UJUMBE wa SMS wa Lema kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Ndg. Mkuu wa Mkoa,
Watu wanapigwa na kuonewa sana Daraja Mbili, na huku wakijigamba kuwa wewe na Mkuu wa Wilaya umewahakikishia usalama wao hawa wahuni, jambo ambalo nisingependa kuamini mapema, ila ujasiri wao na ukaidi wao unaweza kuleta hakika kidogo.
Nelson Mandela alisema, kumnyanyasa mtu hakumfanyi mtu kuwa dhaifu bali humfanya mtu kutafuta njia za kujitetea, hivyo basi tazama uchaguzi kwa jicho la haki na Mungu ndipo amani itakapostawi katika taifa letu, ni hatari kuwajengea watu hofu na mashaka eti dola inaweza kuiba kura na kuonea watu wakati wa uchaguzi.
Hekima ya uongozi ni kupigania haki, usawa na utu.
Tumejipanga kulinda utu wetu na haki zetu na Mungu atusaidie.
Tutakuwa tayari hata kufa kwa ajili ya haki. Ushauri wangu kwako siyo CCM kushinda uchaguzi, bali haki kushinda katika Uchaguzi.

Godbless Lema
 
Hawa mawakala wa CCM wanaoitwa wakuu wa mikoa na wilaya wanakera sana, lakini wajue mwisho wao unakaribia under chadema regime.
 
Lowasa ameapa kulirudisha jimbo la Arusha mjini.Akifanikiwa hapo Urais anajisafishia njia
 
Sikubaliani na upuuzi huu uliofanywa na wahuni wa CCM.

602509_186090904861251_856235684_n.jpg
 
Lowasa ameapa kulirudisha jimbo la Arusha mjini.Akifanikiwa hapo Urais anajisafishia njia
Alishindwa kule kwao na ukweni Arumeru Mashariki, ataweza Arusha mjini?

Na kesho tunamnyoa mvi zote na kubaki kipara hapa Daraja Mbili.
 
Usishangae wakaua mtu halafu waseme ujumbe wa Lema ndo umechangia mtu kuuawa, kama walivyosema juu ya ujumbe wa Dr Slaa na kifo cha Mwangosi.
 
Kuna msemo usemao kuwa " ushikwapo shikamana". Wananchi wa daraja mbili wanatakiwa kuwapa kichapo hao magamba wachache iwapo magamba wamewachokoza. Aluta continua...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom