Ujumbe wangu kwako Mhe. Alex Kimbe

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Mhe. Alex Kimbe wakati nikiendelea kukuombea katika sala zangu, naomba nikupe ujumbe huu kuwa MUNGU YUPO UPANDE WAKO NA ANAKUPENDA SANA. Safari ya binamu duniani ni safari yenye dhoruba kubwa.

Binadamu anapozaliwa anazaliwa akiwa hana kitu chochote, hata nguo anayovalishwa baada ya kuzaliwa ni hisani toka kwa wale anao wakuta hapa duniani.Lakini pia anapokufa ni wahisani tu ndiyo wanamuogesha na kumvisha nguo kama ilivyokuwa wakati wa kuzaliwa.

WanaIringa wanatambua kazi yako ya kutukuka, hata watesi wako wanatambua kuwa ulikuwa unachapa kazi ndo maana wakaingiwa na hofu. Pamoja na njia zote ovu walizotumia kukushawishi ili uwe sehemu yao lakini haukuweza kuwakubalia bali uliamua kukaa upande wa Mungu, hakika Mungu hatakuacha. Lakini pia tambua wana Iringa wapo pamoja nawe.

Pongezi nyingi sana kwa kuamua kukaa upande wa kweli, upande wa Mungu. Vitu vyote walivyokushawishi navyo wataviacha bali roho ya upendo wa kiMungu utakuwa nayo hadi ukamilifu wa dahari. Mungu aendelee kukusimamia na kukulinda katika haki na kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea maneno yenye hekima sana mkuu, Mungu akubariki sana, mwenye sikio na asikie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom