Ujumbe wa leo kwa wanadamu wote

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Ayubu 7:17-18
[17]Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza,
Na kumtia moyoni mwako,
[18]Na kumwangalia kila asubuhi,
Na kumjaribu kila dakika?

Mithali 3:1-8
[1]Mwanangu, usiisahau sheria yangu,
Bali moyo wako uzishike amri zangu.
[2]Maana zitakuongezea wingi wa siku.
Na miaka ya uzima, na amani.
[3]Rehema na kweli zisifarakane nawe;
Zifunge shingoni mwako;
Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
[4]Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
[6]Katika njia zako zote mkiri yeye,
Naye atayanyosha mapito yako.
[7]Usiwe mwenye hekima machoni pako;
Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.
[8]Itakuwa afya mwilini pako,
Na mafuta mifupani mwako.


1 NYAKATI. 28:9
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele

Muwe na siku njema
IMG-20190629-WA0021.jpeg
 
Ayubu 7:17-18
[17]Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza,
Na kumtia moyoni mwako,
[18]Na kumwangalia kila asubuhi,
Na kumjaribu kila dakika?

Mithali 3:1-8
[1]Mwanangu, usiisahau sheria yangu,
Bali moyo wako uzishike amri zangu.
[2]Maana zitakuongezea wingi wa siku.
Na miaka ya uzima, na amani.
[3]Rehema na kweli zisifarakane nawe;
Zifunge shingoni mwako;
Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
[4]Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
[6]Katika njia zako zote mkiri yeye,
Naye atayanyosha mapito yako.
[7]Usiwe mwenye hekima machoni pako;
Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.
[8]Itakuwa afya mwilini pako,
Na mafuta mifupani mwako.


1 NYAKATI. 28:9
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele

Muwe na siku njema View attachment 1143630
Amen,ubarikiwe katika jina la Yesu...
 
Inapokuja Neno la Mungu watu kimyaaaaa ingekua kugegedana coments 500+

Maisha ya milele hujengwa ukiwa hai usitegemee sadaka zako na sala za kuombea wafu zikuokoe na Jehanamu ya moto wa milele

, “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kasha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe… Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena” (Ayubu 14:1-2,14)?



BAADA YA KIFO NI HUKUMU.

"Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;" (Waebrania 9:27)

Mtu amepewa nafasi ya kujitetea, kujirekebisha, kujitakasa akiwa hapa duniani. Mtu akisha kufa mwili unabaki mavumbini na roho inakwenda kutoa hesabu ya mambo aliyoyatenda huku duniani.

Kule hakuna nafasi ya kujitetea kama mahakamani, kule ni kusomewa hukumu kulingana na matendo uliyoyatenda. Hakuna kukata rufaa, ukishahukumiwa kinachofuata ni ni utekelezaji wa hukumu tu.

Sehemu ya pekee ya kujitakasa na kuokoka ni hapa duniani, ukifa ni kuhukumiwa tu. Mtu asijidanganye kuwa atatengeneza matendo yake siku ya mwisho, au eti ataokoka siku ya mwisho.

KUMBUKA baada ya KIFO ni HUKUMU tu, hakutakuwa mjadala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom