Ukahaba Wetu Unatuponza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukahaba Wetu Unatuponza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 29, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ukahaba Wetu Unatuponza

  Tafsiri ya Sanifu ya Kahaba, ni mtu ambaye anajiuza mwili ili ajipatie kipato. Ni mtu ambaye amekubuhu katika fani ya Umalaya na aliyekata shauri kuwa kamwe yeye hata fanya lolote lile bali kujiuza.


  Kuna msemo wa Kiswahili unaosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.

  Ukahaba wetu unaotuponza ni ule wa kujitembeza tukijiuza na kulazimisha kila tunayemhisi kuwa ana pesa au anaweza kutupa pesa, basi sisi humkimbilia na kwa ulegevu mkubwa tunajisalimisha kwake, alimradi katuahidi pesa.

  Hatujali wala kupima kama mtu huyu kweli anatujali, ana hata hisia na kuvutiwa nasi na kama dhamira yake ni kuwa na mapenzi ya kweli na sisi. Sisi tunachojali ni zile pesa atakazotupa, ambazo zitatusaidia kununua kitumbua na chai ya rangi, siku inayofuata na kusubiri mtu mwingine atupe pesa kwa ajili ya chakula na malazi kwa siku nyingine.

  Jinsi mwili wetu ulivyoumbwa na Mungu, hatuuthamini wala kuupa thamani ya maana ambayo yaweza kutufanya tuwe kile Kizuri kinahojiuza na kujipatia si pesa ya hai tuu, bali ni mtaji mkubwa wa hata kuwalisha vitukuu na vilembwe.

  Ni Ukahaba huu wa kukimbilia kujitembeza na kukubali kulaghaiwa na kila mtu hata wale wasio na pesa, ndio unaokomaza umasikini wetu.

  Tanzania ni nchi tajiri sana. Tuna Rasilimali za kila aina, bwelele, tele, topu, kedekede, lakini badala ya kuzitunza vizuri na kuzitumia vizuri, sisi tumeamua kwa nguvu moja na kwa kauli moja kuwaachia mabwana wapitao wanaotuahidi hela, nasi tunawagawia hazina na rasilimali yetu kwa dezo, sawa na mtu kahaba asiyethamini mwili, nguvu na akili zake alizopewa na Mwenyezi Mungu.

  Inashangaza sana, kwa nchi yetu ambayo mwaka 1967, tulitaifisha kila kitu kutoka mikono ya wageni na kuvifanya mali zetu ili sisi wenyewe tufaidi matunda ya maliasili na rasilimali tulizoneemeshwa na Mungu, leo hii tumegeuka nyuma abautani na kuanza kukimbilia kila anayepita tukiomba aje alime, apalilie na kuvuna kwenye shamba letu na sisi tunachoomba ni kakipande cha muhogo na kopo la mbaazi kujisitiri!

  Ni lini tuliingia uvivu na ujuvi wa namna hii, kwamba kila kitu kinatushinda tena kwa hiari na kwa kushindwa kuwa na tija na motisha kufanya kazi na kujitosheleza?

  Je tutawalaumu Wakoloni kama vile Wakorea walivyodai kuwa waliondoka bila kutufundisha jinsi ya kusindika matunda?

  Tumekuwa huru kwa miaka karibu 50 sasa, na kila kazi inatushinda ila tunayoiweza ni kuombaomba na kutumia mpaka tuishiwe!

  Sasa Ukahaba wetu umetufanya tuwe manyang'au, tukikimbilia kuuza kila kitu, kunyang'anyana tonge mdomoni, kuzidiana ujanjaujanja wa nani auze handaki haraka na apate kamisheni yake ya haraka ili aweze kutanua na kurubuni kura za kumfanya awe mtawala wa maisha!

  Hebu tafakari unaposikia kauli kutoka kwa viongozi wan chi wakidai kuwa ni lazima tuweke mazingira mazuri ili wawekezaji waje, halafu linganisha na kauli za wawekezaji ambao wanajiingiza kwa ahadi nyingi, ilhali hata mtaji hawana, ila wanategemea kutuzidi maarifa na ujanja na kutumia mali zetu wenyewe kuwa mtaji wa walichoahidi kuja kuzalisha.

  Hivi karibuni kumekuwa na msukumo mkubwa unaodai kuwa Tanzania ina sera mpya ya "Kilimo Kwanza" ikiwa ni namna eti ya kufufua shughuli za kilimo ambacho tulishadai siku nyingi kuwa ndio uti wa mgongo wa Uzalishaji mali wetu.

  Lakini, ukikaa chini na kutafakari kauli mbiu hii, utabaini kuwa mlengwa na mnufaika wa Kilimo Kwanza si Yule mkulima wa Kisiju au Kingolwira, hata Yule wa Chake Chake na Busanda!

  Mlengwa wa kauli mbiu hii ni Yule Yule Bwana mtanashati, anayetembea akijidai ana pesa za kuja kuwekeza ndani ya nchi yetu.

  Tunadanganyana kuwa eti Mwekezaji atakuja kutufundisha mbinu bora za kilimo na kuinua ubora wa shughuli za kilimo, lakini jiulizeni, Chuo Kikuu cha Kilimo ha Sokoine kinafanya nini? Je vile vyuo vingine vya kilimo vya Uyole, Ukiliguru, Tengeru na kazwalika, vimeshindwa nini kumfundisha Mkulima wa Tanzania ukulima wa kisasa?

  Ikiwa taasisi kama Magereza na SUMA-JKT ambazo kwa miaka mingi zimekuwa na ufanisi mkubwa katika uzalishaji hasa kilimo na kasoro yao kubwa si ukosefu wa Wafanyakazi au Wataalamu bali ni uongozi mbovu, leo hii zinadai eti zinatafuta wawekezaji ili wakodishe ardhi na kuzalisha Chakula, je hamuoni kuwa kuna kasoro kubwa?

  Ni mdudu gani huyu aliyewaingilia viongozi wa Tanzania kwa kila ngazi kuwa kila mmoja keshajisalimisha na kuanza kukimbilia kudai Uwekezaji ndio suluhisho?

  Mbona wawekezaji wa ndani tunao na wataalamu tunao wengi sana lakini iweje tuwanyime ardhi Watanzania wenzetu na tuende kukodisha kwa Saudi Arabia, Korea, India na China?

  Kama lengo ni kusisimua kilimo ha kisasa, je ile program ya mpunga Rufiji iliyofanywa na Wa-Irani wa Uajemi miaka zaidi ya 15 iliyopita haikuzaa matunda?

  Je ule mradi wa Mahindi ya Sasakawa na hata wa Konoike kule Kilimanjaro havikutufundisha ustadi wa kuzalisha mahindi na mpunga wa kutosha?

  Sasa kama tulifundishwa miaka 16-20 iliyopita kulima kwa kisasa na kina Sasakawa, halafu leo tunadai lazima tutafute wawekezaji wan je watufundishe kilimo bora na cha mashine, je tulirudi nyuma na kujiuliza ni kwa nini mradi wa Sasakawa haukuwa na mafanikio?

  Ardhi, ni kitu muhimu sana na mgongano wa ardhi, siku zote ndio umekuwa chimbuko la vita zote duniani. Ndani ya ardhi, iwe ina rutuba au la, kuna hazina kubwa sana ya kutosha. Kuna madini, gesi, mafuta, malisho, maji, na kila unachoweza kufikiri. Mwanadamu mwenyewe aliumbwa kwa udongo ambao ni ardhi!

  Sasa kama hatujajifunza kwa wenzetu, wanavyopigania ardhi kila siku na sisi tunaigawa hovyohovyo kisa mpango wa maendeleo ya Mwekezaji na si Mwananchi wa Tanzania, basi iko siku kitone kimoja ha damu kama kile kilichomwagika kule Buzwagi, Bulyanhulu, Loliondo na Grumeti, kitageuka kuwa mto wa damu, tukichinjana kugombania ardhi.

  Ubaya zaidi ni jinsi Serikali yetu ilivyoamua kushupalia mambo na kukimbilia kulinda maslahi ya mwekezaji na si ya Watanzania Sawa na Kahaba anayempa kipaumbele mtu anayemhonga na kutokujali watoto wake.

  Sasa kama tumeshindwa kuzalisha mali na tunahoweza zaidi ya kuombaomba misaada ni kukimbilia Uwekezaji uchwara uliotuletea TRL,TICTS, ATCL, IPTL, Richmond, Buzwagi na hata kupanua mianya ya uhujumu na ufisadi kama EPA, Meremeta na Rada, kwa nini basi tusiamue kutafuta mwekezaji atakaye kuwa nyapara kwetu sote kuanzia Ikulu na sisi tumtumikie?

  Kuna maana gani kudai tuna Uhuru na tunajitawala ikiwa hatuna hata chembe moja ya kuamsha Uzalishaji?

  Ikiwa Mkorea kafikia hatua ya kutukebehi kuwa hatukufundishwa kusindika matunda na Mkoloni, je tuaminije kuwa huyu anakuja kwa nia nzuri?

  Inasikitisha na inahuzunisha kuwa tumekosa mbinu za kujizatiti na kuzalisha na tunakimbilia kudai tunahitaji wawekezaji. Kama Mzungu, Mwarabu, Mchina, Mhindi na hata Mwafrika mwingine ambaye si Mtanzania anaweza kuja Tanzania na kuzalisha marudufu na kila mmoja wetu akaitika wito na kufanya kazi kwa bidii hini ya mgeni huyu, kwa nini basi tusirudishe Mkoloni ili tuweze kulijenga Taifa letu tukilambwa bakora na mijeledi?

  Ikiwa kwa hiari yetu, tu wavivu na hatutaki kufanya kazi na kwa ufanisi, si heri basi aje nyapara au turudi Utumwani tujue moja kama Wana-Israeli walivyoyakumbuka masufuria ya Pharao walipoondoka utumwani Misri?

  Leo tunakimbilia kuanzisha makongamano, warsha, semina na kila namna ya kijimkutano na si kwamba tunania ya kujifunza na kufanyia kazi tunachokizungumza, bali tunakwenda kupata alaunsi tujenge nyumba ya pili na ya tatu.

  Tumebakia kuwa watu wa mikutano na misafara kutwa kuchwa, tukijilipa mifedha ya ziada ili kutimiza sehemu ya wajibu wetu. Kisha tukishamaliza mikutano hiyo, tunakimbilia kutafuta mwekezaji.

  Mwisho wa haya ni mwili wetu kuchoka na kukosa thamani kutokana na kutumiwa na kila mtu, maana hata pesa tutakuwa hatupokei tena bali tutakuwa tukijiuza bure, tukiwa tumekubuhu na kuchujika!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkuu Reverend,
  Kwa mara nyingine tena ubarikiwe. Umenena!
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ubarikiwe na Bwana, Maana umeongezea kuwa hakuna haja ya kujifunza uchinam Korea na sehemu nyingine, Vyuo vyote walifunga na maabara zote nazo walifunga, Niliwahi kupost post moja hapa ya kumuliza Pinda juu ya umuhimu wa kwenda kujifunza Korea Kilimo?? Sasa baada ya mwalimu Nyerere yote yalikwisha kabisa, Sokoine kuna wataalamu Kibao katika Taifa letu, Sasa kila kitu tunazima nje?? Tazama Mzinga?? Tazama kule Kibaha nako?? Tunaweza kufanya mengi bali akili na mawazo yetu yamepelekewa kuomba pesa. Inahuzunisha mkuu wangu
   
 4. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  RRRK,

  Umenena yote ya msingi. Hakuna la kuongeza ila naamini ipo siku hawa tutawauliza haya maswali mengi na then tutawashikisha adabu !
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev Kishoka,

  Mkuu hali halisi ya Tanzania yetu ipo Kariakoo.. leo hii tunajiuza vibaya vibaya watu wakiuza viwanja vyao au niseme nyumba zao kwa Wachina wakapewa kipande cha juu (top Floor) ktk nyumba ambazo hazina elevator (lift), kazi kwa mwenye nyumba kupanda ngazi ghorofa 10 kila siku sio kitu maadam fedha sii ya madafu tena.. mikataba hiyo haina mwisho wengine miaka 20..Wengine wameuza nyumba na kuuhama mji kwa furaha ya kuwa na dollar mkononi..TZ shilingi haina thamani wala haitamaniki kabisa leo hii...

  Ukienda mijini watu wote wamejipanga nyuma ya matajiri, ni umalaya ule ule.. wabunge, madiwani, wenyeviti wa chama na kadhalika wote hawa ni watu ambao wanamshiko na wafuasi kibao (malaya) nyuma yao.

