UKATA: Kampuni ya Maxcom Africa yatangaza kupunguza idadi ya wafanyakazi wake kutokana na kupungua kwa mapato

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Kampuni ya Maxcom Africa Plc imetangaza kupunguza idadi ya wafanyakazi wake kutokana na kupungua kwa mapato ya kampuni hiyo.

Katika barua iliyotolewa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, imeeleza kuwa, inalazimika kufanya mabadiliko katika mfumo wake wa uongozi na utendaji kazi ili kuongeza ufanisi na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Kutokana na mabadiliko hayo kampuni hiyo imelazimika kupunguza wafanyakazi ili isielemewe na mzigo wa kuwalipa kutokana na mapato kupungua.

kampuni hiyo ambayo iliingia mkataba wa miaka miwili na Wakala wa Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi (UDART), katika kutoa huduma ya ukusanyaji wa nauli, iliacha kutoa huduma hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake mapema mwaka huu.

Chanzo kingine cha kushuka kwa mapato ya kampuni hiyo kinadaiwa kuwa ni kuanzshwa kwa mfumo mpya wa malipo wa serikali, jambo lililosababisha mashirika na taasisi mbalimbali za serikali kucha kutumia huduma za kampuni hiyo na badala yake kuhamia katika mfumo mpya wa malipo wa serikali.

Hapa chini ni barua iliyoandikwa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusu taarifa ya kupunguza wafanyakazi.

C3A44486-59AF-4B9C-87B3-A43BC4D6B174.jpeg
 
Ilikuwa imeajiri wafanyakazi wangapi ?
Ilukuwa inalipa mishahara kiasi gani?
Wamepunguzwa wafanyakazi wangapi?
Mapato yake kwa mwezi yalikuwa sh ngapi?
Ni asilimia ngapi ya mapato yalikuwa yanalipia mshahara?
Mapato yamepungua kwa kiasi gani?
Ilikuwa inalipa kodi sh ngapi?
 
Marekani wanalinda sana private businesses
Sisi twaziharibu
Ngoja nikupe mfano mmoja ndiyo utaelewa matatizo hasa yanayowakumba private sectors wa Tanzania:
Ukisafiri barabara ya Dar to Arusha utakuta hotel zimejengwa katikati mbugani kwa ajili ya kuhudumia wasafiri. Hizi hotel ni za ''wajanja'' wachache ambao waliamua kutumia udhaifu wa serikali yetu kufanya biashara. Wameamua kujenga ndani ya mapori na kuhonga madereva wa mabasi ili wawe wanasimama na abiria wale. Chakula wanachouza wanapanga bei waitakayo kwani wanajua abiria hana cha kufanya. Siku akitokea kiongozi mzuri na kuamua kuwa sehemu ya mabasi kusimama kwa abiria kula ni eg Korogwe, kwasababu ndiyo stendi kuu, wenye haya mahoteli wote watafunga biashara zao.

Tukirudi kwenye mada yetu: Uanzishwaji na Uendeshaji wa baadhi sector binafsi Tanzania umejikita kwenye ujanjaujanja kama wa wenye haya mahoteli. ie. Zilianzishwa zikilenga udhaifu fulani katika seriakli iliyopita.

Mabenki yalikuwa yanategemea ''kucheza'' na fedha za serikali na mashirika yake kutengeneza faida. Mahoteli nayo yalikuwa yanategemea kucheza na serikali ili kupiga fedha za vikao nk.

Hii kampuni inaitwa Maxicom Africa: Je, ilikuwa inategemea tu kufanya biashara na serikali? Au na yenyewe ilianzishwa kiujanjaujanja?

Verdict: Watanzania tuache mazoea ya kuishi kwa madili! Halafu... Nadhani serikali ilinde sector binafsi tu pale ambapo ina umuhimu wa kuwepo. Siyo kampuni inayo-act tu kama middle man ili kupiga fedha kwenye vitu ambavyo havina ulazima.
 
Serikali kutaka kufanya kila kitu kunaua kampuni nyingi ambazo zilikuwa zinaajiri Watanzania moja kwa moja au indirect.
Ngoja tuone mwisho wa mchezo huu
 
Ilikuwa imeajiri wafanyakazi wangapi ?
Ilukuwa inalipa mishahara kiasi gani?
Wamepunguzwa wafanyakazi wangapi?
Mapato yake kwa mwezi yalikuwa sh ngapi?
Ni asilimia ngapi ya mapato yalikuwa yanalipia mshahara?
Mapato yamepungua kwa kiasi gani?
Ilikuwa inalipa kodi sh ngapi?
Hiyo ndio Tanzania ya viwanda
 
Hawa nao wezi tu.... Ni afadhali serikali imewanyanganya uwakala wa baadhi ya huduma
 
Ngoja nikupe mfano mmoja ndiyo utaelewa matatizo hasa yanayowakumba private sectors wa Tanzania. Ukisafiri barabara ya Dar to Arusha utakuta hotel zimejengwa katikati mbugani kwa ajili ya kuhudumia wasafiri. Hizi hotel ni za ''wajanja'' wachache ambao waliamua kutumia udhaifu wa serikali yetu kufanya biashara. Wameamua kujenga ndani ya mapori na kuhonga madereva wa mabasi ili wawe wanasimama na abiria wale. Chakula wanachouza wanapanga bei waitakayo kwani wanajua abiria hana cha kufanya. Siku akitokea kiongozi mzuri na kuamua kuwa sehemu ya mabasi kusimama kwa abiria kula ni eg Korogwe, kwasababu ndiyo stendi kuu wenye haya mahoteli wote watafunga biashara zao. Tukirudi kwenye mada yetu: uanzishwaji na Uendeshaji wa baadhi sector binafsi Tanzania umejikita kwenye ujanja janja kama wa wenye haya mahoteli. ie. Zilianzishwa zikilenga udhaifu fulani katika seriakli iliyopita. Mabenki yalikuwa yanategemea ''kucheza'' na fedha za serikali na mashirika yake kutengeneza faida. Mahoteli nayo yalikuwa yanategemea kucheza na serikali ili kupiga fedha za vikao nk. Hii kampuni inaitwa Maxicom Africa. Je, ilikuwa inategemea tu kufanya biashara na serikali? Au na yenyewe ilianzishwa kiujanja janja?.
Verdict: Watanzania tuache mazoea ya kuishi kwa madili! Halafu... Nadhani serikali ilinde sector binafsi tu pale ambapo ina umuhimu wa kuwepo. Siyo kampuni inayo-act tu kama middle man ili kupiga fedha kwenye vitu ambavyo havina ulazima.
Acha kutetea ukandamizaji wewe
 
Ilikuwa imeajiri wafanyakazi wangapi ?
Ilukuwa inalipa mishahara kiasi gani?
Wamepunguzwa wafanyakazi wangapi?
Mapato yake kwa mwezi yalikuwa sh ngapi?
Ni asilimia ngapi ya mapato yalikuwa yanalipia mshahara?
Mapato yamepungua kwa kiasi gani?
Ilikuwa inalipa kodi sh ngapi?

Maswali yote haya unaweza kuta huna hata kampuni!!!!
 
Back
Top Bottom