UKandamizaji Demokrasia Nchini: WITO wa Kususia na kuinyima ushrikianPOLICE/POLISI

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,277
8,492
Ukisikia tukio la ujambazi POLICE na FFU watafika kwenye tukio baada ya waharifu kuwa wameondoka. Ukisikia mkutano wa Chama Cha Upinzani na hasa CHADEMA POLICE na FFU watafika sehemu ya mkutano masaa mawili kabla ya kuanza mkutano.

Sasa hii inatupatia picha gani, POLICE na FFU ni kwaajili ya kukandamiza demokrasia na kulinda maslahi ya kundi la watu wachache katika jamii - CCM na mafisadi? Ikiwa ndio hivyo POLICE na FFU hawawatendei haki waTZ.

Na kama ndio hali iko hivi Watanzania hawawezi tena kuwa na imani na Jeshi la POLICE kwa ujumla. Na kwa kuwa hawawezi kuwa na imani na Jeshi la POLICE natoa WITO KWA WATANZANIA KUWASUSA, KUWASUSIA NA KUTOWAPA USHIRIKIANO NA KUWAZOMEA POLICE MAHALI POPOTE WALIPO.

Wito
 
naunga mkono hoja pia ila ila tuweke mikakati wenyewe ya kupambana na waarifu maana tunawajua
 
Mie nimeshaacha kuwaunga mkono hao polisi siku nyingi na kauli yao ya kujifanya ulinzi shirikishi kumbe ulinzi haribifu na kandamizaji.yaani wananiudhi sana na uonevu wanaofanya kwa wananchi .siku hizi wamekuwa kama mgambo hawana lolote la maana
 
Huwa nashangaa sana kusikia madai ya POLICE kuwa wamepata taarifa za uvunjifu wa amani kwenye hiyo mikutano. Uvunjifu wa amani utoke wapi wakati ninyi mpo pale kuilinda amani isivunjike. Au basi muwe mnatuambia nyie ndo mmepanga kuleta huo uvunjifu wa amani.

Ina maana taarifa mzopokea ni za Mikutano ya siasa pekee sio za ujambazi. Sasa hivi kila kitu ni Siasa, JWTZ, JKT, FFU, TRAFFIC POLICE, MAGEREZA, UWT/TISS, IKULU, FAMILIA. wapi na wapi.

Dawa yenu kuwasusia.
 
Back
Top Bottom