Ujumbe wa wazi kwa Mhe. Edward Lowassa: Uchaguzi ni wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa wazi kwa Mhe. Edward Lowassa: Uchaguzi ni wako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 27, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]UJUMBE WA WAZI KWA MHE. EDWARD LOWASSA: “Uchaguzi ni wako”[/FONT]
  [FONT=&quot]Na. M. M. Mwanakijiji[/FONT]


  [​IMG]

  Endapo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa (CCM-Monduli) ataendelea na mwelekeo wake wa sasa wa kisiasa na mahusiano yake ya sasa ya kimkakati basi njozi zake za kuja kushiriki tena katika uongozi wa juu wa taifa letu zitakuwa zimefikia ukingoni bila kupiga kelele ya breki. Na endapo nitakachoandika hapa hatakipa uzito wake unaostahili naomba niwe wa kwanza kutanguliza habari mbaya kwake na wale wanaomuunga mkono kuwa atashindwa. He will lose.

  Ninaandika kwa sababu kubwa tatu; kwanza ni kwa sababu ninaamini anapoteza muda kwa kuendelea na machungu ya matukio ya mwaka jana; pili, anapoteza kipaji chake cha uongozi kwa kukaa pembeni ya mijadala ya kitaifa na hivyo kuonekana yuko upande kinyume na maslahi ya taifa na tatu, ni kwa sababu naamini hakuna mtu mwingine anayeweza kumuambia kile nitakachomuambia hapa kwa heshima na taadhima kubwa. Wengine aidha wanamuonea soni, wanamuogopa au kwa namna fulani wanagwaya mbele yake.


  Inaendelea katika attachment...

  Nimeonelea nijitafsiri mwenyewe maana watu wengine wanatafsiri zaidi ya kile nilichosema.

  a. Lowassa anawajibika kwa kujiuzulu kwake Uwaziri Mkuu. Hana wa kumlaumu.

  b. Amechagua upande usio sahihi baada ya kuachia ngazi.

  c. Hawezi kurudi kwenye uongozi wa kitaifa na hivyo ni bora aendelee kukaa upande huo mwingine. It is too costly.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Duh!
  Huo ni ujumbe wa ushauri au ni ujumbe wa kumtisha? Naona kila aya umemalizia kuwa atashindwa iwapo atasita kufuata ushauri wako. Unaamini vipi kuwa ushauri wako ndio sahihi kwa hatima yake kisiasa?

  Uwamuzi wake wa kukaa kimya na kutoshiriki katika mijadala una nafuu au una tatizo gani na hatima yake kisiasa. Inaonekana pengine unajua mengi sana juu ya mipango ya baadae ya Lowassa kiasi cha kuona kuwa sasa anajichimbia kaburi kwa kukaa kimya tu katika siasa za kitaifa.

  Baada ya kujiuzulu Uwaziri Mkuu, Jamii nzima ilikubali kuwa Lowassa ni fisadi, leo hii unashindwa kukiri kuwa u miongoni mwa wale ambao mnasema kuwa ni fisadi? Atasimama vipi kupinga ufisadi ilhali yeye ni fisadi? Naona unajaribu kusema kuwa Lowassa sio fisadi iwapo tu atasimama na kushiriki katika mapambano dhidi ya ufisadi. Je ile dhana ya awali kuwa yeye ni fisadi imepotelea wapi?

  Umedhihaki hatua yake ya kujieleza alipotumia TBC, kwamba haikuwa sahihi. Huku anakubaliana nae kuwa ripoti ya Mwakyembe haikumtaja mojamoja kuwa alishiriki katika ufisadi. Sasa hauoni kuwa hatua aliyoichukua ya kuamua kuelezea yale yaliyomoyoni mwake kupitia TBC ilikuwa ni sahihi baada ya mtafuruku mkubwa Bungeni?

  Kwa ufupi naona bado unaendelea kuwandama watu wengine kupitia mgongo wa Lowassa, zaidi unataka kumuingiza Lowassa kinyamela katika migongano inayorndela sasa baina ya wafanyabiashara fulani hapa nchini.

  Nini lengo lako hasa juu ya Lowassa, Ufisadi na hatima ya Lowassa kama Mbunge?
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  Hii risala lazima ataisoma kwa vituo na tafakari kubwa.
   
 4. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Siku zote MKJJ unaongea naona kama unarukaruka tu ila kwa hili nafikiri you nailed the rock
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Lowassa ni mchafu kama alivyo mfadhili wake Rostam; kwa usalama wa nchi yetu wote wawili inafaa watoswe na ccm kama kweli chama hiki hakitaki kuwalinda mafisadi!!
   
