Ujumbe wa wazi kwa Pinda! -chonde ..fanya vinginevyo pisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa wazi kwa Pinda! -chonde ..fanya vinginevyo pisha!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 24, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Chonde Waziri Mkuu,

  Liambie taifa ukweli wote kuhusu Meremeta zote mbili na kwanini ilikuwa ni lazima kuitengeneza kampuni hiyo. Liambie taifa juu ya wahusika wake na jinsi gani walitajirika kwa kupitia kampuni hiyo; liambie taifa kwanini Jeshi lilijiingiza kwenye biashara ya kuchimba madini kama front ya kile "kingine" walichotaka kufanya; liambie taifa ukweli wote.

  Ndiyo, taifa linaweza kutikisika na wengine wanaweza kuishia kutiwa pingu na hasa wale ambao ni makada wenu wazuri wa CCM na maafande wenye nyota. Liambieni taifa ukweli kwani linastahili hivyo kutoka kwa watawala wake. Msipinde maneno sana na msiwatishe watu kwa kusema "usalama wa taifa".

  Kama ni suala la usalama wa taifa basi waambieni wenye taifa hilo ni jinsi gani kuchimba madini kwa hasara ya mabilioni kulilinda taifa hilo. Waambieni ni jinsi gani kurithishana hisa za kampuni ya serikali kwenye familia ni kulinda usalama wa taifa; waambieni ni jinsi gani kupeana misamaha ya kodi ya magurudumu n.k kwa Meremeta kulilinda usalama wa taifa; waambieni wenye nchi yao ni kwanini MEREMETA NI SEHEMU YA USALAMA WA TAIFA!

  Ndiyo, hata kama hamuwezi kufanya hivyo "hadharani" basi waambieni wawakilishi wa wananchi hao, msiwafiche!

  Si mnakumbuka Iranian-Contra? Si mnakumbuka hadi aliyekuwa Waziri wa Ulinzi alikutwa na hatia na wengine 13 maafisa wa serikali ya Marekani kwa kufanya mambo "kwa nia njema" lakini kwa kulificha Bunge la nchi hiyo?

  Hicho ndicho serikali imefanya na wabunge ovyo wamekubali ulaghai huo (namaanisha wabunge ovyo ovyo). Wabunge wamekubali serikali iwafiche mambo yanayohusu taifa hili na katika upotofu wa mawazo yao wanampiga mkwara mbunge mwingine yeyote yule kulileta jambo hili bungeni. Hawa ndiio maadui wa usalama wa taifa letu.

  Hivyo.. liambieni taifa ukweli mapema. Kama huwezi (kwa kuogopa kusulubiwa) mwache Rais Kikwete alizungumzie kwa uwazi na ukweli..

  vinginevyo... vinginevyo... Litaanza kufunuliwa na magazeti mengine na Cheche litachukua msimamo mkali siku ya Ijumaa. Natafuta watu Dodoma ambao wataweza kuchapa nakala hizo za Cheche na kugawa bure kwa Wabunge.

  Tunatoka kulalamika, tunaelekea kuhamasika. Kama hawataki kulijadili hadharani, watalijadili vyumbani mwao! Msitulazimishe kwa maamuizi yenu kuwa na misimamo mikali (do not force us by your horrible decisions to become radicalized!).

  Hivyo mkuu chonde sana liambieni taifa ukweli, vinginevyo wengine watafanya!
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Juzi Chiluba kasimamishwa mahakamani kama "a common thief". katika vitu alivyosifiwa Levi Mwanawasa (Chiluba's successor) ni jinsi alivyokataa kuitumia hii trump card ya "usalama wa taifa" ili kumkingia kifua Chiluba.

  Tunaona increasingly katika nchi za kiafrika hususan, kwamba hili suala la "usalama wa taifa" linatumika kwa ajili ya maslahi ya wachache.

  Haya mambo ya kusema "usalama wa taifa" yanaibua maswali mengi kuliko majibu, watu tutajiuliza maswali yatakayohatarisha usalama wa taifa kuliko majibu halisi, they are only making it worse.Tutajiuliza, jeshi lilitishia kupindua nchi kama halitapewa "a piece of the pie" in Meremeta? Au ulikuwa ni mpango wa kuiba mali ya umma kwa mwamvuli wa jeshi tu?

  Hawa watu wamekula mpaka sasa wanashindwa kula na kipofu, wamemgusa mkono, kipofu ansstuka, sasa wanakimbilia kusema "Usalama wa taifa".
   
  Last edited: Jun 24, 2009
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Katika hili tutavunja miiko yote iliyomo katika vitabu vyao. Jeshi ni la Wananchi wa Tanzania na siyo la CCM, la Rais, na wala siyo la Serikali. Litaendelea hivyo na jaribio lolote la kulihamisha jeshi toka mikono ya wananchi litakumbana na upinzani ambao haujawahi kutokea. Tukiliachilia jeshi mikononi mwa kikundi cha watu wachache tutakuwa tumesalimisha milele uhuru wetu mikononi mwa mafisadi.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mkuu mkjj,
  uwaziri mkuu wa mh PINDA ni 'plan B',remember?unadhani pinda anaweza kuyafanya tunayoyahitaji wanaharakati?

  mi nadhani fanyaa mchakato wa nakala nyingi huko dodoma,
  mimi kila ijumaa ofisini natoa zangu kumi naamsha cheche za fikra kwa collins wangu
   
 5. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Sitaki kusema mengi.Sawa yawezekana ni kweli meremeta iliwameremetesha wachache lakini swali la kujiuliza ni kwa nini hili limekua gumu kuzungumzwa?lingekua rahisi hivyo basi kwa hii 'jambajamba' wanayotiwa viongozi naamini hata kiduchu kingesemwa
   
 6. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wana kiburi na ubinafsi na ujinga pia hawa viongozi wetu. wizi mtupu.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ugumu wa hili umenikumbusha swala la wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya!list ya wahusika ilikuwepo,ila ilikuwa inapigwa danadana!baadae yule mkuu wa mkoa hapa jijini kipindi kile akaongea 'NIPENI HIYO LISTI MIMI NITAWATAJAAAAA'

  watu wakampelekea,AKAFYATA!KIMYAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.

  mambo haya bwana
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hadi hivi sasa hakuna jambajamba yoyote.. kwa kadiri ya kwamba wabunge wa CCM wako kitanda kimoja na serikali wanajua gharama ya kuliibua hilo.
   
 9. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh, nani mke hapo?
   
 10. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jamani samahani kwa kuwa mkweli. Bila shaka sasa tumefika sehemu inabidi tuchapane bakora ili kuweka mambo sawa. Upuuzi umezidi na unakera.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mwanakijiji usimtegemee pinda kuwa na ujasiri wa aian hiyo. he is just a pawn kwa serikali. ikiwa serikali haitaki patajwe kitu, pinda hawezi kutaja
  pinda kaona nyota ya jaha kwa kuwekwa uwaziri mkuu, usidhani kama anaweza kuchezea bahati kiasi hicho na usidhani kama hajui kuwa yupo pale kibahati tu
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni kawaida ya CCM kufanya wizi eti ni usalama wa taifa. Wasidhani hatujui, mtu wa kwanza kutiwa pingu kama tukiwa makini ni Gen. Robert mboma na mkapa atafuta na hatimaye wengine wengi. ndo maana hata uchaguzi wa mbeya vijijini aliombwa akae kando make mambo yangeanza kubumbuluka...

  jamani waTZ tumechoka.....
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  pointi yangu hii ni kama ilivyokuwa kwa Lowassa.. kama kiongozi wa serikali unajua uovu umetendeka na unashindwa kusimamia haki kwa kuogopa basi ujiuzulu. Kama Pinda ni mwadilifu kama tulivyoambiwa wakati ule basi anayo budi kusema ukweli juu ya hili. Kama hawezi au hataki basi akae pembeni.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani kwe wenye taarifa sahihi juu ya MEREMETA, TANGOLD na MWANANCHI watusaidie tuziweke kwenye magazeti na sehemu mbali mabli ili wananchi wengi waelewe.

