Ujumbe toka kwa Dr. Slaa

Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,323
67
Ndugu Mtanzania Mzalendo,

Lengo la nyaraka hii ni kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu hoja mbalimbalizilizojitokeza kutokana na 'Hoja yangu ya Kuundwa kwa Kamati Teule yaBunge', kuchunguza matumizi mabaya fedha za umma, uwezekano wa uwepo waubadhirifu, uwizi na ufisadi mkubwa ndani ya BOT ambacho ni kioo chauchumi wa nchi yetu, kama ilivyo kwa Benki kuu yeyote duniani.

Katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Jangani tarehe 18 August, 2007 nilitoahadi tarehe 15 Septemba kwa Serikali kuchukua hatua mahususi dhidi yawahusika. Nilitoa tarehe hiyo makusudi. Leo nina nia ya kutoa ufafanuziwa kina zaidi, katika maeneo machache tu katika Tuhuma hizo ili Watanzania walio wengi waelewe hasa ni nini kilichonisababisha kudaikuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge.

1. Utangulizi:

Kwa kifupi nilitoa Tuhuma nzito dhidi ya BOT na watendaji wake wakuundani ya Bunge letu Tukufu, tarehe 25 June, 2007 wakati wa mjadala waHotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu. Jioni hiyo hiyo, wakati wa mafungu kwamujibu wa Kanuni ya Bunge ya 104(1)(2) nikatoa Taarifa ya nia yangu yakuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge.

Tarehe 26 June, 2007 kwa mujibu wa Kanuni hiyo nikawasilisha kwa Katibuwa Bunge Barua yangu ya Taarifa ya nia hiyo kwa mujibu wa Matakwa yaKifungu cha 104(2) ya Kanuni iliyotajwa.

Tarehe 8 Julai, baada yautafiti wa kina, nikawasilisha kwa Katibu wa Bunge 'Maelezo yangu yaHoja ya Kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge'.

Tarehe 13 August, 2007,mchana nikapokea Barua kutoka kwa Mhe. Spika, yenye Kumb.naCA.150/277/01/07 ikinitaka niwasilishe 'vielelezo halisi' ili yeye'akiridhika' apange muda wa Hoja yangu kuingia Bungeni. Jioni hiyo hiyoya tarehe 13 Agosti, 2007 nikawasilisha kwa barua rasmi vielelezo vyote,vikiwa katika Volumes (lV). Barua yangu iliorodhesha Vielelezo (a) to(s).

Tarehe 15 Asubuhi, raia mwema, kutoka Usalama wa Taifa, akanileteawaraka wa kuaminika kuaminika kutoka ndani ya Idara hiyo.

Ushauri uliotolewa baada ya kuchambua mambo mbalimbali unasomeka ifuatavyo:-

"Taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya benki Kuu ilipaswa kuwa siri nahaijulikani ni vipi imeweza kuvuja na kuwafikia wapinzani. Suala hililikifikishwa bungeni linaweza kuwa na athari mbaya kwa serikali, hasakwa kuzingatia kuwa ni vigumu kupata majibu ya hoja hizi za CAG yanayotosheleza.

Ni vema Waziri Mkuu ajulishwe ili itafutwe njia yakuzuia hoja hii kuwasilishwa Bungeni. Idara inaendelea kuchunguza chanzocha uvujaji wa taarifa hiyo" Nilitafakari sana hoja hii. Katika akili ya kawaida, ilionenakanataarifa hii ni ya kweli. Mazingira yaliyojitokeza tarehe 13 Agosti,ambapo Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM, ikiwa ni wajumbe wote waKamati Kuu ya CCM walioko Bungeni, akiwemo na Spika ilikaa toka saa 5hadi saa nane kwenye ukumbi wa Spika.

Taarifa inayoaminika inasema kuwa ajenda kuu ilikuwa hoja ya Mhe. Zitto Kabwe, na Hoja ya Dr. Slaa, zotezikitaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge. Kuhusu Hoja yangu"Maelekezo" mawili inaelekea yaliyotolewa na kikao hicho. Moja ni Spikakuniandikia na kudai apetiwe 'vielelezo Halisi' ili ajiridhishe yeyekabla ya hoja kuingia Bungeni, na pili, Hoja hiyo isipangiwe katikaShughuli za Bunge (Order Paper) katika Mkutano huu yaani Mkutano wa Nanewa Bunge.

Hapo nikajiridhisha kuwa ushauri aliopelekewa Waziri Mkuu ndiounatekelezwa. Na hivyo, nikajua kuwa i)Hoja haitaingizwa Bungeni safarihii, ina inawezekana isipangiwe kabisa hata kikao kijacho,ii) Ucheleweshaji wowote, unaweza kuathiri uchunguzi unaotakiwa, kwanikatika Tuhuma yeyote, hatua za haraka ni muhimu ili kusiwe na nafasiyeyote ya kuingilia uchunguzi.

Kwa vile tuhuma ni nyingi sana, kwa leo naomba niwape mwanga kwenyemaeneo machache tu kama ifuatavyo: 2: TUHUMA ZA MSINGI ZA UBADHIRIFU NDANI YA BOT:

1: BENKI KUU KULIPA DENI LA MERREMETA CO.LTD LA TSHS Bilioni 155 KINYUMENAUTARATIBU:Hapa kuna mambo ya msingi kadhaa Watanzania wanatakiwa kufahamishwa.Kwa muda wa kama miaka mine sasa Wabunge wa Kambi ya Upinzani tumeihojiSerikali ituelezea) Meremeta Co.Ltd. ni mali ya nani na imeandikishwa wapi?b) Mahesabu ya Kampuni hii yanatolewa kwananic) Tanzania inafaidika nini kutokana na Kampuni hii ambayo ilikabidhiwaMgodi wa dhahabu wa Buhemba, Mkoani Mara.

Miaka yote, pamoja na kuhoji Serikali ilishindwa kutoa majibu yakuridhisha, licha ya kusema tu Meremeta ni Kampuni ya Serikali, nainaendeshwa na JWTZ, kwa lengo la kuisaidia kikosi chetu cha NYUMBU.Majibu haya yako kwenye Hansard. Maswali mengine yote hayakujibiwa.Mwaka jana, baada ya kuibana Serikali ilikiri kuwa Kampuni hii ikokwenye hatua ya 'Kufilisiwa'(Liquidation") Majibu haya ya Serikaliyalileta mashaka makubwa sana. Ndipo ilipokuja nia ya kuundwa kwa KamatiTeule kupata ukweli na majibu sahihi ya masuali hayo. Sasa basi Utafitiwangu umeonyesha nini:

a) Meremeta Co.Ltd, tuliyoambiwa ni Kampuni ya Serikali, iliandikishwanchini Uingereza kama 'Offshore Co.' kwa hati ya Usajili na 3424504 kamaPrivate Ltd Co., iliyotolewa London, na Ofisi ya Msajili wa Makampuni,Tarehe 19 August, 1997. Tarehe 3 Oktoba, 1997 Kampuni hiyo ikapata 'Hatiya Kutimiza Masharti' yaani 'Certificate of Compliance Na 32755. utafitihuu unaonyesha kuwa Tanzania inazo hisa 50% katika Kampuni hiyo na Sharemwingine ni Kampuni ya Afrika ya Kusini inayoitwa Triennex Co.Ltd nayoyenye hisa 50%. Uchunguzi wa ziada unaonyesha Kampuni 2 zaidi zina hisamoja moja nazo ni London Law Society Ltd (Hisa 1) na London LawSecretarial Service Ltd yenye hisa moja. Hapa kuna utata mkubwa.

Meremeta ni ya nani? Meremeta ina hisa ngapi? Kama Meremetaimeandikishwa kama Kampuni ya Kigeni Tanzania ni kwanini imepewa fedhaza Walipa kodi wa Tanzania? Na Iwapo Tanzania siyo peke yake yenyekatika umiliki wake, ni kwanini wakati wa ufilisi wake Benki Kuu yaTanzania kwa niaba ya Serikali yaTanzania ililipa Deni lote la Tshs 155,Billioni, ambazo zilibadilishwa na kuwa Dola za Marekani118,396460.36 na kuzipeleka kwenye akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltdya Afrika ya Kusini kupitia Benki ya HSB ya New York.Zingine13,736,628.73 zililipwa Kampuni ya Tangold (nayo tutaieleza baadayekidogo) kwenye akaunti yake iliyoko Corporate Branch Dar-Es-Salaam.

Hoja hizi zilihitaji Kamati Teule kupata ufafanuzi wa Kina. Kwa kuwatumehujumiwa ni vema Watanzania wafahamu kilichoko ndani ya Benki yaoKuu, na Serikali kwa ujumla wake.

b) Watanzania lazima wafahamishwe, Kampuni hii ilipata faida au hasarakiasi gani. Taarifa ya Waziri wa Nishati na Madini inaeleza kuwaMeremeta kwa mwaka 2006/7 imepata Tani 2.7 ya dhahabu. Mapato hayayemeenda wapi? Utata huu unaelezwa vipi iwapo Serikali inaeleza kuwaKampuni ya Meremeta imefilisiwa na shughuli zake kuchukuliwa na TANGOLDLtd.

2: KAMPUNI YA TANGOLD LTD:

Bunge tukufu mara kadhaa limeelezwa kuwa Kampuni hii ni mali ya Serikaliya Tanzania kwa asili mia moja. Hata hivyo utafiti wangu unaonyeshakuwa;-

a) Kampuni ya TANGOLD Ltd, ni Kampuni ya Kigeni, iliyoandikishwa kwamara ya kwanza nchini Mauritius kwa hati ya usajili na. C 205006121tarehe 8th April, 2005 na kupata Hati ya Kutimiza Masharti ( Certificateof Complicance) na. 55661 ya 20th February, 2006 hapa Tanzania.

b) Memorandum and Articles of Association ya Kampuni hii, haionyeshipopote kuwa ni mali ya Serikali wala kuwa ina uhusiano na Serikali.

c) Kifungu cha 7cha Articles hizo zinaonyesha kuwa Hisa zinawezakuhamishwa kwa Baba, mama, mtoto, mke, Babu na kadhalika wa wenye hisa-Hapa kuna zuka utata mkubwa kabisa kuwa Je Serikali inao watu haowanaoweza kuhamishiwa Hisa?

d) Isitoshe, Mahesabu ya Kampuni hii iliyoanzishwa 2005 hayako popote?Je ni kweli ilianzishwa ikakaa tu haikufanya Biashara? Ni kwaniniilianzishwa 'Offshore" na kama ilianzishwa kufanya Biashara imelipa kodikiasi gani ya Serikali.

e) Uchunguzi wa kina wa Hati zilizoko BRELA hazionyeshi popote kuwawakurugunzi wake, wanafanya kazi kwa niaba ya Serikali, kwani FORM zoteza Brela zinaonyesha tu Ukurugenzi au kazi zao kwingineko, lakini siyokuwa wanawakilisha Serikali kama Serikali.

f) Msajili wa Serikali ambaye kwa kawaida ni ndiye anayemiliki Mali zoteza Serikali kwa nia ya nchi si mojawapo wa Wakurugenzi.

g) Kampuni hii ndiyo iliyolipwa fedha tulizoona hapo juu? Fedha hizo nikwa ajili ya nini?Je hapakuwa na haja nzito ya Bunge letu kufanya uchunguzi wa kinakupitia Kamati yake Teule?

3: TUHUMA BOT KULIPA FEDHA KWA KAMPUNIBINAFSI YA MWANANCHI GOLD CO.LTD.

Mwananchi Gold Co.Ltd. imeandikishwa nchini kama Kampuni Binafsi.Katika mwaka wa Fedha wa 2004/2005 na 2006/2007 Kampuni hii imelipwa naBenki kuu jumla ya Dola za Marekani zipatazo 5,512,398.55. Taarifa zaUkaguzi zinaonyesha kuwa hadi 21 Decemba, Kampuni hii ilikuwaimelimbikiza Riba ya Dola za Marekani 62,847.91, sawa na Tshs78,753,459. Hii ni kwa sababu Kampuni hii ilitakiwa kulipa deni lakendani ya Miezi 6, na hadi tarehe hiyo ya ukaguzi, yaani miezi 18 baadayeilikuwa haijalipa hata senti moja. Isitoshe, Deni la Dola za Marekani, 2,807,920, linaonekana kwa taarifaya ukaguzi kudhaminiwa (secured kwa dhahabu ghafi (raw gold)iliyonunuliwa kwa fedha hizo hizo za mkopo.

Yaani Watanzania tumekaangwakwa mafuta yetu wenyewe. Kwa taarifa za BRELA, Benki Kuu inahisa 500 tukatika Kampuni hiyo, na NDC ina hisa 375. Kampuni ya Mwananchi TrustCompany Ltd ina hisa 1,123 na Chimera Co.ltd ina hisa 500.

Kampuni ilisajiliwa kwa Hati na.44962 ya tarehe 12 Desemba 2002 kama PrivateCompany, na kwa maana hiyo hairuhusiwi kuchukua fedha kutoka kwa Umma,yaani kuuza hisa zake kwa Umma wa Tanzania.

Kuna utata mkubwa sanakuhusu hizo kumpanu nyingine za Chimera na Mwananchi Trust, lakini hayotuyazungumze wakati mwingine au katika masuali yenu. Taarifa za ukaguzizinaonyesha kuwa BOT imelipa pia fedha zifuatazo ambazo hazina maelezo:

Tarehe 17/7/2005 File 18003 Temp f/47 Dola za Marekani 95,000 kwaKampuni ya MGCL.

Tarehe 29/0/7/2005 'Allowances' dola 7,500 kwa kampuniya MGCL bila maelezo.

Tarehe 18/01/2006 Transfer( Uhamisho) Tz Embassy,Kinshasa, Dola za Marekani, 1,500,000. Kwa chombo kikubwa kama BOT taarifa yeyote inayoacha wasiwasi haitakiwikabisa, kwani BOT ndio msimamizi wa Taasisi zote za Fedha, ndiyomsimamizi wa Uchumi wa Tanzania nzima.

Je, Hapakuwa na haja ya Kuundwakwa Kamati Teule ya Bunge iwapo Wakaguzi hawajapata hata nyaraka kujuamalipo haya yalikuwa ya nini?

4: TUHUMA ZA JUMLA:

Siku ya Hotuba ya Waziri Mkuu nilitaka pia kupata Ufahamisho kuhusutaarifa zilizokuwepo katika vyombo vya Habari hasa Gazeti la SerikaliDaily News, Issue no. 0856-3812 na 9315 la 22 June, 2007 taarifa ambayohaijakanashwa na Serikali hadi leo kuwa kuhusu Fedha zilizolipwa na BOT kwa makampuni hewa, kiasi cha Tshs 30.8 Billion kupitia Kampuni wakalaya Kagoda Agricultural Ltd. Sababu ya Mashaka katika malipo haya ni kuwaKampuni inasemekana ilisajiliwa Tarehe 29 Septemba, 2005, na ndani yamajuma 8 ilikuwa imekwisha kupewa mkopo huu.

Je, kwa akili ya kawaida,jambo hili halileti utata wowote, na hapahitaji ukaguzi wa kina waKamati Teule. Wakaguzi wa Serikali CAG hata baada ya utafiti wa kinahakuweza kugundua Kampuni hizo, Italy, Ufaransa, Ujerumani, Japan nawala USA. Kwa Taarifa yenu eneo hili pekee ndiyo Serikali ilikubalikufanyiwa Uchunguzi wa kina na kinachoitwa na Serikali na 'ForensicAuditor'.

Kwa kuwa lengo la nyaraka hii ni kutoa picha kwa Watanzania kabla yahatua zaidi nitazochukua Tarehe 15 Septemba, nimeona nitoe haya machachetu ili muyaelewe Hoja ya msingi, utata ulioko, na jinsi Serikaliinavyocheza Rasilimali na Mali ya Watanzania. Narudia kuwa suala hilihalina chembe ya Itikadi hata kidogo bali linaletwa kwenu kwa misingi yaUzalendo na mapenzi mema kwa nchi yetu tu.

Naomba kuwasilisha.

Wenu katika ujenzi wa Taifa letu,

Dr.Willibrod Peter Slaa,
(MB)MBUNGE WA KARATU.


tafadhali tuma kwa wengine unaowafahamu waone hali ya nchi yetu.
 
Already edited bro,

No prob. We're here to serve you!

Wewe usiye onekana, imekuwaje tena umekuwa 'robot'? Are you automating and replacing your 'phyisiological processes' with 'mechanical-digital' components?! :)

SteveD.
 
Wewe usiye onekana, imekuwaje tena umekuwa 'robot'?

Oh yeah? Am a robot... Kila post naisoma japo nyingine naamua kuziacha zilivyo kuona wadau mnazichukuliaje.

BTW: Dr Slaa si member wa JF? Ange-post ujumbe wake huo hapa tungemsaidia kusambaza (members and non members) haraka.

Anyway, w/end ishaanza hivyo!
 
Yaani huu wizi ndo unatuonyesha jinsi tulivyo mazuzu! Sasa kama sio DNA ni nini? labda wasomi wanasayansi mtuambie. IS IT POSSIBLE KWAMBA WAAFRIKA NDO TUNAIBA TUU? Jamani kwa kweli Slaa wewe ni mzalendo kabisa kama hilo neno halijapoteza maana yake halisi. yaani hapa hata asiyemuumini wa chama chochote anaona unyama tunaotendewa watanzania na baadaye akina Tambwe kwa njaa zao wanakuja kuandika pumba zao. Kwa kweli naanza kuamini kwamba TZ hatutaendelea kamwe na CCM ikiwa madarakani! Yaani huu ni more than wizi, tuutafutie jina lingine.

JK upo? au uko na Romano Prodi unaomba msaada kwa ajili ya wateule wako? Maana hiyo misaada na madeni ingawa inatolewa kwa jina letu wenye nchi wanaoifaidi ni wewe na kundi lako.

Lakini unajua wazee hata wakenya waliamka baada ya zile scandal za akina Kamlesh Patni na Moi za Goldenberg za mabillion kuwatingisha. ndipo waliamka waka-claim nchi yao from KANU na sasa wanaweza hata kumfukuza kazi Kibaki. Perhaps na TZ huu unyama ukizidi ipo siku watu watashindwa kuvumilia wataiomba CCM iwarudishie nchi yao.

Its a difficult proposition to convince me that JK HIMSELF is clean kwamba hajui whats happening! No way!
 
Oh yeah? Am a robot... Kila post naisoma japo nyingine naamua kuziacha zilivyo kuona wadau mnazichukuliaje.

BTW: Dr Slaa si member wa JF? Ange-post ujumbe wake huo hapa tungemsaidia kusambaza (members and non members) haraka.

Anyway, w/end ishaanza hivyo!

labda dog amekula password yake...
 
labda dog amekula password yake...

Na hili ndilo tatizo la members wengi. Hujisajili na kusahau password. Just in case kuna mtu amesahau ni vema anifahamishe via email (invisible-AT-jamboforums-DOT-com) nami nitamsaidia ku-reset password yake. Jaribuni kutumia password ambazo ni rahisi kwenu kukumbuka.

Yangu ni 1nv1z1b0
 
Na hili ndilo tatizo la members wengi. Hujisajili na kusahau password. Just in case kuna mtu amesahau ni vema anifahamishe via email (invisible-AT-jamboforums-DOT-com) nami nitamsaidia ku-reset password yake. Jaribuni kutumia password ambazo ni rahisi kwenu kukumbuka.

Yangu ni 1nv1z1b0

Yangu ni ng'obokoyapiyalyankimaNONU :)

SteveD.
 
Tukisema CCM ni mafisadi wanasema tuna wivu,mbona wasijibu hizi tuhuma?majibu yao ni oh,huo ni uzushi tu.Sasa kama ni uzushi mbona mshindwe kusema ukweli,kama Meremeta na Tangold ni makampuni ya serikali,semeni hadharani,na kama siyo ya serikali kanusheni,na mtuambie ni ya nani?Na ni kwa nini tuyalipie madeni,full stop,lakini siyo mijitu mizima akina Kingunge,EL,JK inasimama kwenye majukwaa na kusema huu ni uzushi,tunawaombea laana wala wote mlio kwenye deal chafu.Haki ya Mungu naapa Tanzania haitaendelea kwa uongozi wa CCM.Wtz tuamke,angalia Kenya
walifanya changes bila vita,why not us?
 
Na hili ndilo tatizo la members wengi. Hujisajili na kusahau password. Just in case kuna mtu amesahau ni vema anifahamishe via email (invisible-AT-jamboforums-DOT-com) nami nitamsaidia ku-reset password yake. Jaribuni kutumia password ambazo ni rahisi kwenu kukumbuka.

Yangu ni 1nv1z1b0

Asante na mimi nitajaribu hiyo password niingie niwatese hawa vibaka kama Invisible. Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaa......
 
Kwa hakika huyu bwana amewakalia kooni hawa CCM na sirikali yake.Hata kama hawatuwambii kinachoendelea ukweli wanaupata barabara.Hata tusioona lazima tutasikia tu kwa kuwa Wakumbuke huyu bwana kitaaluma ni Padre,hivyo utafiti wake ni maridhawa kwelikweli.Habahatishi kamwe

Kazi ipo ngd zangu
 
Kampuni za mafisadi Meremeta Co. LTD, Mwananchi Gold Co. LTD, Kampuni ya MGL, Kampuni ya Tangold LTD wanakamua pesa ya walipa kodi bila VISA halafu tunaambiwa sisi ni masikini. Is it?

Maswali magumu hawataki kujibu, che Nkapa where are you?
 
Dr enzi hizo sio mtu wa njaa. Alipoona wanamchanganya akaona potelea mbali bora ya nafsi yake sie tutajijua wenyewe.
Namiss sana hizi harakati...
 
Back
Top Bottom