 6. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mwana Kijiji
  Nimekusoma. Nakubaliana na hoja zako nyingi, isipokuwa maeneo machache ambayo hayakuzingatia kwa undani mambo yafuatayo:

  a) Uamuzi wa Kujiuzuru, Lowassa aliuchukua baada ya kuwasiliana uso kwa uso na JK, usiku wa kuamkia kujiuzuru, Ikulu ya Chamwino. JK alipendekeza mwenyewe huo uamuzi. haukuwa uamuzi wa Lowassa. Yeye tunamjua ni mpambanaji, na angepambana angeshinda. Alikubali ushauri wa JK kwa msingi kuwa akiandika barua ya kujiuzuru, JK atachelewesha kujibu mpaka bunge limalize kikao chake, na ndipo mikakati ifanyike ili kujua ukweli wa ripoti na namna ya kuepusha zahama ile. Baada ya kuandika barua na kumkabidhi, JK usiku wa manane alipata ushauri wa Malecela na Othman na kuamua kuikubali barua ile pasipo hata kuongea tena na Lowassa. Hapo kuna siri nzito. Ni JK peke yake ajuaye.

  b)Utabiri wa kuipangua idara ya Usalama ni wa hatari sana. Ni kweli idara hii imechanganyikiwa na Lowassa anajua hilo. Dawa yake si kuipangua maana hata walio nje ya nafasi ni hoi na wachafu kama walio ofisini. Dawa yake ni kuigandisha yote (freeze) na kuiunda kwa hatua baada ya mafunzo maalum. Baba wa taifa alifanya hivyo kwa JWTZ na hata kwa idara yenyewe baada ya mkewe kuiingilia na kuifanyisha madudu ambayo hakuyapenda. Hivi sasa JK yuko hatarini, kuongoza nchi yenye idara mbili za usalama.

  c) Uchambuzi wa Mwanakijiji, unaonyesha kuwa Lowassa anamhitaji sana JK kuliko kinyume chake. Ukweli uliopo, unaosema, unaoonekana ni kuwa JK anamhitaji sana Lowassa na watu ili awe salama katika nafasi na kazi zake. Ni mdhaifu kiafya na kiuongozi. Madaktari wamweleza afanyiwe upasuaji kumwondolea black out anazopata, lakini kwa ushauri wa watu wasio "professional" amebadili uamuzi kwa kisingizio cha kupata second opinion. Ni mwoga wa kufanya maamuzi mazito. Anahitaji kupata PM anayeweza kufanya maamuzi magumu. Na hana mwingine isipokuwa Lowassa.

  Mwisho, mengine ulosema ni ya msingi lakini ukumbuke, li nchi limegawanyika, kila mmoja anakimbia na kiti chake.
   
 7. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ahsante Mwanakijiji. Kama ningekuwa Lowassa nisingeona aibu kuitisha press conference na kukiri kuisoma barua yako na kuitafakari na kuamua kuifanyia kazi. Tatizo la viongozi wetu na watanzania kwa ujumla ni kuona aibu au kudhani kuomba radhi ni udhaifu. Hili ndilo linalomponza Mkapa sasa.

  Sijui kwa nini hawaioni logic simple kiasi hiki. Kusimama na kuwaambia watanzania "I am sorry for what i did" ni virtue ya hali ya juu sana na inaweza kumsafisha mtu yeyote hata Rostam!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katika hotuba yake kwa Bunge hakuwasiliana na Rais juu ya yeye kujiuzulu. Na believe me, JK hakumtaka ajiuzulu; JK kama wabunge wengine hawakujua Lowassa atajiuzulu vile vinginevyo Spika Sitta angejua juu ya hilo vile vile. Ninachojua ni kuwa JK alikataa kuiona ripoti ya Mwakyembe kabla.

  JK alikuwa Dodoma kwa ajili ya mkutano wa baraza la Mawaziri (soma maelezo yake mweenyewe kwa wazee wa Dar wiki chache baadaye; suala la Waziri Mkuu kujiuzulu halikuwepo). EL alifanya vile wakijua watu kama wanne tu. Yeye, mkewe na wabunge angalau wawili (Hawa nina uhakika walijua).
  ziko tatu; ya Mwang'onda (loyal to Mkapa, EL na RA), ya RO (loyal to JK), na Patriots (loyal to the standard of professionalism ya kazi ya intelligence). Njia pekee ni kuhakikisha TISS inaundwa upya baada ya mabadiliko ya sheria.

  c) Uchambuzi wa Mwanakijiji, unaonyesha kuwa Lowassa anamhitaji sana JK kuliko kinyume chake. Ukweli uliopo, unaosema, unaoonekana ni kuwa JK anamhitaji sana Lowassa na watu ili awe salama katika nafasi na kazi zake. [/quote]

  Naamini JK hamuitaji Lowassa at all, hakuna lolote ambalo EL anaweza kufanya dhidi ya JK. Hakuna. Lakini JK akiamua kumfanyizia anaweza to extreme measures. Hili ndilo the message behind mada yangu. EL na RA bado hawaliamini hili. It'll be too late when they grasp its eventual implications.

  Nadhani hapa uko sahihi sana; tulishadokeza huko nyuma juu ya suala la afya yake. Watu wengi wamekuwa wakizungumzia gonjwa lile lakini kwa karibu mwaka mzima baadhi yetu tunajua juu ya hali yake ya kiafya. Siyo blood clot. It is something more serious. I won't get into that.
   
 9. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii kali, kumbe JK ni mgonjwa. Bado nashindwa kuamini. Isije kuwa ni njama za kumuua ili waje kusingizia alikuwa mgonjwa!
   
 10. C

  Chokona Member

  #10
  May 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  As far as I am concerned.EL na RA bado nafikiri ushauri wa Mzee Ndesamburo wakati akichangia mjadala wa Richmond pale bungeni ulikuwa ushauri makini, na best solution nao sio mwingine bali wa kuwanyonga hadharani that was that, ingekuwa far east Asia EL angejiwajibisha kwa kujinyonga lakini kwa sababu pengine ni mkristo serikali ingechukua ushauri wa mzee na kumsaidia kuwanyoga hivi sijui hii huruma unayomwonea ni ya nini?
   
 11. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Katika hotuba yake kwa Bunge hakuwasiliana na Rais juu ya yeye kujiuzulu. Na believe me, JK hakumtaka ajiuzulu; JK kama wabunge wengine hawakujua Lowassa atajiuzulu vile vinginevyo Spika Sitta angejua juu ya hilo vile vile. Ninachojua ni kuwa JK alikataa kuiona ripoti ya Mwakyembe kabla.
  =============

  MwKjj nami nasema believe me waliwasiliana. EL alitaka JK aitishe kamati ya wabunge wa CCM ili kuzima maasi. JK akasema anaogopa asishtakiwe kwa kuingilia uhuru wa bunge. Ndipo akapendekeza EL aandike barua, na yeye JK atadelay jibu ili mkakati mpya utafutwe.

  Pia, JK aliona ripoti ya Mwakyembe kabla ya kwenda Dodoma. Sitta asingefanya kosa la kwenda Dodoma na Ripoti bila kumshirikisha Mkuu wa Nchi.

  ===============

  JK alikuwa Dodoma kwa ajili ya mkutano wa baraza la Mawaziri (soma maelezo yake mweenyewe kwa wazee wa Dar wiki chache baadaye; suala la Waziri Mkuu kujiuzulu halikuwepo). EL alifanya vile wakijua watu kama wanne tu. Yeye, mkewe na wabunge angalau wawili (Hawa nina uhakika walijua).
  ===============
  Ni kweli hawa wabunge walijua na waliambiwa na EL baada ya kutoka Chamwino usiku ule.

  ziko tatu; ya Mwang'onda (loyal to Mkapa, EL na RA), ya RO (loyal to JK), na Patriots (loyal to the standard of professionalism ya kazi ya intelligence). Njia pekee ni kuhakikisha TISS inaundwa upya baada ya mabadiliko ya sheria.
  ===========
  Mimi nadhani zaidi ya mabadiliko ya sheria, kuna suala la mafunzo yanayoendana na wakati tulio nao. Hii habari ya kuhesabu vizibo vya bia imepitwa na wakati.
  ===========
  Naamini JK hamuitaji Lowassa at all, hakuna lolote ambalo EL anaweza kufanya dhidi ya JK. Hakuna. Lakini JK akiamua kumfanyizia anaweza to extreme measures. Hili ndilo the message behind mada yangu. EL na RA bado hawaliamini hili. It'll be too late when they grasp its eventual implications.
  ============

  Conventionally, unachosema ni sawa, kwamba JK kashika mpini na EL makali. Lakini mimi nadhani kuna kushika mpini lakini ukawa na phobia ya kuona damu, matokeo yake ukakata vidole na kisu kikapitiliza na kukukata wewe. Scenario tuliyo nayo, JK hawezi kuwagusa akina RA na EL akawa salama. Mizengo aliwahi kulisema, akakemewa kesho yake asubuhi kwenye security briefing.
  ======

  Mwisho, tueleze uswahiba wa EL na BWM umetoka wapi na umeanza lini? Au Mwang'onda kawapatanisha!
   
 12. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bravo bravo Mz Mwanakijjiji hap umenena, keep up the fight
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tanzania ina wananchi karibuni milioni 40. Kati ya hao kuna wengi wenye vipaji vya uongozi, nia ya kuongoza na uadilifu. Sioni sababu ya mtanzania kuandika makala ndefu ya kumshauri mtu aliyejiuzuru kwa kashfa ya kukiuka maadili ya uongozi (iwe kashfa za kweli au si za kweli) eti arudi kwenye uongozi wa juu wa taifa!
  Alipewa nafasi, hakufanikiwa kuitumikia kwa kiwango kilichotarajiwa. Watanzania hamuwezi jua mwenyezi Mungu amewaepusha/amemuepusha na nini. Muda huu wa kuandika makala ndefundefu kumlilia yeye arudi ni bora ungetumika kuandika makala za kuwahimiza vijana wajitokeze kwenye harakati za kuongoza nchi na kuwaasa vijana wawe viongozi waadilifu.
  Tunahitaji watanzania wengine wapewe nafasi, walioshindwa wapumzike.


  PS: '' insane is doing the same thing again and again, and then somehow expect different results''
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  MH ana Ukimwi?

  Hii ndo asili ya Safari nyingi kwenda nje? Anakwenda kutibiwa??

  Nakumbuka mwandishi mmoja wa habari alimwuliza MH kama yeye yu mzima na hana Miwaya kama watu wasemavyo mtaani. Yeye akajibu afya yake ni Swano.

  Wait a minute!

  Hivi mimi na wewe tukivua majina yetu haya ya JF na kuvaa yale yaliyoyetu na kuulizwa sawali kuhusu afya zetu, acha ukimwi swali kama mwenzetu umegonga jiwe?
  Kuna mtu atakuwa na hamu ya kueleza ukweli??

  Sijui ni waTZ wangapi wagonjwa wako tayari kukiri wana Ukimwi???
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  May 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ndiyo maana kuna kitu kinaitwa uhuru wa mawazo. Kama wewe unaona makala ya kuhimiza vijana wajitokeze.. andika makala hiyo. Kinakushinda kitu gani?
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Aisee, nimeandika nyingi kweli na naendelea kuandika.
  Hakuna kinachonishinda.
  Ni vyema tukachagua direction muafaka katika kile tunachokiita harakati.
  Cheers...
   
 17. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  =====

  Siku ukiwa huru katika uandishi na uchambuzi hata vipofu watajua kuwa kuna uhuru umetolewa hatimaye!
   
 18. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Leo hii hatutaki kuongelea mambo yaliopita kwa kujwa mimi ninaamini kuwa historia ndio itakuja kusema ukweli juu ya tukio zima la lowasa na jinsi ambavyo ninaamini kuwa hakutendewa haki.........kimsingi anachojaribu kusema Mwkjj ni kuwa Lowasa anaendeleza mkakati fulani na hapo hapo yuko kimya,huu ni wazi kuwa ni uzushi kabisa na inawezekana kuwa wewe ni kati ya wale wanaoogopa vivuli vyao wenyewe,Hamjiamini na ukimya wa Lowasa ametulia na sasa mnamtafuta ili aongee,Lowasa hawezi kuongea kwa kuwa mwanakijiji kasema na kamwe mwkk hana moral authority ya kumchagulia lowasa marafiki....mwacheni Lowasa afanye kazi zzake za jimbo,mwacheni awahudumie wale waliomchagua kwa hiari yao wana wa monduli,mnachojaribu kufanya hapa ni kutafuta namna ya kuficha mapungufu yenu,tangu ametoka mambo mengi yamesimama na Pinda kashindwa kuvaa viatu vya Lowassa.ni aibu kwa wote mlioshangilia mzee wa Mipasho Mwakiembe akibwabwaja hovyo,ni aibu kwa wazandiki wote wa tanzania na ni aibu kwa serikali nzima ya jk inayoshindwa kusimamia na kutimiza malengo waliowaahidi watanzania.
   
 19. Z

  Zahir Salim Member

  #19
  May 27, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi tunasubiri nini sisi Watanzania kuongozwa na Serikali mbovu ya aina hii iliopo Madarakani? hivi hili JESHI limelala kiasi hiki Linashindwa Kuchukuwa Madarakaaaaaaa.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Siku hiyo imepita miaka 15 iliyopita.
  Huo ndio uhalisia wa mambo.
   
Loading...