babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,019
- 17,664
Leo ni siku ya ukimwi duniani na kama kijana ambaye pia niko katika kundi ambalo liko hatarini kwenye maambukizo ya gonjwa hili hatari, naona ni busara kugusia na kutoa hamasa kupitia jumbe mbalimbali zinazotolewa duniani kuhusiana na gonjwa hili. Kutoa utambuzi zaidi na kujumuika pamoja na vijana wenzangu kutafuta na kufuata njia mbalimbali za kuzuia maambukizo zaidi ya huu ugonjwa. Tukijuimika na rais kusema Tanzania bila ukimwa inawezekana kwa sasa na hata vizazi vijavyo.
Ripoti ya mjumuiko kutoka shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na gonjwa hili yaani UNAIDS linaonyesha kwamba maambukizo yanapungua hasa katika kundi la vijana kati ya miaka 15-24. Na katika nchi kumi na tano zilizoathirika zaidi na gonjwa hili maambukizo yamepungua kwa asilimia 25. Hili linachangiwa na kuongezeka kwa matumizi ya kondomu, kuchelewa kujihusisha na mahusiano ya kuingiliana kimwili na mabadiliko ya tabia.
Kutokana na hili kama vijana tunajifunza mambo mawili muhimu. Kwanza, kuwa haya maambukizo bado yapo na yana hatarisha maendeleo ya makundi mballimbali katika jamii na hasa kundi la vijana. Pili, kuna njia ya kupambana na ugonjwa huu kwa kuutokomeza au kuuzia kwa njia mbalimbali. Kama vijana ni muhimu kutambua nafasi yetu katika jamii tukiwa ni chachu ya maendeleo, hivyo inatupasa kuchukua hatua mbalimbali za kulindi afya zetu ili tuweze kuwa tegemezi thabiti. Tujue hali zetu kiafya, kama tuna maambukizi tufuate maelekezo ambayo yatatuwezehsa kuzuia maambukizo zaidi na kuishi miaka mingi zaidi. Na kwa vijana ambao hawajaathirika wachukue hatua mbalimbali za kujilinda wao na wapenzi wao kwa wale walio katika mahusiano na wale ambao bado hawako katika mahusiano wajue afya zao kabla ya kujiingiza na hata wakijiingiza waweze kuchukua hatua mbalimbali za kujilinda.
Kwa ufupi, ujumbe wangu leo kwenu ni kujitambua na kufanya maamuzi sahihi na kuwajibika katika maisha yenu, pata taarifa sahihi na chukua hatua kuyalinda maisha yenu ili tuweze kulitumikia taifa letu kwa nguvu na akili zetu zote.
I'm Hasheem Thabeet and I Approve this Message...
toka:bongostarlink