  Hivyo kumbuka maneno ya FMES kwamba viongozi wetu ni reflection yetu sisi. Kwa maana nyingine sisi wote Wadanganyika tunauza miili yetu - ni MALAYA!
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara kwa jinsi hii basi ukiona kuwa Serikali dhaifu basi na vyama upinzani ni dhaifu, Huwezi kuwa na vyama dhaifu na serikali imara
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Hiii nchi imejaa makahaba wa kisiasa.......
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mkuu ubarikiwe sana sana
   
 9. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duuh hii ya wachina kununua maeneo imenishtua! Tunahitaji kuangalia upya/kurekebisha sheria za umiliki/ukodishwaji ardhi venginevyo kizazi kijacho kitatusuta kwa kuiuza nchi na kuwaachia sefuri.
   
 10. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkuu hii imetulia----lazima tubadilike  Rom
   
 11. G

  Gongagonga Member

  #11
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rev hilo neno kali mno hakuna m-badala wake?
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu amini usiamini in the next 10 years Kariakoo itakuwa Chinatown!
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Rev. Kishoka:

  Mkuu kama unazungumza kutokea Tanzania na ukiwa unaishi Tanzania, nitakupa sikio.

  Lakini kama unazungumzia kutokea nje, labda wageni wanakuja kujaza mapengo ya wewe, Za10, Mkandara, NN mliyoacha kwa kuhamia nje.
   
 14. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ule weimbo wa samaki unatufaa hii nchi. Poleee samaki pole, wanavyokufanya, polee samaki polee wanavyokula jicho. Yani tANZANIA NI KAMA SAMAKI ANALIWA JICHO MKIA ANAGEUZWA NA ANAVUMILIA.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Maneno haya ni mazito na hayataki papara ili kuyajibu. Yanataka kila mtu atafakari na kuona ameegemea wapi. Tukumbuke mustakabali wa nchi yetu hauko kwa watu wachache wanaotuongoza, maana kila siku iendayo kwa mungu wanapoteza credibility ya kuwa viongozi. Wanafanana na ombaomba ninaowaona wamezagaa kila barabara ya mjini Dar, ingawa wao wanaombea kwa watu wa nje.
  Mustakabali wa nchi yetu ni lazima uwe mikononi mwetu sote kwa ujumla wetu.
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mbaya zaidi tunafanya ukahaba tukiwa tumelewa( pesa au whatever) na hatutumii kinga ( kujiuliza whats the catch). Tutapona kweli ningesema Reverend utuombee kwa mungu.

  Sidhani kama hii itasaidia kwani wajinga wanaokaa na kuomba bila kujilinda hawasaidiki. Ni sawa na kuonana na simba mikumi badala ya kukimbia unapiga magoti na kuomba bila kujua kuwa na simba naye anaomba mungu apate chakula!!!!!!!!
   
 17. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Reverend,

  Kama kawaida yako umegonga fact! Swali lilillokuja haraka haraka kichwani ni kama tumekwishafika hapo je tunafanya nini ama tufanye nini kujikwamua na kuikwamua nchi yetu kutokana na haya yote? Tumepe nani ama chama gani kitakachoweza kuwa na viongozi wenye 'maono' kama ya Mchungaji Kishoka ili tuweze kuinusuru nchi yetu?

  If wishes were horses ........ Ningefurahi sana kama wafuatao wangeliweza kuongoza nchi yetu:

  Reverend Kishoka, Mkandara, Jasusi, Joja Kuu, Mzee Mwanakijiji, Bubu Ataka Kusema, FEMS, Companero, Dr. Slaaa, Mbowe, Sitta, Mwakyembe, Mpendazoe, Selelii, Engineer Stella, na wengine walio na msimamo thabiti wa kuelewa kinachokwenda kombo na kutaka yawepo mabadiliko. Serikali ambayo ingeliweza kuundwa na wazalendo niliowataja kwa dhati kabisa ingeweza kuleta mabadiliko ya dhati kabisa nchini mwetu. How do we unite these names?
   
 18. i

  ituganhila Member

  #18
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Re: Ukahaba Wetu Unatuponza!
  Tumedumazwa na fikira za senti kidogo.Ten asilimia imewafanya watanzania kuwa mbumbu wa kufikiri.Wengi hatuna akili kama tunazo hao walio madarakani hawana.Tumewapa nchi wawe wawakilishi wetu katika kushika madaraka.Hao ndo wanaouza nchi.Huwezi kumpa mtu madini kisha ukamwita ni mwekezaji wakati mwananchi hanufaiki kwa lolote.Tumekuwa watu wa dhiki sana kwa sababu tumetaka wenyewe.Watuwasio na uwezo wakufikiri kwa kina ni sawa na makahaba.Nchi imejaa watu wasio ithamini miili yao.Ikiwa hayo machache yanayo ibuliwa ya ubadhirifu wa fedha za nchi na watu wanpeta tu inamaana gani kuwa na utawala usioangalia maslahi ya nchi? Ni nchi yetu inaitwa maskini fukara la kutupwa.Alafu huyo anaeiita hivyo ndo anakuja kuvuna na kuwa tajiri wa kupindukia maana yake nini?Ujinga au nini ukahaba au nini hii au laana!Unasoma unamaliza elimu ya juu unakabidhiwa madaka makubwa ya kusimamia mali ya watu wasiojua kusoma wasio na jeshi na waliosoma pia.Bila aibu una uza nchi! Ajabu sana. Tusipofumbuka tutakwisha.Ni nchi iliyo na maji ya kutosha Tanganyika,Nyanza,Nyasa lakini eti tunalia njaa na kupewa chakula kilichooza au kulia njaa kwa wengine watusaidie.Huu si uvivu wa kufikikri kweli!Watu wasio na machungu wanatoa ardhi kupanda sumu iliyopewa jina zuri la jatropha kumbe ni mibono yenye sumu kali eti kwa madai ardhi siyo nzuri! Ni kwa wenye uwezo mdogo wa kufikiri utamwita mtu umpe sehemu ya thamani ya mali yako na kukufanya mtumwa wake.HATUNA AKILI, HATUTHAMINI CHETU.Mwalimu JK (BABA WA TAIFA alipolinda maslahi ya Nchi alionekana hana akili maana kila kukicha wanatangaziwa watu waje waibe kwa njia uwekezaji.Sisi tunawekeza wapi
  Ukiwa huna uwezo wa kufikir hata upelekwe harvad university bado utakuwa huna akili.Akili siyo ujanja wa kufaulu mitihani pale UD au chuo chochote.Ni uwezo wa kupambanua mambo kwa kina kulinda maslahi ya nchi kwa moyo wote na kuitukana rushwa, Tunagawa mali zetu je kizazi chenye akili kikija kitatufanya nini sisi?Maana hata mifupa yetu italaaniwa kwakuwa hatuna uwezo wa kufikiri. Kama unampa mtu almasi ,Tanzanite,Dhahabu,Uraniua, na mengine mengi kwa kupata kiduchu kweli unaakili.HAKUNA.
  Kweli watu wanajaa maofisini kwamba wanafanya kazi alafu wanaamua kipumpavu ni hatari kwa nchi. UKIONA MZUNGU ANAKUPIGIA MAKOFI KWA FURAHA UJUE NI KEJERI ANAKUIBIA HUYO. UKIONA KILA SIKU UNASAIDIWA BASI WEWE NI ZEZETA HUWEZI KUFIKIRI. UKIMBEBA MTOTO ANAYE TAKAKUTAMBAA KWA KUJIFANYA UNAMUONEA HURUMA.KAMWE HATAWEZA KUTEMBEA HUYO. NCHI IKIOMBA MISAADA KILA SIKU NA WAKAKUPA UJUIJUE UNAKASORO>KWAMBA HUWEZI KUFIKIRI.

  MASHI
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Mch mabwana zetu wanatujua kuwa sisi ni makahaba wa raslimali zetu wanachohitaji kufanya ni kusogeza magari yao yenye dola karibu na miguu yetu. Wenyewe hata hivyo tunajiona ni ma escort aka makahaba wa hali ya juu.
   
 20. m

  muvimba Member

  #20
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  hayo maneno ni mazito sana, tukushukuru sana mwana JF katika hili, kwa ujumla linatia uchungu sana, kuna haja ya watanzania pia kubadilika. inatisha kusikia wachina wanachukua ardhi sijui ni kilimo gani kitafanyika pasipo kuwa na ardhi.
   
Loading...