Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 60
Jamani watanzania wenzangu naombeni kuuliza kuhusu huu ukaguzi unaoendelea kuhusu magari yalioyoibiwa south Africa ni halali?????? mtu umedungiliza umenunua gari lako zuri ili likusaidie ktk kuwahi makazini unafika barabarani unasimamishwa eti makaburu walikague kama ni la wizi huku wewe unachelewa kazini. Swali je kama Mtanzania kaibiwa gari na ameenda South Africa kuomba ukaguzi kama huu ufanyike nchini kwao watakubali.?? Nchi yetu imezidi kuendekeza ngozi nyeupe au kwa sababu Rais wetu anaenda nchi na ulaya kuomba misaada kila kukikucha. Wenzetu Wakenya wamekataa zoezi hili lisifanyike chini kwao vipi sisi tukubari kila kitu wazungu wanachoamua?????