Ujumbe wa leo tukielekea kuumaliza mwaka (uandikeni na msisahau)

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,280
2,000
  • Maisha uliyoyaishi mwaka huu na miaka ya nyuma yatatueleza huko mbeleni kuna nini kama ni uovu ni vema tukatubu sasa na kuomba rehema ila tusiyarudie tena.
  • Kila unalo lipanga na kuamua kutekeleza jua kesho yatakuwa na majibu uyapendayo au usiyo yapenda.
Kama wewe ni baba ni mama au kiongozi ulitumia nafasi yako kuwanyanyasa watoto wa kambo au watoto wa jirani au watoto wengine usitegemee mazuri mbele yako hata kama sio leo hata kesho, na uzuri utasahaulishwa kwanza ili badae ukianza kupokea mateso na kichapo hutakumbuka utaona kawaida na kwenda kuhangaika sehem mbalimbali kwa ajili ya msaada. Kwa wanao tenda mema watafurahia mema ya Mwenyezi Mungu, kwa waovu wataishi maisha yao yote ya mateso.

Kama wewe ni kiongozi unatenda yasiyo mema na walio chini yako wanafuata mkondo kwakuwa wewe una nia iyo ovu basi kumbuka mazingira unayowawekea waliopo chini yako huko mbeleni au siku za badae yatakuwa magumu sana na watamlaani shetani huku wakihangaika sehem mbali mbali kwa ajili ya msaada na wasipate kabisa mwisho wa siku majuto mjukuu ila siri itakuwa ni moja tu basi…..

Kaeni na Amani ya Mwenyezi Mungu nawatakia Kheri ya Krismasi na Mwaka mpya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom