Ujumbe wa wazi kwa Pinda! -chonde ..fanya vinginevyo pisha!

Upande mmoja ninaelewa kuwa kufunua hili kutaitikisa nchi lakini kutolifunua nafikiri kunaitikisa zaidi

Umeiangalia mizani yako vizuri kuona kama hilo la pili ni kweli litazidi la kwanza?Maana kama ni kinyume chake basi hali itakua mbaya zaidi
 
Mkuu siku hizi wanajitangaza kabisa tena waziwazi si sawa na zamani ilikuwa siri. Unakutana na mtu bar mnapata kinywaji na katika kutambulisha anakwambia kabisa mimi ni usalama wa taifa.

mzee mtu kama huyo anawazuga tu.. unless ni mtu wa Mwang'onda. Sheria ya Usalama wa Taifa iko wazi juu ya kujitambulisha au kumtambulisha kuwa kuwa ni mtu wa usalama wa Taifa. Ni kosa kubwa kweli kisheria, kwenye nchi nyingine linabeba adhabu ya kifungo cha maisha!
 
Mkuu siku hizi wanajitangaza kabisa tena waziwazi si sawa na zamani ilikuwa siri. Unakutana na mtu bar mnapata kinywaji na katika kutambulisha anakwambia kabisa mimi ni usalama wa taifa.

Mkuu ni kweli, kuna jamaa alikuwa amelewa kidogo wakawa wanabishana kuhusu ufisadi na ubadhirifu serikalini kwa kejeli akajibu...sisi ndio tunaoufahamu vile tuko ndani ya mfumo...nilimdharau nikaona ni majisifu ya baadhi ya watu lakini huyu jamaa ni kweli anafanya hio kazi...nimedhibitisha
 
Hakuna Jipya kutoka kwa Wabunge wa CCM, Ndugu yangu umesema ukweli kabisa juu ya hili la Meremera na Utumbo mwingine, Waseme ndio watu tutaacha kusema, Mbona Operation za Kijeshi wanatangaza, Vipi Hizi za Meremeta
 
ETI usalama wa taifa! Meremeta iwe sehemu ya usalama wa taifa!!!!! kuna nini cha kiusalama kwa Jeshi la wananchi kumiliki Meremeta? nijuavyo mimi Jeshi la wananchi ni kwa ajili ya usalama wa nchi kutokana na uvamizi na nchi nyingine ( maana usalama wa ndani wapo polisi na mashushu). hivi Idi Amini amerudi tena? kama hajarudi, Tanzania maadui zetu ambao wanatishia usalama wa nchi yetu kwa sasa ni nchi gani? na tuna ugomvi gani nao?Hivi tuna nchi katika zinazotuzunguka au za mbali zinazotaka kutuvamia? Je wanajeshi wa vyeo vya kati na wa chini kabisa ambao ndiyo wapiganaji wameambiwa kuwa wajiandae kupigana na hao maadui? Hii mnayosema ni siri ni siri kwa ajili ya nani kama hao wanaotakiwa kulindwa/ kuhakikishiwa usalama hawajui wanalindwaje? hii ni ajabu chini ya jua - mlindwa hatakiwa kujua undani wa usalama wake ila Vithlan na kampuni ya BAE ndiyo wanaruhusiwa kujua hizo siri kwa sababu za kifisadi?
PINDA NA WENZAKO MJUE WATANZANIA SIYO MABWEGE TENA. IPO SIKU MTASEMA UKWELI MPENDE MSIPENDE.
Ukipatwa na haja unaweza kujichelewesha kwenda msalani kwa muda lakini itafika muda upende usipende utakwenda tu.

Wakati wa CCM na serikali yake kwenda msalani ndo huu......!!!

Mara utasikia TICTS inabaraka za baraza la mawaziri, mara meremeta inahusu usalama wa taifa, ....mara upumbavu mwingine. Hivi ni baraza gani la mawaziri litakubali TICTS iendelee na ujinga inaoufanya hapo bandarini?? au ni baraza la waganga wa kienyeji??

Hivi Kikwete na Pinda mnashindwa nini kuvunja mkataba na TICTS na mkaundatume ya kuendesha bandari yetu? mbona sumaye alivunja jiji dar na kuweka tume chini ya keenja na ikaleta manufaa?? Kuna nini hapo ikulu ?? mbona tunasikia tu hugo chaves anafanya vitu?? Wewe kama rais unashindwa nini??

mtalinda wezi hadi lini?? au na wewe ni mmoja wao?? ni nani asiyejua kwamba Uongozi wa Gen. mboma uliliingiza jeshi ktk hasara kubwa? Akaja Waitara naye akaendeleza libeneke ya kula nchi ??

Ya levy Mwanawasa yanawashinda nini?? Au na wewe unaogopa skendo zako zita kufikisha kortini pindi ukiachia urais? kama siyo wa ogopa nini kumshitaki mkapa??
 
Hakuna kitu kibaya kama kuficha madhambi ya watu wachache ndani ya kazi za usalama wa Taifa.Inawezekana kabisa kama mchezo huu wa kufagialia kila takataka chini ya kapeti la usalama wa taifa utaendelezwa, hiki chombo nyeti kitapoteza credibility yake mbele ya macho ya watanzania.Imefika wakati sasa tuanze kuwa accountable.Kila mtu abebe msalaba wake tuache kubandika misalaba ya watu kwenye vyombo na taasisi nyeti za serikali.
 
WanaJF naomba muongozo, je ni kweli na ni haki kabisa kwa jeshi kutowajibika bungeni? Je waziri wa ulinzi kazi yake ni kusoma na kuomba bajeti ya wizara yake kupita? Je matumizi ya majeshi hayatakiwi kukaguliwa? kwa mtaji nchi hii kila kitu kitafanywa chini ya mwamvuli wa 'usalama wa taifa'! Hatari hii!
 
Wakati wa CCM na serikali yake kwenda msalani ndo huu......!!!

Mara utasikia TICTS inabaraka za baraza la mawaziri, mara meremeta inahusu usalama wa taifa, ....mara upumbavu mwingine. Hivi ni baraza gani la mawaziri litakubali TICTS iendelee na ujinga inaoufanya hapo bandarini?? au ni baraza la waganga wa kienyeji??

Hivi Kikwete na Pinda mnashindwa nini kuvunja mkataba na TICTS na mkaundatume ya kuendesha bandari yetu? mbona sumaye alivunja jiji dar na kuweka tume chini ya keenja na ikaleta manufaa?? Kuna nini hapo ikulu ?? mbona tunasikia tu hugo chaves anafanya vitu?? Wewe kama rais unashindwa nini??

mtalinda wezi hadi lini?? au na wewe ni mmoja wao?? ni nani asiyejua kwamba Uongozi wa Gen. mboma uliliingiza jeshi ktk hasara kubwa? Akaja Waitara naye akaendeleza libeneke ya kula nchi ??

Ya levy Mwanawasa yanawashinda nini?? Au na wewe unaogopa skendo zako zita kufikisha kortini pindi ukiachia urais? kama siyo wa ogopa nini kumshitaki mkapa??
Mkuu Magezi umesema vyema.

TICTS ni ya hao hao unaotaka wavunje mkataba. Wanashindwa kwa kuwa wanafaidika nayo moja kwa moja. Ubinafsi wa namna hii ukiachiwa uendelee kukua, utalimaliza Taifa. Na Taifa hili likimalizika hata hao wanaoiba wakidhani wataishi kwa raha watagundua wamekosea kwa kuwa wataishi kwa karaha kwa miaka yote iliyobaki ya maisha yao. Na hilo litaendelea mpaka kizazi chao cha 4. Laana ya masikini ni laana mbaya sana. Wanaodhani dua la kuku halimfiki mwewe, wajiulize mwewe akifa hubaki angani au hushuka ardhini.

Mafanikio ya serikali yoyote yanategemea nia, mipango na malengo ya serikali na hasa nia na uwezo wa kiongozi mkubwa kabisa wa serikali hiyo (Rais). Siamini kuwa PM anaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kero zinazoikabili nchi. Anachoweza ni kumshawishi kwa msisitizo na bila woga Rais. Hili inaelekea si rahisi kwa uongozi tulionao sasa. Hakuna nia, hakuna mipango wala malengo ya maendeleo. Na ndio maana bajeti yao sasa imewekeza kwenye chai na furniture, kwa maana wanataka kulala maofisini wakiangalia TV na si kufanya kazi. Bajeti za maendeleo zinatengewe pesa chache (zimeshuka sana) ila tunaonyeshwa figures kwamba zimeongezwa (inflation not considered).

Hakuna guarantee yoyote kuwa Rais akiachia wezi watafune rasilimali za nchi atakuwa salama akitoka madarakani. Wananchi wakiamua, wakafanya jitihada, Mkapa na wengine wote wanaweza kufikishwa mahakamani na Rais yeyote hataweza kuzuia. Labda kama anataka kuvuruga amani na utulivu. Tunaanza kufika ukingoni sasa. Wananchi watashindwa kuvumilia. Watadai uhuru wao kwa nguvu. Hili ni la kuepuka kiliko ukoma.

Rais na viongozi wengine wote, watakuwa salama tu endapo watafuata na kuilinda Katiba ya nchi. Hakuna atakaehukumiwa kwa kufanya hivyo. Ila hukumu itawaangukia wote watakaoivunja Katiba hata kama walifanya hivyo "kwa nia njema".

WanaJF naomba muongozo, je ni kweli na ni haki kabisa kwa jeshi kutowajibika bungeni? Je waziri wa ulinzi kazi yake ni kusoma na kuomba bajeti ya wizara yake kupita? Je matumizi ya majeshi hayatakiwi kukaguliwa? kwa mtaji nchi hii kila kitu kitafanywa chini ya mwamvuli wa 'usalama wa taifa'! Hatari hii!

Hakuna chombo chochote cha umma klicho juu ya sheria. Hakuna chombo chochote cha umma ikiwa ni pamoja na JWTZ, UWT na vyombo vingine vyovyote vya ulinzi na usalama vyenye mamlaka ya kufanya mambo kinyume cha Katiba, sheria za nchi au taratibu za utendaji ambazo zote hupangwa na Bunge la JMT. Bajeti za wizara zote hufikishwa Bungeni, hujadiliwa na hurekebishwa kama inabidi hadi kufikia malengo yaliyokusudiwa na kadiri Bunge linavyoona inafaa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Bunge.

Suala la Meremeta linatia kichefuchefu, kwani ni suala ambalo hapo awali lilikuwa likijadiliwa kwa uwazi lilipoanzishwa na wakati ikiwa in operation. Ni mradi ambao serikali ulijivunia nao sana. Ilipoanza kutafuta pesa za wezi wachache, ndipo ikaacha kuwa ikijadiliwa kwa uhuru. Kama issue ni usalama wa Taifa, je kwanini imebidi kwa kipindi hiki na si kingine huko nyuma? Kwanini miaka yote iliyopita Meremeta ilikuwa ikijadilika hadi ilipoanza kuiba pesa za umma?

Nadhani serikali inatakiwa kuacha kutudharau, kutukebehi na kutunyima haki kwa kudhani wote sisi ni mahayawani. Itawa-cost wanasiasa wote wanaodhalilisha wananchi kwa minajili hii. Hata kama watakuwa wameacha siasa, Dhambi hii itawatafuna maisha yao yote.
 
Sitaki kuangalia mbeleni wapi tunakopelekwa na hawa viongozi wetu, cha muhimu tuombe uzima tu na rehema za Mungu.
 
Meremeta: The details Including where its relationship with TPDF starts and ends

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

MEREMETA Limited, the now-defunct company currently at the centre of a growing parliamentary controversy, was initially registered as an offshore firm in the Isle of Man, United Kingdom and filed for bankruptcy hardly a year after starting to produce gold from the Buhemba Mine in Mara Region, it has been revealed.

The Isle of Man is considered one of the world’s most popular tax havens, home to almost 54 billion pounds ($80bn) of offshore bank deposits. The island is especially favoured by companies looking to take advantage of its emphasis on privacy and generous tax benefits.

According to investigations by THISDAY, Meremeta Ltd was initially registered in the island in April 1997 and received certificate of registration number 3424504.

At least two British legal firms, London Law Services Ltd and London Law Secretarial Ltd, were described as �nominal shareholders� of the company.

But going by official records in Tanzania, Meremeta was registered as a 50-50 joint venture project between the Tanzanian Government and a privately-owned South African company, Triennex (PTY) Limited.

In October 1997 - six months after its initial registration in the Isle of Man - Meremeta was granted a certificate of compliance number 32755 by the Business Registration Licensing Authority (BRELA) in Dar es Salaam, thus allowing the company to formally operate in Tanzania.

In February 2003, Meremeta joined forces with the Tanzania People’s Defence Forces (TPDF) in gold mining activities at the Buhemba open pit gold mine in Mara Region, with heavy financial backing from the Bank of Tanzania (BoT).

Insiders say the involvement of the TPDF in the Buhemba gold mining operations was aimed at raising funds to finance the army’s cash-strapped vehicle manufacturing division - Tanzania Automotive Technology Centre, better known as the Nyumbu project.

It is understood that Meremeta was also set up to assist in developing the country’s informal gold mining sector.

In 2005, the company formally announced it had produced 2,075 kilogrammes of gold at a cash cost of $384 per troy ounce of gold.

Apart from the Buhemba Mine, Meremeta also held the Kilamongo and Mwizi deposits, both located south of Buhemba, and the Nyasanero deposit.

But surprisingly in 2006 � just a year after officially beginning gold production � the company declared itself bankrupt, and was formally dissolved.

Informed sources have confirmed to THISDAY that after the liquidation of Meremeta, both the TPDF and the South African company (Triennex) formally pulled out of gold mining activities at Buhemba.

This means that all military involvement in the Meremeta project formally ended in 2006, when the company was declared bankrupt.

Official Government records show that as Meremeta Ltd was winding up its operations prior to liquidation, the BoT paid more than $118m (approx. 154bn/-) to Nedcor Trade Services Limited, a financial services company registered in Mauritius, to offset a guaranteed loan it (the company) had extended to Meremeta.

The central bank raised the funds to pay off the loan to Meremeta through a controversial 155bn/- Treasury bond, in a transaction that later raised serious queries from auditors.

Following the liquidation of Meremeta Ltd, the Ministry of Energy and Minerals announced in Parliament that a wholly-owned Government company, TANGOLD Limited, had been formed and assumed all Meremeta company assets, including the Buhemba Gold Mine.

Investigations by THISDAY established that the BoT then paid another $13.34m (approx. 17bn/-) to TANGOLD through an account at the National Bank of Commerce Limited’s Corporate Branch in Dar es Salaam.

TANGOLD was initially registered in Mauritius - also as an offshore company - in April 2005, with its official address listed as Suite 520, Barkly Whart, Le Caudan Waterfront, Port Louis.

In February 2006, the company was registered in Tanzania with its listed local shareholders including the then BoT governor Daudi Ballali (now deceased); the then Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge; and the then permanent secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja.

Other TANGOLD shareholders are the current PS in the Ministry of Home Affairs, Patrick Rutabanzibwa; and a retired permanent secretary from the Prime Minister’s Office, Vincent Mrisho.

Although the Ministry of Energy and Minerals claimed that TANGOLD was 100 per cent owned by the Government, it has never been explained why the company was originally registered in Mauritius and not Tanzania, and why its articles of association allow the listed shareholders to transfer all or part of their shares to their own next of kin.

TANGOLD is also not listed at the Treasury Registry among companies partly or wholly-owned by the Government, and has thus not been subjected to statutory auditing by the Controller and Auditor General (CAG).

The Government has controversially attempted to silence parliamentary debate on the dubious BoT payments to Meremeta by claiming that the company is a classified military project - despite evidence that the TPDF ceased involvement in the firm in 2006 when it was liquidated.
 
Mkuu siku hizi wanajitangaza kabisa tena waziwazi si sawa na zamani ilikuwa siri. Unakutana na mtu bar mnapata kinywaji na katika kutambulisha anakwambia kabisa mimi ni usalama wa taifa.
Yea, hata waliopo reception nao wanajitafutia ujiko
 
Hivi USALAMA wa taifa ni nani na nini kazi yao?? hata mtaani wanatishia watu, hata siku akikukwaruza na gari kwenye foleni mkwara unapigwa kuliko wa mwanajeshi na unaambiwa njoo st. peters saa flani tupange namana ya kutengeneza gari yako....mimi nafanya kazi ofisi za upande wa chini pale....maofisini nako kuna mabosi wanatishia watu wanawatukana na kudai hamnifanyi chochote ukiuliza unaambiwa aah huyu system kaweka hapa kwa maslahi ya usalama wa taifa...da! mbona huu sio usalama wenyewe??

If at all this is true basi kuna tatizo katika monitoring na evaluation ya hiyo institution. Itakuwa inashangaza kwa mtu anetakiwa kuwa na core values za usalama aka potray habits ambazo zina pingana na hizo values. Any way I know nothing about the institution and have never had any encounter with these people; lakini nadhani kunaumuhimu wa ku impert values za kiuzalendo kwa kila raia ili pamoja na kuwa na defined group pia mere citizens need also to have core values zitakazo tu identify kama taifa na pia kusaidia kulinda usalama wa Taifa letu.

Zamani nadhani JKT, chipukizi zilikuwa zinasaidia I wonder hawa raia wa kesho ambao ni watoto hizo values watazipata wapi. Naona tunakoelekea kutakuwa hakuna core values kwa watanzania, social institutions zetu zina matatizo mengi na badala ya kuleta unit through impertation of core values zina leta divisions amongst raia wa nchi hii. Baada ya vyama vingi kuingia na kuondoa chama kushika hatamu, JKT, chipukizi na siasa ya ujamaa na kujitegemea kama ideology ya taifa in practice kudorora kumekuwa na vacume; na hivyo tume bakiwa na kiswahili tu kama kitu kinacho tuleta pamoja kama taifa na kidogo bado nguvu ya CCM kama chama inasaidia hii unit ambayo ukiiangalia kwa darubini ni tete sana. Any external influence will render our country into shumbles.

I think we need to be serious with the future of our country. Maana sasa hivi ile nidhamu ya kitaifa na uzalendo vina yeyuka taratibu na tabia ya kutunishiana misuli depending on which position one occupies in a society inachomoza taratibu na ghafla tutaanza kuona mashindano dhidi ya wenye 'V' (msuli) kubwa ili atakae shinda aheshimiwe jambo ambalo si rahisi hata kidogo unless kuwe na dictator au mafia na si deomocracy.

God be with us and never let this happen to our beloved country.
 
Nazani Tanzania tunahitaji chombo cha kutufikishia ujumbe kwa serikali, na chombo hichi lazima kitambulike, kiheshimike,na kisifungamane na upande wowote wa kisiasa...naelewa tuna magazeti, Vijarida,radio, TV, NGOs lakni mimi bado naona haitoshi...lazime ifike hatua tuamue kuwa na kitu zaidi ya hivi ile iwe rahisi kumobilize wananchi wanaokerwa na siasa, uongozi, uozo katika serikali hii, serikali imefika hatua imezarau kabisa wananchi, kama vile wao ni mitume na nchi hii ni yao peke yao...
kuongea pekee kwenye mitandao hakutoshi...inatakiwa tujenge network ambayo itahakikisha tunabadilisha sula ya uongozi wa nchi 2010 kwa kuwa na chombo huru,chenye sauti moja, tukishindwa tukubaliane na moja ya vyama vya siasa tena kwa MoU, tukisupport na tukitumie kufanikisha lengo...leo hii wanaokerwa na mambo ya serikali ni wengi sana, lakini je vilio vyao vinasikika???? je tukitaka tuandamane tunawamobilize vipi watu??? ukiacha Zito ambaye ID ake iko wazi, wengi wetu ID zetu ni hidden, kwa hiyo hata uwe na mtazamo gani, bado hatutafanikiwa kiushabiki...ni wakati wa kutoka sasa na kuonyesha mstari...je JF inafikia wangapi??? je tunajuana wote??? ukiacha kutuma thread zetu na replies...tunasaidiaje jamii?? tuna watu wanatuma hoja zenye nguvu na wachambuzi makini tena wengine wanamitandao...is this all....je ukishatuma thread hapa ndio basi???

mtazamo wangu tu...idumu JF
 
Yea, hata waliopo reception nao wanajitafutia ujiko
Kama kuna watu wanafanya hivyo, basi imekuwa kazi isiyo na heshima tena.Wakati wa utawala uliopita my perception about usalama was very negative. Na hii ilitokana na yale niliyokuwa nayaona ya kupenda misifa kwa baadhi ya wahusika waliokuwa wanafanya hiyo kazi.Nafikiri mentality ya baadhi ya wafanyakazi ya kutaka waonekane tofauti haina tija kwa institution yenyewe.Wenzetu wengi duniani wanatumia inteligence zao kuhakikisha they safeguard their interest in then world affairs interms of technology, power, economy etc. Imefika sehemu sasa tuanze kutumia watu hawa kuhakikisha tuna usalama wa kuaminika na tuna information zenye uhakika kwenye mambo mengine ya kuchumi, technologia na biashara.
Kwa mfano, leo hii ni ngumu kwa mkulima kujikwamua kiuchumi hata kama mazao yake yana faida kubwa kwenye masoko ya nje. Hii inatokana na sababu kuwa wakulima wengi wanategemea mawakala wenye uchu wa kujitajirisha na kuwanyonya wakulima na hawana information za kutosha za masoko ya mazao yao. Hawa jamaa wangekuwa ndio our first hand information kwa sababu wako sehemu nyingi tofauti ingawa sijui hasa wanafanya nini. Hata ununuzi wa kitu kama radar, kusingekuwa na haja ya kuwa na wakala uchwara kama tungejipanga vizuri kuwatumia watu hawa. Mbona Israel, Iran etc wanafanya? Kwa mfano, Iran inawezekana kabisa wana silaha nyingi zilizotengenezwa Marekani ingawa kuna embargo.
Pengine ni wakati muafaka wa kuwa waangalifu tena na kufanya vetting sahihi ya nani anastahili aingie kwenye hii institution.Isije ikawa ni sehemu ya kuajiri marafiki au ndugu waliokosa ajira bila kutazama uwezo wao na kujiuliza what value they guys would add to the institution.
 
Chonde Waziri Mkuu,

Liambie taifa ukweli wote kuhusu Meremeta zote mbili na kwanini ilikuwa ni lazima kuitengeneza kampuni hiyo. Liambie taifa juu ya wahusika wake na jinsi gani walitajirika kwa kupitia kampuni hiyo; liambie taifa kwanini Jeshi lilijiingiza kwenye biashara ya kuchimba madini kama front ya kile "kingine" walichotaka kufanya; liambie taifa ukweli wote.

Ndiyo, taifa linaweza kutikisika na wengine wanaweza kuishia kutiwa pingu na hasa wale ambao ni makada wenu wazuri wa CCM na maafande wenye nyota. Liambieni taifa ukweli kwani linastahili hivyo kutoka kwa watawala wake. Msipinde maneno sana na msiwatishe watu kwa kusema "usalama wa taifa".

Kama ni suala la usalama wa taifa basi waambieni wenye taifa hilo ni jinsi gani kuchimba madini kwa hasara ya mabilioni kulilinda taifa hilo. Waambieni ni jinsi gani kurithishana hisa za kampuni ya serikali kwenye familia ni kulinda usalama wa taifa; waambieni ni jinsi gani kupeana misamaha ya kodi ya magurudumu n.k kwa Meremeta kulilinda usalama wa taifa; waambieni wenye nchi yao ni kwanini MEREMETA NI SEHEMU YA USALAMA WA TAIFA!

Ndiyo, hata kama hamuwezi kufanya hivyo "hadharani" basi waambieni wawakilishi wa wananchi hao, msiwafiche!

Si mnakumbuka Iranian-Contra? Si mnakumbuka hadi aliyekuwa Waziri wa Ulinzi alikutwa na hatia na wengine 13 maafisa wa serikali ya Marekani kwa kufanya mambo "kwa nia njema" lakini kwa kulificha Bunge la nchi hiyo?

Hicho ndicho serikali imefanya na wabunge ovyo wamekubali ulaghai huo (namaanisha wabunge ovyo ovyo). Wabunge wamekubali serikali iwafiche mambo yanayohusu taifa hili na katika upotofu wa mawazo yao wanampiga mkwara mbunge mwingine yeyote yule kulileta jambo hili bungeni. Hawa ndiio maadui wa usalama wa taifa letu.

Hivyo.. liambieni taifa ukweli mapema. Kama huwezi (kwa kuogopa kusulubiwa) mwache Rais Kikwete alizungumzie kwa uwazi na ukweli..

vinginevyo... vinginevyo... Litaanza kufunuliwa na magazeti mengine na Cheche litachukua msimamo mkali siku ya Ijumaa. Natafuta watu Dodoma ambao wataweza kuchapa nakala hizo za Cheche na kugawa bure kwa Wabunge.

Tunatoka kulalamika, tunaelekea kuhamasika. Kama hawataki kulijadili hadharani, watalijadili vyumbani mwao! Msitulazimishe kwa maamuizi yenu kuwa na misimamo mikali (do not force us by your horrible decisions to become radicalized!).

Hivyo mkuu chonde sana liambieni taifa ukweli, vinginevyo wengine watafanya!

Mwanakijiji!

Nakushukuru lakini kuwa mkweli ni kwamba unampigia mbuzi Ndombolo ya solo hakika hatacheza labda kama una kisu umchinge hata kama hajangalia kibla atakuwa Halal!!

Huyo Pinda aliyechaguliwa na Matonya has been a Goverment Boy all his life. Gvt's came and went mpaka imepasa yeye kuuvaa uwaziri Mkuu kwa hiyo don't expect much from him kwani anakwenda kwa remote ya JMK!!

