Ukaguzi wa vyeti kufika private(taasisi binafsi)?

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,601
4,086
Wakuu,

Hebu tuondoane presha kidogo.

Hivi hili zoezi ambalo huyu shangazi yangu huyu kalivalia njuga hili la ukaguzi wa vyeti hili litafika na kwenye taasisi binafsi au litaishia hukohuko serikalini? Maana'ke ni muhimu sana wadau kupata data mapema ili kujiandaa kisaikolojia.

Tusaidiane kwa wenye taarifa japo za chini ya kapeti.

Natanguliza shukrani wakuu.
 
Lolote laweza kutokea LAKINI uzuri wa private wanaangalia PERFOMANCE ya mtu kuanzia kwenye Interview mpaka kazi kuliko Division 1 ya kwenye ma vyeti.
 
Ndiyo maana shughuli zao zinazofanana na za umma kama shule ziko juu.Wao ni kazi tu.Ukishindwa kazi huenda wakataka cheti.Production kwanza.
 
Ndiyo maana shughuli zao zinazofanana na za umma kama shule ziko juu.Wao ni kazi tu.Ukishindwa kazi huenda wakataka cheti.Production kwanza.
 
Maisha huku hawawezi Kuja waishie huko huko serikalini sisi hatuna vyeti feki tafadhali sana msije huku
 
Mura unakuja na vyeti fake kazini,utakimbia kazi,wenzio wanakuja na vyeti original muraa!
 
Mkuu na ww unavyofeki; si usepe mapema maana kasema watakagua kwa watu wote.

Jiongeze
 
Tanzania tunaamini makaratasi kuliko performance coz ata hao wenye vyeti original ni fake kichwani mm naamini katika utendaji kazi kwani kuna tofauti ndogo sana wale wenye vyeti fake na original makazini ni ndogo sana tena wale wenye vyeti fake ndo wanajua kazi vzr kuliko wale wengine ntakuwa mjinga eti kumtoa mtu ambae anafanya kazi yake kwa weledi mzr na ufahamu wa kazi yake eti cheti fake coz kinachofanya kazi c vyeti ni mtu
 
Nadhani mnataka kwenda kinyume na haki za binadamu. Haiwezekani mimi sijasoma shule yoyote lakini nimeanzisha kampuni yangu halafu mnitumbue
 
Nadhani mnataka kwenda kinyume na haki za binadamu. Haiwezekani mimi sijasoma shule yoyote lakini nimeanzisha kampuni yangu halafu mnitumbue
kuwa na kampuni ni suala moja na kuwa mtaalamu wa / katika kampuni ni suala jingine.Usihofu mkuu.ni sawa na unamiliki shamba halafu hata jembe hujui kushika na trekta hujui kuendesha lakini shamba linalimwa,kupandwa na kuvunwa kitaalam na wengine
 
Serikalini hakuna vibarua... wote ni waajiriwa kwa taratibu na mikataba kutokana na sheria/kanuni zilizowekwa na mamlaka, taasisi husika zikisimamiwa na serikali kuu. Kwa hiyo serikali inayokulipa mshahara ina haki ya kukukagua kwa lolote na chochote hadi ikajiridhisha. Ndiyo maana ajira nyingi kama siyo zote za serikali zinapitia Utumishi.

Mfano:
Ndiyo maana hata dereva anatakiwa kuwasilisha siyo tu leseni bali na vyeti vya aliposomea udereva kwenye chuo kinachotambulika ikiambata na cheti cha kumaliza darasa la kidato cha nne.

Tofauti na seka binafsi. Dereva anaweza kuajirwa na leseni yake tu, bila cheti chochote kingine na bila kuwa na mkataba wowote. Leseni yako, wadhamini wanaotambulika na barua ya serikali ya mtaa unayoishi..

Ukiomba kazi ya kujiriwa kufagia ofisi serikalini, vyeti ni lazima... ukiomba sekta binafsi, uzoefu wako na ufanisi ni muhumi. Unaweza hata ukawa hujui kusoma au kuandika.


Sekta binafsi siyo tu watu kuwa na vyeti feki.. wengine hawana vyeti kabisa.
 
Back
Top Bottom