Ukaguzi wa pili wabaini watumishi hewa 315 Morogoro

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Idadi ya watumishi hewa katika mkoa wa Morogoro imefikia 315 ikilinganishwa na 122 waliokuwa wamegundulika awali,baada ya kufanyika kwa uhakiki wa kina wa awamu nyingine katika wilaya zote saba zilizopo mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe amesema awali walipokea ripoti ya ukaguzi ambayo hawakuridhishwa nayo hivyo kuamua kufanya ukaguzi kwa mara ya pili na kugundua mkoa una watumishi hewa 315 huku wilaya ya Kilosa ikiongoza kuwa na idadi kubwa ya watumishi hewa 98,Kilombero 48, Morogoro vijijini 38,Mvomero 20,Gairo 13 na Malinyi saba,huku Ofisi ya mkuu wa mkoa na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kukiwa na watumishi hewa watano.

Kuhusu madawati,mkoa wa Morogoro umefanikiwa kuondoa tatizo la uhaba wa madawati kwa shule za sekondari kwa kufikia zaidi ya asilimia 100, wakati kwa shule za msingi ikifikia asilimia 95,hivyo Dk Kebwe kutumia fursa hiyo kuwaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha hadi kufikia Julai 15 wawe wamemaliza tatizo hilo.

Katika uhakiki huo,imebainika shilingi bilioni 2.2 zimelipwa kwa watumishi hao hewa huku milioni 42.8 zikiwa tayari zimerejeshwa.


Chanzo: ITV
 
Hongera Japo angepumuzisha maofisa utumishi kabla ya wakurugenzi hawa ni tatizo la yote hayo wakishirikiana na Wakuu wa idara
 
Kwa nini tusitumie Technology kumaliza haya matatizo. Dah, hebu mtumie salamu Magufuli, hili tatizo dogo sana.
 
Wakuu wa Mikoa wawe wakali kila mwezi kuungalia orodha za Wafanyakazi.Leo mmegundua wafanyakazi Hewa Miezi miwili baadae mnagundua wengine wapya.Hivyo fahamuni watumishi wenu( kaushirika fulani) Wanaelewa fika mambo yanavyopelekwa na hapo hapo Serikali Inaumizwa.Fikiria tu kwa mwezi mmoja mshahara unaolipwa zidisha na Mikoa wanapiga pesa ndefu.BADO MNA KAZI YA ZIADA KWANI MIDAMU KIZAZI CHA WAPIGAJI MNAO KATIKA IDARA ZENU HUSIKA FIKIRIENI JINSI YA KUKIENGUWA
 
Watoeni wote ili waishi kama mashetani, wametuumiza sana hao watu ukiwakuta mitaan dharau nyingi kumbe wanakula hela za watumishi hewa.
 
Tunawasubiri watalaamu wa IT kutoka Rwanda.
Hamna mambo madogo tu haya. Applying technology sio issue, wakati mwingine maamuzi ndio magumu. What to do, when to do, sio mbaya kwenda kuchungulia, maana hata wenyewe kuna mengine wanakuja kuchungulia hapa
 
Wamalize haraka huo uhakiki wao mambo mengine yafanyike, wanatukwamisha na kutuvurugia mipango wengine
 
Teh nadhani baada ya ukaguzi wa vyeti kutakua na upungufu mkubwa sana wa watumishi
Sidhani kama hili zoezi la ukaguzi wa vyeti liyafanyika siriaz maana linaweza ondoka na zaidi ya robo ya watumishi wakiwemo wale ambao kwa sasa wananyadhifa za juu. Ngoja tusubiri tuone labda ajira zitapatikana kwa vijana.
 
Sidhani kama hili zoezi la ukaguzi wa vyeti liyafanyika siriaz maana linaweza ondoka na zaidi ya robo ya watumishi wakiwemo wale ambao kwa sasa wananyadhifa za juu. Ngoja tusubiri tuone labda ajira zitapatikana kwa vijana.
Likifanyika kutakua na upungufu mkubwa sana wa watumishi
 
Back
Top Bottom