  Haiingii akilini unasema eti "meremeta" haiwezi kujadiliwa inahusu usalama wa taifa...? wizi mtupu..!!! Hata samwei sitta haaminiki kwa sababu naye anatetea wizi tu, kwa nini utawala wa TZ usiige angalau 30% ya mambo aliyo acha amefanya Levi Mwanawasa??

  Viongozi wa CCM huwa wanadhani eti kama si wao basi nchi haiwezi kuwepo...!! huo ni upumbafu. Na nasema liwalo na liwe wenye kuchukua hatua chukueni "Bunge la tanzania ni la ovyo ovyo!!" na kama sitta anabisha aruhusu meremeta na wenzake wajadiliwe!!!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Walioko nyumbani wasikose kusoma magazeti ya This Day na Kulikoni ya leo Alhamisi.. na Ijumaa mtusome sisi wengine..
   
 16. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hivi USALAMA wa taifa ni nani na nini kazi yao?? hata mtaani wanatishia watu, hata siku akikukwaruza na gari kwenye foleni mkwara unapigwa kuliko wa mwanajeshi na unaambiwa njoo st. peters saa flani tupange namana ya kutengeneza gari yako....mimi nafanya kazi ofisi za upande wa chini pale....maofisini nako kuna mabosi wanatishia watu wanawatukana na kudai hamnifanyi chochote ukiuliza unaambiwa aah huyu system kaweka hapa kwa maslahi ya usalama wa taifa...da! mbona huu sio usalama wenyewe??
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Watu wanaojitangaza kuwa ni usalama wa taifa, siyo usalama wa taifa. Period.
   
 18. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  ETI usalama wa taifa! Meremeta iwe sehemu ya usalama wa taifa!!!!! kuna nini cha kiusalama kwa Jeshi la wananchi kumiliki Meremeta? nijuavyo mimi Jeshi la wananchi ni kwa ajili ya usalama wa nchi kutokana na uvamizi na nchi nyingine ( maana usalama wa ndani wapo polisi na mashushu). hivi Idi Amini amerudi tena? kama hajarudi, Tanzania maadui zetu ambao wanatishia usalama wa nchi yetu kwa sasa ni nchi gani? na tuna ugomvi gani nao?Hivi tuna nchi katika zinazotuzunguka au za mbali zinazotaka kutuvamia? Je wanajeshi wa vyeo vya kati na wa chini kabisa ambao ndiyo wapiganaji wameambiwa kuwa wajiandae kupigana na hao maadui? Hii mnayosema ni siri ni siri kwa ajili ya nani kama hao wanaotakiwa kulindwa/ kuhakikishiwa usalama hawajui wanalindwaje? hii ni ajabu chini ya jua - mlindwa hatakiwa kujua undani wa usalama wake ila Vithlan na kampuni ya BAE ndiyo wanaruhusiwa kujua hizo siri kwa sababu za kifisadi?
  PINDA NA WENZAKO MJUE WATANZANIA SIYO MABWEGE TENA. IPO SIKU MTASEMA UKWELI MPENDE MSIPENDE.
  Ukipatwa na haja unaweza kujichelewesha kwenda msalani kwa muda lakini itafika muda upende usipende utakwenda tu.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Upande mmoja ninaelewa kuwa kufunua hili kutaitikisa nchi lakini kutolifunua nafikiri kunaitikisa zaidi
   
 20. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu siku hizi wanajitangaza kabisa tena waziwazi si sawa na zamani ilikuwa siri. Unakutana na mtu bar mnapata kinywaji na katika kutambulisha anakwambia kabisa mimi ni usalama wa taifa.
   
Loading...