Uchaguzi 2020 Ukara: Wananchi wamuua mtu aliyetaka kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisya kwa tiketi ya CHADEMA

Mtu mmoja ameuawa asubuhi hii na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya kujaribu kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisha Ukara kwa tiketi ya CHADEMA.

Inadaiwa watu hao wamezingirwa baada ya mgombea huyo kupiga ukunga na ndipo walipozingirwa na kushushiwa kipigo ambapo mmoja ameuawa huku wawili wakifanikiwa kutoroka.

Hilo ni tukio la kwanza la mauaji yanayohusishwa na mambo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo kunatabiriwa kuwepo kwa visa vingi vya vurugu kutokana na sintofahamu ambazo zimeanza kujitokeza.

Habari hii imethibitishwa na Katibu wa kanda ya Victoria- CHADEMA ndugu Zacharia T. Obad
NAOMBA KUSAHIHISHA siyo BWISHA ni BWISYA na pia tukio hiil limetokea UKARA KATA YA NYAMANGA.

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ni kwamba unajifanya hujui kuwa ccm ndio wanaoratibu mambo haya ama? Kila mara nikikuambia toka awamu hii ya tano iingie madarakani tumeona chaguzi zilizoandanwa na ushenzi, ukatili, unyama na uhayawani wa wazi, ulikuwa unadhani natania? Na ukitaka kujua haya ni mambo ya kupanga kabisa, angalia mpaka mkurugenzi na polisi wanafanya haya haya matendo ya kihuni.

Ccm imeshachoka kushindana. Huko kwa waziri mkuu wagombea wa ACT wametekwa na kuachwa na vilema vya maisha. Huko ni kwa waziri mkuu, hao walio chini yake unategemea nini?
Heshima yako mkuu.

Mkuu nimeshaweka maoni yangu humu (nisingependa kurudia) na kuna hoja nyingi nilizojaribu kueleza juu ya shaka yangu kwa uhusika wa ccm kwenye haya matukio, nadhani ukiwa unapitia humu utayaona tu na kama nimekosea kwenye hoja basi pia utakosoa mkuu.

Ila kwa kifupi tu, nitaita wajinga sana ccm Kama kweli wao ndio wanaratibu mauaji na utekaji sababu haina faida kwao badala yake ni hasara tu kwa kujishushie Imani kwa wale ambao bado wanaimani nao.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kutumia mbinu ya kijinga kiasi hiki huku akiwa anatazamwa naamini hata ungekuwa wewe usingefanya hivyo hata mara moja.
 
Historia ya dunia inaoneshakwamba umwagaji damu ukishaanza haukatiki hadi nduli atorokee burigi
 
Hahaha hawa wakara walitakiwa waende Dodoma leo kulinda maslahi ya chama chao, wanaonekana kumudu kazi yao.

Kaijage angekuwa keshamtangaza Lisu mgombea.
 
Kuna sera bilioni kuonesha kushindwa kwa ccm,hata mngemjengea kila mtu nyumba ila kuburuzwa kama unafugwa sio hulka ya binadamu,hukumbuki Nyerer alisema bora mbwa maskini aliye huru kuliko aliyenenepeana na kupewa kila kitu ila kafugwa kwa kufungiwa ndani?
By the way umeme umefika vijijini lakini sasa wanakijiji waliounganisha unakuta hawazidi hata 20 kijiji kizima na hapo ni 27,000,unajua kwa nini? ccm mnafeli sana maana vipaombele vyenu sio vya wananchi.
Mkuu Kwenye UMEME
1/.unafanya wayering
2/.unachora ramani
3/.unakaguliwa (wepesi wako)

NGoma Ipo KWENYE kULIPIa ili upewe risit ,ndo ukafungiwe MITA.

Utaambiwa Mtandao unasumbua ,acha no. Ya simu mtandao ukikaa sawa utapigiwa uje kulipia.

Ndo imetoka hiyo.
Utakaa miaka BUKU mpaka utasahau habari za umeme.

Utaishia kuona kwenye mitandao
umeme nchi nzima 27,000/=.
 
Mtu mmoja ameuawa asubuhi hii na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya kujaribu kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisha Ukara kwa tiketi ya CHADEMA.

