UJUMBE WA MBUNGE: Shukrani, Twende Kazi!

hongera sana mheshimiwa john mnyika. Ulipata ushindi mzuri na wa kujivunia na umeanza vizuri kazi uliyopewa. Mimi pia ni mmoja wa wakazi wa jimbo lako kwani nina makazi kimara na muda mwingi familia yangu inaishi huko, kwa hiyo wewe ni mbunge wangu na ninaona fahari kuwa na mbunge kijana, mbunifu, mwepesi na mchapakazi. Nitaangalia baadaye uwezekano wa kufahamiana na wewe kibinafsi ili kama lipo la kushirikiana na kushikana mikono, basi tufanye hivyo kwa manufaa ya wananchi wakazi wa eneo letu na taifa kwa ujumla.

Nakutakia kila la heri katika utumishi wako. Mungu akutangulie na daima maslahi ya taifa yakae mbele

mungu ibariki tanzania,
mungu ibariki afrika
kidumu chama cha mapinduzi
na wewe taja jimbo lako watu waseme yaliyo ya moyoni bana....
 

WanaJF wenzangu,
Nawashukuru kwa kuniunga mkono katika uchaguzi na kuniwezesha kuwa mbunge wa wote wa Jimbo la Ubungo. Tuendelee kushirikiana kutimiza wajibu katika kipindi cha mwaka 2010-2015 tukitekeleza ahadi jimboni kwa kuweka kipaumbele kwenye Akili, Ajira, Miundombinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Ardhi na Afya (AMUA) kama ifuatavyo:

AKILI:
Akili na vipaji ambavyo kila mwanadamu amejaliwa ndiyo mtaji mkuu wa kujikwamua kimaisha. Kwa hiyo, tushirikiane kuwezesha elimu bora:
· Tuhakikishe ruzuku ya bajeti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, inafika na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya elimu na huduma zingine za muhimu.

· Tutumie sehemu ya fedha za mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo(CDCF) kutoa elimu maalum ya kuwawezesha wananchi kujua haki zao, fursa zilizopo na namna ya kujiendeleza, haswa kwa akina mama, vijana na walemavu. Mfano; haki za mirathi kwa wajane na kukuza vipaji kwa vijana.

· Tuendelee kupigania haki na maslahi ya wanafunzi wote wakiwemo wa elimu ya juu.

AJIRA:
· Tuwezesha kupatikana mitaji, mafunzo ya ujariliamali na kutetea wafanyabiashara na wazalishaji wadogo wadogo wawe na maeneo ya biashara.

· Tuhakikishe vitega uchumi vilivyopo kama kituo cha mabasi Ubungo, Kiwanda cha Urafiki, Songas na kituo cha kiuchumi cha "EPZ", vinatoa ajira kwa wakazi wa jimbo la Ubungo na kuchangia miradi ya maendeleo.

· Tuchochee uwekezaji na uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ili kupunguza hitaji la ajira hasa kwa vijana.

· Tutetee ujira bora na stahili za wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi kama walimu, manesi, polisi, madereva nk.

MIUNDO MBINU:
· Ili kupunguza msongamano katika barabara kuu, pamoja na mbinu zingine tuhakikishe barabara za pembezoni zinajengwa. Mfano: barabara ya Mbezi-Goba, Kimara-Makuburi n.k. Pia turahisishe usafiri wa maeneo ya pembezoni kwa ukarabati wa barabara na madaraja. Mfano: Golani, Mburahati Kisiwani, Msakuzi, King'ong'o, Kwembe, Makoka n.k

· Tupiganie kupunguzwa kwa gharama za kuvuta umeme kwa kujenga hoja bungeni ili gharama za nguzo na nyinginezo ziwekwe kwenye bili ya mteja kama umeme uliolipiwa. Hii itasaidia wengi kuvuta umeme kwa gharama nafuu.
MAJI:
· Tusimamie uwekaji mabomba katika maeneo yaliyorukwa na kuhakikisha DAWASCO inatimiza wajibu wake wa kuhakikisha maji yanatoka wakati wote.

· Tuhamasishe ujenzi wa visima kwenye maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na mtandao wa maji ya bomba kama suluhisho la muda, huku tukifuatilia ufumbuzi wa kudumu katika maeneo hayo.

· Tuhakikishe bei ya maji inayotozwa kwenye Viosk inaendana na viwango vilivyopangwa na mamlaka husika (EWURA).
UWAJIBIKAJI:
· Tupambane na ufisadi kwenye Halmashauri na kuhakikisha fedha nyingi zinazopatikana kila mwaka zinatumika kuwahudumia wananchi, ikiwemo kushughulikia mapungufu yaliyoanishwa na mkaguzi mkuu wa serikali katika vipindi vilivyopita.

· Tuhamasishe wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuchangia fedha na rasilimali nyingine za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakazi wa Ubungo.

· Tufungue ofisi mbili za Mbunge wa Jimbo la Ubungo, ili kila ofisi ihudumie kata saba. Hii itasaidia wananchi kukutana kwa urahisi na mbunge wao kabla ya kwenda kuwawakilisha kwenye vikao vya bunge.

· Tuzisimamie mamlaka za serikali kutekeleza wajibu wake, mathalani EWURA katika nishati/mafuta, SUMATRA katika usafiri, TANESCO katika umeme, TBS katika ubora wa bidhaa nk

USALAMA:
· Tuhamasishe ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo yasiyokuwa na vituo kama Goba na kupanua vituo vya polisi vilivyopo ili kuviongezea uwezo na hadhi katika kuwahudumia wananchi.

· Tushirikiane polisi na viongozi wa kata/mitaa kuhakikisha doria inakuwepo ili kupunguza vitendo vya wizi, ukabaji na ujambazi hususani kwenye maeneo yenye vitendo vingi vya uhalifu
ARDHI:
· Tuhakikishe wananchi wanapewa fidia wanazostahili katika maeneo yote yenye migogoro ya ardhi kama Kwembe,Kibamba,Ubungo Maziwa n.k

· Tuhakikishe viwanja vya umma vilivyouzwa kinyemela na viwanja vya wazi vilivyovamiwa, vinarejeshwa. Mfano: viwanja vya Makurumla, Sinza, Ubungo, Makuburi, Mbezi nk.

· Tusimamie mpangilio mzuri wa makazi na kuhamasisha upimaji wa viwanja ili wananchi wapate hati na leseni za makazi kwa urahisi na kwa bei nafuu.
AFYA:
· Tuhakikishe wanaoishi na UKIMWI/VVU, Wazee, Walemavu na wagonjwa wa kifua kikuu, wanapata huduma za matibabu kwa wakati na kwa fedha za serikali na wadau wengine wa maendeleo.

· Tusimamie vizuri fedha za bajeti ya afya kwa kuhakikisha zinatumika kuboresha huduma katika zahanati za kata na hospitali ya Mwananyamala inayohudumia pia wakazi wa jimbo la Ubungo.

· Tupiganie ujenzi wa zahanati mpya kwenye uhaba wa zahanati.

Inawezekana, Ungana nami -Shiriki Sasa!!
Hongera sana mkuu, umechaguliwa na wananchi na Mungu pia, tumika kana kwamba hutapata nafasi nyingine ya kutumika, hongera tena na tena na Mungu akusaidie ili utimize ahadi zako kwa wananchi

Big up JJ
 
Ndugu mh.J.Myika,tunakushukuru sana kwa ujumbe wako. Mimi binafsi najumuika na watanzania kukutakia kheri na baraka katika kazi zako na za wabunge wote wanaoitakia mema nchi hii. Yapo mengi mtakayopambana nayo maana Tanzania huru inahitaji jitihada zetu,tukiongozwa nanyi basi tutafanikiwa. Kwa ili basi napenda kukuomba unielekeze kwa ili: mimi ni mhasibu/graduate nimehitimu IFM napenda kuingia chadema rasmi,ila nataka nipate kadi ya chadema kutoka kwako,au kwa mwenyekiti au katibu mkuu,hapo ntajisikia faraja na pia naanza mapambazo rasmi. Nataka kujiunga ili nisaidie kujenga chama. Ukweli ni kwamba vijana wengi wanahitaji kujiunga chadema ila hawajapata mtu wa kuwaelekeza,kupitia website ya chama registration inakwama,mfano tangu august nimelodge request,mpaka leo sijajibiwa,nadhani hapo kuna tatizo. Naomba kujua siku na saa ambapo kati ya watu niliowataja watakuwepo lini ofisini ili niweze kufika kuchukua kadi yangu nianze kutimiza malengo katika harakati za uzalendo nilizojiwekea. Nijulishe apa au kupitia rbagoka@gmail.com au nipe namba yako nikupigie. Nakushukuru tena na mola akuongoze!
 
Sijaona hata sehemu moja mwongozo wa JJ kwenye elimu hasa elimu ya juu kwa wapiga kura wake;ieleweke kuwa Jimbo la Ubungo ndipo kilipo chuo cha UDSM lkn sijasoma bado mipango yake endelevu ya kuwaingiza wana Ubungo wengi zaidi kwenye "chuo chao cha nyumbani"

Sera ya CHADEMA kuhusu kuboresha Elimu haina nafasi kwenye Jimbo la Ubungo chini ya JJ?
 
Mh JJ,
Katika suala la afya! ni suala nyeti sana katika maisha ya watu. Magonjwa mengi yanayosumbua watu ni kutokana na ukosefu wa maji ya uhakika. Naimani kama utaweza kutatua hili suala basi utakuwa umeokoa maisha ya watu wengi hata kuwaongezea umri wa kuishi. Siyo siri tuko nyuma sana katika suala hilo, maji yanatakiwa yawepo kila wakati, kwa hiyo ni challenges zako pia kuhakikisha haya yanafanyika.

Katika suala la Elimu! Nitafurahi kama utaweza kuanzisha maktaba kubwa ya jimbo la ubungo ili watu mbali mbali wafike na kujinoa bongo zao. Utakuwa umeonyesha njia nzuri sana katika taifa hili.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
hongera kwa yote ndugu Mnyika!

katika yote uliyoyaainisha hapo juu,ni mazuri na yanafaa sana na wala hayakinzani na yale ya kwenye kampeni zako

lakini sijaona jambo moja ambalo ni la muhimu hasa katika kujenga ajira kwa vijana,kuwaunganisha na hata kuwasaidia

kuepukana na hatari mbalimbali zinazowasonga kwa sasa kama vile magonjwa,tabia za utumiaji madawa ya kulevya pamoja

na biashara za ukahaba na nyinginezo,suala hilo ni MICHEZO.

ningeshauri michezo iwe moja ya vipaumbele vyako vikubwa,kuanzia mpira wa miguu,kwa wote wanaume na wanawake,mipira ya pete

mbio.ningependa kuona baada ya kipindi hiki basi ubungo inapata timu hata moja inashiriki ligi kuu,anzisha ligi za jimbo za michezo mbali

mbali angalau hata mpira wa miguu,hamasisha uanzishaji wa timu kila kijiji,kata na kupata ligi nzuri.ubungo kuna vijana wengi na wana vipaji

pia,kuna maeneo mengi twaweza kutengeneza viwanja vizuri tu vya michezo,michezo mashuleni,vyuoni,waweza hata kuanzisha

ligi za shule zilizoko jimboni,msingi,sekondari,kisha hata vyuo vilivyo ndani ya jimbo,kisha tukahamia mtaani,kuanza ligi za vijana wa mtaani

unaweza,tunaweza,hakuna linaloshindikana,ni mipango mizuri tu kisha uwajibikaji makini.
 
Foleni ya ubungo inatuumiza sana, tusaidie angalau barabara ya baruti kutokea chuo ipitishwe greda ili tunaoenda UDSM na mwenge tutumie njia hiyo
 
Hapa mkuu yale maji ya Mchina kwa nini yanatoka nyumba za wajumbe tu?

Sisi mtaani kwetu toka waweke tulikuwa tunayapata kipindi cha kampeni kwa wiki mara 2 kampeni zimeisha hatuyaoni tena

Fidel80,

1. Nitazingatia hoja yako, ni katika ya kero ninayoikuta maeneo mengi ya jimbo la Ubungo. Wakati nafanya kampeni niliahidi kwamba vipaumbele vitakuwa Akili, Ajira, Miundombinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Ardhi na Afya (AMUA), lakini kutokana na umuhimu wa suala la maji wapo wanaopendekeza kuwa suala liwe kipaumbele cha kwanza. Kama hivyo ndivyo, basi AMUA inaweza kugeuzwa kuwa MAUA(Maji/Miundombinu, Akili/Ajira, Uwajibikaji/Usalama, Ardhi/Afya).

2. Hivi ni vipaumbele, lakini tutavitengenezea pia Mpango Mkakati na Mpango Kazi wa utekelezaji. Pamoja na kuwa na vipaumbele nane, kwa kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano tutakuwa na kipaumbele cha mwaka na ujumbe maalumu(theme) ili kuweza kuhamasisha umma. Kwa mwaka wa 2011 napendekeza kwamba kipaumbele kiwe kwenye sekta ya maji.

3. Nashukuru kwa maoni mbalimbali yanayotolewa, haya ni masuala ambayo tumeona tuyape mkazo zaidi katika jimbo. Hata hivyo kuna mambo ambayo tutayasimia kama usafi(kama sehemu ya afya mazingira), michezo nk. Ila tukiweka vipaumbele vingi sana tutatapakaza sana nguvu na kutakuwa kuna changamoto pia ya kupima ufanisi. Hivyo, ni muhimu tushauriane mambo ya kuyapa mkazo katika kipindi cha 2010-2015. Haya ni masuala ya kijimbo (local issues), ipo siku nitatoa ajenda za kitaifa (national agenda) ambazo nitashiriki kuzisimamia bungeni kwa kurejea pia ilani ya chama na maoni ya umma.

4. Ili mjadala huu uwe wenye maoni tunayoweza kuyaratibu na kuyafanyia kazi kwa urahisi zaidi, ni vyema tukaanza sekta moja baada ya nyingine kujadili kwa kina hatua za kuchukua tukianzia na sekta ya maji. Tunaweza kuwa na SEKTA YA MWEZI, mjadala ukifanyika kwa uratibu na utaratibu kwa mwezi mzima kwa kutokana na 'vichwa' vilivyomo humu ni wazi tunaweza kuleta mabadiliko tunayoyataka. Asanteni kwa michango yenu.

JJ
 
What you have done JJ is excellent.One thing I have to suggest is that,talk to your colleagues I mean MPs to amke a visit to your fans saying thanks for their support.So many members are waiting for you at least to say a word of thanks.Keep it up.We don't need contradictions among yourselves.
 
Viva Mh. Mnyika ila rekibisha kidogo ka sentensi kako wewe si MBUNGE WA UBUNGO bali wewe ni MBUNGE WA TANZANIA, wabunge wa majimbo ni wale wanaotoka CCM tu maana hutetea mambo ya wanakotoka tu (Chama na Mjimbo) na kusahau maslahi ya taifa.
 
kwanza ningependa kuchukua fursa hii kukupongeza sana kwa ushindi mkubwa uliopewa na watu wa ubungo na pili napenda kuwashukuru watu wa ubungo kwa kukuchagua wewe kuwa mbunge na pia chadema kwa kura za urais.

swali langu ni dogo naomba kujua tulipata madiwani wangapi mkoa wa dar es salaam ??.

ushauri:
watumie sana watu JF kama source yako nzuri ya ushauri kwani kuna watu wana information nyingi sana halafu uzuri wake ni kuwa wametawanyika throughtout the world na wana utaalamu wa aina mbalimbali ushauri utakaoupata(constructive one) hata rais JK hawezi kuupata kutoka kwa MAYES MAN wake kwahiyo itumie sana JF utaisadi sana jamii.
 
mnyika angalia tu hao ccm wasitumie janja ya kukusaidia hapo Ubungo ukawa kama zito maana sasa anatushangaza na pongezi zake kwa kiongozi wa c c m halafu anadhani sisi ni mbumbumbu kama yeye!!!!!!!!!!!!!!




a good leader doesnt seek refugees to his enemy otherwise himself is the enemy of the people he lead take care!! sanaaa!!!
 
JJ,

Hongera sana, nimefurahi sana kukuona bungeni.

Huyu bwana ukimsoma, mtu akakwambia "huyu mbunge kaandika haya" unaweza kuelewa huyu ni mbunge anayeelewa kaenda kufanya nini bungeni. Not that other "I am one week in parliament, my phone cannot accommodate all y'all, I am changing vijiwe, and parliament really bores me" stuff.

Pigeni msasa wabunge wenu wasije kuwaaibisha kama walivyokwishaanza hapa. Regia Mtema should closely watch Mnyika and aspire to at least emulate his standards, if she cannot reach them. I mean you may disagree with Mnyika on the contents of what he says as far as philosophical disagreement of policies and political outlooks are concerned, but only a fanatic can say Mnyika is not parliament material, especially since you have so many jokers in there who can't even tell policy from politics.

Mimi issue yangu moja ndogo tu ambayo inaweza kutuonyesha imani kubwa wananchi. CHADEMA kama sikosei ina msimamo wa kuona kwamba mishahara na marupurupu ya wabunge ni mikubwa sana. Hili nimelisikia mheshimiwa Slaa akiliongelea na kulaumu kwamba CCM wanao control bunge hawawezi kupitisha punguzo la mishahara/ marupurupu.

Kama kitendo cha kuwatumia ujumbe CCM na wananchi wa Tanzania, CHADEMA kwa kupitia wabunge wake, inaweza kutoa sehemu ya mishahara na marupurupu hayo ya wabunge wake, na kuichangia katika mfuko fulani wa CHADEMA wa maendeleo ya jamii?

Hili litakuwa na faida kubwa tatu, kwanza litawaonyesha CCM kwamba mbunge hahitaji mshahara mkubwa sana na anaweza kufanya kazi kwa ufanisi bila gharama kubwa sana, pili litawaonyesha wananchi sio tu mbunge anaweza kuishi na kufanya kazi vizuri kwa gharama ndogo tu, bali pia CHADEMA inajali wananchi kiasi cha kuanza kulifanyia kazi hili mara moja hata kabla halijapitishwa na CCM, na tatu, liataipa CHADEMA uongozi katika swala hili pamoja na kufaidisha maendeleo ya wananchi moja kwa moja.

Naona habari za kusubiri kitu kipitishwe rasmi bungeni zitakuwa ndoto na CHADEMA inaonekana kama inatafuta credit za kupinga mishahara mikubwa kimsimamo, lakini tukifika pale panapohusika hasa, penye kuikubali ama kuikataa mishahara hii, CHADEMA inakuwa haina tofauti na CCM.

CHADEMA itaaminika zaidi ikisema kwa vitendo. Siasa za maneno tushazoea Tanzania, tunachotaka kipya ni vitendo.


Kiranga

Asante.

Nakubaliana na wewe hoja ya umuhimu kwa kwenda mbele zaidi ya kusema kwa maneno kuonyesha kwa vitendo katika mambo ambayo inawezekana.

Mwaka 2005 wakati nagombea ubunge kwa mara ya kwanza niliwaahidi wananchi kwamba asilimia 20 ya mshahara nitaikata na kuiingiza kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kama kichochea cha wadau wengine kuchangia zaidi. Miaka michache iliyofuata kukuaanzishwa mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo (CDCF) ambao unatumia fedha za umma, pamoja na upungufu wa kidhana na kidhima wa mfumo wenyewe lakini ni chombo ambacho kinaweza kutumika katika hatua ya sasa. Ingawaje marekebisho makubwa bado yanahitajika katika sheria husika.

Mfuko huu umejikita katika kutumia fedha za umma, hivyo kama mbunge lazima ndiwe na mfuko wa ziada ambao utagusa nguvu za wadau wengine ikiwemo wananchi na sekta binafsi kwa ujumla. Bado nauchambua kwa kina muundo na mipaka ya CDCF na kuona mfumo wa nyongeza uwe na utaratibu upi halafu nitaweka bayana.

Hata hivyo, kwa vyovyote vile kama mbunge nitatoa sehemu ya mshahara na posho kuchangia katika maendeleo ya jimbo kiwango ambacho hakitashuka chini ya milioni 10 kwa mwaka; kiwango ambacho kitakuwa juu ya asilimia 20 ya mshahara niliyoahidi mwaka 2005. Wakati ule nilikuwa natazama mshahara pekee, lakini kipindi cha mwaka 2006 mpaka 2010 nikiwa nje ya utumishi wa bunge kimenipa mtazamo wa ziada kwamba suala linalohitaji kutazamwa zaidi ni posho za wabunge.

Mchango wa kiwango kisichopungua milioni 10 ni mdogo sana, hivyo ni changamoto kama mbunge kutafuta vyanzo vya ziada vya namna mbalimbali, kwa sasa nimeweka lengo la chini la milioni 100 katika kipindi kifupi; lakini katika kipindi kirefu naamini nje ya bajeti ya fedha za umma, mbunge anaweza kabisa kuhamasisha miradi/mipango ya nyongeza ya kiwango kisichopungua bilioni 1 kwa mwaka. Hili linahitaji muda wa kutosha wa maandalizi na ushirikiano na wadau mbalimbali.

Hofu yangu ni kwamba kadiri jitihada zinavyoelekezwa kwenye jukumu hilo la mbunge kuchangia ama mbunge kuwa mhamasishaji wa michango kwa ajili ya miradi ya maendeleo; inapunguza mantiki na muda wa mbunge kutimiza wajibu wa msingi wa kikatiba ambao ni kutunga sheria na kuiwajibisha serikali.

Ni maoni yangu kwamba kwa ajili ya suluhisho la muda mrefu zaidi la changamoto zetu za maendeleo, nguvu kubwa ya wabunge ielekezwe kwenye wajibu wa kikatiba wa wabunge wa kutunga sheria na kuiwajibisha serikali.

Wabunge tukitekeleza wajibu huu vizuri mathalani sheria ikawezesha vyanzo mbadala vya mapato ama kuondoa mianya ya upotevu wa mapato hususani katika rasilimali na kodi tutaweza kupata fedha nyingi zaidi za kutekeleza miradi ya maendeleo kuliko hata tunazochangisha kwa bakuli. Ama wabunge na madiwani tukahakikisha bajeti mwafaka inapitishwa ambayo inaweka kipaumbele kwenye maendeleo badala ya anasa halafu tukaiwajibisha serikali vizuri zaidi kuhakikisha fedha hazipotei kwa ufisadi na tenda zinatolewa kwa kiwango ambacho miradi inatekelezwa kwa ubora na gharama nafuu basi maendeleo yatayopatikana yatakuwa makubwa kuliko kiwango kinachotokana na posho na mshahara wa mbunge.

Mazoea haya ya wabunge kuchangia fedha zao yanadhalisha siasa za ulezi (patronage) na kulea takrima kwa kiwango ambacho wananchi katika uchaguzi wanaweza kuanza kupiga kura kwa kuangalia ni nani ana 'pochi' kubwa zaidi badala ya ni nani anaweza kushiriki vizuri zaidi katika kutunga sheria na kuiwajibisha serikali.

Tunaweza kufanya mambo yanayoonekena ya kawaida sana, lakini yakawa na tofauti kwenye maisha ya watu kuliko kugawa fedha- mfano, leo visima vya umma huku mtaani maji yanauzwa sh 100 mpaka 200 kwa dumu; wakati kwa mujibu wa agizo la EWURA; maji katika vioski vya serikali yanapaswa kuwa shilingi moja kwa lita ambayo ingefanya ndoo ndogo iwe sh 5, ya kawaida sh 10 na dumu sh 20. Mbunge, Diwani na wenyeviti wa mitaa wakishirikiana kusimamia hili tafsiri yake ni kwamba wananchi wa kawaida kabisa, fedha zao ambazo zingetumika kwenye maji pekee zitabaki mifukoni mwao kwa ajili ya matumizi mengine. Mbunge, Diwani na mwenyekiti wa mtaa wakiwabana watendaji kwenye halmashauri na mamlaka kama DAWASCO sehemu kubwa ya matatizo ya mgawo wa maji usiozingatia hali halisi ingepungua uhaba uliosalia ungefahamika bayana kwa ajili ya kupanga uwekezaji mkubwa zaidi wa kuongeza ujazo wa maji toka kwenye vyanzo na kupanua mtandao wa usambazaji. Kinachohitajika ni kurejesha utamaduni wa uwajibikaji; kwa kuanzia na sisi wenyewe, kila mahali tulipo!

JJ
 
Pia kwa kutumia vikao vya kamati kuu; ondoeni vibaraka kama akina Zito Kabwe! Watakiangamiza chama!!
 
Mh. Mnyika,
Nahisi utakuwa umepata msg yangu leo tr 6 Dec kupitia simu yako ya kiganjani. Issue niliyotaka uifanyie kazi ni ya TANESCO kuwapatia umeme makaaji wa maeneo ya Goba hasa mtaa wa Kulangwa ambao pamoja na kuwa na nyumba za kutosha na shule hauna miundo mbinu hasa umeme. Binafsi kama mkaaji wa huko na mkereketwa nilishakwenda TANESCO Kawe na kuwaeleza shida yetu. Walishatuma ma=surveyors mara tatu na jibu wanalotoa siku zote ni eti nyumba zetu ni ndogo na hivyo ni hasara kwao kutuletea umeme. Najiuliza hivi miundo mbinu si chanzo cha kuvutia wananchi kujenga nyumba kubwa? Naomba utusaidie kama mwakilishi wetu.
 
Mheshimiwa, pamoja na pongezi zangu kwako. Je nawe unaamini katika umoja na utaifa ama utajikita zaidi katika uchama?
 
Hongera sana Mheshimiwa, vipi kuhusu usambazaji wa technolojia ya Bio gas kwenye secondary schools(boarding) na kwenye makazi ya watu na au Magereza na zahanati au clinics, kupunguza matumizi ya kuni au mkaa(wood fuel). Vile vile mradi wa utandazaji wa mabomba ya kupitisha maji ya mvua kuondokana na kero ya kufurika maji mitaani nyakati za mvua. Utengenezaji wa malambo kwa kila kata ambayo yatakuwa yana supply clean water for human consuption kwa kutumia palnt ndogo za kupeleka maji hayo kwa kila kata , pasipo kuwategemea Dawasco mgao wao. How about it we ca send you a package of bio gas, clean water project and sewage....if requested. Once again congratulations and I wish you a healthy family and prosperous in your job.
 
yes mnyika!!!! u can
ukienda bungeni naomba utoe hoja ya kupunguza wageni wanaokuja kufanya kazi hapa nchini hasa kwenye sector binafsi hawana sifa wala huwezo wa kufanya kazi kama expart kama wanavyosema kwenye vibali viyao hasa walimu wa international school dar es salaam na zanzibar,pia kwenye migodini na kwenye mahoteli ya kitalii hasa zanzibar na bagamoyo.
tunataka wabunge makini,wabunge wenye uchungu na tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom