Ujumbe wa wazi kwa 'RAIS JK KIKWETE' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa wazi kwa 'RAIS JK KIKWETE'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAZETI, Nov 24, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,559
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  KIKWETE UNAUKANA VIPI UDIKTEKTA?

  Katika hotuba yako ya juzi umeukana udikteta. Pengine ulikuwa sahihi kwa kauli yako lakini katika macho ya watu ambao hayajawakuta na hawafahamu nini kinaendelea katika nchi hii. Kinachokutofautisha na madikteta wengine ni kitendo chako cha kujificha kwenye mwavuli wa kuingia ikulu kidemokrasia.

  Baada ya utangulizi huo naomba nitoe ufafanuzi wa kile nilichokianzisha. Wewe ukiwa kama kiongozi, mkuu wa nchi huwezi kushindwa kuona kile wanachotendewa wananchi wako wa maeneo mbalimbali.

  Katika kampeni zako ulisisitiza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo sahihi ambao utaboresha soko na maslahi ya wakulima. Lakini mkuu kinachotokea ni kinyume, mfumo huu umekuwa unatutesa kwani kwa kazi tuliyoifanya miezi kadhaa kwa taabu kubwa matokeo yake ni kukopwa kwa lazima.

  Mkuu: bila shaka unafahamu kuwa baada ya wakulima wa korosho Tandahimba kuona kuwa huu mfumo wa stakabadhi ghalani ni wa lazima tukaamua kuanzisha umoja wetu. Umoja huu haukwenda kinyume na Mfumo ulioutaka lakini cha kushangaza umekutana na vikwazo ambavyo havijawahi kuonekana. Kupitia kwa mkuu wa Wilaya ambaye ni wewe umemteua na kumleta kataka Wilaya yetu tumekuwa na matatizo makubwa sana, Tunateseka na kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.

  Mkuu: Mwaka huu umeenda mbali zaidi kwani kwa kutumia TAMISEMI umeamua kuuzuia kabisa umoja huu kufanya shughuli zake. Kimsingi haionekani sababu ya muhimu ya kufanya hivyo zaidi ya dhuluma na uonevu kwa wakulima kwani baada ya kuzuiwa umoja huo kilichofuata ni kuwa wakulima wanalazimishwa kukopesha korosho zao TANECU. Ni mateso makubwa sana, Kwa mtaji huu usitegemee kuwa watu watakuja kuipenda CCM abadani!

  TUNACHOAMINI

  Moja ya sababu kubwa za CCM kukataliwa katika Wilaya yetu ni huu Mfumo mbovu wa stakabadhi ghalani, bila shaka unafahamu Wazi kuwa CCM ilianguka katika Wilaya yetu ingawa ndiyo iliyotoa Mbunge (Rafu)
  Wewe na viongozi wa TAMISEMI Hususani Mkuchika mna maslahi yenu kule TANECU (Chama cha ushirika ambacho kinaunganisha wilaya mbili za Tandahimba na Newala huku upande mmoja ukidhulumiwa katika mapato)

  TETESI

  Kwa maneno yanayozungumzwa mtaani (Lisemwalo……….) Huwa unapokea shilingi 100 katika kila kilo moja ya korosho. Ina maana kuwa kama tutauza tani 100,000 za korosho hizo unazidisha kwa 1,000 kisha kwa 100 (Hili sina uhakika lakini ndilo linalozungumzwa yasemekana ndio maana ukamtuma Mkuchika azuie UWAKOTA, umoja wa wakulima wa korosho kufanya kazi yao.

  UJUMBE WANGU KWAKO

  Wanasiasa wa CCM mmekuwa na tabia ya kupenda kusikia mnachotaka kusikia lakini hampendi kusikia mnachotakiwa kusikia. Naomba sasa baada ya kuupata ujumbe huu ubadilike na kuwa msikivu. Tunateseka, mpaka hapa ninapoandika ujumbe huu najua wazi kuwa nimehatarisha usalama wangu, lakini sioni sababu ya kuogopa kwani kabla ya hapo nimeshaanza kuteseka kwa huo mfumo wenu. Kwa hiyo sina cha kupoteza.

  HITIMISHO

  Kitu mnachokipanda katika nyoyo za wananchi hawa masikini lazima siku moja mtakuja kukivuna. Mshahara wa dhambi…………..

  Najua mko juu ya sheria, lakini naomba mtambue kuwa kuna ambaye yuko juu ya sheria zaidi yenu. Najua mmeshika mpini sisi tumeshika makali, lakini tambueni kuwa kuna anaevimiliki hivyo vyote.
  Hatuwezi kuwashitaki kwa yeyote zaidi ya yule ambaye ufalme wa mbingu uko mikononi mwake, naye ni mkuu kwa kila kitu.

  EE, Muumba wa mbingu na ardhi, tunadhulumiwa sisi viumbe vyako tuanaomba utuchukulie kisasi kwa hawa madhalimu.


  Nakala. Mh.M.Pinda (Waziri mkuu, ulilazimisha mfumo wa stakabadhi ghalani pale tulipokuja na mabango ya kuukataa)

  Wako

  GAZETI(P.I)

   
 2. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Poleni sana kaka maana kila nikisoma naona umeandika ukiwa na hasira kali sana.
  Nimesikia kuwa mwaka huu kuna mkopo wa hizo korosho zenu, Hiyo ndiyo CCM.
   
 3. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu serikali kwa hili la kujifanya kuwatetea wakulima kwa kuanzisha mifumo ya kihuni kama stakbadhi ghalani, mara kuuza mazao kwa serikali kwa ajili ya hifadhi, au kuzuia mipaka, huku kukiwa na ruzuku hewa ya pembejeo, ya ama haipo na wakati mwingine haikidhi haja ya walengwa, na kuja kwa muda wanoujuwa wao ili wachukue na kufaidi kwa kuuza huko wajuako tafadhali tunaomba liangaliwe upya.

  Huwezi kuzuia mkulima asifaidi kazi ya mikono yake eti kwa sababu chakula kinaonena hakitatosha hivyo asiuze nje, kumbuka kwa kufanya hivyo inapelekea watanzania wengi kutokufanya kazi ya kilimo wakiamini chakula serikali italeta kama mnavyoona sasa hata baadhi ya wabunge wetu wakikomaa mishipa serikali ipeleke chakula kwenye majimbo yao kuna njaa.

  Nashauri hifadhi hizi ziwe kwa ajili ya mashuleni an si vinginevyo, hawawezi watu hawa wakala bure tu yaani (at the expense ya wakulima), au la subsidy itolewe kwa hawa wakulima kwa kuzingatia hali halisi si kwa hawa cooked wakala.
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kila sehemu jk jk huyu rais vipi mbona kila mtu anamlaumu kweli niamini ukubwa jiwe kila mtu anajisugulia miguu..
   
 5. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana nia ya JK ikawa nzuri kabisa, ila sasa watekelezaji mzee!! ni noma, yaani wateule wa JK minogoni mwao ndiyo wezi na wakwamishaji wa harakati za ukombozi wa kiuchumi, mfano mzuri mcheki Mattaka, alimteua kwa mbwembwe, ona aliyoyafanya, ningekuwa JK ningerudisha adhabu ya fimbo kama mwl.
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  af wa kwanza kuchlazwa bakora atakua nani unadhani??????????????
   
 7. R

  Regghan New Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani mwenye ujasiri wa kumvisha paka kengele?
   
 8. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Kivipi?
   
 9. C

  Caros Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pongezi kwa GAZETI P.I ,umetoa dukuduku lako la moyono bila kumshurutisha mtu au kuchochea hisia KALI!

  Kwa mtazamo wangu nia na madhumuni ya mtandao/mitandao ya kijamii kama huu ni kuchangia mawazo na kuelimishana masuala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia lugha safi yenye staha ambayo hata ukiambiwa usome kile ulichokiandika mbele ya kadamnasi hutaona haya/kigugumizi.

  Hoja yako inayo masuala ya msingi na ninaamini WAHUSIKA watayafanyia kazi,japokuwa kidogo inaonekana hali hiyo imekugusa sana pole sana kama ulivyo tumia IMANI ya kutoka kwa Muumba,nina imani muhusika naye itamgusa kama ilivyo kugusa wewe.

  Kama alivyosema mchangiaji Ng'wanakidiku nami nakubaliana naye kuwa inawezekana Muheshimiwa JK hakuwa na nia/malengo hayo au yaliyo pelekea hali hiyo kutokea.Kwa ufahamu wangu Muheshimiwa hapangi/kuamua kila jambo ingwaje yeye ndiye muidhinishaji mkuu, nikiwa na maana yapo anayo yapanga na kuyatolea maamuzi na mengine yanafanywa na wasaidizi wake.

  Sasa hapo ndipo kwenye tatizo,sitaki kuzungumzia sana masuala ya kiutawala/wasaidizi wake ila kuna mifano mingi tunayo inayo dhihirisha kuwa wasaidizi wengi wa Muheshimiwa hawako makini kiutendaji kiasi kwamba wanampa wakati mgumu sana pindi mambo yanapo kwenda kombo!!

  Naomba niishie hapa,nitoe nafasi kwa wachangiaji wengine!!

  Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Bariki Ulimwengu mzima tuepushe na vurugu za uvunjaji wa Amani....amen!!
   
 10. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Hapa ndipo ninapowalaumu usalama wa Taifa, wanashindwaje kufahamu mambo yanayohatarisha usalama wa nchi yetu, hivi hawa watu wakianza kujilipu tutamlaumu nani. Kama mtoa mada hapo juu anaonyesha wazi hana cha kupoteza, hii ni hatari. Wapeni watu haki zao tuishi kwa amani.
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Wako bize kuandama wapinzani wa kweli!
   
 12. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Huu uchafu ndio sipendi kuusikia... Eti 'ana nia nzuri ila watendaji...' Inawezekana vipi mtu uwe na nia na agenda nzuri halafu ushindwe kuzisukuma wakati umepewa mamlaka yote? Utetezi wa kijinga sana!
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mimi na wewe tukiamua
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Vioi hakuupata huu ujumbe?
   
 15. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,559
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Mkuu umefanya kazi ya ziada kuirudisha hii post, nafikiri sasa ndo watafahamu kwa kiasi gani wanaweza kuitumia JF kiutendaji.
   
 16. b

  bogota the king Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Imekusikia vema, niko safari nje ya nchi natafuta wafadhili wa kununua korosho yenu! now niko safarini ila nitaunda TUME kuchunguza.

  Ni mimi mkuu JK Rahisi wa njii hii!
   
 17. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Bandubandu umaliza gogo
   
 18. drmkumba

  drmkumba Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kilimo kwanza!
   
 19. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280
  ''Even if there is control,without cooperation,there cannot be coercion''
   
 20. Mzee wa kurekebisha

  Mzee wa kurekebisha Senior Member

  #20
  Jan 17, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 155
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Nikiangalia matukio yanayoendele MTWARA na Lindi hii Post inanifanya
  niamini kuwa kweli JF Kuna Magreat Thinker.

   
Loading...