururaaaa tena wa mwisho.
 
Hizo hela za mihogo ndiyo zimfanye mtu ashushe hadhi yake basi huyo demu atakuwa mbururaaaa tena wa mwisho.
wengi si wametemwa, nyumba magari wamerudisha pesa za kuweka mafuta, kupanga sinza, mwenge na kino zimekwisha, magu kabana, starehe tena hakuna wale waliokuwa wanasema migodi inatema sasa wapo selo wanachungulia dirishani kama panya , waliobaki nazo kidogo wamewageukia wake zake, siku hizi kulala saa tano sio nane tisa tena
 
400 anaiona ndogo,hajui kuna wadada wakare wanaahirisha safafri kwa sababu ya 400 times idadi ya ruti
 
Back
Top Bottom