Ukata mkali waitafuna serikali- mgawo wa idara, taasisi wapunguzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukata mkali waitafuna serikali- mgawo wa idara, taasisi wapunguzwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by SG8, Feb 20, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  SERIKALI imesema hivi sasa haina fedha za kukidhi mahitaji ya idara na taasisi zake na kuwataka wananchi kuwa makini katika matumizi ili kukabiliana hali ngumu iliyopo.
  Akizungumza katika mahojiano maalum na MTANZANIA Jumapili ofisini kwake mjini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Ofisa Habari na Mahusiano wa Wizara ya Fedha na Uchumi,Ingiahedi Mduma, alisema pato la serikali hivi linategemea zaidi kodi za wananchi tofauti na miaka ya nyuma.
  Alisema zamani kiasi kikubwa cha fedha za kujiendesha, kilikuwa kikitoka kwa wafadhili.
  Licha ya kutokuwa tayari kufafanua kiundani, ofisa huyo alisema matumizi ya fedha katika baadhi ya halmashauri nchini hayafuati taratibu zinazotakiwa.
  Alisema katika siku za nyuma, halmashauri zimekuwa zikitumia vibaya fedha zinazotengwa kila mwaka,bila kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.
  "Hivi sasa serikali ina upungufu mkubwa wa fedha na hata halmashauri zetu zinachangia kuwepo hali hii, kutokana na kutumia fedha kinyume cha malengo yaliyopangwa,"alisema Mduma.
  "…ni kweli hivi sasa serikali haina fedha kabisa… tunaendelea kujipanga kuona namna gani ya kupambana na hali hii".
  Alisema sababu moja ya kukosekana kwa fedha kumechangiwa na matumizi mabaya ya wakuu wa vitengo, ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao.
  "Unajua kila mhusika hasa halmashauri zetu, zinatakiwa kuainisha bajeti yake ya kila awamu… hivyo wanapotumia fedha hizo kinyume cha maombi yake, awamu inayofuata watakatwa ili kufidia awamu iliyopita,"alisema Mduma.
  Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imeanzisha kitengo cha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha kwa kila halmashauri zote nchini ili kukabiliana na wimbi hilo.
  "Serikali imeanzisha kitengo cha ukaguzi kwa halmashauri ili kukabiliana na wimbi hili, kwani tumebaini fedha zinazoombwa kwa miradi mingi hugeuzwa kwenda kufanya miradi ambayo haikutarajiwa,"alisema Mduma.
  Alisema kutokana na hali hiyo, kila halmashauri imetakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi hizo ili kuokoa jahazi.
  "Ni kweli hakuna fedha si unaona hata hapa ofisini kwangu hakuna hata faili moja… sisi wenyewe hapa kukavu kwa kuwa tunafahamu hali halisi hatuwezi kulalamika wakazane tu kuzikusanya kodi ili tuwagawie haraka kile kinachopatikana,"alisema Mduma.

  MY TAKE: Kuna umuhimu gani wa kuwa na serikali ambayo inafahamu kuwa kuna ubadhirifu halafu inawafumbia macho? rejea malamiko ya Mh. Selasini dhidi ya watumishi wa halmashauri ya Rombo na uamuzi wa serikali wakuwahamisha badala ya kuchukua hatua. Yako wapi matanuzi makubwa tuliyoyaona wakati wa uchaguzi? HAKIKA YEYOTE ALIYEIPIGIA KURA CCM NA AJUTE SASA
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli inasikitisha serikali inajua wapi kuna matumizi mabovu haichukui hatua babala yake inaunda kitengo cha kufuatilia matumizi huko kwenye halmashauri. Wizi mtupu!!!!!!!!!!!
  dhambi kwa aliyeipigia kura ccm
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Serikali yetu huwa inasubiri majanga kugundua matatizo katika uendeshaji wake, haya hayajaonekana leo!!!

  To me this is not a news!!! Wacha waende ende tu, mwisho ni pale watakapopaki mpaka motocade ya prezidaa...

  !@#$*..%#rguh ...s@en..@#...JK and your aides!!!
   
 4. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Moyo unanidunda na nina juta kuwa mateka wa CCM maana nilio wa chagua waliporwa ushindi ............
   
 5. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wanasema waongeze kukusanya mapato ya kodi??? kwani zamani walikuwa hawakusanyi hizo kodi? Mkulu wao yeye kazi kusafiri tu sijui hajui maana ya kuwa na simu, na nasikia eti kaenda Mauritius sijui, what the hell man! mbona wakuu wengine hawasafiri kama yeye? kwa nini asitumie simu! Arghh this is annoying!!
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo lililopo ni kwamba inapojitokeza hali ya ukata, wanao ambiwa kukaza kamba ni wadogo, wakati wakubwa wanaendelea kutumbua kama kawaida; kwa mfano hivi sasa ingelitegemewa kwamba matumizi kama vile ya chai cha ofisini kilichotengewa shs 30 bilioni, usafiri wa daraja la kwanza kwenye ndege, ukaaji kwenye five star hoteli n,k ndivyo vingelianza kupigwa panga.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,646
  Likes Received: 82,373
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kuandika hapa siku za nyuma kutokana na utendaji finyu katika awamu ya kwanza ya Kikwete basi awamu ya pili hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi. Sasa yamekuwa kweli. Na Wafadhili walioandikiwa barua ya kuomba pesa za kuendesha Serikali kati ya sasa na June, 2011 wakiamua kukataa kutoa hata senti moja basi hali ndiyo itakuwa ya kutisha zaidi.
   
 8. p

  paolo Member

  #8
  Feb 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashangaa, lakini walipotueleza Chadema kuhusu upungufu wa Kikwete na chama chake, tukasema wao ni kutoka North, na baadaye ati ni wakatoliki. Kikwete akafilisi Hazina ya nchi akitaka achaguliwe, tukasema Hazina ni yake. Tujute tu na kuapa kutorudia makosa tuliyofanya. Nina hakika ukata huo hauna makali yoyote kwa jeshi la Polisi weala kwa JWTZ. Mkubwa anajidanganya kudhani hao ndiyo kinga yake. Aulize yaliyompata yule wa Tunisia na wa Misri na yale yanayotokea nchi za Kiarabu. Nao pia wanayo majeshi
   
 9. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Tena wafadhili wagome wasitoe hata shilingi.
   
 10. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  oh my God kalimbikizo ka mshahara wangu ka miezi miine sasa itakuwa ndoto kukapata kama hali imeshafikia huko. Kikwete unatupeleka wapi?
   
 11. m

  muafaka Senior Member

  #11
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  na bado unataka kuitwa great thinker!!!!? I don't think you deserve that!! thanks anyway for joining us.
   
 12. PEA

  PEA Member

  #12
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuko wengi kumbe. afadhali wewe unazungumzia malimbikizo, wenzio kibao hatujalipwa tangu tumeajiriwa mwezi ule wa uchaguzi na hatujui tutaanza kulipwa lini kama sio mwaka ujao wa fedha. Products za usanii hizi
   
 13. k

  kayumba JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Ukifuatilia maelezo ya thread yenyewe utaishi kusema bora hiyo hela ya wafadhili isitishwe ili tuweze kuishi kwa jasho letu na tutakuwa makini na matumizi yetu!. Kwanini???

  Huyo mtu wa wizara ya fedha anasema unajua almashauri siku zote uwa wanatumia vibaya pesa na sasa kwakuwa hakuna hela ya wafadhili kimeudwa kitengo cha kuhakikisha matumizi yaliyokusudiwa ndiyo yanatumika!

  Hii inamaanisha wanatumbua pesa kwasababu ni za wafadhili, kama Great thinker utaona kinachofaa nini?
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ingia mtaani sychologically kama wengi weu tulivyo
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Eeh mola wangu; wangazaie hao wafadhali wasitoe hata senti tano mpaka pale serikali irakapomaliza kutekeleza ahadi zote za uchaguzi.
   
Loading...