Ukame wa Madagascar: Watu wanakula 'mchanga uliochanganywa na ukwaju'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,865
Raia wa kusini mwa Madagascar wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju kwasababu ya kiangazi ambacho kimeharibu zao linalotegemewa na wenyeji, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

"Tunauita udongo wenye kuhimili kiangazi kwasababu unaruhusu ukwaju kukua na kutusaidia kukabiliana na kiangazi," AFP imemnukuu mkulima wa eneo Doday Fandilava Noelisona.

"Siku hizi hatutafuti tena chakula bali tunatafuta mbinu za kupata kitu chochote cha kushikilia tumbo."

Matunda ya dungusi ambayo watu huyategemea yamekauka kwasababu ya ukosefu wa mvua.

Aidha, shirika la AFP limemnukuu mkulima mwingine, Avianay Idamy, ambaye anasema amegeukia uuzaji wa makaa kupata pesa za kukidhi mahitaji ya familia yake angalau waweze kula muhogo mara moja tu kwa siku.

Shirika la chakula dunia- WFP, linasema watu milioni 1.5 kusini mwa Madagascar wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.
 

Attachments

  • 1607071185734.gif
    1607071185734.gif
    42 bytes · Views: 1
Fursa kwetu Tz tuwauzie mchele, Mahindi na nafaka zingine.
Hii itaboresha bei ya mchele nchini kuwa juu hivyo kuwapa faida wakulima na wafanyabiashara walioweka Stoku mazao
 
Shimaoli si ndo lugha yao wale watu? Waswahili tukienda awatuteti.
 
Tanzania tuwasaidie hawa ndugu zetu.. wao walitukumbuka kipindi cha Covid.. ni wakati wetu kulipa fadhira..👊
 
Fursa kwetu Tz tuwauzie mchele, Mahindi na nafaka zingine.
Hii itaboresha bei ya mchele nchini kuwa juu hivyo kuwapa faida wakulima na wafanyabiashara walioweka Stoku mazao
Hizo pesa zenyewe za kununua wanazo ,!?
 
Back
Top Bottom