Ukaguzi wa vyakula na vipodozi sasa kufanywa na TBS badala ya TFDA, muswada wa sheria wawasilishwa bungeni

Wewe Utakuwa mwanasheria wa TFDA, na unatetea ujira wako hapo.

Kwanza kabisa, TFDA kiutendaji kwenye chakula wanatekeleza karibia 90% ya kile TBS wanafanya.

Ukisema TFDA aangalie ubora na usalama na TBS aangalie kama bidhaa imekidhi viwango huko ni kudanganya watu.

Hakuna usalama na ubora bila Standards/viwango.

Ili bidhaa iwe salama na bora tunaangalia microbs contents, viwango vya madini hatar, na additives zingine.

Sasa TFDA walikuwa wanakagua hizo mambo kujihakikishia kama zimekidhi viwango vinavyokubalika, na bidhaa hiyohiyo itaenda TBS na kukagua kama imekidhi viwango vyao...

TFDA anakagua premises ya chakula na kusajili, TBS nae anakagua jengo vilevile...

Usifananishe TGDA ya Tz na FDA ya Marekani. FDA ya marekani ana dili na bidhaa za chakula pia sio zote, kama nyama, mayai, kuku FDA haihusiki nayo bali ni wizara ya kilimo na mifugo. Isipokuwa Maziwa ndio FDA anaregulate.

Pia FDA ya marekani wao wana andaa standards na kuzisimamia, yofauti na nyie mnao chukua standards TBS na kuzisimamia.

Nimefanya field TFDA na TBS nikiwa chuo, nakiri kabisa wote mnatekeleza majukumu sawa. Kuna kiwanda kimoja bidhaa zake zilipita vizuri kwenye maabara ya TFDA lakini zikagoma kwenye maabara ya TBS.

Ukiangalia katika EAC, nchi zote hazina mamlaka kama TFDA, wao wana mamlaka kama TBS

Kiufupi, mimi nilikuwa na Options mbili katika hili,
1. Kuhamisha mandates za TBS hasa kwenye chakula na kupeleka TFDA. TFDA waandae standards (najua asilimia kubwa huwa tunakopi na kupaste toka kwa wenzetu). TBS ingedili na bidhaa ambazo si chakula.

2. Kuiondole TFDA kusimamia chakula na kuiachia TBS.

Kweli option namba mbili ndio imetekelezwa.

TFDA mligeuka TRA, maofisa wenu wakifanya ukaguzi sio katika kuboresha bali mlikuwa mpo kwenye kuonesha uwezo wenu wa kufunga biashara za watu. Mkija mnakuja mmevimba na makoti kama madaktari.

RIP TFDA,
Mkuu safi sana, hawa TFDA walishakuwa washenzi sana, walianza kukamata baiskeli za mandazi kukusanya Panadol madukani na kula mikate inayoletwa kama sampuli, ulishaona wapi unaambiwa ulete sampuli ya mkate kila siku kwa mwezi mzima, wanapima nini hapo? kama sio kujipatia vitafunio vya bure.
 
Mkuu safi sana, hawa TFDA walishakuwa washenzi sana, walianza kukamata baiskeli za mandazi kukusanya Panadol madukani na kula mikate inayoletwa kama sampuli, ulishaona wapi unaambiwa ulete sampuli ya mkate kila siku kwa mwezi mzima, wanapima nini hapo? kama sio kujipatia vitafunio vya bure.
hahahahahaha, serikali ina ina mikono mirefu sana, imefanya utafiti na uchunguzi na kuja na majibu sahihi
 
Back
Top Bottom