Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mkuu wa nchi amekataza siasa kwanini ajaribiwe? Kwani msipovaa hayo mashati ya kijani mtaonekana hamkwenda kuzika?

Mkuu wa nchi anakataza siasa lakini yeye ndio kinara wa siasa. Asichotaka na kuweza ni siasa za ushindani. Ila ukifanya siasa kwa mgongo wa ccm hana shida, kwake na wanaccm wenzake siasa zinaanzia pindi cdm na cuf wakijiingiza kwenye jambo. Sasa kama yeye alipokea makada waliohama upinzani na kuhamia ccm kwenye hafla ya kijeshi unategemea nini?
 
Sasa unaweza kuwazuia watu wasivae vile wanajisikia siku hiyo, acheni siasa kwenye mambo yanayowaumiza wengine

Hivi unafahamu watu walivaa tshirt ya Lissu na kutaka kumuombea, kodi za wananchi zikatumika kutuma polisi kuvuruga hilo huku kila aliyekutwa Amevaa tshirt ya Lissu akaishia police?
 
Siasa Tanzania Inatia Kinyaa Yaani Kila Uchao Hadi Eneo Lisilohitaji Siasa Watu Wanaingiza

Tuvumiliane
 
Hapa ndipo kama nchi tunapokuwa wapumbavu kwa ujumla wetu.
Siku ya alhamis SAA 1.22 jioni nikiwa eneo la tukio nilimuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitangaza kusitisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza. Na nikiri wazi sikumsikia akisema ameshauriwa na wataalamu au yalikuwa mawazo yake. Wakati anatoa tangazo lake kulikuwa na divers ndani ya kivuko ambao walitoka na miili kadhaa saa mbili kasoro hivi. Mara baada ya kutangaza kusitishwa kwa zoezi vilio vilisikika mwaloni toka kwa ndugu waliokuwa na matumaini labda kuna watu wako hai ndani. Baada ya kusoma mawazo ya waombolezaji Mkuu wa wilaya ya Ukerewe akalazimika kutuliza hali ya hewa kwa kusema, namnukuu; Ndugu zangu katika hali ya kawaida mtu hawezi kukaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya manne bado akawa hai kama hana vifaa vya kumsaidia kupumua, Sisi viongozi wenu tuna huzuni kama ninyi lakini kazi hii haiwezi kufanyika gizani, mwisho wa kunukuu". Kwa vile watanzania huwa tunaona kauli za viongozi ni kauli za mbingu wengi walitii lakini wachache wenye uchungu walitoa hoja wakaonekana wabishi mbele ya viongozi. Hilo ziwa lililochafuka SAA 1 jioni hapa Ukara ni lipi? Au waliondoka nalo sisi hatukuliona? Kivuko kimezama chini ya mita 100 toka ufukweni, wazoefu wa ziwa mnajua vizuri, hivi hata ziwa likichafuka kwa umbali huo na kwa watu wenye vifaa watashindwa kuendelea na kazi?
Kesho yake baada ya kelele za wananchi na mitandaoni zoezi lilifanyika hadi usiku siku ya Ijumaa. Hizi sababu za ziwa kuchafuka tumeanza kuzisikiaIjumaa jioni baada ya Waziri Mkuu kuwepo na walikuwa wanaongea kama kujikosha tu na Leo ndo zimeletwa hapa kama sababu rasmi.
Siasa zinatufanya watanzania tukose mawazo ya kuhoji hata vitu vya msingi. Nawashangaa vijana wa ccm mitandaoni mnavyokosa utu na kushabikia makosa ya kiutendaji kwa vile tu aliyekosea ni wa Chama chenu. Sidhani kama kuna mwanaccm mwenye uchungu na aliyepotelewa na ndugu/jamaaa/rafiki kama ilivyonitokea Mimi anayeweza kuunga mkono mawazo yenu. Mimi nilisafiri Jumanne na kivuko hicho hicho na alhamis kikapata ajali, lakini maneno ya usalama mdogo ndani ya kivuko yalikuwepo, na bado tulijaa ingawaje si kama siku ya gulio Bugolora. Siku za Gulio mpaka mitumbwi toka Chifule na Chibasi huwa inasadia kutokana na wingi wa watu.
Mbunge wa Ukerewe kawa mkweli kwamba kivuko kilifanyiwa ukarabati, napo ni kuwekewa injini mpya tu na hoja kuu hata kwenye baraza za madiwani ni kupatiwa kivuko kipya na kikubwa zaidi.
Acha nikae kimya Nina majonzi.
Daaah Mkuu maelezo yako yamenihuzunisha sana. Watu wanaropoka humu kwa kutetea ujinga kwa sababu tu hawajaondokewa na Ndugu zao .
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
Ni vema angekaa kimya kuliko kutangaza usitishaji wa uokoaji.Kama kuna watu wameokolewa siku mbili baada ya tukio je tungeendelea na uokoaji tungeokoa wangapi?
 
Majibu hovyo kabisa. Mimi ni auditor wa usalama na mifumo ya usalama mahali pa kazi kwa ngazi ya kimataifa.

Ajali hii imetuumiza sote lakini kama Taifa, kuna uzembe wa hali ya juu.

Kwenye usalama huwa tunasema, 'All accidents are avoidable except natural disasters and terrorism.

Baada ya maombolezo, nitafafanua uzembe uliofanyika na uwezekano wa ajali zinazosubiriwa.
Tupo standby tunasubiri uchambuzi wako.
ova
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom