Ujumbe ukufikie....

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,335
1,778
Burudani ni sehemu kubwa ya maisha yangu napenda music kwa kiwango kikubwa sana na nafuatilia music kwa kiwango kikubwa sana sababu music ni faraja ya maisha yangu .Bongo flava siipendi sababu sababu imejaa wana music wengi wenye tungo nyepesi zisizo na tija wala mashiko .ila kuna wana music wa bongo flava wananifanya nisikilize Bongo flava.

Namsikiliza Ben Paul na wimbo wake Moyo Mashine ni tungo nzuri sana yenye ujumbe mzuri na imeimbwa kwa lugha rafiki na lahaja nzuri sana ,Ben Paul amekosa bahati katika tasnia ya music wa Bongo Flava ijapokuwa ana karama nzuri sana ya kuimba ,sababu wanamusic wengi wenye pesa na majina makubwa Tanzania hawana ubora wake wa Tungo zake.

Ni kazi rahisi sana kuichukia Bongo flava ila ni vigumu sana kuchukia Tungo za Bongo flava sababu Ben Paul anaweza kukufanya uwe na siku nzuri,Fid Q akukufanya upende Bongo HipHop ,G Nako Wara Wara daima hutizendea haki chorus zote ambazo ameziimba .When you are happy, you enjoy the music. But, when you are sad you understand the lyrics.#BongoFlava
 
Ni vizuri kuona washabiki pia tunawasaidia kusambaza nyimbo zao.

Mimi siufahamu, nifafurahi ukiuuweka humu niusikilize.
 
Wewe ndo hujui...wimbo huo mtunzi ni goodluck gozbert but benpol kautendea haki sana na pia hata nyimbo nyingine zote za benpol ni nzuri na zibabeba ujumbe mpana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom