Ujumbe wa Leo: Usiingie kwenye mahusiano kwa sababu ya imani ya mtu, kila kitu kipe nafasi yake kwa wakati wake

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
28,240
63,347
1. Usioe au kuolewa na mtu kisa anahofu ya Mungu!, kwasababu swala la imani ni swala la uelewa na muda wowote mtu anaweza kubadili mawazo,ama kuamini tofauti na alivyokuwa akiamini awali!. kwa ufupi ni kwamba usaliti hutoka kwenye wema.

Tafuta mtu muelewa mwenye upeo wakuweza kujua thamani yako hata kama atakuwa anaamini tofauti ila akishaijua mipaka yake ni afadhari kwenu wote.

2. Kila kitu kipe nafasi yake kwa wakati wake.
Uzuri wako, elimu, fedha, ujuzi na mambo mengine kede uliyobarikiwa yatumie kunufaisha mapenzi yako na sio iwe fimbo kwa mwenzako! kwamaana kuna maisha baada ya hivyo ulivyonavyo na hizo ni nyenzo tu zakujengea furaha ya maisha yako.

Niwatakie siku yenye heri, utamu na utimamu.

Angalizo: Inahitajika fikra kiasi ili uweze kunielewa vyema nilichokiandika,usije ukashupaza shingo kisa ufinyu wa fikra zako.
 
IMG_20240616_123903_960.jpg
 
Back
Top Bottom