Ujumbe wangu kwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wangu kwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Nov 11, 2010.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Siyo siri kwamba Mhe. Sita ameleta mapinduzi makubwa kwenye utendaji wa mojawapo ya mihimili ya uongozi hapa nchini. Chini ya uongozi wake wa bunge watanzania wengi wamepata mwamko wa kisiasa na wameanza kufuatilia utendaji wa wawakilishi wao ndani ya vikao vya bunge. Kutokana na utendaji wake huo, wa Mhe. Sita alitengeneza maadui zake wengi kutoka ndani na nje ya chama chake cha ccm. Maadui waliokuwa hatari ni wale wanaotoka ndani ya chama chake ambao wengi wao ni mafisadi wakubwa. Kwa nguvu yao ya kifedha hatimaye wamemwangusha na kumwondoa kwenye kiti kikuu cha enzi.

  Ndugu zangu wabunge hususan wazalendo mnaoipenda kwa dhati nchi yenu, msifanye kosa kuwachagua akina mama waliopitishwa na ccm. majina hayo yamepitishwa kwa nguvu ya kifisadi ili kukiponya chama chao na vidonda vilivyotokana na uongozi wa Mhe. Sita. Wanataka bunge letu lililoanza kupata umaarufu ndani na nje ya bara letu la afrika, lianze kusinzia tena.

  Watanzania tunawaomba tena tupo chini ya miguu yenu, tafadhali mchagueni Mhe. Marando ili kuendeleza kazi iliyoanza kufanywa na Mhe. Sita. Hiyo itakuwa ni zawadi yenu ya kwanza kwa wapiga kura wenu tangu mpate huo uheshimiwa.

  Mungu ibariki Tanzania,
  Mungu ibariki Afrika.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mwenye masikio ya kusikia.....
   
Loading...