Ukanda mmoja, njia moja na maonyesho ya uagizaji ya China ni mtazamo wa pande nyingi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,025
Na Ronald Mutie

VCG111356550135.jpg


Safari ya masaa 14 kutoka mji wa Hamburg nchini Ujerumani hadi mji mkubwa wa kibiashara wa China Shanghai ndio mfano hai wa mafanikio ya miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Tangu mwaka 2013 Rais Xi Jinping alipopendekeza wazo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, miradi ya uunganishaji kama vile reli, barabara, bandari na viwanja vya ndege imefungua zaidi dunia na kurahisisha biashara na kukuza uchumi.

Wiki moja kabla ya Maonesho ya nne ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China (CIIE) kuanza, treni ya mizigo ya China iliwasili Shanghai kutoka Hamburg, Ujerumani, ikikamilisha safari yake ya kwanza kwenye njia hiyo mpya.

Treni hiyo ilikuwa imebeba bidhaa za kuonesha kwenye maonyesho hayo.

Mtazamo wa China ni kuwa huwezi kukuza uchumi bila miundo mbinu, na kwamba China haiwezi kupata maendeleo peke yake bila kushirikisha nchi nyingine.

Ukanda Mmoja, Njia Moja na Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji yanayoandaliwa na China ni mtazamo wa kuhimiza maendeleo ya pande nyingi na dunia yenye hatima ya pamoja.

Ukweli ni kwamba nchi nyingi za Afrika na hata ulaya zingependa kupata mgao wa soko kubwa la China, lakini bila miundo mbinu na mipango ya kuwezesha biashara haziwezi kufikisha bidhaa kwenye soko hilo.

Hivyo China kwanza imezingatia kujenga miundo mbinu ya uchukuzi na baadaye kufungua jukwaa kwa nchi zote duniani kujinufaisha na soko lake.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kampuni ya uendeshaji ya treni hiyo mjini Shanghai Wang Jinqiu, kutumia treni badala ya njia ya kawaida ya baharini ilipunguza muda wa usafiri kwa nusu.

Ikiwa na zaidi ya njia 70, huduma ya treni ya mizigo imetoa usaidizi wa usafiri kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi na maeneo kando ya Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Reli mpya inayounganisha Hamburg na Shanghai sio tu inarahisisha uchukuzi lakini pia inaangazia ushawishi unaokua kwenye maonesho ya kimataifa uangizaji.

Miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja imekua na kuwa jukwaa kubwa zaidi la ushirikiano wa kimataifa duniani.

Takwimu zinaonyesha kuwa biashara ya China inayohusiana na bidhaa kwenye nchi zilizo na miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ilifikia dola za kimarekani trilioni 9.2 kati ya 2013 na 2020.

Yakiwa ni maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji na ambayo ni ya ngazi ya kitaifa, CIIE pia imekua na kuwa na manufaa kimataifa kwa kukuza biashara.

Miongoni mwa takriban makampuni 3,000 yaliyohudhuria maonesho ya mwaka huu, zaidi ya makampuni 600 yanatoka nchi 50 kwenye Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Rwanda nchini China Abikunda Samuel, anasema kuwa ushiriki wa awali katika maonyesho hayo ya CIIE umesaidia watumiaji wa China kujifunza zaidi kuhusu bidhaa maarufu za Rwanda, kama vile mafuta ya pilipili na kahawa, ambayo alisema ni "kahawa bora zaidi duniani.

Baadhi ya chapa za Rwanda zimepata mwelekeo wa biashara ya mtandaoni wa China kwa ushirikiano na waandaji maarufu wa mauzo ya moja kwa moja mtandaoni.

Anasema Uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara ulioanzishwa kati ya China na Rwanda kupitia maonyesho hayo umetoa fursa nyingi za ajira kwa wakulima wa Rwanda, na hivyo kunufaisha uchumi wa nchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom