Ujuzi kwanza pesa baadae

Ryan The King

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,788
2,688
Habari wakuu!

Kwa nini Bara la Afrika ni Masikini? Umasikini wa Afrika unasababu nyingi sana. Zipo sababu zenye mizizi ya Kihistoria hapa ndipo suala la biashara ya utumwa na ukoloni inapojitokeza.

Lakini pia suala la Ujinga halitopuuzwa kabisa. Umasikini wa bara la Afrika unamuunganiko wa moja kwa moja na Ujinga wa wenyeji wenyewe. Kama ilivyosemwa na Wenye hekima wa kale katika magombo yakuwa; Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ndivyo ilivyo.

Katika maendeleo suala la Ujuzi ni suala muhimu lenye manufaa. Ni suala nyeti na lenye tija. Ili maendeleo yaje kwa uthabiti basi sharti yaletwe na ujuzi Fulani.

Ujuzi huweza kuwa ujuzi wa kubuni majengo, kubuni mitindo ya nguo, kubuni Miundo ya nyumba, kubuni mapishi mapya, Kubuni vya zana za usafirishaji n.k.

Ujuzi ni ujuzi tuu ilimradi ulete maendeleo pasi na Hasara kwenye jamii.

Ujuzi kwanza Pesa badae. Hii ndio kanuni namba moja kama si mbili kwenye maendeleo au Utajiri.

Shida ni kuwa watu hupenda pesa sana kuliko ujuzi jambo ambalo huwapa pesa za muda mchache na hatimaye uzeeni kuishia katika umasikini wa kutupa. Tumeshuhudia watu kadhaa zama I walikuwa na pesa lakini Leo ni masikini wa kuomba ugali. Looh! Inasikitisha.

Hata mwanajeshi kabla ya kuingia Vitani hapewi silaha kwanza bali mafunzo na mbinu lukuki yatakayomsaidia vitani. Badae ndio hupewa Silaha na namna ya kuitumia.

Hata katika maisha ya kawaida. Mtu hupaswa kulewa maujuzi lukuki ili aimudu vita ya Maisha na ndipo upewe Pesa ambayo ndiyo Silaha.

Hata upewe Bilioni moja za Dokta Shika, kama hujui mbinu na huna ujuzi wowote basi vita ya maisha itakudondosha.


Vijana hudhani Kuwa na Pesa ndio kufaulu maisha. Ni sawa na mtu umpe Ak47 na hajui kuitumia alafu adhani atashinda vita.

Umri wa kupata ujuzi ni Kuanzia 0-25.
Hapa hakikisha unaujuzi wowote mbali na kile ulichosomea. Kwa mfano ikiwa wewe Ni Mhasibu basi jitahidi uwe na kaujuzi kapembeni kama;
-Ususi na Ukinyozi
-Upishi
-Upambaji
-Ushonaji n.k.

Ujuzi huu utautumia kwa muda wako Wa ziada kujipatia pesa. Bara la Afrika pengine ndilo ambalo vijana wake hawana ujuzi muhimu(Basic Skills) kama Ujuzi wa kutengeneza umeme, Kushona nguo, utunzaji wa Bustani n.k.

Wito: kila kijana ahakikishe anakuwa na Ujuzi zaidi ya mmoja alafu aone kama atakosa pesa. Hata vitani ukiwa na mbinu moja na Silaha Moja upo katika hatari kuu inayoweza sababishwa na mazingira kama kunyesha kwa mvua au Kuvuka mto.

Karibuni.
 
Nakuunga mkono mleta mada natamani kama mada hii ingeeleweka hasa na vijana wa umri tajwa kwani hicho ndicho kipindi cha kujituma na kuangaika kupata maujuzi ...Badala ya kuangaika na mambo yasiyo na msingi ktk maisha
 
Nakuunga mkono mleta mada natamani kama mada hii ingeeleweka hasa na vijana wa umri tajwa kwani hicho ndicho kipindi cha kujituma na kuangaika kupata maujuzi ...Badala ya kuangaika na mambo yasiyo na msingi ktk maisha
Hili wengi hatulijui. Ndio maana tunaishia lawama kwa serikali. Tunaposema vijana ndio wenye nguvu na ndio hupaswa kufanya kazi
 
Back
Top Bottom