Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
UJUMBE WA MUNGU KWA LISU NA MAGUFULI
Na, Robert Heriel
ZINGATIA; Maneno yaliyowekolezwa (Bolded word)
Ama kwa hakika hakuna kazi ngumu kwa binadamu kama kusema ukweli na kutenda kwa haki. Haya nimeyaona kwa macho yangu, na kuyashuhudia mimi mwenyewe wala sio kwa kuhadithiwa.
Je ni nani awezaye kusimama mbele ya wakuu na kusema ukweli, Ni nani asiyeogopa kumuonya mwenye mamlaka. Ama ni nani awezaye kuutazama uso wa Mtawala na kumkaripia pale atelezapo na kufanya kwa uovu.
Basi mimi Taikon hali nikijua hatari inayoweza kunikabili, nikajitia ujasiri, nami nikaapa kwa jina la Mungu wangu kutetea haki, tena nikasema; nitasema ukweli pasipokuogopa uso wa mtu. Hata hivyo sikusahau kuomba hekima kwa Mungu, kwa maana kumuonya Mfalme yahitaji hekima, tena kumkaripia Mtawala yahitaji busara na kujitoa kwa dhati.
Basi ikiwa nilikengeuka kwa tamaa zangu, tena ubinafsi uliniendesha, hata nikampendelea mtawala muovu, nikashindwa kusema iliyo kweli na kumkemea, basi Mungu atanihukumu.
Tupo katika uchaguzi, ni baina ya Mzee wangu Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli na Kaka yangu Mhe. Tundu Antipas Lisu. Wote ninawaheshimu katika haki, wema na uadilifu. Wote ni ndugu zangu katika nchi hii. Jambo moja la muhimu kwa yeyote atakayechaguliwa bila kujali mimi nimemchagua nani, kwanza nitamuunga mkono kwa yaliyomema, haki na uadilifu. Lakini kwa mabaya nitamkosoa, kumkemea, na kumkaripia. Nafahamu ugumu wa kumuonya Mtawala, lakini kwa vile sio kwa nia mbaya basi nitafanya.
Leo nitawapa ujumbe wa Mungu kutoka katika Kitabu cha Yeremia; Naomba kunukuu
YEREMIA 22;
1Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nenda katika ikulu ya mfalme wa Yuda, uwape watu ujumbe huu: 2Wewe mfalme wa Yuda unayekikalia kiti cha enzi cha mfalme Daudi, pamoja na watumishi wako na watu wako wanaopita katika malango haya, sikilizeni neno langu mimi Mwenyezi-Mungu.
3. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tendeni mambo ya haki na uadilifu. Mwokoeni mikononi mwa mdhalimu mtu yeyote aliyenyanganywa mali zake. Msiwatendee vibaya au ukatili wageni, yatima na wajane wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa.
4. Kama mkishika neno hili nililowaambia basi, wafalme wanaokikalia kiti cha enzi cha Daudi wataendelea kuingia kwa kupitia malango ya ikulu hii. Watapita pamoja na watumishi wao na watu wao, wakiwa wamepanda farasi na magari ya farasi. 5Lakini kama hamtatii maneno haya, mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwa nafsi yangu kwamba mahali hapa patakuwa magofu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
6. Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu ikulu ya mfalme wa Yuda:
“Ingawa waonekana kuwa mzuri kama nchi ya Gileadi
kama kilele cha Lebanoni,
Lakini naapa kuwa nitakufanya uwe jangwa,
uwe mji usiokaliwa na watu.
7Nitawatayarisha waangamizi dhidi yako,
kila mmoja na silaha yake mkononi.
Wataikata mierezi yako mizuri,
na kuitumbukiza motoni.
8“Kisha watu wengi wa mataifa watapita karibu na mji huu, na kila mmoja atamwuliza mwenzake: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameutenda hivi mji huu mkubwa?’ 9Wenzao watawajibu, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaiabudu miungu mingine na kuitumikia.’”
10. Msimlilie mtu aliyekufa,
wala msiombolezee kifo chake.
Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,
kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.
11. Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Shalumu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyetawala baada ya Yosia baba yake, na ambaye aliondoka mahali hapa: “Shalumu hatarudi tena mahali hapa, 12bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii.
Ujumbe juu ya Yehoyakimu
13“Ole wako Yehoyakimu
wewe unayejenga nyumba kwa dhuluma
na kuiwekea ghorofa bila kutumia haki.
Unawaajiri watu wakutumikie bure
wala huwalipi mishahara yao.
14Wewe wasema:
‘Nitalijenga jumba kubwa,
lenye vyumba vikubwa ghorofani.’
Kisha huifanyia madirisha,
ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi,
na kuipaka rangi nyekundu!
15Unadhani umekuwa mfalme
kwa kushindana kujenga kwa mierezi?
Baba yako alikula na kunywa,
akatenda mambo ya haki na mema
ndipo mambo yake yakamwendea vema.
16Aliwapatia haki maskini na wahitaji,
na mambo yake yakamwendea vema.
Hii ndiyo maana ya kunijua mimi Mwenyezi-Mungu.
17. Lakini macho yako wewe na moyo wako,
hungangania tu mapato yasiyo halali.
Unamwaga damu ya wasio na hatia,
Mungu awasaidie mnapolitafakari neno hili.
Nakala zifike kwa:
1. Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli
2. Mhe Tundu Antipas Lisu
Pia Ziwafikie;
1. Wenyeviti na Makatibu wote wa Vyama vya siasa
2. Viongozi wa Nyanja zote za kitaifa na kijamii
Ipende nchi yako, penda watu wako. Kuwa Mzalendo.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es Salaam