Ujumbe wa kwaresma 2019 toka TEC

Adilinanduguze2

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
1,189
1,569
UJUMBE WA KWARESMA 2019 ULIOTOLEWA NA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA TEC

FAMILIA KANISA LA NYUMBANI NA NI SHULE YA IMANI NA MAADILI

Wapendwa Waumini,
Kaka na Dada katika Familia ya Mungu,
Na Watu Wote wenye mapenzi Mema,
TUMSIFU YESU KRISTU!

UTANGULIZI

1.1 Ujumbe wa Kwaresima 2019

Kama ilivyo ada kila mwaka, sisi Maaskofu Katoliki hutoa ujumbe mahsusi katika kipindi cha Kwaresima. Kila ujumbe huwa na dhamira maalum ya kuzingatia, ili katika kujitafakari na kuamsha upya maisha yetu ya Imani Katoliki na Maadili yake, tutambue zaidi na tukiri kwa dhati jinsi hali yetu ilivyo mbele ya Mungu ambaye ndiye chanzo cha utakatifu, na sisi kama wadhambi tulio safarini kuelekea huo utakatifu. Hivyo basi, kwa mwaka huu wa 2019 baada ya kuadhimisha miaka 150 ya Kanisa Katoliki Tanzania mwaka jana 2018, tumeona ujumbe wa mwaka huu uzingatie dhamira inayohusu familia zetu. Dhamira hii ni “Familia kama Kanisa la Nyumbani na Shule ya Imani na Maadili”. Kwa mwaka huu basi, tutafakari kwa namna gani hili lifanyike kwa kuzingatia kuwa Familia ya Kikristu ni Shule ya Imani Katoliki na Maadili yake.

SURA YA KWANZA
FAMILIA NI MSINGI WA JAMII YA KIBINADAMU

1.1 Mwaka 2019 kuwa Mwaka wa Familia:

Matunda ya Adhimisho la Jubilei, Miaka 150 ya Uinjilishaji
Kwa kuzingatia hayo, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, pamoja na kuwa na dhamira hiyo, tumeuteua mwaka huu wa 2019 kuwa ni Mwaka wa Familia, kama ishara na fursa ya kutafakari kwa undani zaidi matunda ya adhimisho la Jubilei ya Miaka 150 ya Kanisa Katoliki Tanzania kama Familia ya Mungu. Uamuzi huo unajengwa juu ya sababu kuu nne za msingi kuhusu mwaka huu wa 2019.

Kwanza, ni miaka ishirini na mitano tangu ilipoazimishwa Sinodi ya kwanza ya Afrika, ambapo Kanisa lilikubaliana na mtazamo wa Kiafrika kuwa Kanisa ni Familia ya Mungu. Kwa hivyo, kiimani na kijamii binadamu anakiri kwamba familia ndiyo msingi wa jamii ya kibinadamu, na hivi kuijenga familia imara ni kuwa na jamii na Kanisa imara. Mababa wa Kanisa walielezea familia kuwa ni kiini cha kwanza na cha uhai wa jamii. Kama tunavyosoma kutoka Ecclesia in Africa , “Kwa kuwa Muumba wa vitu vyote ameanzisha ushirika wa mume na mke kama asili na msingi wa jamii ya kibinadamu, familia ni kiini cha kwanza cha uhai wa jamii.” (Ecclesia in Africa no. 85 ).

Lakini Kwaresima hii tunaalikwa kutambua utume wa Familia kupitia wanafamilia ambao wengi wao ni walei, kama Mababa wa Kanisa wanavyotuambia kwenye Mtaguso wa Pili wa Vatikano: “Ni juu ya walei ,kutokana na wito wao, kutafuta ufalme wa Mungu wakiyashughulikia mambo ya dunia na kuyaelekeza kadri ya Mungu. Wanaishi ulimwenguni, yaani katika kazi zozote na shughuli za kidunia na katika mazingira ya kawaida ya maisha ya kifamilia na ya kijamii, ambayo maisha yao yamefungamanishwa nayo. Hapo wanaitwa na Mungu kusaidia kuutakatifuza ulimwengu, kama kutoka kwa ndani, mithili ya chachu, katika kuyatimiza majukumu yao wenyewe, wakiongozwa na roho ya kiinjili, na hivyo wamdhihirishe Kristo kwa wengine, waking’aa hasa kwa ushuhuda wa maisha yao, imani, matumaini na mapendo. Kwa hiyo yawahusu hao kwa namna ya pekee kuyatangaza na kuyapanga mambo yote ya kidunia, ambayo wamefungamana nayo, ili daima yafanyike na kukua kadri ya Kristo na kuwa kwa sifa ya Muumba na Mkombozi”( Lumen Gentium no. 31 ). Ili hiki kitelezeke inabidi familia iwe imara kiimani na kimaadili.

Pili, mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka ishirini na tano tangu pale Umoja wa Mataifa ulipotamka kuwa mwaka 1994 ni mwaka wa familia. Ni vema tukanukuu maneno ya msingi kuhusu nia ya Umoja wa Mataifa kwa kutenga mwaka huo kuwa ni mwaka wa familia.Umoja wa Mataifa ulitamka kwamba:
“Familia inaunda kitengo cha msingi cha jamii na kwa hiyo inahitaji kuhakikishiwa uangalizi maalum. Hivyo basi, ulinzi mpana kabisa iwezekanavyo na msaada husika lazima vitolewe kwa familia zote ili nazo ziweze kuchukua majukumu yake ndani ya jamii, kutokana na matakwa ya Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu, Tamko kuhusu Ustawi na Maendeleo ya Kijamii, na Mkataba wa Kufutilia Mbali Namna Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake” [1] .

Familia ni kitovu/kiini cha jamii (cell of the society ) na ni lazima ijengeke katika hadhi ya binadamu kadri ya hulka ya binadamu iliyokusudiwa na Muumba, na sivyo inavyotafsiriwa bila kurejea kwa Mungu.Hii ndiyo italeta umaana wa familia kuwa msingi wa jamii. Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili anathibitisha kuwa ukweli unaojikita kwenye hulka upo kwenye jamii tayari kama wote tuko kwenye hulka aliyoitengeneza Mungu kama wote tunakubaliana naye. “The splendour of truth shines forth in all the works of the Creator and, in a special way, in man, created in the image and likeness of God (cf. Gen 1:26). Truth enlightens man’s intelligence and shapes his freedom, leading him to know and love the Lord” ( Veritatis Splendor page no.1).

Tatu, mwaka huu pia ni mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 tangu Halmashauri ya Walei ya Kanisa Katoliki ilipoanzishwa mwaka 1969. Kwa kuwa Halmashauri ya Walei katika ngazi zake zote inayo Kamati Ndogo inayohusika na Familia na Malezi, ni haki na ni vema Dhamira ya Familia ikawa ndiyo kiini mwafaka cha ujumbe wa Kwaresima kwa mwaka huu tunapoidhimisha Jubilei hiyo. Na hasa kwa sababu zaidi ya asilimia 90 ya Waumini Wakatoliki ni walei wanaotakatifuza malimwengu kupitia maisha ya kitume katika familia zao, kama baba na mama, au babu na bibi, au mjomba na shangazi, au kaka na dada, shemeji au binamu. ( Gaudium et Spes , no. 43 / Lumen Gentium , no. 31, 33).

Nne , mwaka huu pia ni adhmisho la mwaka wa Jubilei ya Dhahabu (Miaka 50) tangu chama cha kitume kinachowaunganisha wanafunzi wote Wakatoliki walioko sekondari; chama kinachojulikana kwa jina la Young Catholic Students, au kwa kifupi YCS. Kwa kuwa vijana bado wako chini ya wazazi wao na familia kwa upana wake kimalezi na kimakuzi, ni mwafaka basi tukatafakari kwa namna gani familia zinaweza kuwa kweli shule za Imani Katoliki na Maadili Yake kwa vijana hawa ambapo kwa sasa tunaona wengi; idadi yao kitakwimu ni takribani zaidi ya milioni moja na laki saba kidato cha kwanza hadi cha sita. Hiki chama cha kitume katika jubilei yao ya miaka hamsini hatuna budi kama familia tutafakari upya tuwaongezee malezi gani ili wawe raia wema zaidi, na hatimaye waweze kuwa msingi katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani na mbinguni.

1.2 Haja na Hoja ya Kuitafakari Familia

Leo hii, baada ya neema, baraka na mwanga zaidi wa Jubilei ya miaka 150 kuhusu nini maana ya kuwa Mkristu; maana na utume wa Familia ya kikristu ni vitu ambavyo haviwezi kuendelea kuchukuliwa juujuu tu; ni lazima vitamkwe kwa dhati, vielezwe upya, vitetewe bila mashaka yoyote, na wanafamilia wenyewe watoe ushuhuda kwa jamii nini maana ya familia, kuwa ni Kanisa la nyumbani, na hivyo kuwa ni Shule ya imani na maadili.

Sababu kuu ya kuwa na msimamo thabiti juu ya familia ni nini na ndoa na maana halisi ya ndoa, ni kwa sababu leo hii kuna dhana potofu na hata nadharia zisizo sahihi zinazolenga kuhalalisha vitendo vinavyopelekea kutenganishwa kwa ndoa na familia.
Kutenganisha huku kunatokana na dhana yenye maana potofu ya ndoa inayotolewa kwamba ndoa ni maridhiano ya wawili bila kufungamanishwa na jinsia zao. Hii ni maana potofu inayotetewa na baadhi ya jamii. Hii ni dhana iliyopotoka kihulka (unnatural), kiimani na kimaadili. Imani Katoliki na maadili yake inapingana kabisa na mtazamo wa namna hii, au hoja zinazoweza kutokana na mtazamo kama huo.
Hii ni kwa sababu Muumba wa vitu vyote ameisimika taasisi ya familia kwa kuweka muungano wa kindoa kati ya mwanaume na mwanamke kuwa ndiyo chanzo na msingi wa jumuiya ya kibinadamu, yaani familia.

Kwa maana hiyo, familia ndiyo kiini cha kwanza cha uhai wa jamii. Siku zote tutilie maanani kuwa katika mpango wake Mungu Muumba, mahali pa msingi ambamo watu wanajifunza kuwa watu ni kwenye familia. Hii inamaanisha kuwa ni katika familia ambamo kila mtoto kwanza anajifunza uwepo wa Mungu, kumpenda Mungu huyu, kutenda yanayoendana na huyu Mungu na mtoto huyu kutamani kuungana na Mungu huyu milele. Mtoto hupokea haya kutoka kwa wazazi wake na walezi wake, yaani kutoka kwenye familia.

1.3 Changamoto Zinazoikabili Familia ya Sasa

Kazi kubwa ya Kristo ilikuwa ni kumkomboa mwanadamu dhidi ya dhambi na matokeo yake mabaya (Rej.Lk. 4:18-19; Lk. 5:20, 27-32). Kanisa kama mwili wa fumbo wa Kristo linao wajibu wa msingi wa kuendeleza kazi ya Kristo kwa wanadamu. Mahali pazuri pa kufanya kazi hiyo ni kupitia familia ambapo mtu hupata uhai na malezi ya kiutu na kiroho.
Kwa kuzingatia hali ya sasa na changamoto zake katika familia na ndoa jitihada zozote za kuelimisha jamii juu ya mpango wa Mungu kwa kila binadamu hapa duniani, lazima familia zetu zijipange kukabiliana na changamoto zile zinazoukabiri ulimwengu wetu wa sasa katika karne ya ishirini na moja na nchi yetu ya Tanzania ikiwemo. Changamoto hizo ni kama vile:-
· Talaka,
· Ndoa za utotoni
· Uchumba sugu
· Ndoa za mitaala
· Kukosa uaminifu ndani ya ndoa
· Ndoa za kurithi wajane
· Ndoa za Jinsia moja
· Ndoa baada ya ndoa ya kwanza halali
· Ndoa zisizo na watoto
· Kubadili maumbile
Ø Familia za mzazi moja
Ø Familia zenye mchanganyiko wa Imani
Ø Familia zinayoishi katika mazingira magumu ya uchumi
Ø Familia zenye watoto walemavu
Ø Familia zisizo na mzazi hata mmoja
Ø Familia zisizoishi imani
Ø Familia zisizo na maadili
Ø Familia zilizopoteza uwezo wa kulea
Ø Familia zisizo na kipato.
Asili ya matatizo katika ndoa na familia ni pamoja na:-

1.3.1 Utamaduni na Mazingira.

Tunaishi katika historia yenye mazoea, mila, desturi na mapokeo ya wazee wetu. Iko sehemu ya utamaduni wetu isiyokubaliana na ukweli wa kimungu ambao ni wa lazima katika kuishi ndoa safi na familia bora. Mpaka sasa katika mazingira yetu zipo tamaduni zinazoruhusu talaka, ndoa za utotoni, uchumba sugu, ndoa za mitaala, “nyumba ndogo”, ndoa za kurithi wajane, ndoa za jinsia moja na ndoa baada ya ndoa ya kwanza halali.
Ni jukumu la kila mkristu, ndani ya familia, kuchekecha utamaduni wake, kwani kumekuwa na chenga zisizopita katika chujio la Kristo aliye Mwanga wa maisha yetu.

1.3.2 Harakati za kila mmoja ambazo zinalenga moja kwa moja kuibomoa familia

Harakati hizi zinatangaza na kupigia upatu uhuru usio wa kweli kwa mwanadamu. Zinapotosha ukweli kwa kutenganisha ukweli wa maisha na ukweli wa asili katika viumbe na maumbile yao. Maisha ya kiroho, maisha ya ndoa na familia, yanakuwa ni jambo binafsi na la faragha bila kuhusisha jamii na wala kumhusisha Mungu. Uhusiano wa mtu na jamii unahuishwa katika sheria tu ambazo jamii inazitunga na kuzibadili mara kwa mara.
Matokeo mabaya ya harakati hizi ni kukithiri kwa ubinafsi, kuenea na kuzagaa kwa matukio yenye kuchochea waziwazi tamaa za ngono kati ya watu wa rika zote. Wimbi kubwa la maisha huria, bila malengo wala kanuni na nidhamu ya kukataa malengo mema.

Kuongezeka kwa mifarakano ya ndani ya nafsi na hivyo mifarakano kati ya mtu na mtu ndani na nje ya familia kunakoshuhudiwa na matatizo ya msongo wa mawazo, hali ya kukata tamaa.
Harakati hizi zimejaa kwa wengi, na pia mtazamo potofu kuhusiana na maadili katika ndoa na familia. Na hivi mtu kufikia mahali kujiaminisha kwamba maisha yanawezekana bila Mungu na bila utu.
Msimamo huu haumwezeshi mtu kupokea na kudumisha tunu njema za maisha ya ndoa na familia, ambazo kuasisi tunu hizo huzifanya ndoa na familia zifanyike katika kweli na zidumu na kusitawi na kuzaa matunda.
Changamoto za ndoa na familia kimsingi ni changamoto za kukubali na kupokea tunu za maisha ya ndoa na familia. Tunahitaji kujihoji mbele ya Kristo juu ya wito wa kuwa wavumilivu, wasamehevu, wenye kiasi na wenye subira Rej. 1Kor.13:1-8).

Tunahitaji kujipima tena kama tunazithamini na kuvutiwa nazo zile heri nane alizozitangaza Bwana wetu Yesu Kristo ambazo ni usafi wa moyo, upole, unyenyekevu, upatanisho, kuudhiwa kwa ajili ya haki, kukubali kushindwa/kudhulumiwa kwa sifa na utukufu wa Mungu (Mt.5:3-12).
Tunahitaji kujithamini mbele ya Mungu, kuona thamani ya upendo wa Kristo kwetu na wa yule aliyetupatia Kristo. Maana “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye” (Rum.8:32). Hakuna anayeweza kututenga na upendo wa Kristo (Rum.8:35-39).
Utatuzi wa matatizo mengi katika ndoa unajikita kimsingi katika changamoto ya kurudisha sura njema ya maagano kati ya Mungu na katika utakatifu kati ya Kristo na Kanisa lake (Rej.Waefeso 5:21-25).

Wakristo wenye ndoa na ni wazazi kwa njia ya ubatizo wao wanawajibika kutoa mchango wao wa pekee kwa ajili ya kufafanua mafundisho na tunu za kiinijli katika mazingira na tamaduni mbalimbali za leo ambamo kwazo wanafamilia huishi maisha ya familia. Wanandoa kwa namna ya pekee wamestahilishwa jukumu hilo kwa sababu ya karama yao na jukumu lao la kisakramenti hasa sakramenti ya ndoa. Wanandoa kwa kuheshimu mpango wa Mungu hubeba jukumu kuu la kuwa wazazi ambapo hukubaliana na wito wa Mungu kuwaleta duniani watoto. Mungu huendeleza kazi yake ya uumbaji na kuendeleza uhai wa kimwili na kiroho kwa kuwatumia wazazi. Hivi kukubali kuwa mwanandoa ni kukubali jukumu la kuuweka uhai wa binadamu kuwa ni jukumu la kimungu linalomtaka mtu amsikilize Mungu Muumbaji na anaye- takatifuza.

1.4 Hali ya Familia katika Ulimwengu wa Leo

Katika ulimwengu wa leo, familia hujikuta katika hali ambayo uhuru wa mtu binafsi huonekana kuwa na nguvu kubwa katika kufanya maamuzi juu ya maisha ya ndoa. Kwa watu wenye kufuata utamaduni huu huathiri tunu za ndoa zinazotokana na Injili. Hulka ya binadamu na utu wa mwanandoa huonekana kutenganishwa na kusudio la Mungu la kumuumba mwanadamu. Mungu amemuumba mwanadamu kwa sura na mfano wake yaani ukutanapo na mwanadamu kwa kutumia milango ya fahamu na akili unapaswa kuuona uwepo wa Mungu aliye hai.

Ni dhairi ya kuwa leo hii ipo hali mbaya ya udhalilishaji wa tunu za msingi kama vile:-
– Maana isiyo ya sahihi ya kinadharia na kiutendaji kuhusu uhuru wa wote waliooana kwa kuhusiana wao kwa wao;
– Mawazo potofu kuhusu uhusiano wa mamlaka kati ya wazazi na watoto;
– Hali halisi ya matatizo ambayo kwayo familia hupata katika kurithisha tunu za familia
– Kuongezeka kwa idadi ya talaka
– Pigo la uharibifu wa mimba
– Utumiaji wa daima wa madawa ya kuua kizazi
– Kujitokeza dhairi mwelekeo wa fikra za uzuiaji wa mimba n.k.

Kwa hiyo maisha hayatambuliwi kama ni zawadi na baraka, bali kama ni hatari kuu ambayo inabidi kujihadhari nayo.
Hali hii ndiyo imetufanya sisi Maaskofu wa Tanzania kuwaletea tafakari juu ya familia ili Kanisa liweze kupambana na hali ya upotoshaji wa matumizi ya uhuru binafsi juu ya ndoa na familia. Mwanadamu aliye nje ya mpango wa Mungu juu ya ndoa na familia amesababisha uvunjivu wa mahusiano kati ya mtu na Mungu na hata kati ya mtu na mtu kadri ya msemo wa Mt. Augustino, mgongano wa hali ya mapendo ya kumpenda Mungu kiasi cha kudharau nafsi na kupenda nafsi kiasi cha kumdharau Mungu (St. Augustine, De Civitate Dei, XIV, 28: CSEL, 40: II56-57).

Licha ya mchango chanya wa utandawazi na mwingiliano wa tamanduni mbalimbali mwanafamilia aliyelelewa na kujilea kwa kuheshimu mpango wa Mungu amejikuta katika giza pale anapojikuta katika utamaduni ambapo mtu anajipangia kila kitu juu ya ndoa na familia bila kumhusisha muumba wake. Tuliwaona wana waisraeli na hata desturi za jamii mbalimbali siku za nyuma walivyompa Mungu nafasi ya pekee katika kufanya maamuzi yao juu ya ndoa na familia.

Hali ya kumweka Mungu pembeni katika masuala yahusuyo ndoa na familia inasababisha upotoshaji mkubwa juu ya maana ya ndoa na familia. Kupotosha huku kumepelekea kuwa na baadhi ya watu kushindwa kujenga mshikamano na Kristu aliye mkombozi pekee wa mwanadamu. Watu wanaopotosha mpango wa Mungu juu ya ndoa na familia wanaweka mazingira magumu kwa kazi ya Yesu Kristo na hata kusababisha utawala wa Yesu Mfufuka usiwe bayana kwenye jamii. Yesu amekuja kuunda jamii inayotokana na familia zinazoongozwa na Neno la Mungu ambalo ni chakula kiletacho uzima wa milele kwa wanafamilia.
Ili kurejesha uelewa sahihi na maisha sahihi ya wanandoa na wanafamilia watu wote tunaalikwa na Huruma na Upendo wa Mungu unaotualika kuongoka. Na hapa kitakachotupatia mwanga katika safari ya kuuelekea wongofu, ni Maandiko Matakatifu, yaani Biblia Takatifu pamoja na nyaraka mbali mbali za Mababa Watakatifu.

SURA YA PILI
2.0 FAMILIA KATIKA BIBLIA KWA UJUMLA

Kwa kuwa chimbuko la Imani Katoliki ni Kristu Mfufuka, ambaye anaendelea kuilea jamii ya kibinadamu kama Mkombozi pekee wa binadamu wote hatuna budi kuyatumia Maandiko Matakatifu katika kuielewa familia. Yesu huyu aliyezaliwa Nazareti katika jamii na familia ya Kiyahudi anaendelea kuongea na binadamu kupitia maisha katika yeye, na kupitia Maandiko Matakatifu, tunayoyapata kwenye Biblia Takatifu.
Turejee baadhi ya sehemu za Maandiko Matakatifu na desturi za Kiyahudi ili kujenga msingi na hoja ya kiimani kuhusu maana ya kuiona familia kuwa ni shule ya Imani na maadili.

2.1 Nafasi ya Familia katika Agano la Kale

Uelewa wote wa Kiyahudi juu ya maisha ya familia, uwe mzuri au mbaya ulitegemea sana Maandiko Matakatifu hasa kitabu cha Mwanzo 1:26-28:
“ Mungu akasema, ‘Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.’ Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia. Mungu akawaambia, ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi’”.
Kadiri ya Maandiko Matakatifu familia ni taasisi inayounganisha mwanaume na mwanamke, na hawa ndiyo wanaoleta mwendelezo wa uhai wa binadamu wengine na kuunda jamii ya kibindamu inayotawala dunia.

2.2 Nafasi ya Mtoto na Familia katika Agano la Kale

Wayahudi walifurahia na kuheshimu familia, lakini hasa familia pana ilikuwa tunu ya pekee. Kwa namna hii hakukuwa na nafasi ya walea pweke wala watu wa jinsia moja kuoana kwa maana katika hali kama hizo kusingewezekana kujenga familia yoyote.
Kupata watoto wengi tangu mapema kulikuwa jambo muhimu na la baraka. Haya ndiyo yanayofafanuliwa na Zaburi ya 127. Zaburi hii inasifia baraka ya kupata watoto wengi mtu angali kijana maana angeliweza kusaidiwa nao mapema, mathalani, kutetewa mahakamani. Mzazi aliruhusiwa kuwatumia watoto wake wa kiume kama mashahidi wa upande wake. Ndipo tunaposoma, “ Watoto ni riziki kutoka kwa Mungu Mwenyezi, watoto ni tuzo lake kwetu sisi. Watoto walio na nguvu ni kama mishale mikononi mwake askari. Heri mtu aliye na mishale hiyo kwa wingi. Hatashindwa atakapokabiliana na adui mahakamani” (Zab 127:3-5). Kwa namna hii inaeleweka kwa nini kuzaliwa kwa watoto kulikuwa matukio ya furaha kubwa ndani ya familia.

2.3 Maisha ya Ndoa kadiri ya Sheria ya Kiyahudi

Awali ya yote, Wayahudi walilichukulia suala la kuoa na kuolewa kama amri ya kimungu kwa sababu ya amri iliyotolewa wakati wa uumbaji. Mwa 1:28 ilieleweka kama uanzishwaji wa taasisi ya ndoa na maisha ya familia. Hivi useja uliokuwa ukifanyika huko Qumran lilikuwa jambo la nadra sana. Ni kwa sababu hiyo, Yesu na Paulo, hapo mbele, walipoeleza kwamba mtu angeliweza kuacha kuoa au kuolewa kwa ajili ya ufalme wa Mungu, waliwashtua Wayahudi wengi (rej. Mt 19:1-12, 1Kor 7:1-16. 25-35).
Kwa kadiri ya uelewa wa Kiyahudi au wa kirabbi, maisha ya ndoa ndiyo yalikuwa hali mujarabu kwa kila mwanaume na mwanamke. Ndipo, kwa Wayahudi, mtu kuoa au kuolewa lilikuwa wajibu wa kidini. Wayahudi walifundishana kwamba maisha ya familia ndiyo yalikuwa utimilifu wa utu. Hata hivyo, aliyewajibika kuingia katika maisha ya ndoa alikuwa mwanaume siyo mwanamke. Kwa mwanamke haikuwa lazima kuolewa isipokuwa alishauriwa asiishi peke yake. Hivyo ndivyo ilivyotafsiriwa katika Kitabu cha Mwanzo 1:28.

2.4 Jinsia ya wenye Kuoana

Je, wenye kuoana wawe watu wa jinsia zipi? Mintarafu watu wa jinsia gani, Biblia nayo haina utata, ni mume na mke yaani watu wawili wa jinsia tofauti. Hao ndiyo watu wanaoweza kuzaana na kutimiza agizo la kuijaza dunia (Mwa 1:28). Matakwa ya Mungu ni watu wawili wa jinsia mbili tofauti. Tena, watu wawili wakitofautiana jinsia ndipo tunapoweza kusema mmoja anaoa na mwingine anaolewa.
Wanaume wawili hatuwezi kusema mmoja anaoa na mwingine anaolewa mpaka mmoja ahesabiwe kuwa mume na mwingine ageuzwe kuwa mke, jambo linalogeuza maumbile aliyowatakia Mungu. Watu wa jinsia mmoja ni kama chanya na chanya au hasi na hasi, hawawezi kutimilizana. Mwanamume na mwanamume hawawezi kuwa mwili mmoja wala wanawake wawili hawawezi kuwa mwili mmoja.

Marufuku ya Biblia ambayo hatuna mamlaka ya kuibadili imeandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22-24 hivi, “Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kama kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo. Kamwe usilale na mnyama ili usijitie unajisi, mwanamume au mwanamke yeyote kamwe asifanye hivyo, kufanya hivyo ni upotovu. Msijitie najisi kwa kufanya mambo hayo kwani kwa sababu ya mambo hayo nayafukuza mataifa yaliyo mbele yenu kwa vile hufanya hayo na kujitia najisi. Nchi yao ilitiwa najisi nami nikaiadhibu nayo ikawakataa wakazi wake.”
Hii ndiyo kawaida ya neno la Mungu kwenda kimuhtasari. Kumbe, haikuwa lazima kuorodhesha hapa kila aina ya dhambi. Maovu ya aina hii tunayosema yote yanamedokezwa na kumaanishwa hapa.
Lakini, kwa kuwa neno la Mungu linapokezana mafundisho, maovu ya sampuli hii, yaani dhambi hizi, zimedokezwa na kukemewa kwa msimamo usioyumba siyo tu katika Agano la Kale bali hata kwenye Agano Jipya.
Tunasoma, “Kwa sababu walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika,wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege na ya wanyama na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo, Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakibadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili, wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa…. Wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu ya kwamba wayatendao hayo wastahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana na wayatendao” (Rum 1:21-28,32).

2.5 Nyumba ya Familia

Maisha ya familia yaliwekewa makazi. Heshima ya familia ilikuwa pia kuwa na nyumba, yaani makao. Basi, mintarafu mahali familia zilipoishi, zamani hizo, familia nyingi za Kiyahudi ziliishi kwenye nyumba ndogo ambazo kimsingi zilikuwa chumba kimoja tena kisichokuwa na dirisha (rej. Lk 15:8). Nyumba ilikuwa haifungwi; stoo peke yake ndiyo iliyokuwa ikifungwa (rej. Mt 6:6). Usiku familia nzima ililala pamoja na kujifunika shuka moja (rej. Lk 11:7). Kwa kuonesha uhai wa familia, taa za majumbani mwa Wayahudi zilikuwa hazizimwi siku zote. Kuzimika kwa taa hizo kulimaanisha kifo cha familia. Ilikuwa wajibu wa mama kutafuta mafuta taa ya familia isizimike. (Mit 31:18).

2.6 Malezi ya watoto katika imani na maadili kwa Wayahudi

Katika sehemu tuongelee kwa karibu zaidi jinsi Biblia inazungumzia makuzi ya watoto wa Kiyahudi, malezi yao na kufundishwa kwao hata kuwa watu wa imani na maadili stahiki. Tuanzie mwanzoni kabisa, yaani tuanzie tangu kuzaliwa kwa watoto.

2.6.1 Masuala ya Kuzaliwa Mtoto

Mojawapo ya furaha za familia ya Kiyahudi ilikuwa ni kupata uzao. Ndipo familia za Kiyahudi zilifurahia sana ujauzito wa mama kwa sababu zilitambua kwamba ujauzito ulikuwa ndiyo ishara ya Mungu kuwabariki na kuwajalia kushiriki kazi ya uumbaji kwa ajili ya kuijaza dunia (rej. Mwa 1:27-28). Lakini kwa kutokana na ufinyu wa elimu ya viumbe (biolojia), walikuwa na miiko mingi waliyodhani inalinda ujauzito.

2.6.2 Siku ya Kuzaliwa Mtoto

Siku ya kuzaliwa mtoto ilikuwa na mambo yake pia. Katika siku yenyewe ya kuzaliwa mtoto, wakunga na tabibu walihitajika kumsaidia mwanamke anayezaa katika utungu wake. Wahudumu hao walisamehewa mambo mengi hata shughuli za Sabato. Yaani waliruhusiwa hata kuivunja Sabato.

2.6.3 Malezi ya Watoto

Kimsingi, malezi ya mtoto wa Kiyahudi yalikuwa ya kidini. Kupanga uzazi kuliendana na kipindi cha kunyonyesha. Wayahudi walihimizana kuwanyonyesha watoto wao kwa miaka miwili au mitatu na walipaswa kulelewa kidini kabisa.
Watoto walipoanza kusema tu, walifundishwa kutamka mambo matakatifu na majina mbadala ya Mungu, ndiyo Adonai, Maqom, Shem na Shamaim. Mintarafu sala, “Shema” (Kum 6:4-9) ilikuwa ndiyo sala ya msingi. Watoto walipofikisha miaka mitano walifundishwa kusoma Maandiko Matakatifu.
Watoto wa kiume, tofauti na watoto wa kike, walipaswa kuhudhuria masomo ya chekechea kwenye sinagogi ya karibu. Watoto wa kiume walipofikisha umri wa miaka 12 walipaswa kushika sheria ya Musa. Walipofikisha umri huo, walifanyiwa ibada maalumu ( Bar Mitzvah ) na tangu wakati huo waliruhusiwa rasmi kusoma masomo ya kiliturujia kwenye sinagogi. Shuleni kwao wanafunzi wote walitakiwa kujifunza masimulizi ya tukio la Kutoka Misri.
Injili ya Luka 2:41-45 inasimulia jinsi Maria na Yosefu walivyomlea Yesu Kristo kidini. Walimlea kwa kadiri ya sheria ya Kiyahudi. Utamaduni wa kitalmudi ulielekeza kwamba watoto hata wadogo sana walitakiwa kufika hekaluni wakati wa sikukuu. Ndiyo kisa Yesu hakuachwa pembeni. Kwa kawaida, wavulana walifikia balehe walipofikisha umri wa miaka 12 na ni kuanzia wakati huo walipoanza kuwa huru kwa kiasi fulani. Jambo hili ndilo linaloeleza, siku ile ya kupotea Yesu, kwa nini wazazi wake mwanzoni hawakuwa na wasiwasi sana na mahali alipokuwapo kwa vile “walidhani kuwa yumo katika msafara”. Wazazi hao walianza tu kuhangaika mwishoni mwa safari ya siku moja.

2.6.4 Malezi Endelevu ya Watoto

Wazazi waliwaanzishia watoto wao, hasa wa kiume, malezi ya imani na maadili au dini kwa ujumla. Baada ya kufundishwa dini nyumbani na kuzoeshwa sala na kuingizwa katika desturi ya kushika sheria ya Musa, watoto wa kiume walipenda wenyewe kujifunza dini kwa kina kutoka kwa marabbi maarufu. Ndipo watoto walipojichagulia wenyewe walimu na kujipatia elimu kutoka kwao. Kujipatia elimu huku kuliitwa “kukaa chini ya miguu ya mwalimu” au “kumfuata mwalimu.”
Shuleni, ndiyo katika kumfuata mwalimu, Myahudi alijifunza sheria ya Musa, historia ya kutoka Misri, namna ya kufafanua Torati, mambo ya imani kwa ujumla na maadili. Kwa kufundishwa maadili, Wayahudi walitumia vitabu vya hekima, hususan, kitabu cha Yoshua ben Sira, kama vitabu vya kiada.
Ndani ya vitabu vya hekima Wayahudi walifundishwa mambo mbalimbali, mathalani, mambo ya kuwaheshimu watu, kulea watoto, kazi, urafiki, afya, furaha, nidhamu katika kunywa divai, ukweli wa mateso, ukweli wa kifo, ujasiri na sifa za watu wa zamani, utawala, umuhimu wa hekima na kadhalika. Mambo hayo yalifundishwa kwa mitindo ya kukaa pamoja kwa amani, kuulizana maswali, kujadiliana na kupeana mifano.
Mtu alikaa chini ya miguu ya mwalimu au alimfuata mwalimu kwa takribani miaka 38 ndipo alipofuzu na mtu akawa Farisayo au Mwandishi wa sheria. Aliyefuzu kama Farisayo aliweza kuwa mwalimu na yeye kufuatwa na wanafunzi wa kwake. Aliyefuzu kama Mwandishi wa sheria aliweza kuwa mnakili vitabu vitakatifu na kufanya kazi za uwakili au uhakimu.
Hata hivyo, matokeo ya jumla ya kujiendeleza katika dini yalikuwa kila baba kuweza kumudu vyema shughuli ya kuisimamia familia yake katika kuikuza, kuilea na kuidumisha katika mambo ya dini kama tulivyoona wajibu za baba.

2.6.5 Ukomo wa Watoto Kuwatunza Wazazi Wao

Watoto walipaswa kuwatunza wazazi wao maisha yao yote, yaani mpaka kufa kwao (rej. Mit 23:22 na YbS. 3:1-16). Kutokuwa na mwisho kwa wajibu huo wa kuwatunza wazazi ndiko kulikowafanya watoto jeuri au wakorofi kutumia vibaya kanuni ya “korbani”, yaani kuweka wakfu mali zao ili kukwepa kuzitumia katika kuwatunza wazazi wao (rej, Mk 7:9-13). Kanuni hiyo ilisema mtu akiweka mali yake wakfu, yaani kumwekea Mungu, alikuwa haruhusiwi kuitumia kuwasaidia wala kuwatunzia wazazi wake. Kwa namna hii kanuni hii ilitumika vibaya na Yesu alifuta tabia hii (rej. Mk 7:8-13).
Kutokana na ukweli wa wajibu wa watoto kuwatunza wazazi wao mpaka kufa kwao, tunapata ushahidi kwamba Yesu alikuwa mtoto wa pekee kwa Bikira Maria na Yosefu, maana kama angelikuwa na kaka na dada zake wa damu, Yesu asingelimkabidhi mama yake kwa mwanafunzi aliyempenda. Kama wangelikuwapo ndugu zake wa damu, Yesu angelipata urahisi mkubwa wa kuwakumbusha wajibu wao wa kumtunza mama yao mpaka kufa kwake. Tena mahangaiko hayo hayo ya Yesu, ya kumkabidhi mama yake kwa mwanafunzi aliyempenda, yanatudokezea kwamba wakati Yesu anakufa, Yosefu alikuwa ameshakufa, vinginevyo asingelithubutu kumtenganisha mama yake na baba yake huyo (rej. Yn 19:25-28).

2.6.6 Uonevu kwa Akinamama

Maisha ya ndoa ya Kiyahudi yalihusisha mambo mawili magumu, talaka na kurithi wajane. Kati ya Wayahudi kulikuwa na uonevu mkubwa uliojengwa juu ya maisha ya ndoa. Wayahudi walipojaribu kufafanua Kumbukumbu la Torati 24:1-4 iliyotoa ruhusa mume kumwandikia talaka mkewe na kumfukuza toka nyumbani mwake, yaani kumwacha, marabbi wawili wakubwa waliwagawanyisha watu. Suala lenyewe lilikuwa juu ya maana ya “neno ovu” (erwat dabar ) ambalo lilimruhusu mume kumwacha mkewe kwa sababu yake. Rabbi Hillel aliwafundisha Wayahudi kwamba waliruhusiwa kuwaacha wake zao kwa sababu yoyote ( erwat dabar ) walioiona wenyewe kuwa nzito. Rabbi Shamai hakuleta nafuu yoyote maana naye aliruhusu talaka ingawa yeye alisisitiza kuwepo sababu nzito inayohusiana na kuonekana kwa uchi wa mke, kama vile, ugoni au kuvaa ovyo mbele ya watu.
Kuhusu hili,hata Yesu mwenyewe alipinga sana desturi ya talaka kama tunavyosoma katika Maandiko Matakatifu; “ Wafarisayo kadhaa walimjia, wakamwuliza kwa kumtega, “Je, ni halali mume kumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?” Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke, na akasema: kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba na mama yake, ataungana na mke wake nao wawili watakuwa mwili mmoja?” Kwa hiyo wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe!” (Mt. 19:3-6).
Shauri la kurithi wajane lilikuwa la ajabu sana. Wayahudi walikuwa wanahimizana kurithi wajane kwa sababu walau tatu. Mosi, walitaka kuhakikisha mali ya ndoa iliyokoma kwa kifo cha mume haiendi mbali. Pili, walikusudia kumsitiri mjane asifikwe na taabu sana.

Tatu kwa kuwa waliamini kwamba Mungu atakuwa anawataka watu walioona ushahidi wa kumwonesha mtoto waliomzaa walitaka kutatua tatizo la kukosekana ushahidi wa aina hiyo kwa watu waliopata bahati mbaya ya kutokuwa na mtoto walipoishi pamoja. Ilikuwa kwamba kama kaka alimwacha mjane pasipo mtoto, ndugu yake au jamaa yake alipaswa kumchukua mjane na kumzalia mtoto, mtoto alihesabika kuwa mali ya marehemu (rej. Kum 25:5-10). Jambo hili liliwakandamiza akina mama kwa sababu waliweza kufedheheshwa kwa kukataliwa na shemeji au ndugu za marehemu na pengine alitakiwa kumgonja shemeji mdogo akue hadi aweze kuamua kumchukua au kutomchukua.
Kuhusu kurithi wajane, Yesu katika Luka 20:27-38 alijibu swala la jane kuwa ni mke wa nani baada ya ufufuko.

2.6.7 Majumuisho ya Maelezo ya Agano la Kale

1. Kuthamini familia:
Maisha ya familia yalithaminiwa sana na Wayahudi hivyo kuoa na kuolewa zilikuwa hali zilizotegemewa kutokea katika maisha yao.
2. Kutayarisha uchumba mwema:
Waliotarajia kuoana walijipatia kipindi cha walau mwaka mmoja kujiandaa kwa maisha ya familia.
3. Kufunga ndoa vizuri:
Maisha ya familia yalianzishwa rasmi siku ya harusi, bibi harusi alipoingizwa nyumbani mwa bwana harusi.
4. Kukataa mahusiano ya kujamiiana kati ya ndugu:
Mipaka ya kujamiiana iliainishwa katika Torati ya Musa (rej. Law 18).
5. Kukataa mahusiano ya kujamiiana yasiyo ya kawaida:
Kujamiiana kinyume na maumbile au na wanyama kulikatazwa na Torati (rej. Law 18).
6. Kukataa ndoa za jinsia moja:
Watu wa jinsia moja walikatazwa kujamiiana sembuse kuoana.
7. Kudumu katika maagano ya ndoa:
Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, Musa aliwaruhusu Wayahudi kuachana, lakini ilikuwa kinyume na matakwa ya Mungu (Kum 24:1-4, Mt 19:1-12).
8. Kutunza usafi na utakatifu wa ndoa:
Ugoni ulipata adhabu kali. Aliyefumaniwa alipewa adhabu ya kupiga mawe hadi kufa.
9. Kutunza mimba vyema:
Mimba zilitunzwa kwa miiko kadhaa iliyopaswa kushikwa na mama mjamzito.
10. Kuangaliwa watoto na kupewa majina mazuri:
Watoto waliangaliwa sana, wakanyonyeshwa kwa kipindi cha kufaa na walipewa majina yenye maana fulani kusudi wapate kuhamasika na sifa zinazoendana nayo.
11. Kupanga uzazi:
Miaka miwili au mitatu ya kunyonyesha watoto ndiyo iliyowatumika kupanga uzazi. Idadi ya watoto haikuwa na ukomo.
12. Kulea watoto vyema:
Watoto walilelewa na wazazi wote wawili, lakini baba aliwaangalia watoto wa kiume kwa namna ya pekee na mama watoto wa kike. Mintarafu kusoma, watoto wa kiume walijichagulia wenyewe walimu wa kuwafundisha Torati kwa kina.
13. Wanafamilia kutunzana na kushika majukumu husika:
Wanafamilia waligawana majukumu. Baba alikuwa na majukumu yake na mama sawia. Hata watoto walikuwa na yao.
14. Kusaidiana kwa udumifu:
Wazazi waliwalea watoto mpaka walipoanza maisha ya familia wenyewe. Kutoka hapo kazi iliwageukia watoto kuwatunza wazazi wao mpaka walipoaga dunia. Watoto kukwepa majukumu ya kuwatunza wazazi wao kwa kuweka mali zao wakfu (“korbani”) ilikuwa ni uhuni wa kusikitikiwa.

15. Kutoachana ovyo:
Ijapokuwa talaka iliruhusiwa, ugumu wa kulipa mahari ulipunguza talaka za ovyo ovyo. Mara nyingi ni kifo kilichomaliza maisha ya ndoa.

2.6.8 Usafi wa Ndoa na Maisha ya Familia

Ya kwamba ndoa inatakiwa kuwa na usafi wa pekee inadokezwa katika maneno ya Kristo pale alipokuwa anajibu swali aliloulizwa na Mafarisayo kama ni kweli kwamba waume wanaweza kuwapa talaka wake zao na kuwaacha kwa sababu yeyote. Yesu alifuta misimamo ya akina Hillel na Shammai akisisitiza kwamba agano la ndoa halifunguliki (Mt 19:3-6).
Kwa kusema hivyo alimaanisha vile vile kwamba ndoa ni agano la watu wawili tu, mume mmoja na mke mmoja. Kwa kusema hivyo alionesha uharamu wa mitara. Hapo hapo kwa kusema hivyo alidokeza uharamu wa mahusiano yoyote yasiyozingatia jinsia hizo tofauti za mume na mke. Na hiyo maana yake lilikuwa dokezo la uharamu wa mahusiano yote yaliyo kinyume na mume na mke, yaani mahusiano kama ya mwanaume na mwanaume, mwanamke na mwanamke au mwanadamu na hayawani. Aidha, maneno yake hayo yalifunga mwanya wa mtu kujibadili jinsia au mtu kujitengeneza ili awe na jinsia zote mbili. Haya yote yanasomeka katikati ya mistari ya Mt 19:1-12.Soma aya hizi huku ukitafakari vyema nawe utaona jinsi kina chake kilivyo kirefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha kumbe nao wakitishwa wanatishika?! Siasa hawakugusa, ngoja tusubiri wa KKKT tuone, Wachungaji wametuacha kondoo njia panda. Hivyo kila mtu kivyake sasa.
 
Kusoma ujumbe huu inahitaji muda na umakini. Nitakuwa nasoma kidogo kidogo mpaka J. tano nitamalizia. Ila ndoa za utoto nimezinote. Mkome mnaoozesha watoto wakimaliza la saba.
 
Ujumbe ni wa kinadharia zaidi na wenye woga wa kuelezea uhalisia wa maisha ya sasa katika nchi husika. Ni kutimiza wajibu tu wa kutoa waraka.
 
Siasa na maonyo yako palepale akili yako imeshindwa kung'amua hilo.

Serikali iliyokutuma kupost inatambua ndoa ya kiserikali na talaka. Hapa warakani kinachohubiriwa ni kwamba ndoa za namna hiyo ni ushetani maana familia ni mke mmoja na mme mmoja.

Kwa hiyo mwaka huu hawataki siasa ni mwendo wa familia tu!!
Siasa Zimeepukwa Mwaka Huu
Hahaha kumbe nao wakitishwa wanatishika?! Siasa hawakugusa, ngoja tusubiri wa KKKT tuone, Wachungaji wametuacha kondoo njia panda. Hivyo kila mtu kivyake sasa.
 
Si lazima watamke moja kwa moja ndipo ujue kuna siasa au la. Wakishatamka neno Haki za Binadamua ni pamoja na haki za wanaoonewa kama watoto na wanaoteka watu kama Mo, Roma Mkatoliki na wanaotandikwa risasi mchana kama Tundu Lissu.

Umoja wa Mataifa ulitamka kwamba:
“Familia inaunda kitengo cha msingi cha jamii na kwa hiyo inahitaji kuhakikishiwa uangalizi maalum. Hivyo basi, ulinzi mpana kabisa iwezekanavyo na msaada husika lazima vitolewe kwa familia zote ili nazo ziweze kuchukua majukumu yake ndani ya jamii, kutokana na matakwa ya Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu, Tamko kuhusu Ustawi na Maendeleo ya Kijamii, na Mkataba wa Kufutilia Mbali Namna Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake” [1]
 
UJUMBE WA KWARESMA 2019 ULIOTOLEWA NA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA TEC
.
WARAKA WA KWAREZIMA 2019 KUTOKA KURASINI: MUHTASARI, UFAFANUZI, UHAKIKI NA MAPENDEKEZO YA ASKOFU MLEI
(Toleo la Kwanza: 07 Machi 2019; Maboresho ya karibuni: 01 Julai 2019)

1551999269512.png

Picha: Dk. Charles Kitima (kushoto) ambaye ni Katibu Mkuu wa TEC kwa sasa Pamoja na Maaskofu Kadhaa wakifurahia jambo fulani la kuchekesha kwa kushirikiana na Rais John Pombe Magufuli

Wapendwa:
  • Padre Dk. Chales Kitima, Katibu Mkuu wa TEC;
  • Maaskofu wa TEC na Makardinali;
  • Mapadre na wachungaji;
  • Waseminari, mafrateri na mashemasi;
  • Wanataaluma Wakristo wa Tanzania (CPT);
  • TYCS, UKWATA, VIWAWA, WAWATA, na Baraza la Walei wa TEC;
  • Wakristo Wakatoliki, Walutheri, Wapentekoste, Wasabato na Walokole;
  • Wabunge na Madiwani;
  • Mawaziri, Ma-RC, Ma-DC, Ma-DED, ma-DEO, ma-WEO, na ma-VEO;
  • Waseminari wastaafu wote;
  • Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopitia seminari;
  • Ma-DSO, Ma-RSO, Ma-ZSO na Ma-TISS baki wote;
  • Dk. Modestus F. Kapilimba, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa;
  • Na Watanzania baki;
Nawasilimia kwa jina la Kanuni ya Kuona, Kuamua na Kutenda.

1. UTANGULIZI


Nikiwa naongozwa na Katiba ya Kanisa (Lumen Gentium 1964, par. 10 & 37) pamoja na Sheria za Kanisa (Canon Law 1983, par 212 (3) ), nakuandikieni kama Padre na Askofu Mlei kuhusu dosari zilizomo kwenye Waraka wa Kwarezima Kutoka Kurasini (2019), uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki wa Tanzania (TEC), ambao baada ya hapa nitaurejea kama Waraka (2019).

Waraka (2019) ambao umesainiwa na Maaskofu Katoliki 34 umetolewa wakati mbapo jamii jenzi inatekeleza mradi wa kuunda imani ya jamii ya Taifa, yaani “national social doctrine,” kwa kuwianisha imani za jamii mbadala zifuatazo: secularism, marxism, postmodernism, new spirituality, islam, & christianity.

Lengo la mradi huu, unaosukumwa na roho ya uekumene, ni kufananisha, kutofautisha na kupatanisha imani hizi mbadala kwa kuangalia sekta zifuatazo: theology, philosophy, ethics, physics, chemistry, biology, psychology, sociology, law, politics, economics, history, sexology and mathematics.

Hoja ambayo Waraka(2019) unaipendekeza na ambayo ninainyoshea kidole ni hoja inayosema yafuatayo:


  1. Kwamba, "mintarafu watu wa jinsia gani [wenye uwezo wa kufanya tendo la ngono ya ndoa], Biblia nayo haina utata, [kwani inasema kuwa watu wenye uwezo huo] ni mwanamume na mwanamke yaani watu wawili wa jinsia tofauti [kwa sababu kuna yamkini ya 17% inayoonyesha kwamba, watianaji wenye jinsia tofauti pekee]... ndiyo watu wanaoweza [kuwa mwili mmoja (Mwa. 2:24)], kuzaana na kutimiza agizo la kuijaza dunia,” kwa kupitia tendo la ngono inayofanyika kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, bila kutumia kingamimba, na kwa kuhakikisha kuwa jenitali zinabadilishana manii ya kike na manii ya kiume.
  2. Kwamba, hata kama yamkini ya kutokuwepo kwa mkamilishano wa rutuba ya uzazi miongoni mwa jozi ya watianaji wenye rutuba ni 83% ndani ya kila mwezi, hata kama kutokuwepo kwa mkamilishano wa rutuba ya uzazi miongoni mwa jozi ya watianaji wagumba ni 100%, na hata kama yamkini ya kutokuwepo kwa mkamilishano wa rutuba ya uzazi miongoni mwa jozi ya watianaji waliovuka umri wa kwenda hedhini ni 100%, lakini bado kila jozi ya watianaji hawa nayo hugeuka "mwili mmoja" kupitia tendo la ngono inayofanyika kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, bila kutumia kingamimba, na kwa kuhakikisha kuwa jenitali zinabadilishana manii ya kike na manii ya kiume.
  3. Na kwamba, kwa hiyo, wanandoa ambao ni watianaji wagumba na wanandoa ambao ni watianaji waliovuka umri wa kwenda hedhi huwa wanafanyi tendo la ngono ya ndoa ambalo ni sawa na tendo la ngono ya ndoa linalofanywa na jozi ya watianani wenye mkamilishano wa rutuba ya uzazi.
Kama nitakavyoonyesha, hoja hii imekuwa sababu ya kuufanya Waraka(2019) kuwa "unfocused, verbose, vague, scotosis-laden, disinformative, miseducative and inconclusive."

Kimsingi, dokezo la pili linaambatana na utata unaopingana na ukweli wa kisayansi na kifalsafa. Ni dokezo lenye kuambatana na utata mkubwa wa kisarufi, kisayansi, kietiolojia, kisemantiki, kisemiolojia, na kiteolojia

Utata huo unaanzia kwenye matumizi ya neno "wanaoweza (who can)" kana kwamba ni neno linaloeleza ulazima, wakati linaeleza uyamkini tu.

Kifalsafa, tunasema kuwa maneno kama vile "can/could, can't/couldn't, will/would, won't/wouldn't, may/might, shall/should, shan't/shouldn't, must/mustn't" ni maneno ambayo ni vitenzi visaidizi vinavyoonyesha kuwepo au kutokuwepo kwa uwezekano (auxilliary modal verbs). Kuwepo kwa uwezekano kunamaanisha yamkini iliyo kati ya 1% na 100% wakati kutokuwepo kwa uwezekano kunamaanisha yamkini ya 0%.

Waraka(2019) haujajipambanua vizuri zaidi ya kuendeleza ujambazi wa kifalsafa kama wanavyofanya Maaskofu wa Amerika na Australia.

Kwa mfano, mwaka 2015, Baraza la Maaskofu la Australia, kupitia waraka wake, “The Catholic Church, Marriage and Same-Sex Attraction: Frequently Asked Questions (2015),” walifafanua upya “maana ya umoja na maana ya uzazi,” kupitia swali namba tano (5), ukurasa wa 10-11, katika namna ambayo inaonyesha wazi kwamba nao wanaunga mkono huu ujambazi wa kifalsafa (sophism).

Walisema kwamba “because of their sexual difference, husband and wife can truly become one flesh,” kwamba “catholic theology, therefore, sees sexuality within marriage as having a threefold purpose or meaning,” kwamba “sex is unitive,” kwamba “sex is procreative,” na kwamba “sex is parental.”

Nalipongeza na kulilaumu Baraza la Maaskofu Katoliki la Australia. Nalipongeza kwa ufafanuzi bora zaidi kuhusu "maana ya umoja na maana ya uzazi."

Lakini nalilaumu kwa sababu ya dosari tatu. Dosari moja inatokana na matumizi ya neno “can” bila kueleza ni lini "modality" ya "possibility" inayorejewa inakuwa kweli na lini haiwi kweli.

Dosari ya pili inatokana na kutumia maneno yenye maana nyingi ndani ya hoja moja (equivocation) bila kuwambia wasikilizaji ukweli huo. Mfano ni neno "sex" linaloweza kumaansha "ngono" au "tabaka la watu wenye jenitalia zinazofanana."

Na dosari ya tatu inatokana na kuchanganya "modality" ya "possibility" na "modality" ya "necessity." Mfano, kama tunatumia neno "sex" kumaanisha "ngono," basi, maneno “sex is unitive,” “sex is procreative,” na “sex is parental” yanapaswa kuondoka katika modality ya "necessity" na kuingizwa katika "modality" ya possibility" kama ifuatavyo: “sex is [sometimes] unitive,” “sex is [sometimes] procreative,” na “sex is [sometimes] parental.”

Dosari zote tatu zinawaweka Maaskofu Katoliki hawa katika kundi moja la majambazi wa kifalsafa waitwao “sophists.”

Kwa mfano tena, Maaskofu wa Amerika, mwaka 2009, waliandika Waraka wa Kichungaji wenye maneno yafuatayo:

“The unitive meaning is distorted if the procreative meaning is deliberately disavowed… Likewise, the procreative meaning of marriage is degraded without the unitive… The unitive and the procreative purposes are meant to be inseparable. In this way, the procreative requires the unitive, just as the unitive is ordered to the procreative. These are two connected meanings of the same reality.” (Marriage, Love and Life in the Divine Plan: A Pastoral Letter of the United States Conference of Catholic Bishops (2009), p. 15-16).

Maneno haya yakisomwa kwa umakini, jambo moja liko wazi. Yanakwepa kusema lolote juu ya uhusiano wa kietiolojia uliopo kati ya "maana ya umoja" na "maana ya uzazi." Kwa mfano, neno "requires" hapo juu linaongelea uhusiano wa sababu na matokeo (etiological relation) kati ya "maana ya umoja na maana ya uzazi."

Katika mtazamo wa kisemiolojia (semiological perspective) alama yenye maana nyingi (polysemic signifier), kama lilivyo tendo la ngono endapo likichukuliwa kama alama, haiwezi kutumika kwenye sentensi moja katika namna ambayo inabeba maana zote mbili kwa mpigo. Maneno yenye maana zilizo sawa (synonymic signifiers) ndiyo huweza kutumika kwa mpigo katika sentensi moja ili kuongeza msisitizo.

Lakini pia, katika mtazamo wa kietiolojia (etiological perspective), "maana ya umoja" sio "necessary and sufficient requirement" kwa ajili ya "maana ya uzazi." Badala yake kuna uhusiano wenye sura ya "probabilistic cause."

Maaskofu Katoliki wote duniani wamesoma metafizikia, mantiki na epistemolojia. Wanajua tofauti kati ya "necessary cause, sufficient cause, necessary and sufficient cause, na probabilistic cause." Pia, wote wanajua tofauti kati ya "physical necessity, metaphysical necessity, logical necessity na moral necessity."

Lakini bado wanaendelea kufanya ulagai kwa kuandika katika namna ambayo inawafanya wasomaji wasione tofauti kati ya ukweli wote na ukweli nusu nusu. Wanatumia mbinu ya "deception by omission" na waakti mwingine "deception by equivocation." Huu ni ujambazi wa kifalsafa.

Kwa hapa itoshe kuwakumbusha tu kwamba, ujambazi ni ujambazi bila kujali kama jambazi katumia silaha ya bunduki, shoka, panga, mkuki, kisu, wembe, matendo au maneno yenye sura ya ulagai wa kifalsafa (sophism).

Hivyo basi, kwa kuzingatia kazi nzuri ambayo tayari imekwisha kufanywa kupitia mradi wa MKIJATA, naona kwamba, Waraka (2019) unazo dosari nyingi kwa sababu hii. Hivyo, tafakari hii imegawanyika katika sehemu kadhaa kwa ajili ya kutetea rai anuwai katika mtiririko ufuatao:

  1. Waraka unapiga marufuku matumizi ya kingamimba kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.
  2. Waraka unapiga marufuku kutenganishwa kwa ndoa na familia kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.
  3. Waraka unatumia metafizikia ya ujinsia wa binadamu inayokiuka kanuni za kietiolojia
  4. Waraka unatumia kanuni za sayansi ya ujinsia zinayopingana na kanuni mamboleo za embryolojia ya binadamu
  5. Waraka umeshindwa kutaja fasili ya ndoa yenye kuwasaidia Watanzania kupata jawabu la swali linalohusu habari ya ndoa ni kitu gani na sio kitu gani
  6. Waraka unapiga marufuku ndoa za jinsia moja kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.
  7. Waraka unapiga marufuku mapenzi ya kigumba kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.
  8. Waraka unafundisha juu ya ndoa na familia kwa kutumia athropolojia ya kijinsia iliyopitwa na wakati
  9. Waraka umetumia Misahafu na Mapokeo kama vyanzo vya kimaarifa lakini ukasahau vyanzi vingine muhimu kama vile sayansi asilia, sayansi za jamii, sayansi za kimahesabu, na falsafa.
  10. Waraka umeshindwa kueleza kinaganaga tofauti kati ya hulka ya kibinadamu na hulka isiyo ya kibinadamu
  11. Waraka unatumia sababu zinazoyumba kutetea dhana kwamba ngono ya wagumba inaisababishia hasara jamii kwa kuwa inapunguza fursa za ongezeko la watu duniani.
  12. Waraka unatumia mbinu za kimachiaveli kuwaziba midomo wakosoaji wa Kanisa kama alivyokuwa anafanya Papa Gregory wa karne ya 13
  13. Hitimisho
  14. Mapendekezo kwa Vigogo wa Kurasini na wadau baki.
1. Waraka unapiga marufuku matumizi ya kingamimba kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.

Katika Waraka (2019) kuna hoja ya kupinga matumizi ya kinga mimba, kama vile vidonge na kondomu (contraceptives), na hivyo, kwa njia ya mzunguko, kuna hoja ya kupinga matumizi ya kondomu kama kinga ya magonjwa ya kingono (sexual prophylactics).

Napendekeza kuijadili hoja hii hatua kwa hatua, kwa kutumia muundo wa mantiki ya Ki-Aristotle, ambapo hoja hiyo inaanza na muundo wa kimantiki ufuatao:

  • Kwamba, kwa mujibu maadili asilia yanayotokana na "hulka ya binadamu" inayotambuliwa na Biblia ni kosa kila wakati, kila mahali na kwa kila mtu kujihusisha na tabia "iliyopotoka kihulka" (1).
  • Kwamba, mwenendo wa kupanga uzazi kwa kutumia mbinu za kisasa ni tabia "iliyopotoka kihulka" kwa sababu inaizuia jozi ya watianaji kugeuka mwili mmoja (2);
  • Kwamba, na kwa hiyo, kutokana na namba 1 na 2 hapo juu, kupanga uzazi kwa kutumia mbini za kisasa ni tabia haramu kimaadili(3).
Lakini, sikutrarajia kuwasikia Maaskofu Katoliki wakifufua hoja hii tena. Bosi wao Papa akishasema kwamba msimamo wa Kanisa ni huu, vigogo wa Kurasini wanapaswa kutii na kufafanua msimamo huo kwa waumini.

Kimsingi, anachokisema Papa Francis ni kwamba, hakuna tendo la binadamu ambalo ni haramu kila mahali, kila wakati na kwa kila mhusika. Yaani, "there are no intrinsically evil acts."

Kwa mantiki hiyo hiyo, naona kwamba, hoja hii inayopinga uzazi wa mpango kwa kutumia mbinu za kisasa haipaswi kujadiliwa kwenye waraka wa Kanisa linaloongozwa na Papa Francis.

Hoja hii katika ukamilifu wake, na ikiwa katika muundo rasmi wa kimantiki imeandikwa kwa Kiingereza katika Kiambatanisho J. Kwa hapa chini naifafanua kwa Kiswahili ili kutoa mwanya kwa "wabongo" kuelewa haraka ninachokisema kwenye hoja hiyo.

Pointi yangu ya msingi ni kwamba, kinyume na mtazamo wa Bosi wa Maaksofu Katoliki, wao wameandika Waraka wa Kwarezina Kutoka Kurasini (2019) unaopinga matumizi ya kingamimba, japo hizi nyenzo muhimu katika vita dhidi ya familia zenye ukubwa unaozidi uwezo wa wazazi.

Kwa hiyo, hebu tudadisi hoja ya Maakofu kwa kina ili kujua nani mwenye hoja iliyo na mashiko kati yao na Papa Francis. Nitazingatia maandiko ya Stein(2009) na Anderson (2013).

Katika hatua ya pili, hoja ya kupinga kingamimba inayoanzia kwenye dhana ya “mwili mmoja,” kama ilivyoelezwa kupitia Waraka (2019), na kufupishwa hapo juu, inaweza kuendelezwa kama ifuatavyo:

  • Kwamba, sheria ya maadili asilia, yenye kuzingatia hulka ya binadamu kama inavyotamkwa katika Biblia, inaonyesha kwamba, kila tendo la ngono lisiloweza kuwaruhusu watianaji kugeuka mwili mmoja wakati wa kutiana ni haramu kimaadili (4).
  • Kwamba, wakati jozi ya watianaji wanaotumia kingamimba hawawezi hugeuka mwili mmoja wakati wa kutiana, jozi ya watianaji wasiotumia kingamimba hugeuka mwili mmoja kila wakati wa kutiana (5).
  • Na kwamba, kwa hiyo, kutokana na (4) na (5) hapo juu, inafuata kimantiki kwamba, kila tendo la kutiana kwa kutumia kingamimba ni haramu kimaadili (6).
Hata hivyo, naona kwamba, hoja hii inayo matatizo katika madokezo yote mawili. Kwa mfano, kwa nini dokezo la kwanza linasema kuwa, “kila tendo la ngono lisiloweza kuwaruhusu watianaji kugeuka mwili mmoja wakati wa kutiana ni haramu kimaadili?”

Kwa mujibu wa ufahamu wangu, hakuna sababu nzuri ya kutetea mtazamo huu. Lakini, kwa hapa itatosha kuonyesha ubovu wa hoja hii kwa kujielekeza katika dokezo la pili.

Naona kuwa, sio madai ya kweli mara zote kusema kwamba, “jozi ya watianaji wasiotumia kingamimba hugeuka mwili mmoja kila wakati wa kutiana,” kama dokezo namba (5) linavyodai.

Sasa tunafahamu kuwa, wanawake wote ni wagumba kwa zaidi ya 83% katika maisha yao yote.

Kwa hiyo, hata kama wanaume wanaojamiiana nao wana rutuba ya uzazi, bado wanashiriki katika baadhi ya matendo ya ngono ya jenitalia kwa jenitalia yasiyoweza kufanikisha kuzaliwa kwa mwili mmoja wenye rutuba ya uzazi hapa na sasa hivi.

Tendo la ngono kati ya jozi ya watu wa aina hii, ni kama zoezi la watu wawili waliosimama pande mbili za magoli ya mpira wa miguu, wakiwa na bunduki, na wakiwa wanajaribu kupiga risasi angani ili zikutane juu hewani.

Tangu sekunde ya kufyatua risasi, hii jozi ya wafyatuaji inaweza kuitwa “mwili mmoja” wa wafyatuaji, yaani, “one firing organsm.” Lakini, kama mfyatuaji wa upande mmoja hana risasi katika bunduki yake, hawezi kutuma risasi hewani.

Na hivyo, hakuna mkamilishano wa kimchakato, kiasi kwamba, tukio la kuzaliwa kwa “mwili mmoja” wa wafyatuaji linabatilika tangu mwanzo, kwani hakuna msukumo wa kietiolojia (efficient cause) kwa ajili kuasisi mchakato husika. Yaani, “null and void ab initio.”

Kwa ajili ya kuonyesha dosari hii kwa ukamilifu, hebu tuone hoja mpya, lakini yenye muundo wa kimantiki kama ule wa hoja ya awali inayoanzia kwenye dhana ya “mwili mmoja” kupinga kingamimba.

Hoja hii mpya inahusisha jozi ya mke na mume yenye sifa ya ugumba, angalau kwa mtu mmojawapo:

  • Kwamba, sheria ya maadili asilia, yenye kuzingatia hulka ya binadamu kama inavyotamkwa katika Biblia, inaonyesha kwamba, kila tendo la ngono lisiloweza kuwaruhusu watianaji kugeuka mwili mmoja wakati wa kutiana ni haramu kimaadili (7).
  • Kwamba, kila jozi ya watianaji wenye ugumba, haiwezi kugeuka mwili mmoja wakati wa kutiana (8).
  • Kwamba, na kwa hiyo, kutokana na namba (7) na (8), kila jozi ya watianaji wagumba, hufanya kitendo haramu kimaadili (9).
Hata hivyo, duniani kote, sheria za kidini na kiserikali zenye kuratibu maisha ya ndoa, zinawaruhusu mwanamke na mwanamume ambao ni wagumba kuoana na kutiana kila wanapojisikia kufanya hivyo.

Kwa hiyo, inawezekana dokezo mojawapo katika hoja iliyo mbele yetu ni batili au au hoja nzima ni batili.

Watetezi wa hoja inayoanzia dhana ya “mwili mmoja” lazima waunge mkono dokezo la 7, ambalo linawawezesha kupinga matumizi ya kinga mimba.

Na kwa kuzngatia ushahidi wa kisayansi kuhusu michakato ya kifiziolojia, kiteliolojia na kietiolojia katika mwili wa binadamu (Myar 1974; Torley 2005), hawawezi na hawapaswi kukataa dokezo la 8.

Kwa hiyo, watetezi wa hoja inayoanzia dhana ya “mwili mmoja” kupinga kingamimba wanajikuta njia panda. Wanaweza kuchagua njia mojawapo kati ya njia mbili zinazowezekana.

Katika njia moja, wanaweza kukubali dokezo la 9, ambalo ni hitimisho la kimapinduzi, kwa vile hakuna sheria ya ndoa duniani inakubaliana nalo, na pia linakiuka haki ya wanawake waliovuka umri wa hedhi kufunga ndoa.

Na katika njia ya pili, wanaweza kuamua kukubali kwamba, mtiririko wa kimantiki unaohusisha dokezo la 7, 8 na 9 ni batili kimantiki.

Lakini, wakichukua msimamo huo, inabidi pia wakubali kwamba, mtiririko wa kimantiki unaohusisha dokezo la 4, 5 na 6 ni batili kimantiki, na watakuwa wamepoteza hoja yao ya msingi. Kwa hiyo, wanajikuta katika mtanziko.

Kwa ujumla, mjadala huu unaonyesha jambo moja muhimu. Pasipo mkamilishano wa rutuba ya uzazi kati ya mwanamke na mwanamume, uamuzi wowote wa kutetea uhalali wa “ngono ya kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike” miongoni mwa jozi ya watianani wagumba na wakati huo huo kupopoa “ngono ya kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike” miongoni mwa jozi ya watianani wanaotumia kingamimba unakuwa ni uamuzi wa kubahatisha na usioungwa mkono na dhana ya “mwili mmoja.”

Kwa hiyo, hoja ifuatayo inaweza kutumika kuhitimisha mjadala huu, pasipo kuacha chembe ya mashaka:

  • Kwamba, Kama watu wawili hawawezi kufanya ngono inayowawezesha kugeuka “mwili mmoja,” basi hawana sifa ya kufanya tendo la ngono ambalo ni halali kimaadili (10).
  • Kwamba, Lakini, mwanamke na mwanamume ambao ni wagumba wanaruhusiwa na sheria zote duniani kufunga ndoa na kufanya tendo la ngono kila wanapojisikia kufanya hivyo (11).
  • Kwamba, na kwa hiyo, kutokana na namba (10) na (11), tukio la kugeuka mwili mmoja kupitia tendo la ngono sio sifa mtambuka kwa ajili ya kuitambulisha kila jozi ya watianaji halali inayofahamika duniani (12).
Kama hivyo ndivyo, kuna sifa gani ya msingi inayozitofautisha jozi za watianaji wenye rutuba ya uzazi na jozi za watiananji wasio na rutuba ya uzazi?

Kwa kuzingatia utata unaoigubika hoja inayoanzia kwenye dhana ya “mwili mmoja” kupinga kingamimba, njia pekee inayobaki kwa ajili ya kutetea ukuu wa ngono ya jenitalia kwa jenitali miongoni mwa watianaji wenye rutuba, ni kutumia hoja zinazojikita kwenye ubaya wa madhara ya ngono ya jenitalia kwa jenitali miongoni mwa watianaji wanaotumia kingamimba.

Hoja mojawapo inaanzia kwenye umuhimu na ulazima wa kusukuma gurudumu la uhai kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hoja hii inao muundo ufuatao:

  • Kwamba, Kila binadamu ni kiumbehai, kwa maana kwamba, anao mwili mmoja wenye viumgo mbalimbali vyenye uwezo wa kushirikiana kufanya kazi kuu tatu: kuendeleza maisha ya kimwili, kuzaa watoto na kuwalea hadi wawe watu wazima wenye uwezo wa kujitegemea (13).
  • Kwamba, Tofauti na ilivyo kwa wanyama hayawani, kama Taifa la watu halitaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba watoto wa binadamu wanazaliwa na kupata malezi ya muda mrefu kutoka kwa wazazi wao, rika ya watu wazima hatimaye itatoweka, na hatimaye Taifa zima kufutika(14).
  • Kwamba, na kwa hiyo, kutokana na namba (13) na (14), kila Taifa linalotaka kuendeleza uhai wake lazima liweke mfumo thabiti wa kijamii na kisheria kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto wanazaliwa na kulelewa, mfumo ambao ni lazima uwe ni jumuiya ya watianaji wenye rutuba ya uzazi wasiotumia kingamimba, ambao huitwa ndoa (15).
Baada ya hitimisho hili kufikiwa, madhara hasi ya kingamimba dhidi ya jukumu la kuendeleza uzao wa binadamu yanachomekwa kama ifuatavyo:
  • Kwamba, ngono inayowawezesha wahusika kugeuka mwili mmoja, tofauti na ngono ya kingamimba, ndio chimbuko la ndoa inayofaa kwa ajili ya kuzaa na kulea watoto wachanga (16).
  • Kwamba, kila aina ya ngono ya kingamimba huzuia kuzaliwa kwa mtoto(17).
  • Kwamba, na kwa hiyo, kutokana na namba (16) na (17), Taifa linapaswa kutetea ngono inayowawezesha wahusika kugeuka mwili mmoja na kukataza kila aina ya ngono inayowazuia wahusika kugeuka mwili mmoja (18).
Hata hivyo, kama kila aina ya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja itakatazwa kutakuwa na madhara kwa baadhi ya ndoa halali. Nitatoa mifano michache.

Mosi, fikiria msichana ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa wa selimundu (circle cell anemia). Huyu ameshauriwa kitabibu kwamba asibeba mimba katika maisha yake yote. Huyu bado anayo haki ya kuolewa kama atajitokeza mvulana wakapendana.

Akipaikana mvulana wakakubaliana kufunga kizazi na kuoana, hiyo ni ndoa halali. Katika maisha yao yote watakuwa wanafanya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja. Sheria za nchi na sheria za kidini zinaruhusu.

Pili, fikiria msichana amesoma mpaka shahada ya ya tatu, anahitimu akiwa na miaka 40. Kibayolojia, ukomo wa hedhi kwa mwanamke ni miaka 36.

Hivyo, huyu hana matarajio ya kuzaa motto, lakini bado anayo haki ya kufunga ndoa kama akipata mwanamume wakakubaliana. Kama wakifunga ndoa, watakuwa wanafanya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja katika maisha yao yote. Sheria za nchi na sheria za kidini zinaruhusu.

Na tatu, ushahidi wa kitafiti uliopo unaonyesha kuwa, baadhi ya wanandoa hufanya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja—ngono ya kukutanisha mdomo wa kiume na uke—kwa ajili ya kuwaandaa wanawake ambao wana vilainishi haba katika uke.

Hivyo, aina hii ya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja humsaidia mwanamke kupata mlainiko wa kutosha kwa ajili ya kuendelea na ngono ya kukutaisha uume na uke kwa ufanisi.

Aidha, ushahidi wa kiutafiti uliopo unaonyesha kuwa, baadhi ya wanandoa hufanya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja —ngono ya kukutanisha mdomo wa kike na uume—kwa ajili ya kuwaandaa wanaume ambao wana msimiko dhaifu.

Hivyo, aina hii ya ngono iliyo kinyume cha maumbile humsaidia mwanamume husika kupata msimiko ulio madhubuti kwa ajili ya kuendelea na ngono ya kukutanisha uume na uke kwa ufanisi.

Kwa hiyo, dokezo la (18), hapo juu, halipaswi kukubalika kama kanuni ya jumla kwa kila jozi ya watianaji.

Na hoja hii inazo maana kubwa mbili: Mosi, kitendawili cha nafasi ya ngono iliyo kinyume cha maumbile ya mwili mmoja ndani ya ndoa ya mwanamke na mwanamume hakijateguliwa kwa ukamilifu kupitia Waraka wa Kwarezima Kutoka Kurasini(2019).

Na pili, Waraka wa Kwarezima Kutoka Kurasini(2019) umeshindwa kujipambanua kinaganaga kuhusu swali, “ndoa ni kitu gani na ndoa sio kitu gani?” Swali hili likijibiwa vizuri na kwa ukamilifu katazo dhidi ya kingamimba halitasikika tena.

2. Waraka unapiga marufuku kutenganishwa kwa ndoa na familia kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.

Waraka (2019) una upogo kuhusiana na tamko lake kwamba "kutenganishwa kwa ndoa na familia" ni kosa mara zote, kila mahali na kwa kila mtu. Kuna mifano mingi inayokanusha tamko hili.

Kwa mfano, mwanamume akifunga ndoa na mwanamke aliyekoma kwenda hedhi wanakuwa wamechagua kutenganisha ndoa na familia na sheria zinaruhusu jambo hili.

Mume na mke wakifanya tendo la ngono wakati mwanamke yuko katika majira ya ugumba wa kila mwezi wanakuwa wamechagua kutenganisha ndoa na familia .

Mume na mke wakifanya tendo la ngono wakati mwanamke yuko katika majira ya rutuba ya kila mwezi, lakini wakaamua kutumia kingamimba, kwa vile hawataki mtoto mwingine kwa sasa, wanakuwa wamechagua kutenganisha ndoa na familia.

Pia, Padre aliyekula kiapo cha useja anakuwa ametenganisha ngono na ndoa. Kutenganisha ngono na ndoa ni kutenganisha ndoa na familia. Hivyo, mapadre wanatenganisha ndoa na familia.

Yote haya ni "matumizi ya uhuru binafsi juu ya ndoa na familia”yanayopingwa na waraka wao wenyewe. Lakini, kila binadamu mwenye akili na utashi anayo mamlaka juu ya kufanya maamuzi kama haya kadiri dhamiri yake inavyomruhusu.

Lakini, hoja inayohusu kutenganishwa kwa ndoa na familia inapaswa kujadiliwa kwa kina zaidi ili kuonyesha wapi Maaskofu wa Kurasini wamejikwaa.

Ni maoni yangu kwamba, Waraka (2019) umeshindwa kutofautisha kati ya jumuiya inayoitwa ndoa na jumuiya inayoitwa familia, kwa kiwango ambacho kinawanyima Watanzania mwanga wa maarifa unaowawezeha kufanya uchanganuzi wa kinaganaga kuhusu maswali mawili yafuatayo: (a) Ndoa ni kitu gani na sio kitu gani? (b) Familia ni kitu gani na sio kitu gani? Kwa hapa nitajielekeza zaidi katika hili swali la pili.

Naona kuwa Waraka (2019) unafuata mafundisho ya Padre Austin Fagothey (2000), ambaye anasema kwamba, “jumuiya ni muungano wa kudumu kati ya watu zaidi ya mmoja walio chini ya mamlaka moja ya kimaadili na wanaowajibika kushirikiana katika kufukuzia lengo la pamoja,”

Kwamba, “familia ya kimapokeo ni jumuiya inayohusisha mume au baba, mke au mama, na watoto wao wa damu.”

Kwamba, “familia ya kimapokeo ni jumuiya ya nyumbani yenye mikono miwili au jumuiya ndogo mbili. Kuna mkono wa ulalo, ambao ni ushirika wa mke na mume, ujulikanao kama jumuiya inayoundwa na jozi ya watianaji (conjugal society).

Na kuna mkono wa wima, ambao ni ushirika wa wazazi na watoto, ujulikanao kama jumuiya inayoundwa na utatu wa baba, mama na mtoto, yaani jumuiya ya walezi (parental society).”

Kwa lugha nyingine, "jumuiya ya watianaji (‘conjugal society’)" inaitwa "one-flesh unity" au "organic bodily union." (Girgis, Ryan, George 2012).

Aidha, Fagothey (2000) anasema kwamba, “ndoa ya kimapokeo ni jumuiya au muungano wa kudumu kati ya mwanamume na mwanamke unaotokana na mkataba, ambao kupitia kwake mwanamke na mwanamume hupeana haki za kutumiana kimwili kupitia tendo la ngono inayokutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike.”

Hata hivyo, Fagothey(2000) anajipotosha na kuwapotosha Maaskofu wa TEC, waliokitumia kitabu chake wakati wakiwa walimu na wanafunzi wa Seminari Kuu, katika mambo mawili.

Kwanza, Fagothey(2000) anapotosha kwa kusema kwamba, “ndoa na familia sio jumuiya mbili zilizo tofauti, bali pande mbili za jumuiya mmoja kubwa.”Hataji jina lake. Labda tungesema jumuiya inayoitwa ndoa-familia!

Na pili, Fagothey(2000) anapotosha kwa kusema kwamba, “kwa mujibu wa unasibu, na sio kwa mujibu wa ulazima, familia ya kimapokeo inaweza kuwa na mkono mmoja pekee, yaani jumuiya ya watianaji wagumba, lakini hili sio jambo la kawaida ya kitakwimu.”

Usahihi wa mambo ni kwamba, ndoa na familia ni “jumuiya (societies)” mbili tofauti ambazo zinaweza kuwa na muungano wenye sura ya “sababu-hadi-matokeo (cause-to-effect connection).”

Yaani, kuna “uhusiano wa kietiolojia (etiological connection)” kati ya jumuiya inayoitwa ndoa na jumuiya inayoitwa familia. Ndio kusema, ndoa ni chanzo na familia ni matokeo.

Na ndoa ya kimapokeo sio chanzo cha jumuiya ya familia pekee, kwani kuna jumuiya nyingine nyingi ambazo chimbuko lake ni ndoa ya kimapokeo pia. Mfano ni kampuni ya watoto wa familia moja, ambayo ni jumuiya ya kiuchumi (economic society).

Kwa hiyo, naona kuwa, Fagothey(2000) amechanganya kimakosa mtiririko huu kwa kuruhusu chanzo na matokeo kubadilishana nafasi, pale anaposema kwamba, "childless couples form a family in its conjugal relation." Kinachoongelewa hapa ni "potential family" wakati jozi ya watianaji haina "procreative potentiality." Huu ni ulaghai.

Kuhusu maneno haya, Fagothey(2000) anadai kwamba, “accidentally, a traditional family may have one component only, that is the conjugal society only, but this is not the normal case.”

Hata hivyo, ukawaida wa kitakwimu (statistical norm) sio ukawaida wa kimaadili (moral norm) kama ambavyo sio kanuni ya jumla (universal norm). Enzi za kufundishana kwa kutumia maneno yenye undumila kuwili wa maana (equivocation) namna hii zimepita.

Kwa hiyo, Fagothey(2000) alipaswa kuwa wazi na kusema kwamba: “accidentally, and not essentially, a traditional marriage and a traditional family may be causally connected, but this is a particular case and not a universal case.”

Kwa ujumla, tunaweza kusema kuwa, kwa sababu ya hofu ya "kutenganishwa kwa ndoa na familia", waraka umeshindwa kueleza maana ya neno “kugeuka mwili mmoja kwa njia ya kutiana (one-flesh unity via conjugal union),” na hivyo kushindwa kabisa kuwasaidia wananchi kujibu kwa usahihi swali lifuatalo: Ndoa ni kitu gani?

Waraka (2019) umeendeleza makosa ya Waraka Kutoka Vatikani (1968) uitwao Humanae Vitae unaokataza tabia ya kutenganishwa kwa tendo la ndoa na mimba tarajiwa. Waraka huu unatamka haya:

"Each and every marital act must of necessity retain its intrinsic relationship to the procreation of human life(Pope Paul VI, Humanae Vitae 1968, par 11)."

Lakini, hivi karibuni Papa Francis alipindua mtazamo huu kupitia ibara ya 304 ya Waraka wake wa Amoris Laetitia. Papa Francis anasema:

“[G]eneral rules … cannot provide absolutely for all particular situations (Amoris Laetitia 1986, par. 304).”

Kwa mfano, mwanamume akiamua kuoana na mwanamke ambaye amevuka siku zake za kwenda hedhi, wawili hawa wanakuwa wamechagua kutenganisha ndoa na familia.

Kwa hiyo, nimeshangaa kuona kwamba, Waraka (2019) bado unasema kwamba, "kutenganishwa kwa ndoa na familia" ni kosa kila mahali, kila wakati na kwa kila mtu.

Kwa ujumla, Waraka (2019) umeendeleza utata wa siku nyingi unaozunguka maneno "mwili mmoja" tangu 1968 kupitia ibara ya 12 ya Humanae Vitae.

3. Waraka unatumia metafizikia ya ujinsia wa binadamu inayokiuka kanuni za kietiolojia

Waraka (2019) unapinga “kutenganishwa kwa ndoa na familia.” Huu ni mwendelezo wa mafundisho ya Papa Paul VI kupitia Humanae Vitae kwamba,

“This particular doctrine [that each and every marital act {also known as uncontracepted and inseminatory penis-to-vagina sex act, entails an} intrinsic relationship to the procreation of human life], often expounded by the magisterium of the Church, is based on the inseparable connection, established by God, which man on his own initiative may not break, between the unitive significance and the procreative significance which are both inherent to the marriage act (Pope Paul VI, Humanae Vitae 1968, para. 12)."

Marufuku dhidi ya “kutenganishwa kwa ndoa na familia” katika Waraka (2019) ni tafsiri sisisi ya maneno “the inseparable connection … between the unitive significance and the procreative significance” yaliyo katika Humanae Vitae (1968).

Ibara ya 2366 na 2369 katika Katekisimu Katoliki (1993) ya Kiswahili zinayatafsiri maneno "unitive significance and the procreative significance” kama “maana ya umoja na maana ya uzazi.” Lakini mimi ningeyatafsiri kwa kutumia maneno "maana ya kutiana na kuzaliana."

Katika ukamilifu wake maneno haya yanamaanisha, “maana ya umoja [wa kimwili kupitia tendo la ndoa]” na “maana ya uzazi [kupitia utungo wa mimba unaoanzisha familia ya baba, mama na mtoto].”

Askofu Patrick O'Boyle (1971) wa Marekani aliwahi kuongelea uhusiano uliopo kati ya maana hizi mbili kwa kutumia maneno yafuatayo:

“The meaning of human sexuality is that a man and a woman can start a new person only by first becoming one flesh.”

Anachosema O'Boyle (1971) ni kwamba, “maana ya umoja” ni chanzo wakati “maana ya uzazi” ni matokeo. Na kwa sababu ya matumizi ya neno "can," kila mwanafalsafa aliyesoma metafizikia na kufuzu anaelewa kuwa hii ni "modal statement" ambayo ukweli na uwongo wake haviwezi kutofautishwa mpaka pale parameta za mazingira ya ulimwengu mwafaka zitakapokuwa zimetajwa.

Yaani, ni kauli inayoweza kuwa kweli katika "Ulimwengu wa parameta zinazounda seti ya U1." Na inaweza ikawa ni kauli isiyo kweli katika "Ulimwengu wa parameta zinazounda seti ya U2." Kuficha ulimwengu unaohusiana na "modal statements" ni mbinu mojawapo ya ujambazi wa kifalsafa (sophism).

Lakini, kwa hapa, na hasa, kwa ajili ya hoja ninayotaka kuijadili hapa tuchukulie kwamba kuna ulimwengu wa mazingira chanya (causally positive background) yanayoweza kuruhusu matokeo yanayoongelewa na Askofu Patrick O'Boyle.

Ndio kusema kwamba, kuna uhusiano wa sababu na matokeo, au tuseme uhusiano wa kietiolojia, kati ya “maana ya umoja” na “maana ya uzazi.” Lakini, kauli hii haiwezi kueleweka kama msomaji haelewi maana ya kauli kwamba “tukio A ni chimbuko linalosababisha matokeo ambayo ni tukio B.” Kisawe cha kauli hii ni tamko lisemalo kwamba “tukio B ni matokeo yanayosababishwa na chimbuko A.” Metafizikia ya sababu na matokeo (etiology) inao msaada mkubwa katika kuweka bayana maana ya kauli hizi.

Sayansi ya bayolojia inatufundisha kwamba, mchakato wa kuzaliana kijinsia inazo hatua kumi na moja (11) zifuatazo:

Gametogenesis, heterophilic attraction, copulation, fertilization, compaction, cavitations, hatching, implantation, organogenesis during gestation, delivery, parenting, and gametogenesis (Lee na George 2008:126-127).

Kama tukiongea kwa kutumia misamiati inayotumika kwenye metafizikia ya sababu na matokeo (metaphysics of causality auetiology), basi tutasema kwamba, katika tendo la ngono inayofanyika kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, kuna uhusiano wa kietiolojia kati ya "unitive-in-effect event" na "procreative-in-effect event."

Kwa mujibu wa metafizikia ya sababu na matokeo inayoongozwa na nadharia ya mahesabu ya yamkini (probability), kama ilivyojadiliwa na Hume (1975) na Eells (1991) na kuripotiwa na Gallow (2017) kanuni ya kietiolojia ifuatayo yahusika hapa:

"Given a causally positive background K, an event C is a cause of an event E, iff: the probability of E given the occurrence of C under K is greater than zero [P(E/C&K)>0]and the probability of E given the occurrence of C under K is greater than the probability of E given the non-occurrence of C under K [P(E/C&K)>P(E/C'&K)]."

Tunafahamu kwamba, sharti la kwanza [P(E/C&K)>0] halitimii katika tendo la ngono kati ya wagumba, kwani, katika tukio hilo yamkini ya mimba ni ziro. Kwa hiyo, maneno yafuatayo yanapoteza uhalali wa kuwa kweli mara zote:

“each and every marital act {also known as uncontracepted and inseminatory penis-to-vagina sex act, entails an} intrinsic relationship to the procreation of human life (Pope Paul VI, Humanae Vitae 1968, para. 12)."

Kuna njia nyingine ya kuonyesha ukweli huu. Na njia hiyo ni kuongelea metafizikia ya sababu na matokeo (metaphysics of causality au etiology) kwa mtazamo wa "regularity" badala ya "probability."

Kwa mujibu wa etiolojia ya Hume (1975) na Eells (1991) kama ilivyofafanuliwa na Gallow (2017):

"The sentence 'C-in-type event' causes 'E-in-type event' can mean any of the following four possibilities: That, for some member c in class C and some member e in class E, member c causes member e; or that, for some member c in class C and every member e in class E, member c causes member e; or that, for every member c in class C and some member e in class E, member c causes member e; or that, for every member c in class C and every member e in class E, member c causes member e."


Hivyo, kwa kuwa kietiolojia, kugeuka mwili mmoja ni chimbuko (cause) na kuzaa mtoto ni matokeo (effect), mjadala kuhusu ndoa ya kimapokeo ni mjadala kuhusu uhusiano wa sababau na matokeo uliopo kati ya "unitive-in-effect event," kwa upande mmoja, na "procreative-in-effect event," kwa upande mwingine.

Kimsingi, kwenye nukuu hiyo hapo juu, nafasi ya maneno "C-in-type event" inachukuliwa na maneno "unitive-in-type event," na nafasi ya maneno "E-in-type event" inachukuliwa na maneno "procreative-in-type event."

Sio kila tendo la ngono linalofanyika bila kingamimba na kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike husababisha mimba. Hivyo, ni wazi kwamba, kutoka kwenye nukuu hiyo hapo juu, kauli inayotuhusu hapa ni:

"For some member c in class C and every member e in class E, member c causes member e."

Kwa njia hii, ni wazi kwamba, kuna wakati maneno "unitive-in-type sex event" yanashindwa kuwa "unitive-in-effect sex event," hata kama parameta baki katika mazingira ya tendo la ngono zinakuwa tayari kuunga mkono ujio wa "procreative-in-effect sex event."

Hapa, kuna tatizo ambalo chanzo chake sio dosari iliyo katika parameta ya kimazingira, bali, kuna dosari ambayo imo katika parameta za ndani ya mchakato wa kuzaliana kijinsia. Tatizo hili linaweza kutokea kwa sababu zilizo katika michakato ya kifiziolojia inayounda mduara wa kuzaliana kijinsia (intrinsic conditions) au kwa sababu zilizo sehemu ya mazingira yanayouzunguka mchakato huo (extrinsic conditions).

Mfano wa sababu zilizo sehemu ya michakato ya kifiziolojia ni kutokuwepo kwa yai pevu au kutokuwepo kwa mbegu za kutosha katika manii. Na mfano wa sababu zilizo sehemu ya mazingira ni mifereji ya falopia iliyoziba au shingo la tumbo la uzazi lililojibana kiasi cha kuzuia mbegu kupenya.

Sababu zote mbili ziko nje ya udhibiti wa jozi ya watianaji. Lakini, sababu ya kwanza ikitokea inaizuia jozi ya watianaji kugeuka mwili mmoja wa kifiziolojia. Hata hivyo, sababu ya pili ikitokea haizuii jozi ya watianaji kugeuka mwili mmoja wa kifiziolojia.

Hivyo, kwa mtazamo wa kietiolojia, mbali na kile kinachoitwa “extrinsic [or circumstantial] parameters which are beyond the control of the copulating pair" pia kuna “intrinsic [or non-circumstantial] parameters which are beyond the control of the copulating pair.”

Ndio kusema kwamba, kuna matendo ya ngono yanayofanyika kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jemitalia ya kike, na pasipo kutumia kingamimba, lakini ambayo hayaisaidii jozi ya watianaji kugeuka mwili mmoja. Na matendo haya ni halali kimaadili na kisheria, japo Waraka (2019) hauyatambui. Huu ni ukiukaji wa kanuni za kanuni za kietiolojia kuhusiana na ujinsia wa binadamu.

Kwa ujumla, Waraka umeshindwa kuonyesha “sababu ya lazima na inayojitosheleza” kwa kiwango cha kuiwezesha kila jozi ya watianaji “kugeuka mwili mmoja” kila mara na kila mahali

Katika metafizikia ya sababu na matokeo (metaphysics of causality), kuna tofauti kati ya sababu inayojitosheleza (sufficient cause), sababu ya lazima na isiyojitosheleza (necessary and insuffficient cause/ probabilistic cause), na sababu ya lazima na inayojitosheleza (necessary and sufficient cause).

Sababu inayojitosheleza (sufficient cause) ni sababu ambayo uwepo wake unachangia kiasi cha asilimia 100% katika ujio wa matokeo fulani, kiasi kwamba uwepo wake mahali popote na wakati wowote lazima usababishe ujio wa matokeo hayo.

Kwa mfano, tukio la kupoza maji mpaka nyuzijoto sifuri za sentigredi ni sababu inayojitosheleza katika kuhakikisha kwamba maji yaliyoganda na kuwa barafu yanatokea. Mfano wa pili wa Sababu inayojitosheleza ni ukweli kwamba, ukila ugali lazima utakwenda haja kubwa baadaye, japo vyakula vingine pia vinaweza kuzalisha matokeo hayo.

Sababu ya lazima na isiyojitosheleza (necessary and insuffficient cause/ probabilistic cause), ni sababu ambayo uwepo wake unachangia kiasi cha asilimia kidogo katika ujio wa matokeo fulani, lakini mchango wake hautoshelezi kusababisha ujio wa matokeo hayo. Kwa mfano tena, tukio la kufanya ngono ni sababu ya lazima lakini isiyojitosheleza kulingana na mahitaji ya mimba kutokea; tukio la kupevuka kwa mbegu za kiume kwa kiwango cha kutosha ni sababu ya lazima lakini isiyojitosheleza kulingana na mahitaji ya mimba kutokea; na tukio la kupevuka kwa yai la kike ni sababu ya lazima lakini isiyojitosheleza kulingana na mahitaji ya mimba kutokea. Kila tukio hapa, linayo yamkini ya kuchangia kwenye ujio wa mimba, lakini kwa asilimia fulani iliyoi chini ya 100%.

Mfano wa pili wa Sababu ya lazima na isiyojitosheleza ni ukweli kwamba, kupatikana kwa hewa ni sababu ya lazima na isiyojitosheleza katika kumfanya mtu aendelee kuishi, kwani pamoja na kupata hewa bado anaweza kufa kama akikosa chakula, akiugua malaria au ugonjwa mwingine wowote na kukosa matibabu.

Na mfano wa tatu wa Sababu ya lazima na isiyojitosheleza ni ukweli kwamba, moshi wa sigara ni sababu ya lazima na isiyojitosheleza katika kumfanya mtu kuugua kansa ya mapafu, kwani sio kila mvuta sigara huugua kansa ya mapafu.

Katika mifano hii mitatu, endapo yamkini ya mchango wa tukio A katika ujio wa tukio B ni ziro, tunsema kuwa ujio wa tukio B hauwezekani (impossibility). Na kama yamkini ya mchango wa tukio A katika ujio wa tukio B ni kubwa kuliko ziro, tunsema kuwa ujio wa tukio B unawezekana (possibility).

Sababu ya lazima na inayojitosheleza (necessary and suffficient cause), ni sababu ambayo uwepo wake unachangia kiasi cha asilimia 100 katika ujio wa matokeo fulani, kiasi kwamba, kuwepo kwake mahali kutasababisha ujio wa matokeo hayo, na kutokuwepo kwako kutazuia ujio wa matokeo hayo. Kwa mfano, tukio la kufanya ngono, tukio la kupevuka kwa mbegu za kiume kwa kiwango cha kutosha, na tukio la kupevuka kwa yai la kike, ni matukio matatu ambayo yakikutana, yanaunda sababu moja mseto (one compound cause) inayojitosheleza kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mimba inatokea.

Kwa ujumla, uwezekano (possibility) wa tukio unakuwepo endapo tukio hilo litajiri katika seti ya parameta zinazounda ulimwengu husika, tuseme ulimwengu U1, na sio vinginevyo, wakati ulazima (necessity) wa tukio unakuwepo endapo tukio hilo litajiri katika kila ulimwengu unaowezekana bila kujali parameta zilizo ndani yake.

Yaani, kauli kuwa, “Kuna uwezekano kwamba tukio X linasababisha tukio Y” ni usemi wa kweli katika ulimwengu U1 unaojumuisha seti ya parameta maalum pekee na sio vinginevyo; wakati, kauli kuwa, “Kuna ulazima kwamba tukio X linasababisha tukio Y” ni usemi wa kweli katika kila ulimwengu U2, U3,....,Ui,...., Un, ambalo kila ulimwengu Ui unaojumuisha seti ya parameta zake pekee.

Kwa hiyo, sasa turudi kwenye swali letu kuu. Je, “sababu ya lazima na inayojitosheleza” kwa kiwango cha kuiwezesha kila jozi ya watianaji “kugeuka mwili mmoja” kila mara na kila mahali ni ipi? Ni jenitalia ya kiume kukutana na jenitalia ya kike? Ni jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike kupokezana ute wa kiume (manii ya kiume) na ute wa kike (manii ya kike)? Ni kuwepo kwa yai lililopevuka katika tumbo la uzazi? Ni kuwepo kwa mbegu za kiume zilizopevuka kwa kiwango kinachotosha katika mifuko ya korodani?

4. Waraka unatumia kanuni za sayansi ya ujinsia zinayopingana na kanuni mamboleo za embriyolojia ya binadamu

Kimsingi, Waraka (2019) unasikilizana sana na nadharia ya kuzaana kijinsia inayoitwa "homunculus theory of reproduction" na hausikilizani na nadharia ya kuzaana kijinsia inayoitwa "gametogenesis theory of reproduction."

Tofauti kati ya nadharia hizi mbili, ni kama tofauti iliyopo kati ya nadharia ya mfumo wa sayari ya Wagriki (geocentric theory of the universe) na nadharia ya mfumo wa sayari iliyobuniwa na kina Corpenicus (heliocentric theory of the universe).

Wagriki walisema kuwa dunia ni tambarare kama meza na inazungukwa na jua, wakati kina Corpenicus walisema kuwa dunia ni duara na inalizunguka jua. Nadharia ya Wagriki tayari imekufa. Vivyo hivyo, nadharia ya kuzaliana kijinsia inayoitwa "homunculus theory of reproduction" imepitwa na wakati.

Kwa ufupi, "homunculus theory of reproduction," ilikuwa nazo kambi mbili. Kulikuwa na kambi iliyosema kuwa kwenye spematozoa kuna kiluwiluwi cha binadamu aliyekamilika (homunculus) ambacho hupandikizwa katika tumbo la uzazi kwa njia ya ngono. Hii ilijulikana kama kambi ya “spermist preformation theory.”

Na kwa upande mwingine, kulikuwa na kambi iliyosema kuwa kwenye ovamu kuna kiluwiluwi cha binadamu aliyekamilika (homunculus) ambacho huanguliwa na kisha kupandikizwa katika tumbo la uzazi kwa msaada wa spematozoa zinazogongagonga ukuta wa nje wa ovamu mara tu baada ya tendo la ngono. Hii ilijulikana kama kambi ya “ovist preformation theory.”

Kwa sasa, kambi ya “spermist preformation theory” na kambi ya “ovist preformation theory” zimezikwa na wanasayansi. Nadharia inayofafanua michakato iliyomo katika mduara wa kuzaana kijinsia (sexual reproduction cycle) ni "gametogenesis theory of reproduction."

Kimsingi, "gametogenesis theory of reproduction" inasema kuwa ovamu na spematozoa huungana na kuunda seli moja mpya inayokuwa chimbuko la bindamu mpya; na kwamba, yamkini ya kupevuka kwa ovamu ndani ya mwili wa mwanamke ni 17% katika kila siku 30 za mwezi.

Katika mtazamo wa "gametogenesis theory of reproduction" kauli ifuatayo sio ya kweli: kwamba "katika mazingira yaliyo na uchanya wa kietiolojia, kila tendo la ngono linalofanyika kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, bila kutumia kingamimba, na kwa kuhakikisha kuwa jenitalia zinabadilishana ute, linaweza kusababisha mimba." Inakuwa kweli ndani ya "homunculus theory of reproduction," ambayo imechuja.

5. Waraka umeshindwa kutaja fasili ya ndoa yenye kuwasaidia Watanzania kupata jawabu la swali linalohusu habari ya ndoa ni kitu gani na sio kitu gani

Japo mada kuu ya Waraka (2019) ni “ndoa na familia”, bado umeshindwa kutaja fasili ya ndoa yenye kubeba vigezo vinavyokidhi mahitaji ya ulazima na utoshelezo wa kimaana (necessary and sufficient definition of marriage) ili kuwasaidia wasomaji kupata jawabu la swali lifuatalo: Ndoa ni kitu gani na sio kitu gani?

Kwa mfano, ukisema kwamba “kapela ni binadamu mtu mzima wa kiume ambaye hajafunga ndoa” unakuwa umetoa fasili ya neno “kapela” yenye sifa mbili muhimu zifuatazo:

Mosi, ukapela unatambulishwa kwa vigezo vinne, yaani, ubinadamu, utu uzima, uanaume na hali ya ndoa, ambapo, kila kigezo kilichotajwa kati ya hivi vigezo vinne ni lazima kiwepo ili kumtambulisha kapela, lakini peke yake hakitoshelezi utambulisho wa kapela. Hii ni sifa ya ulazima ((necessity)

Na pili, kuna dokezo kwamba, vigezo vyoe vinne kwa pamoja vinatosheleza hitaji la kumtambulisha mtu ambaye ni kapela. Hii ni sifa ya utoshelezo (sufficiency).

Kwa hiyo, fasili hii ya “kapela” inabeba vigezo vinavyokidhi mahitaji ya ulazima na utoshelezo wa kimaana (necessary and sufficient definition of bachelor) ili kuwasaidia wasomaji kupata jawabu la swali lifuatalo: Kapela ni kitu gani na sio kitu gani?

Raia yangu ni kwamba, Waraka (2019) umeshindwa kuwasaidia Watanzania kupata fasili ya ndoa inayokidhi sifa muhimu za udadavuzi wa maana ya neno "ndoa."

Sifa kuu za ndoa zilizotajwa na Waraka (2019) ni: uwepo wa mkamilishano wa kijinsia kupitia jozi ya mwanamke na mwanamume, uwezekano wa kugeuka mwili mmoja, utayari wa uzaana, uaminifu, umoja usiovunjika hadi kifo, na ridhaa huru kati ya mwanamke na mwanamume.

Vigezo hivi vimetajwa katika Sheria za Kanisa Katoliki (1983) kwenye ibara ya 1055 (1) na 1055 (2). Pia, vigezo hivi vimetajwa katika Sheria za Makanisa ya Mashariki kwenye ibara ya 776. Kwa mujibu wa vifungu hivi vya sheria za Makanisa haya, hivi ndivyo vigezo sita, ambavyo kwa pamoja, vinakidhi mahitaji ya ulazima na utoshelezo wa kifasili (necessary and sufficient definition) ili kuwasaidia wasomaji kupata jawabu la swali linalohusu “ndoa ni kitu gani na sio kitu gani.”

Fasili ya ndoa iliyomo katika vifungu hivi inatofauisha kati ya mambo mawili muhimu. Kwanza kuna “the subject of matrimonial consent,” ambayo ni jozi ya mwanamke na mwanamume. Na pili, kuna “the object of matrimonial consent,” ambayo inatajwa kuwa ni “the [complemetary and] reciprocal gift of self (can. 1057 (2)).”

Lakini, katika fasili hii, kigezo muhimu zaidi ni “uwezekano wa kugeuka mwili mmoja” pamoja na “uwezekano wa kuzaana,” dhana ya kwanza ikiwa ni chanzo na dhana ya pili ikiwa ni matokeo.

Hii maana yake ni kwamba, ndoa za wagumba zisizo na sifa ya uwezekano wa kugeuka mwili mmoja sio ndoa inayotambuliwa na sheria za Makanisa haya.

Hapa, fasili tajwa inakumbana na changamoto ya mifano kanushi ifuatayo: ndoa zisizo rasimishwa kisheria, maisha ya mpito yeye sura ya ukimada, wazazi wasioishi na mwazazi wenza, wazazi wa kike wa kukodiwa, ndoa za jinsia moja, ndoa za majike-dume, ndoa za watu waliobadilisha jinsia zao, ndoa za majaribio, ndoa za mkataba, talaka za kimahakama, ndoa za vijana wagumba, ndoa wa watumia kingamimba, ndoa za vikongwe.

Yaani, “cohabitation, free unions, single parenthood, surrogate motherhood, same-sex marriages, hermaphroditism, transsexualism, trial marriages, contract marriages, civil divorce, barren marriages, conracepting marriages and post-menopausal marriages.”

Katika ndoa hizi hakuna “uwezekano wa kugeuka mwili mmoja” wala “uwezekano wa kuzaana,” japo nchi mbalimbali huko Amerika, Ulaya na Afrika zinazitambua kama ndoa halali kisheria.

Na hili ni tatizo la muda mrefu ndani ya Kanisa Katoliki. Tangu Papa Paul VI alipotangaza Waraka wa Humanae Vitae (1968), kitendawili hiki lilidunda katika kumbi za mijadala ya Wanataaluma Wakristo duniani kote, lakini zaidi huko Amerika.

Huko tayari kulikuwa na ndoa nyingi za vijana waliokuwa tayari wameamua kuishi kama wanandoa wagumba baada ya kufunga uzazi kwa sababu za magonjwa ya kijenetiki kama vile ugonjwa wa selimundu, ndoa za wazee wagumba, na ndoa za jinsia tofauti zinazotumia kingamimba.

Makundi haya niliyoyataja yakahoji kama, nayo yana haki zote za ndoa kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria za Kanisa, katika mipaka ya Waraka wa Humanae Vitae (1968).

Wanataaluma Katoliki wa Amerika wakakubaliana kwamba, kabla ya kuongelea usawa wa ndoa zote hizo mbele ya sheria za nchi na sheria za kidini, ni muhimu kwanza likajibiwa swali kuhusu "ndoa ni kitu gani na sio kitu gani."

Kwa kuwa ni Wakristo, tafakari yao ilikuwa inaanzia kwenye Biblia. Haraka wakagundua kuwa, kwa mujibu wa Agano la kale (Mwa. 2:24) sifa kuu ya ndoa ni jozi ya watianaji kugeuka "mwili mmoja" kupitia tendo la ngono linalofanyika kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, kuhakikisha kwamba manii yanakojolewa kwenye jenitalia ya kike, na bila kutumia kingamimba.

Lakini, wakakumbuka kuwa, kwa mujibu wa Agano Jipya (1Wakor. 6:16), hata kahaba na mteja wake kwenye danguro wanadaiwa kugeuka "mwili mmoja" kupitia tendo la ngono wanalolifanya kwa kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, kuhakikisha kwamba manii yanakojolewa kwenye jenitalia ya kike, na bila kutumia kingamimba.

Hivyo, kitendawili kikazuka: Kugeuka mwili mmoja kupitia tendo la ngono maana yake nini? Polepole mijadala ikabainisha mambo kadhaa kuhusiana na swali hili.

Mosi, walibaini kwamba, kuna "mwili mmoja wa kifiziolojia" (physiological one flesh unity), ambapo, kama hakuna mazingira hasimu, fiziolojia za kiume na kike zinaweza kukamilishana katika lengo moja la uzazi (physiological complementarity).

Pili, wakagundua kwamba, "mwili mmoja wa kifiziolojia" unaweza kuwa chimbuko la "mwili mmoja wa mimba" (embryonic one flesh union), yaani, mtoto mpya kinachotokana na muungano wa spematozoa ya mwanamume na ovamu ya mwanamke.

Tatu, wakagundua kwamba kuna "mwili mmoja wa kisaikolojia" (psychological one flesh unity), ambapo, tukiweka kando ubakaji, akili ya kike na kiume zinakamilishana katika malengo ya pamoja, kupitia tendo la ngono, hata kama halina fursa ya kusababisha uzazi (psychological complimentarity).

Nne, iligundulika kwamba, mke kijana hana rutuba ya uzazi kwa 83% ya siku za kila mwezi lakini katika siku hizo zote bado Biblia inasema kuwa jozi ya watianaji hawa wanaofanya tendo la ngono ya kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike hugeuka mwili mmoja pia.

Tano, iligundulika kwamba, wanandoa wanawake waliokoma kwenda hedhi hawana rutuba lakini bado Biblia inasema kuwa jozi ya watianaji hawa wanaofanya tendo la ngono ya kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike hugeuka mwili mmoja pia.

Sita, iligundulika kwamba, wake waliokwanguliwa kizazi hawana rutuba lakini bado Biblia inasema kuwa jozi ya watianaji hawa wanaofanya tendo la ngono ya kukutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike hugeuka mwili mmoja pia.

Na saba, wakakumbuka kwamba, kila tendo linalofanywa na binadamu kwa makusudi linazo fainali mbili. Kwa upande mmoja, kuna fainali ya mtendaji (finality of the operator), ambayo kwa kilatini wanasema "finis operantis." Na Kwa upande mwingine, kuna fainali ya tendo (finality of the operation), ambayo kwa kilatini wanasema "finis operis."

Kwa mfano, walibaini kuwa, katika mfano wa fundi saa na saa anayoitengeneza kuna mambo mawili. Fainali ya kitendo cha kutengeneza "saa ya ukutani" ni kuhesabu muda, wakati fainali ya mtengeneza "saa ya ukutani" ni kutafuta kipato.

Vivyo hivyo, wakabaini kuwa, fainali ya tendo la ngono inaweza kuwa ni uzazi, uasherati, ubakaji, wakati fainali ya mtendaji anayeshiriki katika kutekeleza tendo la ngono ikawa kutafuta kipato, kutoa shukrani, kufariji, kutafuta anasa, au kuburudisha.

Katika mazingira haya, swali kuu likazuka: Kama sifa kuu ya tendo la ngono ya ndoa ni kuiwezesha jozi ya watianaji kugeuka “mwili mmoja," maneno “mwili mmoja" maana yake nini hasa?

Hatimaye zikazuka kambi mbili. Katika upande mmoja, kukazuka kambi ya Maaskofu Katoliki, ikiongozwa na Wanataaluma Wakristo waliojiita “Wataalam wa Maadili Asilia Mamboleo (New Natural Lawyers),” waliosisitiza kuwa hata watianaji wagumba hugeuka mwili mmoja, kwa maana kwamba, nao wanashiriki katika "unitive-type sex acts."

Sababu yao ikawa kwamba, watianaji wagumba wanashiriki katika "hatua ya kwanza" iliyo katika mchakato wa kuzaliana kijinsia (sexual reproduction cycle) wenye hatua kumi na moja (11) zifuatazo:

Gametogenesis, heterophilic attraction, copulation, fertilization, compaction, cavitations, hatching, implantation, organogenesis during gestation, delivery, parenting, and gametogenesis (Lee na George 2008:126-127).

Katika kusisitiza mtazamo wao, Maaskofu walisema kuwa kutiana ni kutekeleza mradi kama ilivyi kutekeleza miradi ifuatayo: kufanya utafiti, kuwinda swala, kucheza mechi ya mpira, na kusomea kazi. Kwamba kuna kupata na kukosa lakini jina la mradi haibadiliki kwa sababu ya kukosa.

Katika kambi ya pili, kulizuka kambi ya wanamageuzi (revisionists). Hawa walisisitiza kwamba, katika mchakato wa kuzalina kijinsia, kutiana sio hatua ya kwanza, bali ni hatua ya tatu. Kisha wakasisitiza kuwa, metafizikia ya sababu na matokeo (etiology) haiko upande wa Maaskofu.

Walifafanua kuwa, katika tendo la ngono ya ndoa, tunachoongelea ni uhusiano wa kietiolojia kati ya "unitive-in-effect event" na "procreative-in-effect event."

Wakaongeza kusema kuwa, kwa mujibu wa metafizikia ya sababu na matokeo (metaphysics of causality auetiology) kwa mtazamo wa mahesabu ya yamkini (probability), kama yalivyojadiliwa na Hume (1975), Eells (1991) na Gallow (2017) kanuni ya kietiolojia ifuatayo yahusika:

"Given a causally positive background K, an event C is a cause of an event E, iff: the probability of E given the occurrence of C under K is greater than zero [P(E/C&K)>0] and the probability of E given the occurrence of C under K is greater than the probability of E given the non-occurrence of C under K [P(E/C&K)>P(E/C'&K)]."

Wakahitimisha kuwa, sharti la kwanza [P(E/C&K)>0] halitimii katika tendo la ngono kati ya wagumba, kwani, katika tukio hilo yamkini ya mimba ni ziro. Kwa hiyo, wanamageuzi wakahitimisha kwamba, msimamo wa maaskofu hauwezi kusimama.

Mpaka hapo ukazaliwa mtanziko unaoanzia kwenye maana ya maneno "mwili mmoja" yanamaanisha "gimba moja” aukiumbehai kimoja." Maaskofu wakashikilia msimamo kwamba kila jozi ya watianaji, bila kujali kama ni wagumba au vinginevyo, hugeuka “kiumbe hai” kimoja, na wanamageuzi wakashikilia msimamo kwamba jozi ya watianaji wagumba haiwezi kugeuka “kiumbe hai” kimoja.

Kwa hiyo, hatimaye yakazaliwa maswali makuu yafuatayo: Kiumbehai ni kitu gani na sio kitu gani? Vitu gani vinazo sifa za kuhesabiwa kama viumbehai? Na jozi ya watianaji ni miongoni mwa vitu vinavyoitwa viumbehai?

Kimsingi, ni kazi ya wanabayolojia na wanafalsafa wa bayolojia kujibu maswali haya. Na kufikia miaka ya 2000, tayari wanasayansi na wanafalsafa wengi wanakubaliana kwamba, swali “Kiumbehai ni kitu gani na sio kitu gani?” linaweza kujibiwa bila kuacha chembe ya shaka kama ifuatavyo:

Kwa mfano, wanabayolojia wengi wanakubaliana na Queller na Strassmann (2009, 2010, 2016) kwamba: “An organism is a unit in which all the subunits have evolved to be highly cooperative, with very little conflict ('in the direction of a common end').” (Queller & Strassmann 2009:3144, 2010:605, na 2016:1)

Ndio kusema kwamba, “Kiumbe hai ni kitu chenye mwili mmoja ambao una viungo mbalimbali vilivyogawana majukumu yenye kukamilishana kiasi kwamba utekelezaji wa majukumu hayo unafanyika kwa ushirikiano mkubwa na msuguano kidogo.” (Tafsiri yangu)

Na wanafalsafa pamoja na wanateolojia wengi wanakubaliana na Pruss (2000, 2015) anayefundisha kuwa, “An organism is an entity united in an integrated action of itself directed at … two ends: self-preservation and reproduction.” (Pruss 2000: 76),

Anachosema Pruss (2000) ni kwamba: “Kiumbe hai ni kitu chenye mwili mmoja ambao una viungo mbalimbali vilivyogawana majukumu yenye kukamilishana kiasi kwamba utekelezaji wa majukumu hayo unaviwezesha viungo vyote kufanikisha kwa pamoja lengo la kuhifadhi maisha binafsi na kuzaliana .” (Tafsiri yangu)

Kisha, Pruss (2000) anafungamanisha fasili hii na dhana ya ndoa kwa kusema kuwa, “Kwa kuzingatia uchambuzi unaoongozwa na mitazamo ya kiteliolojia kuhusu maisha ya viumbe hai, kusema kuwa mwanamke na mwanamume kwa pamoja wanageuka kiumbehai kimoja [wakati wa kutiana] ni kumaanisha kwamba wanashirikiana katika kitendo kimoja ambacho lengo lake ni… kuhifadhi uhai binafsi na kuzaliana.”

Baadaye, Pruss (2015:16) anahitimisha hoja yake kwa kusema kuwa: “Kitu kinachounganisha viungo mbalimbali ndani ya mwili mmoja wa kiumbe hai sio kugusana kwa viungo hivyo, bali, ni ukweli kwamba, viungo hivyo vinashirikiana kufanya kazi zake ili kufanikisha lengo la pamoja.”

Ni maoni yangu kwamba, fundisho la ndoa kwa mujibu wa "kanuni ya mwili mmoja" linaweza, na linapaswa kueleweka ndani ya mipaka ya fasili hizi zinazosisitiza wazo la uwepo wa "michakato ya kiteliolojia” ndani ya mwili ambao ni kitovu cha utambuzi na maamuzi yanayoanzia ndani ya mwili husika, kama sifa kuu ya kila kiumbe hai

Tayari Myar (1974) na Torley (2005) wametusaidia kutofaitisha kisayansi kati ya teliolojia ya kifiziolojia na teliolojia ya kisaikolojia (physiological teleology versus psychological teliology).

Kwa hiyo, kuna viumbe hai wa kifiziolojia na viumbe hai wa kisaikolojia. Vivyo hivyo, kuna ndoa za kifiziolojia na ndoa za kisaikolojia. Hili ni hitimisho lisiloweza kikanushika kisayansi na kifaksafa.

Hata hivyo, Maaskofu Katoliki na washauri wao wa kitaaluma (New Natural Lawyers) hawataki kusikia utofautisho huu kwa sababu moja tu: ukitambua uwepo viumbe hai wa kisaikolojia unaweza kuwa umetambua uwepo wa ndoa za jinsia moja.

Katika msimamo huu wa Maaskofu Katoliki, silaha pekee iliyobaki mikononi mwao ni upanga wa Kimachiaveli, yaani hoja haramu ifuatayo kwa ajili ya kuziba midomo wakosoaji wake:

  • Kama "mtu X" akiunga mkono kiumbehai chenye umoja wa kisaikolojia anakuwa anaunga mkono ushoga;
  • Kila mtu anayeunga mkono ushoga anakuwa ni shoga;
  • Kwa hiyo, "mtu X" ni shoga.
Hata hivyo, hoja hii ni batili kwa sababu madokezo mawili ya kwanza hayasemi ukweli. Kwa mfano, kama Kila mtu anayeunga mkono ushoga ni shoga; kwa nini tusiseme pia kwamba, Kila mtu anayeunga mkono wanawake, kama Maskofu Katoliki walivyofanya, ni mwanamke pia?

Mpaka hapo, Maaskofu Katoliki wanapoteza hoja. Wanalazimika kurudi mezani na kupanga maelezo yao vizuri kuhusu swali, “Ndoa ni kitu gani na sio kitu gani.”

Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi, Kiambatanisho B kinaeleza kwa kina jawabu kwa swali “Kiumbe hai ni kitu gani na sio kitu gani?”

6. Waraka unapiga marufuku ndoa za jinsia moja kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.

Waraka (2019) umepinga ndoa za jinsia moja, kwa kueleza kwamba, kupitia ndoa za jinsia moja wahusika hawawezi kugeuka “mwili mmoja.” Lakini, kuna ndoa halali za jinsia tofauti ambazo haziwaruhusu wahusika kugeuka “mwili mmoja.”

Kwa hiyo, tunarudi tena kwenye swali letu la msingi: “Ndoa ni kitu gani na sio kitu gani?” Katika Kiambatanisho F nimejadili kwa kirefu hoja dhidi ya ndoa za jinsia moja na dosari zake ili kuwapa nafasi Maaskofu Katoliki kujibu kwa hoja, badala ya vitisho na ulaghai.

7. Waraka unapiga marufuku mapenzi ya kigumba kwa kutumia sababu zinazoyumba kutetea marufuku hiyo.

Waraka (2019) umepinga mapenzi ya kigumba kati ya watu wa jinsia tofauti, kwa kueleza kwamba, kupitia mapenzi hayo wahusika hawawezi kugeuka “mwili mmoja.”

Lakini, kuna ndoa halali za jinsia tofauti ambazo zinafanya matendo ya ngono yanayokutanisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike bila kuwaruhusu wahusika kugeuka “mwili mmoja.”

Kwa hiyo, hapa pia, tunarudi tena kwenye swali letu la msingi: “Ndoa ni kitu gani na sio kitu gani?” Katika Kiambatanisho G nimejadili kwa kirefu hoja dhidi ya ndoa za jinsia moja na dosari zake ili kuwapa nafasi Maaskofu Katoliki kujibu kwa hoja, badala ya vitisho na ulaghai.

8. Waraka unafundisha juu ya ndoa na familia kwa kutumia athropolojia ya kijinsia iliyopitwa na wakati

Katika Waraka (2019), kuna upogo mkubwa katika parameta ya taaluma ya ujinsia (sexology), kwa kiwango ambacho kinakwaza mradi wa kujenga imani ya jamii ya kitaifa.

Yaani, waraka huu unafafanua “hulka ya binadamu” katika namna ambayo haiwaelimishi wananchi vya kutosha juu ya ujinsia wa binadamu kama unavyofahamika leo kupitia miwani ya mapokeo, misahafu, sayansi, na falsafa.

Sasa tunafahamu kuwa, kuna "mibetuko ya kijinsia mitatu inayofahamika. Kuna uandrofilia, ugainofilia na uambifilia. Yaani, kuna "androphilic, gynephilic and ambiphilic sexual orientations." Na kila mbetuko tajwa ni sehemu ya "hulka ya binadamu" inayotajwa katika Waraka (2019).

Kwa hiyo, kuna "hulka ya binadamu mwanamke" ambaye yuko katika kundi la watu wenye uandrofilia, na "hulka ya binadamu mwanamume" ambaye yuko katika kundi la watu wenye ugainefilia. Pia, kuna "hulka za binadamu" zifuatazo: ushoga, usagaji, ujinsiageu, ujinsiapindu na ujikedume (GLBTI). Wote hawa ni raia halali wa Tanzania.

Hivyo, maneno "hulka ya binadamu" yanazo maana nyingi zinazopaswa kufafanuliwa kila mara yanapotumika.

Lakini, Waraka (2019) hautambui ukweli huu. Hivyo, kuna haja kwa Maaskofu Katoliki kuziba pengo lililojitokeza hapa.

Maana za baadhi ya maneno ya msingi yaliyotumika kwenye Waraka (2019) zimefafanuliwa katika Kiambatanisho D ili kuonyesha utata unaojitokeza kwenye Waraka (2019). Kwa hapa nitagusia maneno machache muhimu kulingana na kitu ninachotaka kusisitiza.

Kisayansi, neno "mwanamume" linaweza kuwa na maana mbili au zaidi. Kuna watu ambao ni wanaume kwa umbile la nje (phenotypical males) lakini ambao wana umbile la kike kwa ndani (genotypical females).

Na kuna watu ambao ni wanawake kwa umbile la nje (phenotypical females) lakini ambao wana umbile la kiume kwa ndani (genotypical males).

Katika mazingira haya ya kisayansi maneno kwamba, "Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke" (Walawi 18:22-26) yanapaswa kutafsiriwa upya.

Wanateolojia makini hawawezi kukwepa ukweli huu wa kisayansi halafu wakatekeleza jukumu lao la kujenga "imani ya jamii ya Taifa" kwa kuzingatia alama za nyakati. Maaskofu Katoliki wanapaswa kujipanga upya katika eneo hili.

9. Waraka umetumia Misahafu na Mapokeo kama vyanzo vya kimaarifa lakini ukasahau vyanzi vingine muhimu kama vile sayansi asilia, sayansi za jamii, sayansi za kimahesabu, na falsafa.

Maaskofu Katoliki wameandika Waraka (2019) kwa ajili ya kusisitiza fundisho la ndoa kama “mwili mmoja” lisemalo kwamba kwamba, "wakati wa tendo la kutiana kati ya mwanamke na mwanamume, lakini sio kabla yake wala baada yake, kila tendo la ngono ya kukutanisha jenitalia ya kike na jenitalia ya kiume huiwezesha jozi ya watianaji kugeuka mwili mmoja, gimba moja, kiumbehai kimoja ('one flesh, one body, one organism')."

Hili ni fundisho lililotajawa Mwanzo 2:24 zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Ni fundisho ambalo asili yake ni dini ya Kiyahudu, na sio Ukristo. Wayahudu wanayo namna yao ya kutafsiri fundisho hili. Wakristo wa mwanzo wanayo namna yao pia waliyoipendekeza na hiyo tafsiri ikakwa sehemu ya mapokeo ya Kanisa la leo.

Wanasayansi na wanafalsafa nao wanayo nafasi yao katika kujenga imani ya jamii. Kuna mkanganyiko wa kiteolojia, kisayansi na kifalsafa juu ya fundishi hili. Wanachosema wanasayansi ndio ukweli mamboleo. Ni vigumu dunia ya millennia ya tatu kubaki ni mtumwa wa historia ya zama za mawe.

Kwa mfano, sasa tunafahamu kuwa, katika soko la "imani za kijamii" yapo mafundisho kuwa kila mwanamke ni mgumba kwa 83% ya maisha yake. Mafundisho haya yanaingia katika soko linalotumiwa Maaskofu wa TEC na kuwekwa kama mawazo mbadala, kwa hoja zenye ushahidi. Kigezo cha ushindi ni ukweli, na sio ubabe.

Hatimaye, wanunuzi wa "imani za jamii" kutoka kwenye soko hili ndio wataamua upande gani unafanya kazi ya "kuozesha akili na mioyo ya walimwengu" kwa kubadilisha "uovu" kuwa "tunu."

Tukumbuke kuwa, Maaskofu hawana mamlaka ya kugeuza uwongo kuwa ukweli. Kifalsafa, "uwongo" ni uovu wa kiaskiolojia (axiological evil) na ukweli ni tunu ya kiaskiolojia (axiological good).

Uovu ni kazi ya shetani, tunu ni kazi ya Mungu. Kwa hiyo ni sawa kupinga, "agenda ya kugeuza imani na maadili" kwa kubadilisha "uovu" kuwa "tunu."

Wakosoaji wa Maaskofu wanafanya kazi hii, na hivyo, kulinda imani ya jamii ya Taifa zima, kama ilivyo dhamira ya Maasjofu Katoliki.

Kwa uhakika, sote hatuna mamlaka ya kuugeuza uwongo kuwa ukweli, au kugeuza uovu kuwa tunu. Tatizo ni kwamba, kuna kitu Maaskofu wanakiita "tunu," lakini mimi naona kuwa kitu hicho ni "uovu."

Kwa ufupi, kauli ambayo Maaskofu wa Kurasini wanaiteta, na ambayo wakosoaji wake wanaikataa kwa kuweka ushahidi mezani, ni hii hapa, kwamba:

"each and every marital act [also known as uncontracepted and inseminatory penis-to-vagina sex act, entails an] intrinsic relationship to the procreation of human life ( Humanae Vitae, para. 12)."


Wakosoaji wanasema kwamba hii ni kauli ya uwongo na kwa miaka 50 sasa Maaskofu Katoliki wamekuwa wanasema kwamba hii ni kauli ya ukweli. Utetezi wa mtazamo wa wakosoaji wa Maaskofu umo katika Kimbatanisho J.

Kwa ujumla, hapa itoshe kusema kuwa, hoja ya Maaksofu imewasilishwa kwa kutumia maneno 10,600 (Tazama Kiambatanisho cha Waraka husika).

Lakini, yafaa kudokeza kuwa, Maana ya ndoa na familia kwa mtazamo wa Biblia, kama ilivyojadiliwa katika Waraka (2019) imefupishwa vizuri katika makala ya Budziszewski (2005), anayesema haya:

“Kiapo cha ndoa ni ahadi ya hiari inayohusisha pande mbili, yenye kufanyika kwa mujibu wa sheria za nchi, na sheria za Mungu, kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, ambao ni watu wazima, wasio na undugu wa karibu wa damu, ambapo wahusika huamua kuondoka kwa wazazi wao na kuhamia katika makazi yao kwa ajili ya kuzindua muungano wao kupitia matendo yanayoweza kuzalisha umoja wa kimwili (‘mwili mmoja,' 2:24), na baadaye kuyaendeleza matendo haya kila mara kwa ajili ya kutengeneza mazingira yanayowawezesha kuanzisha familia yao ('zaeni,' 1:28) na kusaidiana kiuchumi na kijamii ('msaidizi,' 2:23) pasipo kutengana mpaka kifo kinapowatenganisha.”

Katika fasili hizi kuna mawazo ya msingi kumi na mbili yanayopaswa kufafanuliwa, kusudu sababu za uwepo wake katika fasili hii zieleweke na kukubalika. Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi tazama Kiambatanisho E.

Lakini, Maaskofu na Wakosoaji wao wanakubaliana kuhusu fasili hii, isipokuwa kuhusu maeneo machache tu, kama ifuatavyo:

Mosi, wakati maneno “mwili mmoja” yanachukuliwa na Maaskofu Katoliki kumaanisha “kiumbe hai mmoja wa kifiziolojia,” wanafalsafa na wanabayolojia sasa wanaongelea uwepo wa “kiumbe hai mmoja wa kisaikolojia” pia.

Pili, Wakati maadili yaliyo katika mpango wa Mungu yanasema mume mmoja mke mmoja (Mwa. 2:23-24), kuna mifumo ya maadili mbadala inayoruhusu ndoa za mume mmoja wake wengi, ndoa za wake wengi mume mmoja, ndoa za wake wengi waume wengi, na uzinzi;

Tatu, Wakati maadili yaliyo katika mpango wa Mungu yanasema ndoa ni kati ya mwanamke na mwanamume (Mwa. 2:23-24), kuna mifumo ya maadili mbadala inayoruhusu ndoa za jinsia moja;

Nne, Wakati maadili yaliyo katika mpango wa Mungu yanasema mke na mume washirikiane (Mwa. 2:18), kuna mifumo ya maadili mbadala inayoruhusu ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake;

Tano, Wakati maadili yaliyo katika mpango wa Mungu yanasema ndoa ni muungano wa kudumu (Mwa. 2:24; Mat. 19:3-6), kuna mifumo ya maadili mbadala inayoruhusu talaka, ndoa za majaribio na ndoa za mkataba;

Sita, Wakati maadili yaliyo katika mpango wa Mungu yanasema ndoa ni chanzo cha familia (Mwa. 1:28), kuna mifumo ya maadili mbadala inayoruhusu kufunga kizazi na kutumia kingamimba;

Na saba, Wakati maadili yaliyo katika mpango wa Mungu yanasema ndoa ni muungano kwa ajili ya kujenga umoja wa kimwili (Mwa. 2:24; Walawi 18:22-24), kuna mifumo ya maadili mbadala inayoruhusu matendo ya ngono yaliyo kinyume cha maumbile.

Ni wazi kwamba, mipango mbadala inayoruhusu mambo yanayokatazwa na mpago wa Mungu wa Biblia ni upotoshaji wa mpago wa Mungu huyo. Lakini, hoja lazima ijengwe na Maaskofu Katoliki ili kuonyesha ni kwa nini Mpango wa Mungu wa Biblia ni halali na mipango mbadala ni haramu.

Napendekeza kwamba, haitoshi kutamka mpango wa Mungu wa Biblia kwa kunukuu Biblia na kuondoka kwa kutumia kisingizio kwamba, hiyo ni “marufuku ya Biblia ambayo hatuna mamlaka ya kuibadili.” Hiki ni kisingizio dhaifu kwa sababu zaidi ya nne. Kwa mfano:

  • Kuna aya zinaruhusu utumwa, mifano ni: 1 Petro 2:18; Wakolosai 3:22-23; Walawi 25:44.
  • Kuna aya zinasema kuwa jua linaizunguka dunia, mifano ni: Joshua 10:12-13, 2 Wafalme 20:11, Zaburi 93:1, 104:5, Mhubiri 1:5, Isaya 30:26, Isaya 38:8, 1 Wathesalonike 4:16-18 na Habakuki 3:10-11.
  • Kuna aya zinatoa ruhusa ya kula nyama ya mtu katika nyakati ngumu, ambapo mifano ni: Hesabu 28:53-57, Walawi 26:29, Yeremia 19:9, Ezekieli 5:10, Maombolezo 4:10.
  • Na kuna mistari ya Biblia inaruhusu mauaji ya kimbari bila kutofautisha kati yawatoto, wazazi na mifugo wasio na hatia, mfano ukiwa: Gharika Kuu, Mwa. 6:9-9:17.
Utumwa, uwongo, kula nyama za watu na mauaji ya halaiki kuanzia watoto hadi wanyama wafugwao ni mafundisho ya kishetani. Hivyo, hizi ni baadhi ya aya za shetani zilizo katika Biblia. Kwa sababu hiyo, haya ni mafundisho haramu kisheria na kikatiba hapa Tanzania.

Na kwa sababu Maaskofu wanawajibika kutii sheria za nchi, wanalazimika kuungana na Watanzania wote katika kulinda Katiba na sheria za nchi na kupuuzia mawazo haya ya kishetani yaliyo katika Biblia.

Kwa hiyo, sio kila kitu kilichoandikwa katika Biblia kinayo hadhi ya kuwa sehemu ya "imani ya jamii ya Taifa" (national social doctrine) katika milenia ya tatu. Maaskofu wanayo mamlaka ya kupuuzia mistari ya Kibiblia yenye harufu ya kishetani au kishirikina. Ndio maana wanasoma falsafa miaka mitatu kabla ya kusoma teolojia miaka mitatu.

Aidha, napendekeza kwamba, haitoshi kujitetea kwamba, “dhambi hizi zimedokezwa na kukemewa kwa msimamo usioyumba" tangu Agano la Kale" mpaka "kwenye Agano Jipya.”

Kitabu kinachoitwa "Agano Jipya" chenye kuongelea Maisha ya Yesu kina umri wa miaka 2000 sasa. Hivyo, katika uhalisia, Sehemu hii inatupatia Taarifa za "Agano la Jipya," kama ikifananishwa na "Agano la Kale" kabla ya Yesu.

Lakini, leo hii kuna Taarifa za "Agano Jipya Zaidi" linalohusisha Taarifa za ugunduzi wa Kisayansi pamoja na Udadavuzi wa falsafa uliofanyika baada ya Yesu kufa.

Hii ndio sababu Kanisa linasisitiza kuwa kuna vyanzo vinne vya maarifa, yaani, Misahafu, Mapokeo, Urazini, na Uzoefu (Scriptures, Tradition, Reason & Experience).

Mimi natofautisha kati ya "Urazini wa kisayansi na urazini wa kifalsafa," yaani "scientific reason versus philosophical reason." Kwa hiyo, naongelea vyanzo vitano.

Lakini bado kuna tatizo jingine. Pia, kuna undumila kuwili wa kimaana (equivocation) unaoyazunguka maneno "mwili mmoja" ambao hauwezi kuondoka kwa sababu pekee ya kwamba umevumiliwa kwa miaka 2000.

Kwa hakika, huu undumila kuwili wa kimaana unafuta madai kwamba kuna "msimamo usioyumba" kuhusu maana ya ndoa kama "ushirika wa mwili mmoja," yaani "one flesh unity."

Kuwavisha "joho la ushoga" au "gauni la usagaji" wakosoaji wa jambo hili kusudi kuwaondolea "mwanga wa uadilifu mbele ya jamii," na hivyo kuwaziba midomo kibabe, hakutatui tatizo husika.

Kama Maaskofu wa TEC wanavyojua fika, undumila kuwili wa kimaana (equivocation) unaohusiana na maneno "mwili mmoja" ni ushahidi halisi wa tatizo la kuyumba kifikra ndani ya Kanisa Katoliki lililozaliwa tangu 1968 kupitia ibara ya 12 ya Humanae Vitae.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kadiri dunia inavyobadilika, kuna haja ya kuzisoma alama za nyakati na kutafuta majibu mapya kwa maswali makongwe, bila kusahau kutafuta majibu mapya kwa maswali mapya.

Upekee wa Kanisa Katoliki ni ukweli kwamba, siku zote limekuwa ni kanisa linalojitenga na tabia ya kufanya "copy and paste" ya mistari kutoka kwenye Biblia. Lakini, safari hii, Vigogo wa Kurasini wamebadilisha gia angani.

Kwa mfano, kuiba ni kitendo haramu kimaadili, lakini uharamu wake hautokani na ukweli pekee kwamba Misahafu inasema hivyo. Lazima kuna sababu iliyomfanya mwandishi wa Misahafu kusema hivyo. Sababu hiyo lazima utolewe na kutetewa kimantiki ili hata wale wasioamini katika Misahafu wapate sababu ya kuunga mkono hoja. Waraka waKwarezima Kutoka Kurasini (2019) ulipaswa kufanya kazi hii.

Kulingana na muhtasari wa waraka hapo juu, basi, ilitarajiwa kwamba, waraka ujenge hoja kamilifu za kuonyesha uharamu wa tabia zinazolalamikiwa. Sayansi, metafizikia, sosiolojia, seskolojia, uchumi, politolojia, mahesabu na taaluma nyingine zinayo nafasi kubwa hapa.

Lakini, Maaskofu Katoliki hawajajipambanua vizuri. Ni kama wanabaki kuwa watumwa wa “maagizo kutoka juu” badala ya kujishughulisha kifikra na kusema kitu kinachoeleweka. Wanapaswa kupiga hatua ya ziada kitaaluma.

10. Waraka umeshindwa kueleza kinaganaga tofauti kati ya hulka iliyo ya kibinadamu na hulka isiyo ya kibinadamu

Waraka (2019) umejenga hoja ifuatayo dhidi ya tabia "iliyopotoka kihulka," yaani, tabia iliyo kinyume cha maumbile ya binadamu:

  • Kwa mujibu maadili asilia yanayotokana na "hulka ya binadamu"inayotambuliwa na Biblia ni kosa kila wakati, kila mahali na kwa kila mtu kujihusisha na tabia "iliyopotoka kihulka" (1).
  • Mwenendo X ni tabia "iliyopotoka kihulka"(2);
  • Kwa hiyo, kutokana na (1) na (2), mwenendo X ni haramu kimaadili(3).
Hoja hii inakwama kwa sababu ya dokezo la kwanza kubeba maneno "hulka ya binadamu" yenye maana zaidi ya moja, kama tutakavyoonyesha baadaye.

Lakini, hoja haiwezi kuhakikiwa kikamilifu mpaka pale "mwenendo X" unapokuwa umefahamika kwa uhakika. Waraka (2019) umetaja mienendo ipatayo 25 na kuutambulisha kila mmoja kama tabia "iliyopotoka kihulka."

Katika orodha hiyo, kila tabia inafungamana na mbetuko asilia ulio sehemu ya binadamu. Kwa mfano, kuna wanawake ni androphilic wakati wengine androphobic, kuna wanaume ni gynophilic wakati wengine ni gynophobic, baadhi ya watu ni gamophilic wakati wengine gamophobic. Kwa hiyo, hoja ya kimaadili lazima ieleze ni “hulka” ipi inaongelewa na kwa nini.

11. Waraka unatumia sababu zinazoyumba kutetea dhana kwamba ngono ya wagumba inaisababishia hasara jamii kwa kuwa inapunguza fursa za ongezeko la watu duniani

Kuna hoja inasema kwamba, kutumia kingamimba ndani ya ndoa ni kitendo kinachosababisha maumivu kwa jamii, kwa sababu kinapunguza fursa za ongezeko la watu.

Hoja hii inakumbana na mifano kanushi kadhaa. Kwa mfano, useja wa mapadre unapunguza fursa za kuongezeka kwa idadi ya watu katika jamii. Lakini, hakuna anayesema kwamba, uamuzi wa kuwa padre ni uamuzi haramu kimaadili.

Kwa ujumla, ukweli kwamba, jamii inahitaji ongezeko la watu kwa njia ya kuzaana, haumaanishi hitimisho la kimantiki kwamba, kila mwanajamii anapaswa kuzaa watoto. Pia, ukweli kwamba, jamii inahitaji ongezeko la watu kwa njia ya kuzaliana, haumaanishi hitimisho la kimantiki kwamba, kila tendo la ngono lazima lifanyike bila kutumia kingamimba. Aidha, ukweli kwamba kuzaa watoto ni jambo zuri, haumaanishi hitimisho la kimantiki kwamba ugumba ni jambo baya kimaadili.

Kwa hiyo, ukweli kwamba, uamuzi wa mtu unapunguza fursa za ongezeko la watu ni ushahidi usiotosha katika kuthibitisha uharamu wa kimaadili katika maamuzi na matendo husika. Hivyo, pingamizi linakufa.

12. Waraka unatumia mbinu za kimachiaveli kuwaziba midomo wakosoaji wa hoja za Kanisa kama alivyokuwa anafanya Papa Gregory wa karne ya 13

Waraka (2019) unatumia kanuni ya Umachiaveli kufanya kazi ya uenjilishaji. Umachiaveli huu umejitokeza katika sura tatu. Umachiaveli wa kwanza ni kutumia maneno yenye maana tofauti ndani ya hoja moja (deception by equivocation). Kwa mfano, tuangalie tena kwa kina maneno yaliyo katika aya ya 12 ya Humanae Vitae (1968).

Katika aya hii ninahitaji tuagalie zaidi mafungu ya maneno haya: "unitive significance," "procreative significance," "unitive ... and the procreative ... qualities," na "the the fundamental nature of the marriage act [is] ... uniting husband and wife in the closest intimacy..."

Mafungu haya manne yanabebwa na neno "unitive." Lakini, neno hili halina maana moja. Tuangalie ushahidi wa Kamusi za Kiingereza.

Kwa mujibu wa "American Heritage Dictionary of the English Language (2016)," neno “unitive” ni kivumishi kinachomaanisha “serving to unite” au “tending to promote unity.”

Kulingana na "The Collins English Dictionary (2014)," neno “unitive” ni kivumishi kinachomaanisha “tending to unite,” “capable of uniting” au “characterized by unity.”

Na kwa kutumia "The Random House Kernerman Webster's College Dictionary (2010)," tunaona kuwa neno “unitive” ni kivumishi kinachomaanisha “capable of causing unity,” “serving to unite,” “marked by union,” au “involving union.”

Hivyo, neno "unitive" ni kivumishi kilicho na mnsaba na nomino ya "unity," ambayo ni kisawe cha nomino "union." Maneno "unity" na "union" ni visawe vya neno "umoja" kwa Kiswahili. Na hapa tunaongela "umoja wa jozi ya watianaji," yaani, "the unity of a copulating pair."

Hii ni jozi ya miili miwili au magimba mawili (two bodies) yaliyoungana na kutengeneza "kitu kikubwa kimoja ambacho ni muungano wa vitu vidogo viwili" kupitia tendo la ngono.

Vitu viwili ni vitu vingi. Hivyo, tunaongelea dhana ambayo wanametafizikia huitaja kama "the unity of a compound substance," yaani "umoja wa kitu kikubwa kimoja ambacho ni muungano wa vitu vidogo vingi ."

Katika metafizikia, neno "unity" linaweza kumaanisha viti tofauti kama likitanguliwa na vinyumbulisho (qualifiers) kama vile spatial, temporal, diachronic, synchronic, behavioral, integrative, cohesive, meriological, semiotic, causal, bodily, organic , mechanical, chemical, physical, intentional, psychological, physiological, teleological, teleonomic, teleomatic, coital, sexual, mathematical, social, political, economic, contraceptive, orgasmic, heterophilic, homophilic, pedicative, fellatiative, axillary, masturbatory.

Metafizikia ya "kitendawili cha umoja na wingi" inayo mengi ya kusema kuhusu jambo hili. Naongelea "the problem of one and many" au "the problem of unity and multiplicity" au "the problem of unity and diversity" au "the problem of singularity and plurarity" (Mayr 1974, Wilson 1999, Hoffman na Rosenkrantz 1997, Meirav 2003, Qingyun 2015).

Matini ya Theology 101 katika seminari kuu katoliki (Grisez 1983:
http://twotlj.org/G-2-9-E.html) yanaongelea “the part-whole relationship between the marital act’s two meanings.” Maneno haya ni ushahidi kuwa ibara tata ya 12 katika Humanae Vitae (1968) inaongelea “copulating pair” kama "organic meriological unity” hata kama "jozi ya watianaji" ni wagumba. Hapa waseminari wetu wanajingishwa kwa kulishwa sumu ya ukoloni wa kimawazo (colonization of the mind).

Umachiaveli wa pili, ni kutumia maneno yanayosema ukweli nusu nusu ili kuizuga akili ya hadhira (deception by omission). Mifano ni mafungu ya maneno kama vile: Kusema "sex is unitive" badala ya "[penovaginal] sex is [sometimes] untive," "sex is procreative" badala ya "[penovaginal] sex is [sometimes] procreative," "sex is parental" badala ya "[penovaginal] sex is [sometimes] parental," na "sex is marital" badala ya "[penovaginal] sex is [sometimes] marital."

Hata ayabya 12 katika Humanae Vitae inashabikia umachiaveli huu kama ifuatavyo: "the marriage act, while uniting husband and wife in the closest intimacy, also renders them capable of [sometimes] generating new life (Humanae Vitae 12)."


Na Umachiaveli wa tatu ni kumshambulia mleta hoja badala ya kujielekeza kwenye kujibu hoja. Ni kama ambavyo Kanisa Katoliki la Karne ya 13 chini ya Papa Gregory lilivyokuwa linafanya.

Kumshambulia mleta hoja badala ya kujibu hoja ni Umachiaveli, ambao kimsingi inapaswa kupingwa na Mt. Paulo (War. 3:8)."

Kwa mfano, nimeona mahali fulani Waraka (2019) unatuhumu watu kutumia “pesa nyingi" kupotosha maadili ya jamii kwa kujaribu kugeuza uovu kuwa tunu. Hawakutoa ushahidi wowote wa fedha hizo.

Huu ni utekelezaji wa mkakati huu: "kama mtu anahimiza matumizi ya kondomu basi tumwondolee mwanga wa uadilifu mbele ya jamii kwa kumtuhumu kuwa anaunga mkono ngono iliyo kinyume cha maumbile ya uzazi (“unnatural sex”), jambo ambalo ni sawa na kuhimiza mapenzi ya kishoga."

Hata hivyo, sio madai ya kweli kusema kwamba, kuhimiza matumizi ya kondomu au kingamimba baki ni sawa na kuhimiza ushoga.

Lakini, utekelezaji wa mkakati huu wa Kimachiaveli sio mkakati wa jana wala juzi.

Katika karne ya 13, Papa Gregory aliteua shirika moja la Mapadre kufanya kazi kama Idara ya Usalama wa Taifa la Roma. Kazi yao kuu ilikuwa kuwawinda wakosoaji wa Papa na kuwarudisha kwa Mungu au kuwamaliza.

Mkakati wa kuwamaliza ulikuwa ni huu: "kama mtu anampinga Papa basi tumwondolee mwanga wa uadilifu mbele ya jamii kwa kumfungulia kesi ya kufanya ngono kinyume cha maumbile (“unnatural sex”)."

Utekelezaji uliendelea kwa muda mrefu. Ilipofika mwaka 1432, kikosi cha makachero wa Kipapa, kikaanza kazi ya kusimika visanduku maalum vilivyoitwa “tamburi” mitaani na kuwataka wananchi wawataje watuhumiwa wa ushoga na uhaini dhidi ya Papa (Conrad and Schneider 1992:172ff).

Operesheni hii ilitekelezwa zaidi katika miji ya Florence na Venice, ambako zilijengwa “mahakama za kuwashughuikia watuhumiwa wa mapenzi ya kishoga (“sodomy courts”).

Uliitwa mkakati wa “kuitakasa miji kwa kufagia mashoga” wote, yaani “purging the city of sodomy.” Uhomofobia ukaota mizizi ndani ya jamii kupitia mikono ya Kanisa Katoliki.

Ni kama ilivyokuwa kule Mkoani Dar es Salaam mwaka jana. Unaweza kudhani Kanisa Katoliki lilikuwa nyuma ya zile operesheni za serikali ya mkoa chini ya Mhe. Paul Makonda.

Kwa ujumla, katika kipindi cha miaka 70, kila mwezi watu waliokuwa wanatuhumiwa kwa “ushoga” kupitia "tamburi" ni maelfu!

Kesi hizi zilisikilizwa kwa haraka na watuhumiwa kutiwa hatiani kwa kutumia mashahidi wa kutumwa. Mifano hai ya kesi za kubumba namna hii zikiwa zinaendeshwa na Serikali ya Italia kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki ipo.

Mfano mmoja ni kesi ya tuhuma za kishoga iliyomhusu kiongozi mkuu, “the Grand Master," wa Shirika la Kitawa lililotwa “the Knights Templars," aliyeitwa Jacques de Molay. Alituhumiwa kwa ushahidi hafifu na akauwawa kwa kuchomwa moto hadharani mwaka 1314.

Na mfano mwingine ni kesi iliyomhusu Leonardo da Vinci, yule mwamamahesabu na mchoraji maarufu wa michoro mizuri kama ule wa Mona Lisa aliouandaa kama tafsiri yake ya aya za Mwanzo 1:27; 2:21 na 2:24. Makuhani hawakupenda tafsiri hiyo.

Hivyo, mwaka 1476 Leonardo alitungiwa kesi ya kubumba kwa kutuhumiwa kufanya mapenzi ya kishoga, akahukumiwa na kufungwa miezi 2, lakini baadaye watu wakamtetea na akaachiwa huru.

Umachiaveli uliokuwa unatekelezwa na Kanisa Katoliki enzi hizo huko Italia umeanza kutekelezwa hapa Tanzania tangu miaka ya karibuni, hasa tangu Askofu Methodius Kilaini akiwa Askofu Msaidizi huko Dar es Salaam.

Na sasa Waraka wa Kwarezima Kutika Kurasini (2019) unaendeleza mkakati huu ulio haramu kimaadili na kisheria.

Hivyo, naona kuwa waraka huu ni mwendelezo wa Umachiavelli hatari ndani ya Kanisa Katoliki, kama ilivyokuwa inafanyika tangu Karne ya 13. Tabia hii haikubaliki katika milenia ya tatu.

13. Hitimisho

Kwa kuhitimisha nasisitiza dosari zifuatazo katika Waraka (2019) :

Mosi, Waraka umeshindwa kutoa fasili ya neno "ndoa" iliyo yakinifu na yenye kutosheleza aina zote za ndoa. Ndoa kati ya watianaji walio wagumba ni jumuiya iliyo katika kategoria tofauti na ndoa ya jozi ya watianaji wasio wagumba.

Pili, Waraka unapotosha umma kwa kuufanya uamini kwamba "theluthi ya ukweli" ni sawa na "ukweli wote" kadiri suala la "hulka ya kijinsia ya binadamu" inavyohusika. Mibetuko ya kijinsia ni zaidi ya uheterofilia. Kuna uhomofilia na uambifilia.

Tatu, Waraka unapotosha umma kwa kuufanya uamini kwamba "kutenganishwa kwa ndoa na familia" ni kosa mara zote, kila mahali na kwa kila mtu. Kuna mifano mingi inayokanusha tamko hili, mfano muhimu ukiwa mtindo wa maisha ya useja waliouchagua Mapadre na Maaskofu Katoliki.

Nne, Waraka umeandikwa chini ya msukumo wa hulka ya Kimachiaveli. Kwa sehemu fulani, umeandikwa kwa ajili ya kushambulia wakosoaji wa hoja za Kanisa Katoliki badala ya kujibu hoja zao. Pia unatumia kanuni za utapeli wa kifalsafa (sophism) kama mbinu ya uenjilishaji.

Na tano, Waraka umeshindwa kuchota busara kutoka visima vyote vitano vya maarifa ya Kimungu. Yaani, Misahafu, Mapokeo, Uzoefu, Urazini wa Kisayansi na Urazini waKifalsafa (Scriptures, Tradition, Experience, Scientific Reason and Philophical Reason). Waraka umeyasahau haya matatu ya mwisho.

14. Mapendekezo kwa Vigogo wa Kurasini na wadau baki

Kutokana na yote yaliyosemwa hapo juu, napendekeza kwamba yafuatayo yafanyike katika Tanzania ya milenia ya tatu:

MOSI, Sheria ya Ndoa (1971) irekebishwe kwa kuongeza kifungu kifuatacho:

“(1) Subject to section (2) below, a marriage may be solemnized between any man and any woman, if neither party has a spouse living at the time of the marriage.

(2) Section one shall not apply to couples who have been medically proved to be permanently infertile , if they are willing to engage in polygamous marriage for reasons of bearing and rearing children in order to preserve their lineage, and if they have secured permission from the Head of the State or his duly appointed representatives in local government authorities."


PILI
, Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Marekebisho ya 2002) irekebishwe kwa kuongeza kifungu kifuatacho:

“Every person having a husband or wife living, who shall marry any other person, whether married or single, in a territory over which the United Republic of Tanzania has exclusive jurisdiction is guilty of an offense called polygamy and shall be punished by imprisonment for a term not less than 30 years or by a fine not less than 30 million Tanzanian shillings.”

TATU
, Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Marekebisho ya 2002) irekebishwe kwa kuongeza kifungu kifuatacho:

Crime against the sanctity of marriage :

(1) Any person who seduces, overpowers, and subsequently engages, insexual intercourse with another person who is and whom he knows or has reason to believe to be married to the third person, without the consent or connivance of that third person, and where such sexual intercourse does not amount to the offence of rape, is guilty of the offense of adultery, and shall be punished with imprisonment for a term which is not less than 30 years, or a fine not less than TZS 50 Million, or both.

(2) In such a case the seduced person shall not be punishable, and no person other than the husband or wife of the seduced person shall be deemed to be aggrieved by any offense punishable under this section.


NNE,
Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Marekebisho ya 2002) irekebishwe kwa kuongeza kifungu kifuatacho:

Crime of causing birth out of wedlock:

(1) Any person who seduces, overpowers, and subsequently engages, in sexual intercourse with another person who is not one's marriage partner, and ultimately causes the birth of a child out of wedlock, is guilty of the offense of causing birth out of wedlock, and shall be punished with imprisonment for a term which is not less than 30 years, or a fine not less than TZS 50 Million, or both.

(2) In such a case the seduced person shall not be punishable, and no person other than the parents or blood relatives of the woman shall be deemed to be aggrieved by any offense punishable under this section.


TANO,
Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Marekebisho ya 2002) irekebishwe kwa kuongeza kifungu kifuatacho:

“154A. Mwanamume yeyote atakayefanya ngono iliyo kinyume cha maumbile pamoja na mwanamume mwingine hatakuwa na hatia kisheria, endapo, wote wawili ni watu wazima, wameridhiana, kitendo hicho kimefanyika kwenye faragha, sio kitendo cha kibiashara, wote wawili ni watu ambao wamo katika kundi la watu wenye ujinsia haba (sexual minorities), na hadhi zao za kijinsia zinatambuliwa na mamlaka kama vila wazazi, matabibu, watalam wa ustawi wa jamii, RITA au mamlaka nyingine kama hizo.”

SITA
, Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Marekebisho ya 2002) irekebishwe kwa kuongeza kifungu kifuatacho:

“154B. Mwanamume yeyote atakayefanya ngono iliyo kinyume cha maumbile pamoja na mwanamke yeyote hatakuwa na hatia kisheria, endapo, wote wawili ni watu wazima, wameridhiana, kitendo hicho kimefanyika kwenye faragha, na sio kitendo cha kibiashara.”

SABA,
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wanataaluma Wakristo wa Tanzania (CPT), Profesa Josaphat Kanywanyi, anapaswa kuhakikisha kuwa CPT wanaanzisha mijadala ya kitaaluma kuhusu swali "kiumbehai ni kitu gani na sio kitu gani?" ili kwa njia hiyo CPT waweze kutoa mchango wake wa kitaaluma kwa Kanisa la Tanzania na nje ya Tanzania.

Wana CPT ambao ni wanakemia, wanafizikia, wanabayolojia pamoja na wanafalsafa wa bayolojia ndio wenye jukumu hasa katika kujibu swali hili kupitia midahalo ya kitaaluma.

Kazi ya Walei walioko CPT ni kulisaidia Kanisa kwenda na wakati kwa kuzingatia ukweli wa kirazini kulingana na taaluma zao. Na kuhusu swali "kiumbehai ni kitu gani na sio kitu gani?" napenda kusisitiza wito wangu kwa kutumia marejeo yafuatayo:

"Cleland, C. & Chyba, C. (2007). Does ‘life’ have a definition?. Printed In W. T. Sullivan & J. A. Baross (Eds.), Planets and life (Cambridge: Cambridge University Press;2007, p.119-131)."

NANE,
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, afanye haraka sana kupiga marufuku matini yanayotumika katika seminari kuu kwenye somo la "Theology 101," na hasa yale yanayopatikana hapa www.twotlj.org, kwa sababu baadhi yake yanakiuka kanuni ya ukweli pale yanaposema kuwa "kila jozi ya watianaji wagumba hugeuka mwili mmoja wakati wa kujamiiana kama ambavyo kila jozi ya watianaji wenye rutuba ya uzazi hugeuka mwili wakati wa kujamiiana."

Kuendeleza mafundisho haya ni kuwajingisha waseminari na kuendeleza ukoloni wa mawazo yaliyo potofu kisayansi na kifalsafa ulimwenguni hasa pasipo sababu za msingi. Muda wa ukoloni wa aina hii mepita.

TISA, Mkuu wa Idara ya usalama wa Taifa, Dk Kapilimba, anapaswa kuchukua hatua za haraka kuboresha mitaala yake ili kuwawezesha Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kupata uelewa wa msingi kuhusu ujinsia wa binadamu (sexology), na hasa ujinsia wa binadamu wenye maumbile tata (sexual minorities).

Nimefuatilia mienendo ya ma-TISS kadhaa na kujiridhisha kwamba hawana weledi wa kutosha katika eneo hili. Pia, wengi wanasumbuliwa na homophobia.

Kwa sababu hii wanakuwa watu wa kupayuka hata siri za kiofisi kwenye baa na kila mahali. Hatimaye wanawachafua watu wanaowafuatilia hata kabla ya kupata ushahidi wa kuthibitisha tuhuma walizo nazo.

Katika hili la pili, ma-TISS wanakiuka misingi ya "ukachero." Huwezi kumchunguza mtu kwa siri kama mtu huyo tayari anajua kwamba unamchunguza kwa siri. Kanuni ya kwanza ya ukachero ni hii: "out-think your target." Yaani, "mtu unayemchunguza anapaswa asijue unachofikiri juu yake." Hii ni kanuni ya jumla katika kazi za upelelezi hata kama tukiwaweka kando ma-TISS.

Kuhusu suala la ujinsia tata, ma-TISS wengi niliowafuatilia wanakiuka kanuni hii kwa sababu ya mihemuko na kiwewe kinachotokana na maarifa haba ya taluma ya ujinsia. Kazi kwako Dk. Kapilimba.

NA KUMI, napendekeza kwamba, wanateolojia Katoliki, popote walipo duniani, wanapaswa kutafakari kwa makini maneno ya Dr. Lonergan, na kisha kujiepusha kabisa na magonjwa ya "scotoma" na "scotosis" kila mara wanapojadili nafasi ya ujinsia wa binadamu katika maisha ya watu.

1559049156271.png


Kwa ukamilifu wa hoja ya Lonergan, rejea: Frederick E. Crowe & Robert M. Doran (Editors), Collected Works of Bernard Lonergan, Volume 3, Insight: A Study of Human Understanding, 5th Edition, (London: Longmans, Green and Co.;1957/2005, p.215-27)

Kwa marejeo ya jumla angalia KIAMBATANISHO C (kimerekebishwa 15 Juni 2019).

Wenu katika ujenzi wa Imani ya Jamii ya Taifa,

Mama Amon,
Rais wa Baraza la Maaskofu Walei Tanzania,

BAMAWATA.
 

Attachments

  • KIAMBATANISHO A--CHIBUKO LA MBETUKO WA KIJINSIA NI MALEZI AU MAUMBILE.docx
    26.9 KB · Views: 45
  • KIAMBATANISHO B--KIUMBEHAI KINA SIFA ZIPI NA VITU GANI VYENYE SIFA YA KUITWA VIUMVE HAI.doc
    47.5 KB · Views: 37
  • KIAMBATANISHO D--FASILI YA MISAMIATI MUHIMU.docx
    42.2 KB · Views: 35
  • Kiambatanisho F, Tathmini ya hoja dhidi ya ndoa za jinsia moja.docx
    17.3 KB · Views: 27
  • KIAMBATANISHO G-- HOJA KUHUSU NGONO ILIYO KINYUME CHA MAUMBILE.docx
    19.8 KB · Views: 25
  • Maaskofu Katoliki Tanzania--Ujumbe wa Kwaresima 2019--Vatican Website.docx
    64.9 KB · Views: 30
  • APPENDIX H--A CASE STUDY ABOUT AFRICAN PROBLEMS.docx
    18.6 KB · Views: 20
  • 1554453938950.png
    1554453938950.png
    222.1 KB · Views: 91
  • 1554454257922.png
    1554454257922.png
    163.6 KB · Views: 98
  • 1554454501784.png
    1554454501784.png
    47 KB · Views: 84
  • 1554802375982.png
    1554802375982.png
    101.4 KB · Views: 78
  • 1554802910005.png
    1554802910005.png
    81.2 KB · Views: 84
  • family photo.png
    family photo.png
    374 KB · Views: 100
  • wedding couple.png
    wedding couple.png
    186.2 KB · Views: 85
  • 1554903335437.png
    1554903335437.png
    110.9 KB · Views: 106
  • KIAMBATANISHO J--HOJA KUHUSU MATUMIZI YA KINGAMIMBA.doc
    326.5 KB · Views: 10
  • KIAMBATANISHO C--MAREJEO MUHIMU.doc
    58.5 KB · Views: 10
Kwa mara ya kwanza TEC wamenigusa kwa kufanya kazi ambayo wanatakiwa kufanya. Walichoandika ndio jukumu la kwanza la kazi ya uchungaji ambayo Mwenyezi Mungu amewakabidhi.
Waumini naomba wachukulie serious waraka huu. Sio wa kisiasa. Ni wa kiroho zaidi
 
Kwa mara ya kwanza TEC wamenigusa kwa kufanya kazi ambayo wanatakiwa kufanya. Walichoandika ndio jukumu la kwanza la kazi ya uchungaji ambayo Mwenyezi Mungu amewakabidhi.
Waumini naomba wachukulie serious waraka huu. Sio wa kisiasa. Ni wa kiroho zaidi
Ooohooo wamekugusa sehemu gani mkuu? Vp baada ya kuguswa ume feel aje? By the way wewe in Me au KE?
 
Binadamu hawezi kutenganishwa na siasa. Siasa ni maisha. Au wewe ulitaka siasa zipi mkuu?

Kitu chochote kinachohusu kushawishi watu ni siasa. Ukisoma vizuri hapo, mwanzo mwisho kuna siasa.

Otherwise, haujausoma.
 
Binadamu hawezi kutenganishwa na siasa. Siasa ni maisha. Au wewe ulitaka siasa zipi mkuu?

Kitu chochote kinachohusu kushawishi watu ni siasa. Ukisoma vizuri hapo, mwanzo mwisho kuna siasa.

Otherwise, haujausoma.
Moral values will make good politicians. Imagine it the church takes the front seat. Who is going to do balance and check?
The most important work of the church is to mold the believers to the standards that are acceptable to all. Short of that is a disastrous approach
 
=========WARAKA KAMILI HUU HAPA===

Tazama Kiambatanisho

Vyanzo husika:

  • Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kiongozi, 12(2019): 12-13.
  • Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kiongozi, 13(2019):12-13.
  • www.vatican.va
 

Attachments

  • Ujumbe wa Maaskofu Katoliki TanzaniaKwa Ajili ya Kwaresima 2019.pdf
    576.9 KB · Views: 25
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom