niukweli usiopingika tatizo la mashoga kubwa kuliko tunavyofikri kuna watu wengi sana wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja haijalishi ameoa au la..na mbaya zaidi wengine wanafamilia na wanafanya kazi nzuri sana lakini wanafanya kwa siri kubwa sana..sasa sijui tufanyaje?
Niliuliza hapo juzi kuwa hivi ni kweli hakuna mashoga Tanzania? Kuna tabia ya kinafiki sana ya watu kujidai watakatifu kwamba ushoga ni mambo ya kizungu, wakati huku mtaani wapo.
mDah! Hata kulawiti imeshakuwa ni haki ya binadamu!!!!! Si ajabu miaka michache ijayo kutakuwa na "haki za binadamu" pia za wanaotaka kujamiiana na watoto/wanyama. Msitushinikize kuukubali uhayawani ambao unaruhusiwa katika nchi zenu.
UK yataka Tanzania itambue haki za mashoga |
PERTH, Australia UINGEREZA imetoa shinikizo la kutambua haki za mashoga kwa nchi zinazoendelea na kutishia kusitisha misaada yake kwa nchi zinazokiuka agizo hilo. Waziri Mkuu David Cameron amesema Uingereza ina mpango ya kusitisha misaada yake kwa nchi ambazo sheria zake hazitambui ndoa za jinsia moja na mashoga. "Nimeshawajulisha baadhi ya wakuu wa nchi kuhusu suala hilo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Perth, Australia," alisema Cameron kupitia BBC.Nchi 41 kati ya nchi 54 wanachama wa Jumuiya ya Madola, zina sheria zinazopinga ndoa za jinsia moja. Suala la haki za binadamu ni moja ya agenda ambazo viongozi kadhaa walishindwa kuafikiana katika mkutano huo ambao rais Kikwete pia alihudhuria. Cameron alisema: "Tunasema hii ni moja ya vitu vinavyoongoza sera yetu ya misaada kwa mataifa mbalimbali na tayari tumeanza kuitekeleza katika maeneo kadhaa," alisema. Aliendelea: "Nchi zote zinazopata misaada kutoka kwetu (Uingereza), zinapaswa kukubaliana kikamilifu na sera hii ya haki za binadamu," alisema. Cameron alisema ameshazungumza na nchi mbalimbali za Afrika kuhusu suala hilo na utekelezaji wake utafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo, William Hague. Kukomesha vizuizi vya ndoa ya jinsia moja, ilikuwa moja ya mapendekezo yaliyomo katika ripoti ya ndani ya matarajio ya baadaye ya Jumuiya za Madola. Katika mkakati huo, Uingereza imetishia kusitisha sehemu ya misaada ya bajeti kuu kwa nchi zisizokubaliana na msimamo huo lakini imeahidi kwamba haitaondoa bajeti yote. Nchi ya Malawi imeshaathirika na mpango huo wa Uingereza kwa sehemu ya misaada yake kusitishwa kutokana na misimamo yake kuhusu haki za mashoga. Nchi ambazo huenda zikafuatia hivi karibuni ni Uganda na Ghana. Cameron ameieleza BBC kuwa nchi zinazopokea misaada kutoka Uingereza zinapaswa kuachana na sheria kandamizi. Lakini akaeleza kuwa ingawa sio rahisi nchi kubadilika ghafla, ni bora zikaanza sasa mchakato wa mabadiliko hayo kuliko kuendelea kubweteka. "Hili ni suala ambalo tunaendelea kulisukuma ili lifanikiwe na tumejiandaa kuwekeza hela pia katika kuhakikisha tunafanikiwa lakini ninashaka kwamba hatuwezi kutegemea mabadiliko hayo kuja mara moja," alisema. Mjadala mzito ulioibuka katika bunge la Uganda mwaka 2009 kuhusu ndoa za mashoga, ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ya Uingereza. Mwaka huu mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga nchini Uganda David Kato alipigwa hadi kifo kutokana na kuongoza kampeni hizo. Bunge la Nigeria sasa linaendelea kujadili Muswada wa kuzuia ndoa ya jinsia moja ikiwamo kuweka adhabu kali kwa watu wanaosadia au kuhamishwa kufungwa kwa ndoa hiyo. Source: Mwananchi |