Ujumbe wa wazi wa Mwenyekiti Bavicha taifa kwa Mhashamu Baba Askofu Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Baba Askofu salamu. Kwanza nakutakia heri ya Krismas na mwaka mpya.

Ninakushukuru pia kwa ajili ya mahubiri/ maoni yako kuhusu mwaka 2020 kama yalivyochapishwa katika gazeti la Mwananchi.

Umesema kutokana na changamoto za uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 umetaka tusameheane kwa yote yaliyotokea.

Nafikiri unajua kabisa ni nini kilitokea kilichosababisha CCM kujitangazia ushindi bara na visiwani kwa zaidi ya 95% katika Bunge na zaidi ya 80% kwa kura za urais.

Baba Askofu ni bahati mbaya haya yote yanatokea katika kipindi ambapo kanisa limechagua kunyamaza kimya (Bila kutoa msimamo wa pamoja) na badala yake kazi hiyo imebaki kwa watumishi mmoja mmoja kama Askofu Mwamakula, Bagonza, Padri Kitima, Sheikh Ponda, Sheikh Rajabu Katimba na wengine wachache. Jamii inajiuliza kwa nini mmechagua kukaa kimya?

Nataka kusema nini?, tangu Askofu Kakobe na Niwemugizi walivyochunguzwa uraia wao. Tumeona watumishi wengi wa Mungu mmechagua kurudi nyuma na kuacha dhuruma izidi kutawala katika taifa letu.

Mhashamu baba Askofu, huku uraiani sisi ambao ni waumini wa dhehebu la Kikatoliki, wananchi wenzetu wasiokuwa waumini wa dhehebu letu wanahoji, ule msimamo wa kanisa letu kuikemea serikali kama ulivyokuwepo wakati wa serikali ya Kikwete umekwenda wapi?

Wacha tuyaache hayo. Nirejee kwenye ajenda yako ya kusameheana.

Baba Askofu kama mpatanishi wa kiroho na kijamii naamini unaifahamu misingi ya upatanishi kati ya pande mbili zinazo umizana.

Wacha nikupe picha kidogo. Mwishoni mwa mwaka jana Tume ya taifa ya Uchaguzi na Spika wa Bunge wamajitangazia wabunge wao wa viti maalumu kuwa eti ni wabunge wa Chadema na ikawaapisha. Chadema kama taasisi tukakaa tukaona tuchukue hatua za kinidhamu za kuwafuta uanachama.

Spika wa Bunge akasema piga ua garagaza watabaki bungeni. Akajitokeza Spika wa Bunge mstaafu Pius Msekwa akasema hawa wamepoteza sifa. Ndugai akajitokeza hadharani akawaambia waandishi wa habari acheni kuwahoji wastaafu njooni mnihoji mimi. Bado mlikaa kimya!

Haya ya uchaguzi, mengi yanajulikana mauaji ya wafuasi wa upinzani, polisi kubeba kura za mabegi ili kuingiza kwenye maboksi, kukamata viongozi wa upinzani na kuwapa kesi kama za ugaidi, uhujumu uchumi, uvamizi Nk. Bado mlikaa kimya tu.

Baba Askofu wakati unasema tusameheane Kuna wanachama wa Chadema zaidi ya 200 wako magereza kwa kesi nzitonzito. Jimbo la Tunduma peke yake kuna mahabusu zaidi ya 50 jimbo moja tu. Na lenyewe mmechagua kukaa kimya.

Haya na mengine mengi yanaumiza sana kiasi cha kufikirisha kuwa huenda visasi vikawa suruhu yake maana labda pande zote zikiumia mnaweza kuitana kujadiliana kwa ajili ya Amani.

Baba Askofu sisi kama Chadema tunasema "No Hate No Fear". Hatuna haja ya kulipiza visasi ila tuanataka HAKI itamalaki katika taifa.

Baba Askofu nimekueleza haya si tu kukueleza wewe peke yako juu ya hisia zangu na za vijana wenzangu ninaowaongoza, Bali kuwaeleza viongozi wote wa kiroho kuwa tunahitaji msaada wenu katika kuleta utengamano katika taifa letu.

