Ukaguzi wa simu unaofanywa na shivacom utakapo huduma ya mpesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukaguzi wa simu unaofanywa na shivacom utakapo huduma ya mpesa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mnozya, Sep 6, 2011.

1. m

mnozya JF-Expert Member

#1
Sep 6, 2011
Joined: Feb 25, 2009
Messages: 207
Likes Received: 20
Trophy Points: 35
Wakuu habari za majukumu?

Leo nimekutana na kali ya mwaka katika duka la Shivacom lilopo Samora Avenue karibu na makutano ya Morogoro road na Samora avenue, wanaopafahamu ni karibu na JJ Restaurant.

Nilikwenda kudeposit hela kwenye MPESA yangu, dada wa kihindi akaniambia lete hiyo handset yako. Nikamuuliza ya nini? Akasema nataka niiangalie kama ya kwako NIKAMWAMBIA hufahamu kuwa hupaswi kukagua simu yangu? Nikamuuliza huoni kuwa unaingilia privacy zangu? Nikamwambia Ok nawasiliana na Vodafone kujua hiyo policy yao kwa undani AKASEMA ni si policy ya vodafone bali ya Shivacom.

Baada ya kumkatalia akaniambia nenda sehemu nyingine.

Nimeandika haya kwa kifupi ili jamii ijue public ijue kuwa ina haki kwa mujibu wa sheria kutoingiliwa haki ya kuwa na usiri kwa mambo binafsi

Aidha nawaomba waandishi wa habari walifanyie utafiti hili ili isaidie kulinda haki na utu wa mteja. Iliniuma maana nilijiuliza watanzania wenzangu wasiojua haki zao za kisheria si wanadhalilishwa na hao wahindi?

Atakayehitaji ushirikiano wangu naomba ani PM

2. Likwanda

Likwanda JF-Expert Member

#2
Sep 6, 2011
Joined: Jun 16, 2011
Messages: 3,854
Likes Received: 45
Trophy Points: 145
Hii mpya, ngoja tuone wanajua watasemaje.

3. Chimunguru

Chimunguru JF-Expert Member

#3
Sep 6, 2011
Joined: May 3, 2009
Messages: 9,843
Likes Received: 270
Trophy Points: 180
What i know ni kwamba kuna kitu kinaitwa direct deposit yaani wewe uliyeingia kwenye duka la shivacom unataka kumtumia nduguyo pesa huruhusiwi kutoa namba ya nduguyo akatumiwa pesa moja kwa moja na wakala. Unachopaswa kufanya ni ku deposit kwenye simu yako wewe uliyefika pale kwa wakala halafu umtumie huyo ndugu yako.

Ukaguzi si kuangalia nini kilichopo ktk simu, yako unapotuma pesa na kutoa pesa meseji itaingia kwenye simu yako wakala anachofanya kujiridhisha ni kukuomba simu yako ili aone kweli ile sms imeingia kwako?

Kama ulitoa namba ya mtu wa tatu yule wakala ata reverse ile pesa yote irudi kwako na kukushauri u deposit kwako kwanza. ukienda kwa wakala akakubali direct deposit voda wakigundua till inafungiwa. Fraud ni nyingi sana zinazotokana na direct deposit mteja anaweza piga simu voda akasema kaibiwa na wakala.

Kwenye kutoa pesa kuna wizi mkubwa unendelea. so hizo ni mbinu za kujiridhisha kwamba mteja ni yeye aliyepo mbele yako na si mtu nwingine wa tatu, hiki ni kidogo ninachokifahamu.

4. BONGOLALA

BONGOLALA JF-Expert Member

#4
Sep 6, 2011
Joined: Sep 14, 2009
Messages: 13,782
Likes Received: 2,392
Trophy Points: 280
hata mimi huo mtindo wa vodafone mpesa unaniudhi sana,sihitaji tena kutumia huduma hiyo.wanalazimisha utembee na simu ya vodacom muda wote!TCRA naomba waingilie kati haraka sana ukaguzi huo wa sim card usio rasmi

5. m

mnozya JF-Expert Member

#5
Sep 6, 2011
Joined: Feb 25, 2009
Messages: 207
Likes Received: 20
Trophy Points: 35
Mi simu yangu alitaka nimpe hand set approve kama kweli ni simu yangu. Nadhani nimekuwa direct na nimeeleweka

6. BornTown

BornTown JF-Expert Member

#6
Sep 6, 2011
Joined: May 7, 2008
Messages: 1,716
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
huyo mama/dada wa kihindi kakupenda sasa alitaka akupe simu yake kijanja umtwangie sema tu ww hukuelewa somo....@joke

but pole kwa yaliokukuta

7. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#7
Sep 6, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,102
Likes Received: 22,141
Trophy Points: 280
Lazima wa verify kama kweli ni simu yako, kuna tatizo lipi hapo. Hujasikia wizi na utapeli wa Mpesa kwenye masimu?

Kwani walikuambia wanataka kusoma meseji zako? au walikwambia wanataka kuona namba zako za simu?

Kila simu ina identification kuanzia kiwandani ilipotengenezwa, sasa kwa nini iliwekwa hiyo?

Mambvo mengine msiyachukulie kijuujuu tu, siku hizi kuna wizi aina nyingi na alivyofanya ni sawasawa, kama umeona unaonewa nenda kwingine mbona mawakala ni wengi tu?

8. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#8
Sep 6, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,102
Likes Received: 22,141
Trophy Points: 280

Hiyo ni kweli kabisa hata mimi nimeshafanyiwa na ni kitu cha kawaida kabisa.

9. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#9
Sep 6, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,102
Likes Received: 22,141
Trophy Points: 280
Kuna wizi umeingia kama alivyoueleza chimunguru post #3, voda wanafanya hivyo kukulinda wewe na wateja wengine kutokana na utapeli ulioingia kutokana na simu.

10. dmaujanja1

dmaujanja1 JF-Expert Member

#10
Sep 6, 2011
Joined: Nov 24, 2008
Messages: 225
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
Kwa kifupi dada alitaka kuthibitisha kama namba uliyotoa niya kwako au unamtumia ndugu yako via wakala kitu ambacho hakiruusiwi.
Mimi kwa mazingira yangu ni jambo la kawaida nimelizoea labda wewe huo utaratibu umekuwa mgeni kwako. Lengo lao kuu nikuepusha usumbufu kama kutatokea usumbufu wa aina yoyote ile

11. RasJah

RasJah JF-Expert Member

#11
Sep 6, 2011
Joined: Nov 5, 2009
Messages: 697
Likes Received: 17
Trophy Points: 35
Hilo balaa nilishakutana nalo hapo hapo samora kwa huyo mdada wa kidosi mwembamba hivi... Mbaya zaidi unaanza kujieleza kwa wale walinzi wao wenye magwanda yakupauka.. Niliondoka bila kinga nikaenda pale kwenye container oposite na exim bank

12. Mr. Miela

Mr. Miela JF-Expert Member

#12
Sep 6, 2011
Joined: Aug 2, 2007
Messages: 242
Likes Received: 2
Trophy Points: 35

Ukweli ni kwamba direct deposit inapunguza faida kwa voda kwani kumtumia mtu pesa kwa kutumia simu yako unakatwa mia mbili na yeye wakati wa kutoa atakatwa pesa kulingana na kiwango anachotoa! kwa maoni yangu kuwe na deposit charge!

13. Shark

Shark JF-Expert Member

#13
Sep 7, 2011
Joined: Jan 25, 2010
Messages: 20,071
Likes Received: 7,282
Trophy Points: 280
Chukua taimu huko!!

14. E

Evergreen Senior Member

#14
Sep 7, 2011
Joined: Jun 6, 2011
Messages: 145
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

Sure,ni swala la kibiashara zaidi kuliko usalama kwa wateja,direct deposit inapunguza Transactional fee!!

15. N

Natasha Ismail JF-Expert Member

#15
Sep 7, 2011
Joined: Jul 14, 2008
Messages: 511
Likes Received: 153
Trophy Points: 60
Usiogope,ni suala la kibiashara tu kumbuka nao wapo pale kwa faida ukimwekea mtu direct hupunguza faida.Mlichoshindwa kuelewana ni lugha tu nia yake alitaka kuproove kama wewe kweli ni owner wa hiyo simcard,period.

16. M

MWENDAKULIMA JF-Expert Member

#16
Sep 7, 2011
Joined: Jul 17, 2009
Messages: 961
Likes Received: 23
Trophy Points: 35
Kuna wakati msg inachelewa kufika kwa recepient je itabidi asubiri hadi msg itkapoingia ili mhindi ajiridhishe hata kama ni masaa mawili? Nadhani ni vizuri kuomba kitambulisho cha anaye deposit pesa siyo simu yake

17. Dio

Dio JF-Expert Member

#17
Sep 7, 2011
Joined: Feb 8, 2011
Messages: 1,278
Likes Received: 4
Trophy Points: 135

kwelı kabısa FF

18. M

MWENDAKULIMA JF-Expert Member

#18
Sep 7, 2011
Joined: Jul 17, 2009
Messages: 961
Likes Received: 23
Trophy Points: 35

Wakuu si kuna vitambulisho kwa nini wasicheki hivyo?Kwa mfano wakati unataka kutoa pesa mbona wanacheki kitambulisho why not wakati wa kuweka? I suppose watu hutumia vitambulisho kutengenezewa hizo account za mpesa kwa hiyo no way majina yanaweza kusigana.Tumieni vichwa kufikiri!! Kupekua simu za watu ni kuingilia privacy period!

19. M

MWENDAKULIMA JF-Expert Member

#19
Sep 7, 2011
Joined: Jul 17, 2009
Messages: 961
Likes Received: 23
Trophy Points: 35
Well said.Soon you'll have to drop your id as it'll no longer be representing your character!Big up Mkuu,baelezee.Kwa hiyo kama mtu ameisahau simu yake nyumbani (majority ya watu wa mijini wana simu zaidi ya moja)asipate huduma?

20. M-pesa

M-pesa JF-Expert Member

#20
Sep 7, 2011
Joined: Sep 4, 2011
Messages: 605
Likes Received: 11
Trophy Points: 0
Nachojua ni kwamba alitakiwa aombe kitambulisho, then amwambie mteja mapema kwamba pesa hazitumwi kwa third party moja kwa moja kutoka kwa agent. Wakikubaliana hapo ndo transaction inakuwa initiated na agent.
Msg ambayo agent ataipata baada ya transaction pia inatosha ku-verify pesa zimekwenda kwa nani.

Loading...