Inadaiwa watu hao wamezingirwa baada ya mgombea huyo kupiga ukunga na ndipo walipozingirwa na kushushiwa kipigo ambapo mmoja ameuawa huku wawili wakifanikiwa kutoroka.

Hilo ni tukio la kwanza la mauaji yanayohusishwa na mambo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo kunatabiriwa kuwepo kwa visa vingi vya vurugu kutokana na sintofahamu ambazo zimeanza kujitokeza.

Habari hii imethibitishwa na Katibu wa kanda ya Victoria- CHADEMA ndugu Zacharia T. Obad
Yes haya ndio mambo tunayotaka kusikia kutoka kwa wananchi, BAVICHA amkeni pigeni kisawa sawa hadi akili ziwakae sawa hongereni sana bado watoto wa Sryoo.
 
Hii roho mbaya ya kutekana inaonekana kushamiri. Kama waliweza kumthibiti wasingemua ili tujue ni akina nani waliowatuma.....
Yaani hili la kutaka asiuliwe ndo tujue waliomtuma, wakati inajulikana kabsa. Hao ndo wametoa fundisho nzr kwamba watu wamechoka na ushamba wanaofanya ccm
 
Kuna sera bilioni kuonesha kushindwa kwa ccm,hata mngemjengea kila mtu nyumba ila kuburuzwa kama unafugwa sio hulka ya binadamu,hukumbuki Nyerer alisema bora mbwa maskini aliye huru kuliko aliyenenepeana na kupewa kila kitu ila kafugwa kwa kufungiwa ndani?
By the way umeme umefika vijijini lakini sasa wanakijiji waliounganisha unakuta hawazidi hata 20 kijiji kizima na hapo ni 27,000,unajua kwa nini? ccm mnafeli sana maana vipaombele vyenu sio vya wananchi.
Kweli kamanda!
Ndio maana tunasema Lisu akichukua nchi tutang'oa nguzo zote huko vijijini. na hizo hospitali alizojenga zikae tayari. Na tutarudisha vyeti feki kama kawa.
Hatutaki maendeleo ya vitu sisi.
Maendeleo gani hayo wakati hatuko huru kuropokaropoka na kuandamana
 
Ndio mana nikasema kuwa kama ni kweli wao ndio wanaratibu hayo basi watakuwa ni wapumbavu wa kiwango Cha lami.
Yaani uende kujianika kabisa kurusha mawe kwenye msafara wa kiongozi wa upinzani huku ukiwa umevaa nguo za chama chako? Una akili kweli kichwani kweli hapo? Mi siamini Kama ni wajinga kiasi hiki mkuu.

Yaani wachome ofisi ya CHADEMA Arusha na tuhuma, lawama na zingo lote la ubaya kutupwa kwao kisha eti kabla ya watu hawajasahau kilicho tokea huku kila Kona wakisemwa vitaya eti wanakwenda kuchoma ofisi nyingine ya CHADEMA Mbeya? hata Kama akili huna kabisa lakini huwezi kufanya vitu vya namna hiyo, siamini kabisa kama ni wajinga wa kiwango hiki mkuu.
Tatizo ni ushabiki kwasasa wanachama wa Ccm wanaamini hata akikuua alhatqfanywa lolote, na wanaamini akifanya jambo la kuumiza wapinzani atapandishwa cheo ndio maana wanaofanya hawajifichi wapo hadharani
1.Makonda alimpiga vibao jaji Joseph warioba akapewa ukuu wa wilaya.
2.Alexender mnyeti alihamasisha na kutoa rushwa kuhamisha wapinzani kujiunga Ccm akapewa ukuu wa mkoa.
3.Mkuu wa wilaya (mpya) wa Arusha alitoa kauli ya kumuua zito hadharani akapewa ukuu wa wilaya
4.Sabaya ametukana wapinzani akapewa ukuu wa wilaya

Haya yote yanafanyika mchana kweupe na hawa wanaofanya haya wanajianika hadharani ili wapate uteuzi
Na hawatofanywa lolote polisi imewakamata kama Geresha tu ila polisi haina nguvu yoyote juu ya wana CCM

TANZANIA NI YETU SOTE TUWE WAZALENDO NYUMBA IKIUNGUA HAKUNA ALIYE SALAMA.
 
Back
Top Bottom