Niseme nini tena? Nikuombe mambo 2.

1. Ielezeni serikali iachilie huru watuhumiwa na wafungwa wote wa kisiasa.

2. Ungana nasi katika VUGUVUGU la kudai KATIBA MPYA.

Nakutakia kila la Kheri katika utumishi wako.

Wasalaam.
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa.
jpambalu@gmail.com
 
Askofu tapeli tu huyo. Anafukia ile kashifa yake ya Kuhongwa mapesa.....nitakuja kueleza siku nyingine.Ni njaa tu
 
Niseme nini tena?. Nikuombe mambo 2.

1. Ielezeni serikali iachilie huru watuhumiwa na wafungwa wote wa kisiasa.

2. Ungana nasi katika VUGUVUGU la kudai KATIBA MPYA.

Nakutakia kila la Kheri katika utumishi wako.

Wasalaam.
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa.
jpambalu@gmail.com
Huyu Askofu ni mnufaika wa hela za escrow hivyo hawezi kamwe kukemea maovu kwani na yeye ni muovu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Pambalu ana interest alishindwa ubunge nyamagana kaandika hisia zake za kushindwa kwenye barua ilitakiwa mwisho aandike mbunge aliyeshindwa pambalu
 
Mwambieni huyo mwandishi wa barua kuwa Mha. Kilaini hatumii smart phone! Kama analojambo la kumfikishia amfuate Bukoba
 
badala yake kazi hiyo imebaki kwa watumishi mmoja mmoja kama Askofu Mwamakula, Bagonza, Padri Kitima, Sheikh Ponda, Sheikh Rajabu Katimba na wengine wachache. Jamii inajiuliza
Ni wajinga wachache Sana wanaoamini kuwa ni lazima na nimhimu Kwa Jambo Lenu liungwe mkono na kila raia!!

Ni wajinga wachache Sana wanaoamini na kuunga mkono Madai ya Chadema eti kulitokea upolaji wa Kura kipindi cha uchaguzi!!

Ni upuuzi mtupu kuamini uwongo wa Kura feki zilizozagaa mitaani, ukitaka kujua kuwa ilikuwa ndio kichocheo na propaganda za kuwaamisha wananchi ili waingie Mtaani Kwa mandamano, angalia tu mpango wa kuwaingiza mtaani wananchi ulipobuma, hakuna aleenda mahakamani kudai haki hiyo

Wale waliokuwa wakionesha makaratasi ya Kura feki, wakidai wameyakamata ktk vituo vya kupigia Kura kwenye maeneo ya majimbo Yao, ndio wamekuwa wa Kwanza kukubali kuwa Walishindwa na kuingia bungeni wakiwa kama wabunge wa viti maalumu!!

Wengine kina nyie tunawaona ni wahuni tu, kazi yenu Kwa sasa ni kufoka mkiwa mitandaoni pekee, maana wengi wenu hamna ubunge sasa
 
Kilaini ni msomi wa viwango vya juu na anatumia smartphone na tupo naye kwenye group la wasapu la Wakatoliki na Facebook yupo.
Basi umshauri huyo mwandishi amfuate huko wasapu na facebook, huku ni JF, Kilaini hayupo!
 
Askofu tapeli tu huyo. Anafukia ile kashifa yake ya Kuhongwa mapesa....Ukatoliki ni utapeli na ufisidi tuu....nitakuja kueleza siku nyingine.Ni njaa tu

Hiyo conclusion yako ukatoliki Ni utapeli imebase wapi. Nothing is evil in itself. Wewe Ni Nani hasa. Siasa zako za kibangi Bangi isikufanye uingize imani na za watu. Wewe ulipo Hapo umefanya mema mangapi na Makosa mangapi. Na bado Ni mwanadamu na sio Mnyama. Kama unashindwa kukontrol hisia za utu wako hizo hoja utajenga kwa kutumia nini. Inverse proportionality. Chini kukiinuka juu kunaporomoka. Grow up.
 
Back
Top Bottom