He can't come in the open akazungumza its the other strategy ya CCM look at the poshy life ya Wakuu wa Majeshi wastaafu baada ya awamu ya Ruksa Gen. Mboma is in gold ana utajiri usiokuwa na mfano look at MAHITA the uneducated Cop turned IGP!! mwangalie Upson!!! Look at Ornel Malisa the list is long waangalie na waliokuwa chini yao!!!

Madhambi waliyofanya in collaboration with CCM fisadis watahakikisha no changes in their lifetime!!

Kwa hiyo vita ni kali hao waliojimilikisha Oysterbay yote na maghorofa yanayochipua day and night pamoja na sehemu nzuri katika miji yote watatakiwa tuwatundike !!! No surrender no way back no retreat

The list of PAPA's listed by Mengi is another short sight ya kutudanganya those few indians kama kuna nyumba za Subash si angalau kazijenga hawa wapuuzi walijigawia sasa mbaya ni yupi? Aliyepewa kiwanja na akina Lowasa akajenga au aliyepora that is where I beg to differ na Mengi by 100%
!!!
 
Mna deal na wrong guy hapa. "Mtoto wa mkulima" kishasema yupo tayari kusulubiwa lakini atendelea kukomaa tu.

Si tuliambiwa na wahenga ukitaka kuua nyoka lamba kichwa? sasa mbona mna deal na mkia?
 
Hii ndo ki-inzi alienda kufuatilia Uswisi nini? Naisubiria kwa hamu...wacha nipate kijarida changu...tehehehe. Raha Kweli!!!
 
Chonde Waziri Mkuu,

Liambie taifa ukweli wote kuhusu Meremeta zote mbili na kwanini ilikuwa ni lazima kuitengeneza kampuni hiyo. Liambie taifa juu ya wahusika wake na jinsi gani walitajirika kwa kupitia kampuni hiyo; liambie taifa kwanini Jeshi lilijiingiza kwenye biashara ya kuchimba madini kama front ya kile "kingine" walichotaka kufanya; liambie taifa ukweli wote.

Ndiyo, taifa linaweza kutikisika na wengine wanaweza kuishia kutiwa pingu na hasa wale ambao ni makada wenu wazuri wa CCM na maafande wenye nyota. Liambieni taifa ukweli kwani linastahili hivyo kutoka kwa watawala wake. Msipinde maneno sana na msiwatishe watu kwa kusema "usalama wa taifa".

Kama ni suala la usalama wa taifa basi waambieni wenye taifa hilo ni jinsi gani kuchimba madini kwa hasara ya mabilioni kulilinda taifa hilo. Waambieni ni jinsi gani kurithishana hisa za kampuni ya serikali kwenye familia ni kulinda usalama wa taifa; waambieni ni jinsi gani kupeana misamaha ya kodi ya magurudumu n.k kwa Meremeta kulilinda usalama wa taifa; waambieni wenye nchi yao ni kwanini MEREMETA NI SEHEMU YA USALAMA WA TAIFA!

Ndiyo, hata kama hamuwezi kufanya hivyo "hadharani" basi waambieni wawakilishi wa wananchi hao, msiwafiche!

Si mnakumbuka Iranian-Contra? Si mnakumbuka hadi aliyekuwa Waziri wa Ulinzi alikutwa na hatia na wengine 13 maafisa wa serikali ya Marekani kwa kufanya mambo "kwa nia njema" lakini kwa kulificha Bunge la nchi hiyo?

Hicho ndicho serikali imefanya na wabunge ovyo wamekubali ulaghai huo (namaanisha wabunge ovyo ovyo). Wabunge wamekubali serikali iwafiche mambo yanayohusu taifa hili na katika upotofu wa mawazo yao wanampiga mkwara mbunge mwingine yeyote yule kulileta jambo hili bungeni. Hawa ndiio maadui wa usalama wa taifa letu.

Hivyo.. liambieni taifa ukweli mapema. Kama huwezi (kwa kuogopa kusulubiwa) mwache Rais Kikwete alizungumzie kwa uwazi na ukweli..

vinginevyo... vinginevyo... Litaanza kufunuliwa na magazeti mengine na Cheche litachukua msimamo mkali siku ya Ijumaa. Natafuta watu Dodoma ambao wataweza kuchapa nakala hizo za Cheche na kugawa bure kwa Wabunge.

Tunatoka kulalamika, tunaelekea kuhamasika. Kama hawataki kulijadili hadharani, watalijadili vyumbani mwao! Msitulazimishe kwa maamuizi yenu kuwa na misimamo mikali (do not force us by your horrible decisions to become radicalized!).

Hivyo mkuu chonde sana liambieni taifa ukweli, vinginevyo wengine watafanya!
Mkuu M/Kijiji,
Katika moja ya post zako wiki iliyopita uligusia kuwa tutegemee mambo makubwa jana J5 na kesho Ijumaa. Kwa nia njema kabisa ama kutoka kwako au kwa kupitia mwanajf yeyoye humu( huenda nimepitwa) ningependa nifahamishwe nini kikubwa kilitokea jana hasa hasa kuhusiana na mstakabali wa Taifa letu. Sikutoi kwenye mada yako hii ila ni vema nikajua kwamba labda hili ni moja ya makubwa ambayo ulikusudia kuyajadili. Narudia tena kwa kusema ni kwa nia njema tu ya kutaka kujua.
 
Meremeta: The details Including where its relationship with TPDF starts and ends

But surprisingly in 2006 � just a year after officially beginning gold production � the company declared itself bankrupt, and was formally dissolved.

Informed sources have confirmed to THISDAY that after the liquidation of Meremeta, both the TPDF and the South African company (Triennex) formally pulled out of gold mining activities at Buhemba.

This means that all military involvement in the Meremeta project formally ended in 2006, when the company was declared bankrupt.

Official Government records show that as Meremeta Ltd was winding up its operations prior to liquidation, the BoT paid more than $118m (approx. 154bn/-) to Nedcor Trade Services Limited, a financial services company registered in Mauritius, to offset a guaranteed loan it (the company) had extended to Meremeta.

The central bank raised the funds to pay off the loan to Meremeta through a controversial 155bn/- Treasury bond, in a transaction that later raised serious queries from auditors.

Following the liquidation of Meremeta Ltd, the Ministry of Energy and Minerals announced in Parliament that a wholly-owned Government company, TANGOLD Limited, had been formed and assumed all Meremeta company assets, including the Buhemba Gold Mine.

Investigations by THISDAY established that the BoT then paid another $13.34m (approx. 17bn/-) to TANGOLD through an account at the National Bank of Commerce Limited's Corporate Branch in Dar es Salaam.

TANGOLD was initially registered in Mauritius - also as an offshore company - in April 2005, with its official address listed as Suite 520, Barkly Whart, Le Caudan Waterfront, Port Louis.

In February 2006, the company was registered in Tanzania with its listed local shareholders including the then BoT governor Daudi Ballali (now deceased); the then Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge; and the then permanent secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja.

Other TANGOLD shareholders are the current PS in the Ministry of Home Affairs, Patrick Rutabanzibwa; and a retired permanent secretary from the Prime Minister's Office, Vincent Mrisho.

Although the Ministry of Energy and Minerals claimed that TANGOLD was 100 per cent owned by the Government, it has never been explained why the company was originally registered in Mauritius and not Tanzania, and why its articles of association allow the listed shareholders to transfer all or part of their shares to their own next of kin.

TANGOLD is also not listed at the Treasury Registry among companies partly or wholly-owned by the Government, and has thus not been subjected to statutory auditing by the Controller and Auditor General (CAG).

The Government has controversially attempted to silence parliamentary debate on the dubious BoT payments to Meremeta by claiming that the company is a classified military project - despite evidence that the TPDF ceased involvement in the firm in 2006 when it was liquidated.
This is all that need to be said.

Meremeta issue is not unspeakable in any way.

The involvement of TPDF was not clear in the records and shareholders have nothing to do with TPDF. It is said that, Meremeta (not TPDF) joined forces with TPDF in gold mining. This means that, TPDF was doing mining with Meremeta as separate entities aiming at one goal (kind of confusing).

Is it right to say, that TPDF's involvement in Meremeta's operations was simply managerial than ownership? How many percent did TPDF inject/own in Meremeta? How much was TPDF's shares in Meremeta? How does the issue of National security got to do with this kind of business (that aimed at raising funds for purchasing army vehicles)?

And TANGOLD? Common guys, we are taken for a ride.
 
Mbona taifa lenyewe halipo salama kama kuna idara ya 'usalama wa taifa?'. Watu wanawaweka vihiyo kwenye idara nyeti kama hiyo ya inteligensia afu unategemea taifa liwe salama? No. Noooooooooooooooo!
Kukubali hili, labda ubongo wangu ubadilike kuwa kamasi.
 
Back
Top Bottom