Ukata serikalini: Jk ungesimama kidete kutekeleza haya mawili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukata serikalini: Jk ungesimama kidete kutekeleza haya mawili...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tutafika, Feb 4, 2012.

 1. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 160
  Mwanzoni ilianzia kwa wapinzani (kina Zitto) kwamba serikali imefilisika, imeishiwa, haikopesheki..n.k, kama kawaida CCM wakaona hii hoja ni kweli lakini ikibebwa na wapinzani, itakua balaa!, haraka haraka Mkulo alikanusha vikali sana. Tukaendelea kuchechemea katika ukweli ule (Ukata), mara migomo ikaanza kuibuka ya watoto wa vyuo na walimu nao wakaanza vitisho (kama kawaida yao), baadae ikabidi Mkulo awahi haraka sana kupanua mkopo kutoka benki za ndani, basi tukapumua kidogo.

  Sasa ndani tumekopa tumemaliza, Nje ndio tulishamaliza zamani, hatuna pa kukimbilia kukopa ili kuendelea kuficha ule ukweli (Ukata), tunalazimika kusema ukweli, liwalo na liwe!

  Ghafla Mkuchika akapiga mbiu, jamani ukataaaaa!, JK nae akadakia, UKATAAAAA! (Ila tuko makini hatuwezi kumtuma Mkulo yule yule kusema hili japo mambo ya ukata na ukwasi ndie anaehusika zaidi), Haya!

  SASA NDUGU YANGU MPENDWA JK, Kwanini ulilainika ukasitisha utekelezaji wa mipango hii ambayo ulijaribu ''kuthubutu''?

  1. Mpango wa kutenganisha biashara na siasa

  2. Mpango wa kuondoa msamaha wa kodi katika taasisi za dini

  Inawezekana hukuzibuni wewe na aliezibuni hakukushawishi vya kutosha kwamba utekelezaji wake ingekua mkombozi mkubwa kutoka katika janga la ukata!, au inawezekana kelele za Wafanyabiashara, Maaskofu na Masheikh zilikutisha sana!, au inawezekana yote hayo sio sababu hata kidogo iliyokufanya ukachelea kutekeleza hiyo mipango. NAKUSHAURI USIKOMAZE SHINGO, GEUKA MZEE!
   
 2. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 866
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Do! leo nina hasira sana labda baadaye!
   
 3. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,151
  Likes Received: 1,355
  Trophy Points: 280
  Ukata untokana na serikari kushindwa kukusanya kodi hasa kwa wafanyabiashara wakubwa na wafadhili wa ccm na ufisadi wa viongozi
   
 4. B

  BMT JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 569
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  yeye alikta hazna kuna hela za ktosha tka serkal ya mzee mkapa,bila hiana wala mafindofindo akaanza safari za kujtangaza kimataifa nakmbuka mwaka 2006 pekee alisafiri mara 78 nje ya nchi,pili bla kufkiria akapanua baraza la mawaziri,makatbu wakuu na manaibu wao,uteuz huo ukizingatia zaidi urafiki na wala s utendaji wa mtu,ikaja ishu ya richmond-dowans hapo ndo ikawa ndo mwsho wa kikwete,makusanyo ya kodi yakaanza kushuka,nawahakikishia kfka 2015 watanzania tutalia kilio cha mtu mzma
   
 5. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 160
  Wabunge nao naona wanamkomalia, ndio kabisa atachanganyikiwa, ushauri basi tena
   
 6. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,254
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Walioipigia ccm kura walaaniwe milele kwa hila, umbumbu na tamaa zao,
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Mar 9, 2015
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,105
  Likes Received: 1,390
  Trophy Points: 280
  Ukata SERIKALINI UMEFIKIA HATUA MBAYA ...

  WALIO NA NDUGU MAGEREZANI WAFUATILIE..KWAKUWA WALIOTOKA WANASEMA ....HALI YA CHAKULA ,MALAZI NA MADAWA MAGEREZANI IMEKUWA MBAYA NA KUSABABISHA BAADHI KUFA HASA WANAOTUMIA MADAWA YA ARV ...KWA KUKOSA LISHE ..
  HAYA NI MADAI MAZITO WENYE NDUGU ZENU JELA ULIZIENI ...

  HATA KWA MAVAZI YA ASKARI HASA MAGEREZA ..IMEKUA TABU SANA...BADALA YA KUPATA MAVAZI KILA MWAKA WAKO ASKARI WANA MIAKA MITATU HAWAJAPATA MIGAO .......

  ZAIDI YA MISHAHARA AMBAYO NAYO INASUA ..TAAISISI NYINGI ZINAPUMULIA MASHINE

  EEH Hii MIEZI 8 Bairiki JK ATUVUSHE SALAMA
   
Loading...