Ukata umepiga hodi, CCM waahirisha Mkutano wao Mkuu wa Chama kwa mara ya kwanza

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Chama cha Mapinduzi CCM, Kimeahirisha mkutano wao mkuu uliokuwa umeitishwa kwa dharula. Mkutano huo ulikuwa wakutane mwisho mwa wiki hii lakini umeahirishwa kwa kile walichodai ni kusaka fedha kwa ajili ya kuuitisha mkoani Dodoma.

Katika taarifa yake ya Mei mwaka huu, Ole Sendeka alinukuliwa akisema kuwa "dhamira ya kufanya Mkutano Mkuu Maalum utakaomkabidhi Magufuli uenyekiti iko pale pale, bali kilichopo sasa ni kutafuta fedha za kugharimia mkutano huo wa Juni.

Ole Sendeka alisema kwenye taarifa hiyo kuwa taratibu za kutafuta fedha za kuendesha mkutano huo zinaendelea na kwamba zikikamilika ndipo tarehe itapangwa". Inaelezwa kuwa chama hicho kinahitaji walau Sh. bilioni moja kwa ajili ya kufanikisha gharama za mkutano huo maalum.

Mkutano Mkuu wa chama hicho uliompitisha Magufuli kuwa mgombea urais wa chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana, walilipwa Sh 400,000 kila mmoja baada ya kuwapo Dodoma kwa siku tatu.

Kwa maana hiyo kukosekana fedha za mkutano huo maalum kwa sasa, ni pigo kwa sababu kunachelewesha uenyekiti wa Rais Magufuli. Rais Magufuli lazima apewe chama iwe isiwe kwani hata B. Mkapa, alimkabidhi chama Kikwete mapema kabla ya muda wake haujaisha.

Mei 4 mwaka huu, lilijitokeza kundi linalodaiwa kumshinikiza Mwenyekiti wa sasa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete asimkabidhi uenyekiti Rais Magufuli kabla ya muda wake kumalizika.

kuna hofu imejengeka ndani ya mtandao wa sasa wa CCM kwamba akikabidhiwa madaraka ya chama, Rais Magufuli atawatimua kama anavyofanya Serikalini.

Akiwa mkoani Singida kwenye sherehe za miaka 39 ya CCM, Kikwete alikaririwa akisema kuwa sherehe hizo ndizo za mwisho kwake, kauli inayomaanisha kuwa atamwachia nafasi hiyo Rais Magufuli mapema. CCM wanatete..wanatetemeka..tete..wanatetemeka.

Hahahaaaa...Kweli CCM wamefulia, kwa taarifa yako hadi sasa CCM bado inadaiwa na wasaniii mbalimbali wakiwamo wa filamu marufu kama ‘Bongo Movie’ na pia baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya (bongofleva) ambao walishiriki bega kwa bega katika mikutano ya kampeni ya chama hicho pesa imekata kabisa.

Ndani ya CCM hata pale makao makuu sasa hivi wanatembea kwa mguu na kupanda daladala, sababu ya Uchaguzi wa Mwaka 2015. Uchaguzi wa 2015 unadaiwa kukusha kibubu cha chama hicho kikongwe Tanzania.

Tangu Kuzaliwa kwake, CCm haijawahi kuishiwa hela hadi iahirishe Mkutano wake mkuu.

Nasikia kuna viongozi wa Juu hawataki kuachia madaraka ndo maana vikao vinaahirishwa. Kikao hiki ndo kilikuwa cha kumpa Rais Magufuli Uenyekiti wa Chama cha CCM.

CCM wanatete..wanatetemeka..tete..wanatetemeka.

Walizoea vya bure, mwaka huu imekula kwa CCM. Acha CCM waisome namba. Sasa Mzigo wa kuendesha chama umewalemea wabunge wa CCM, hutaki kuchangia chama siku ya kura za maoni jina lako linakatwa juu kwa juu.
 
tatizo sio pesa kwani hakuna chama chenye vyanzo vingi vya pesa kama CCM iwe halali au haramu kwani wanamiliki viwanja ,majengo na mali nyingine ukiachilia mbali ruzuku ila ukweli mwenyekiti hataki kung'oka kwani anajua akitoka madudu yatakayoibuliwa pale atasahaulika milele
 
Inawezekana na agenda ya mzee wa Msoga kumkabidhi kijiti Mzee wa kutumbua majipu nayo ikawa ndiyo sababu kuu ya kigugumizi cha kuitisha kikao hicho, kwa kuwa wenye chama wanahisi huyo mtumbua majipu atawasomesha namba ile mbaya....
 
downloadfile-28.jpeg


swissme
 
Nadhani suala la fedha kama sababu ya kuahirisha mkutano wamelichomekea tu kwakua Baba Riz hayuko tayari kumkabidhi chama mapema. Hata hivyo hiyo nayo haimsaidii kwakua 2017 sio mbali, na JPM nae akipewa hapo baadae anaweza akamuanika tu. Kama ameshakua Rais ni ampishe tu maana hakuna njia nyingine, mengine ni sawa na kut...oza matatizo utayapata tu
 
tatizo sio pesa kwani hakuna chama chenye vyanzo vingi vya pesa kama ccm iwe halali au haramu kwani wanamiliki viwanja ,majengo na mali nyingine ukiachilia mbali ruzuku ila ukweli mwenyekiti hataki kung'oka kwani anajua akitoka madudu yatakayoibuliwa pale atasahaulika milele
ni kweli kabisa
 
Chama cha Mapinduzi CCM, Kimeahirisha mkutano wao mkuu uliokuwa umeitishwa kwa dharula. Mkutano huo ulikuwa wakutane mwisho mwa wiki hii lakini umeahirishwa kwa kile walichodai ni kusaka fedha kwa ajili ya kuuitisha mkoani Dodoma.

Ndani ya CCM hata pale makao makuu sasa hivi wanatembea kwa mguu na kupanda daladala, sababu ya Uchaguzi wa Mwaka 2015. Uchaguzi wa 2015 unadaiwa kukusha kibubu cha chama hicho kikongwe Tanzania.

Tangu Kuzaliwa kwake, CCm haijawahi kuishiwa hela hadi iahirishe Mkutano wake mkuu.

Nasikia kuna viongozi wa Juu hawataki kuachia madaraka ndo maana vikao vinaahirishwa. Kikao hiki ndo cha kupanga ratiba ya Uchaguzi ufanyike lini.

Parapanda limelia parapanda, CCM parapanda limelia, parapanda!
Waache waisome namba, walifikiri wanawakejeli wapinzani sasa inakula kwao! Tutaheshimiana tu mwaka huu.
 
tatizo sio pesa kwani hakuna chama chenye vyanzo vingi vya pesa kama ccm iwe halali au haramu kwani wanamiliki viwanja ,majengo na mali nyingine ukiachilia mbali ruzuku ila ukweli mwenyekiti hataki kung'oka kwani anajua akitoka madudu yatakayoibuliwa pale atasahaulika milele
Ampishe hankuna njia nyingine
 
Tatizo CCM mlizoea kuendesha shughuli za chama kwa kutumia pesa ya pesa za walipa kodi wote qa tz....sasa mmekwama.
 
Back
Top Bottom