UJUMBE WA MBUNGE: Shukrani, Twende Kazi!

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240

WanaJF wenzangu,
Nawashukuru kwa kuniunga mkono katika uchaguzi na kuniwezesha kuwa mbunge wa wote wa Jimbo la Ubungo. Tuendelee kushirikiana kutimiza wajibu katika kipindi cha mwaka 2010-2015 tukitekeleza ahadi jimboni kwa kuweka kipaumbele kwenye Akili, Ajira, Miundombinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Ardhi na Afya (AMUA) kama ifuatavyo:

AKILI:
Akili na vipaji ambavyo kila mwanadamu amejaliwa ndiyo mtaji mkuu wa kujikwamua kimaisha. Kwa hiyo, tushirikiane kuwezesha elimu bora:
· Tuhakikishe ruzuku ya bajeti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, inafika na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya elimu na huduma zingine za muhimu.

· Tutumie sehemu ya fedha za mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo(CDCF) kutoa elimu maalum ya kuwawezesha wananchi kujua haki zao, fursa zilizopo na namna ya kujiendeleza, haswa kwa akina mama, vijana na walemavu. Mfano; haki za mirathi kwa wajane na kukuza vipaji kwa vijana.

· Tuendelee kupigania haki na maslahi ya wanafunzi wote wakiwemo wa elimu ya juu.

AJIRA:
· Tuwezesha kupatikana mitaji, mafunzo ya ujariliamali na kutetea wafanyabiashara na wazalishaji wadogo wadogo wawe na maeneo ya biashara.

· Tuhakikishe vitega uchumi vilivyopo kama kituo cha mabasi Ubungo, Kiwanda cha Urafiki, Songas na kituo cha kiuchumi cha “EPZ”, vinatoa ajira kwa wakazi wa jimbo la Ubungo na kuchangia miradi ya maendeleo.

· Tuchochee uwekezaji na uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ili kupunguza hitaji la ajira hasa kwa vijana.

· Tutetee ujira bora na stahili za wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi kama walimu, manesi, polisi, madereva nk.

MIUNDO MBINU:
· Ili kupunguza msongamano katika barabara kuu, pamoja na mbinu zingine tuhakikishe barabara za pembezoni zinajengwa. Mfano: barabara ya Mbezi-Goba, Kimara-Makuburi n.k. Pia turahisishe usafiri wa maeneo ya pembezoni kwa ukarabati wa barabara na madaraja. Mfano: Golani, Mburahati Kisiwani, Msakuzi, King’ong’o, Kwembe, Makoka n.k

· Tupiganie kupunguzwa kwa gharama za kuvuta umeme kwa kujenga hoja bungeni ili gharama za nguzo na nyinginezo ziwekwe kwenye bili ya mteja kama umeme uliolipiwa. Hii itasaidia wengi kuvuta umeme kwa gharama nafuu.
MAJI:
· Tusimamie uwekaji mabomba katika maeneo yaliyorukwa na kuhakikisha DAWASCO inatimiza wajibu wake wa kuhakikisha maji yanatoka wakati wote.

· Tuhamasishe ujenzi wa visima kwenye maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na mtandao wa maji ya bomba kama suluhisho la muda, huku tukifuatilia ufumbuzi wa kudumu katika maeneo hayo.

· Tuhakikishe bei ya maji inayotozwa kwenye Viosk inaendana na viwango vilivyopangwa na mamlaka husika (EWURA).
UWAJIBIKAJI:
· Tupambane na ufisadi kwenye Halmashauri na kuhakikisha fedha nyingi zinazopatikana kila mwaka zinatumika kuwahudumia wananchi, ikiwemo kushughulikia mapungufu yaliyoanishwa na mkaguzi mkuu wa serikali katika vipindi vilivyopita.

· Tuhamasishe wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuchangia fedha na rasilimali nyingine za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakazi wa Ubungo.

· Tufungue ofisi mbili za Mbunge wa Jimbo la Ubungo, ili kila ofisi ihudumie kata saba. Hii itasaidia wananchi kukutana kwa urahisi na mbunge wao kabla ya kwenda kuwawakilisha kwenye vikao vya bunge.

· Tuzisimamie mamlaka za serikali kutekeleza wajibu wake, mathalani EWURA katika nishati/mafuta, SUMATRA katika usafiri, TANESCO katika umeme, TBS katika ubora wa bidhaa nk

USALAMA:
· Tuhamasishe ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo yasiyokuwa na vituo kama Goba na kupanua vituo vya polisi vilivyopo ili kuviongezea uwezo na hadhi katika kuwahudumia wananchi.

· Tushirikiane polisi na viongozi wa kata/mitaa kuhakikisha doria inakuwepo ili kupunguza vitendo vya wizi, ukabaji na ujambazi hususani kwenye maeneo yenye vitendo vingi vya uhalifu
ARDHI:
· Tuhakikishe wananchi wanapewa fidia wanazostahili katika maeneo yote yenye migogoro ya ardhi kama Kwembe,Kibamba,Ubungo Maziwa n.k

· Tuhakikishe viwanja vya umma vilivyouzwa kinyemela na viwanja vya wazi vilivyovamiwa, vinarejeshwa. Mfano: viwanja vya Makurumla, Sinza, Ubungo, Makuburi, Mbezi nk.

· Tusimamie mpangilio mzuri wa makazi na kuhamasisha upimaji wa viwanja ili wananchi wapate hati na leseni za makazi kwa urahisi na kwa bei nafuu.
AFYA:
· Tuhakikishe wanaoishi na UKIMWI/VVU, Wazee, Walemavu na wagonjwa wa kifua kikuu, wanapata huduma za matibabu kwa wakati na kwa fedha za serikali na wadau wengine wa maendeleo.

· Tusimamie vizuri fedha za bajeti ya afya kwa kuhakikisha zinatumika kuboresha huduma katika zahanati za kata na hospitali ya Mwananyamala inayohudumia pia wakazi wa jimbo la Ubungo.

· Tupiganie ujenzi wa zahanati mpya kwenye uhaba wa zahanati.

Inawezekana, Ungana nami -Shiriki Sasa!!
 
Thanks Mh. Mmbunge... kwanza hongera sana ...... kazi ni nzuri isiyo na kifani.... nawajibika kuungana na wewe kuunga mkono yote ya akili yako uliyoyaainisha na uwajibikaji kwa umma uliokupa heshima na thamani kuwawakilisha... kutakua na faraja na matumaini ya maisha ya watanzania

Ningefurahi zaidi kama ungeweza kuweka wazi pia msimamo na mipango yako kuhusu Demokrasia na ukuuaji wake hapa nchini.... ukizingatia suala la uchaguzi huru na haki jambo linaloigusa tume ya uchaguzi na moja kwa moja, hivyo basi tupe msimamo wako na mikakati amboyo youte haya yanelenga wazi wazi kwenye ukweli wamba umefika wakati watanzania wanahitaji katiba mpaya ... ukizingatia hii tuliyonayo sasa kwa lugha ya kigeni na yenye tafasiri sahihi kabisa tunasema ... "It is OBSOLETE"
 
Hongera sana, jimbo la ubungo watu wana kiu ya maendeleo iliyozidi mapenzi ya vyama ukilijua hilo utafanikiwa.
 
Nakushukuru. Vipaumbele hivyo ni vya kijimbo, nitasimamia pia vipaumbele vya kitaifa kupitia bunge na suala la katiba mpya ni moja ya hoja/haja nitakazoshiriki kwa uzito mkubwa kwa ajili ya kuleta mustakabali mwema wa demokrasia na maendeleo katika nchi yetu

JJ
 
Tumefurahi sana kukupata ww kama mbunge wetu, ila swali langu moja tumefanikiwa kupata madiwani wangapi kwenye jimbo letu?
 
Tumefurahi sana kukupata ww kama mbunge wetu, ila swali langu moja tumefanikiwa kupata madiwani wangapi kwenye jimbo letu?

Tononeka,

Asante. Jimbo la Ubungo tumepata madiwani sita wa kata: Kimara, Saranga, Sinza, Ubungo, Makuburi na Mbezi. Tunatarajia pia kupata madiwani wa nyongeza kutokana na viti maalum vya wanawake

JJ
 
Nashukuru Mbunge wangu lile tuta la Stop over vp ulilifanyia kazi mwenyewe?
 
MAJI:
· Tusimamie uwekaji mabomba katika maeneo yaliyorukwa na kuhakikisha DAWASCO inatimiza wajibu wake wa kuhakikisha maji yanatoka wakati wote.

Hapa mkuu yale maji ya Mchina kwa nini yanatoka nyumba za wajumbe tu?

Sisi mtaani kwetu toka waweke tulikuwa tunayapata kipindi cha kampeni kwa wiki mara 2 kampeni zimeisha hatuyaoni tena
 
Umesikika Mnyika.......!
Tunakuamini Mnyika......!
Tuna matarajio makubwa sana hapo Ubungo....!
Mungu awatangulie
 
Hapa mkuu yale maji ya Mchina kwa nini yanatoka nyumba za wajumbe tu?

Sisi mtaani kwetu toka waweke tulikuwa tunayapata kipindi cha kampeni kwa wiki mara 2 kampeni zimeisha hatuyaoni tena

Na Kwenye mahoteli hasa mitaa ya Sinza...toka Januari hatujabahatika (hata kwa mgao) kupata hata katone..
Mkuu shughulikia hii taabu..
 
JJ,

Hongera sana, nimefurahi sana kukuona bungeni.

Huyu bwana ukimsoma, mtu akakwambia "huyu mbunge kaandika haya" unaweza kuelewa huyu ni mbunge anayeelewa kaenda kufanya nini bungeni. Not that other "I am one week in parliament, my phone cannot accommodate all y'all, I am changing vijiwe, and parliament really bores me" stuff.

Pigeni msasa wabunge wenu wasije kuwaaibisha kama walivyokwishaanza hapa. Regia Mtema should closely watch Mnyika and aspire to at least emulate his standards, if she cannot reach them. I mean you may disagree with Mnyika on the contents of what he says as far as philosophical disagreement of policies and political outlooks are concerned, but only a fanatic can say Mnyika is not parliament material, especially since you have so many jokers in there who can't even tell policy from politics.

Mimi issue yangu moja ndogo tu ambayo inaweza kutuonyesha imani kubwa wananchi. CHADEMA kama sikosei ina msimamo wa kuona kwamba mishahara na marupurupu ya wabunge ni mikubwa sana. Hili nimelisikia mheshimiwa Slaa akiliongelea na kulaumu kwamba CCM wanao control bunge hawawezi kupitisha punguzo la mishahara/ marupurupu.

Kama kitendo cha kuwatumia ujumbe CCM na wananchi wa Tanzania, CHADEMA kwa kupitia wabunge wake, inaweza kutoa sehemu ya mishahara na marupurupu hayo ya wabunge wake, na kuichangia katika mfuko fulani wa CHADEMA wa maendeleo ya jamii?

Hili litakuwa na faida kubwa tatu, kwanza litawaonyesha CCM kwamba mbunge hahitaji mshahara mkubwa sana na anaweza kufanya kazi kwa ufanisi bila gharama kubwa sana, pili litawaonyesha wananchi sio tu mbunge anaweza kuishi na kufanya kazi vizuri kwa gharama ndogo tu, bali pia CHADEMA inajali wananchi kiasi cha kuanza kulifanyia kazi hili mara moja hata kabla halijapitishwa na CCM, na tatu, liataipa CHADEMA uongozi katika swala hili pamoja na kufaidisha maendeleo ya wananchi moja kwa moja.

Naona habari za kusubiri kitu kipitishwe rasmi bungeni zitakuwa ndoto na CHADEMA inaonekana kama inatafuta credit za kupinga mishahara mikubwa kimsimamo, lakini tukifika pale panapohusika hasa, penye kuikubali ama kuikataa mishahara hii, CHADEMA inakuwa haina tofauti na CCM.

CHADEMA itaaminika zaidi ikisema kwa vitendo. Siasa za maneno tushazoea Tanzania, tunachotaka kipya ni vitendo.
 
Mnyika

Hongera sana. Mi nina ombi ambalo naomba uliwakilishe huko kwa wabunge wengine NDANI YA MJENGO.

Kwa Upande Dsm, BAGAMOYO tuna chanzo ki1 tu cha maji ambacho ni Mto RUVU. SAsa Mwenyezi Mungu asipoleta Mvua Basi Tumekwisha Mto Unakauka na hivyo Maji Hakuna Dsm wala B'moyo. NDICHO KITU KILICHOPO KWA SASA KWANI MAJI NI YA MGAO KWA ZILE SEHEMU YANAPOTOKA?

Hv kweli kwa miaka 50 ya Uhuru hatuna chanzo Mbadala cha Maji safi na salama isipokuwa Mto RUVU.

Ebu Kaeni na wataalamu hata ikiwezekana kusafisha maji ya Bahari yaweze kutumika (Japo najua ni Expensive sana) basi iwe hivyo kwa sababu MAJI NI UHAI. MAJI NI KILA KITU.

Mbona wenzetu wanaweza. kwani nini CC 2shindwe?? hata kwa mkopo wa WB sawa tu ki finance hiyo project ilimradi maji watu wanapata.

Usipoangalia 2015 haurudi kwani mm ni mkazi wa hapo Ubungo kwa Miaka mingi. Watu wanataka Maji Basiiiiiiiiiiii

Maji Basi
 
Mwanzo mzuri, Mpango kazi pia utasaidia kujua na kufuatilia utekelezaji pamoja na kushirikisha wadau mbali mbali.
 
JJ,
Kama kitendo cha kuwatumia ujumbe CCM na wananchi wa Tanzani, CHADEMA kwa kupitia wabunge wake, inaweza kutoa sehemu ya mishahara na marupurupu hayo ya wabunge wake, na kuichangia katika mfuko fulani wa CHADEMA wa maendeleo ya jamii?.

unawatega?
 
Hongera sana Mnyika, wewe ni Jembe matarajio yetu ni kuwa wwanachi wa Ubungo watapata maendeleo sasa.Mi siishi Ubungo ila ningetamani kuwa na mbunge kama wewe.Ushauri wangu kwa CHADEMA:

1.CHADEMA ni chama kinachopendwa sana na vijana na hata baadhi ya watu wazima, tatizo ni kuwa hakijaenezwa sana huko mikoani, mfano moro sifahamu wapi makao makuu ya CHADEMA yako, mimi kadi nilikata dar, sasa ni wakati wa kikitangaza chama hadi vijijini bara na visiwani.

2.Mtaji wa CHADEMA ni vijana wa mtaani na wale walioko vyuoni, kwa walioko vyuoni ni wajibu wa chama kuja vyuoni kama SUA, MZUMBE nk kuongea na wanachuo kwani mfano SUA lipo tawi la wanachuo ambao ni wanachama wa CCM licha ya kuwa sio ndani ya eneo la chuo ila wana kiongozi wao pale kwa hio taarifa nyingi na kadi hutolewa pale kwa nini CHADEMA tushindwe? Hili lifanyike ili tuvune wanachama wengi toka vyuoni ambao mi naamini ndio mtaji wetu wa kukamata dola 2015, na wale wa mtaani ni kufungua matawi ya CHADEMA hadi level ya kaya kumu kumi.

3.Tofauti zilizotokea pale bungeni kati yenu na CUF zinatia doa upinzani na kuwapa nguvu CCM kuwa hamna nguvu, jitahidini mvunje haya makundi ili muwe na nguvu ya kutetea hoja pale bungeni, kama CUF wanaona hawajapewa unaibu wa kiongozi wa kambi ya upinzani wapeni na pia swala la mawaziri vivuli liangaliwe vizuri kuwe na usawa ili kusije tokea tena mtafaruku.

4.Hoja nzito kama za ufisadi zikishindikana kupelekwa bungeni kwani yule Spika si mzuri yuko kiCCM zaidi ni vema hata zikasemewa nje ya bunge kama kwenye midahalo na mikutano pale mwembe yanga au jangwani, muwe makini sana na Spika Ana kawekwa na kikundi cha watu kwa maslahi yao na CCM wanajua atazuia kila hoja zitakazo letu bungeni hasa zinazoanika ufisadi wao.

5.Simamieni kwa umadhubuti suala la kufanya marekebisho katiba, katiba ya sasa ni ya kidikteta na inakandamiza wapinzani na haitoi muanya wa chama kingine kutawala nchi zaidi ya CCM, hii iwe hoja ya kwanza kwenye kikao cha febuari.


Yangu ni hayo tu kwa leo,ila ukitoa email yako ni vema ili tukuarifu yale yanayotokea huku tuliko, yako mengi yanayokera, kiufupi ufisadi sasa uko kila sehemu.

Mungu akubariki sana.
 
unawatega?

Siyo kuwatega, wao wenyewe ndio wamelisema hili kama issue, sasa nataka watuonyeshe tu kwamba wako serious na wanaposema sio wanasema kwa ulaghai wa kisiasa bali kwa ukweli wa dhamira zao.
 
Mnyika Mbunge tunashukuru kuja kutujuza vipaumbele unavyotaka kufanya na wananchi naomba wewe na mbunge wako wa kawe muangalie maeneo ambayo munaweza kushinikiza yakajengwa kuwa bustani za majimbo ili wananchi wapate mahali pa kupumzika na kukutana kwa mfano maeneo yaliyokuwa yakichimbwa michanga na kokoto yakasawazishwa yakawekwa sawa na kupandwa miti na maua kwa wananchi kujipimzisha na taabu za kila siku
 
WanaJF wenzangu,
Nawashukuru kwa kuniunga mkono katika uchaguzi na kuniwezesha kuwa mbunge wa wote wa Jimbo la Ubungo. Tuendelee kushirikiana kutimiza wajibu katika kipindi cha mwaka 2010-2015 tukitekeleza ahadi jimboni kwa kuweka kipaumbele kwenye Akili, Ajira, Miundombinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Ardhi na Afya (AMUA) kama ifuatavyo:

Inawezekana, Ungana nami -Shiriki Sasa!!
JJ Mnyika,
asante sana kwa hili, mimi binafsi nafarijika sana kuona kijana ulionyesha nia kwa dhati, ukajenga hoja kwa wananchi wa jimbo lako la Ubungo, hoja zikaeleweka, wakakupa ridhaa yao kwa kukuchagua, sasa unarudi kwanza kuwashukuryu, pili kuwa mipango mkakati wa utekelezaji wa yale uliyoahidi.

Hiki ilichokifanya ndicho nimekuwa nikimuomba Dr. Slaa akifanya tangu ile siku ya kutangaza matokeo. Onyesha shukrani kwa kidogo kilichopatikana na wape wafuasi wenu matumaini ya a way forward,

Amini usiamini, hakuna jimbo ambalo CCM imeumia sana kulikosa kama jimbo la Ubungo, hapo ndipo ulipo ufungua wa kuingia jiji la Dar es Salaam, ndipo kilipo kitovu cha elimu, UDSM na ndipo yalipo makazi ya wanachi wenye umasikini uliotopea Manzese etc, hivyo kitendo cha kushikwa na upinzani ni kutuma taarifa nzito kwa wengine wote, CCM sio chama cha ukombozi, wala cha walala hoi bali ni Chadema.

Determinant ya kifo rasmi cha CCM jijini Dar es Salaam, kimebebwa kwenye mabega yako wewe na Mhe. Mdee, baada ya kuaminiwa na kupewa, sasa Dar esSalaam nzima inasubiri kwa hamu mtafanya nini na kama mtawapa watu kile walichokitarajia, 2015, CCM inafungashwa virago majimbo yote ya mijini wanayoyashikilia hata wakipiga kampeni usiku na mchana.

JJ Mnyika, wewe umeshaonyesha, kwamba ni organizer, kwa wadhifa wako kama Naibu Katibu Mkuu, tumia nafasi hiyo kuwaimarisha wale wenzenu ambao wamechaguliwa sio kwa sababu ya uwezo wao, bali watu walishaichoka CCM kupita kiasi. Kwa vile uongozi ni karama, na sio wote wanayo, nyinyi wachacher wenye karama hiyo ndani ya Chadema, mkiongozwa na baadhi ya viongozi wenu wakuu wenye karama hiyo, itumieni collectively kuiboost Chadema yote, vinginevyo....

Kusema kweli, nimekuwa shuhuda wa siasa za nchi hii kwa kipindi kirefu, lakini hakuna kipindi ambacho nimekuwa inspired kama kipindi hiki in particular kazi nzuri Chadema iliyoifanya.

Wish you all the best!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom