Ujumbe na ushauri wangu kwa Rais Magufuli

alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
2,366
3,109
Nianze kumshukuru Mungu kwa neema na upendo wake kwetu sote na pamoja na yote tunayopitia yaliyo nje na ndani ya uwezo wetu ashukuriwe Baba Mungu kwa Kristo Yesu mwana wake wa pekee kwa upendo wake usioelezeka siku mpaka siku.

Ndugu Mheshimiwa Raii wangu mpendwa naomba nikusalimu na nikupe Hongera kwa kuendelea kututumikia sisi wananchi wa Tanzania kwa kadri Mungu alivyokupa neema yake ili kusudi lake litimie ndani yako wewe mpakwa mafuta.

Mheshimiwa Rais wangu napenda pia nikupe pole kwa changamoto mbalimbali za kiuongozi, na kiulezi unazopitia ukiwa kama Raisi na Mlezi hasa katika kipindi hiki kigumu cha Maradhi ya mlipuko.

Ndugu Rais wangu inahitajika Moyo mkuu na wa ujasiri sana hasa kipindi hiki kuendelea kusimama na Mungu alie hai bila kua na Moyo wa uoga na Hofu pamoja na changamoto zozote tunazopitia sasa. Mtume Paulo anaandika ujumbe katika biblia akisema je? Ni kipi kitanitenganisha na upendo wangu kwa Mungu Baba? Je? Ni Njaa? Ni Maradhi? Au ni Mauti? Au je nini chochote kile???? Mwisho anasema Hakuna. Maana mambo yote hayo ni ubatili na kusudi la Mungu ndilo litakalosimama. Mheshimiwa Raisi wangu Mithali 29:25. Inatupa faraja zaidi katika hali zozote tunazopitia.

Rais wangu ni ukweli usiopingika kipo kizazi Chenye kuasi lengo Lao kila siku nikuona hatupigi hatua katika kuendelea vyema na kipo macho katika utoaji wa taarifa zilizo hatarishi na zenye kuleta taharuki kila uchwao. Usiogope Rais wangu na kufadhaishwa sababu mambo Haya yamenenwa toka kizazi hadi kizazi kua ni kizazi chenye kuasi na kifurahiacho yaliyo maovu. Rais wangu naomba tafadhali soma hapa Mithali 29:27. Sisemi wewe Rais wangu kua ni Mwenye Haki maana hilo alijua yeye aliyetuumba bali mimi nasema kwa namna ya kile ulichokitumainia kua ni cha haki kwa sababu ulimjua Mungu awezaye kutenda kwa mambo ya kuogofya, na hakika naungana nawe katika kumtumainia yeye huku tukiendelea kuchukua tahadhari zaidi.

Mheshimiwa Rais wangu tambua kua wakati ulionao sasa ndicho kipimo halisi cha wewe kujenga na kukumbukwa na kizazi hadi kizazi na zaidi kujipatia rehema kwa Mungu wako umtumainiaye ama lah kughairi imani yako na kuharibu kwa kushindwa kuwa na tumaini naye, lakini mimi kama kijana mdogo tu naomba nikusisitize Rais wangu tembea na kusudi la Mungu bila kusita, kuchoka na wala kukata tamaa ni hakika ya kua wapo watu nyuma yako katika imani wakikuombea usonge mbele na wala hutodhurika.

Rais wangu usichoke kusoma ujumbe wangu, naomba uuzingatie sababu sina nafasi ya kuonana na wewe kwa ukaribu na kukushauri ila ni imani yangu kristo atakufunua utausoma ujumbe huu nawe utaufanyia kazi kwa kadri ikupendezavyo.

Mheshimiwa Rais kuongoza watu ni kazi Ngumu sana Mungu mwenyewe walimshinda kwa mambo yao hata akawateketeza kama Sodoma na Gomora ama pia wakati wa Nuhu na hata safari ya wana wa Israel toka misri kwenda kanani kuna muda Ardhi ilifungua kinywa chake na kuwameza baadhi sababu ya ukaidi wao kwa Mungu na Musa. Hivyo hata leo kwa baadhi ya sehemu ni marudio tu ya kile kilichotukia awali.

Mheshimiwa Rais wangu kila mtu sasa yupo kimya hata viongozi wa dini na serikali uliowachagua wote wapo kimya bila kusema chochote au ushauri mathubuti,( huko nisiongelee sana) hasa katika changamoto hizi za kawaida tunazopitia.

Raisi wangu mpendwa kama mjumbe wako katika imani naomba sasa nikushauri nini ufanye nasi sote tufanye ili tumshinde mwovu la hila zake zote.

Naomba Ndugu Mheshimiwa Rais wangu nikushauri uitangazie Nchi juu ya kufunga na kumlilia Mungu kwa mfungo mzito na wa kujitoa kwa kila mtu awaye yoyote kwa imani ya kristo Yesu, ningeshauri mfungo huu uchukue wiki tatu tu. Na baada ya hapo Mungu wetu alietushindia Magumu tuliyopitia hapo awali yeyote yale na hata sasa atakwenda kutuvusha kwa mambo yote na kutufanya kwa upya wake.

Mwisho.

Mheshimiwa Rais nikutie Moyo na Mungu akupe nguvu, hekima na Maarifa ili utukufu wake ushudiwe kwako na kila mwenye mwili akiri uwepo wa Mungu alie hai tumtumainiaye.

Maana imeandikwa tusitegemee akili zetu tu bali katika kila jambo tumtegemee Mungu Baba.
 
Malipo ni hapa hapa Duniani.Yupo wapi Ben saanane?
Nani alimmiminia Lissu risasi?

Uovu katika kuja,kupoteza,kudhulumu mali za watu,kudhulumu haki za watu,uchafuzi wa uchaguzi.Haya yote yana malipo na watanzania wapo wanasubiri pigo takatifu atakalopata mtu fulani.

Tupo tutafika tu
 
Nawashauri kabla ya kufunga na kuomba tubuni dhambi zenu hadharani kwa kuvaa magunia, maana damu za kina Mwangosi, Mawazo, zinawalilia,vinginevyo maombi yenu ni kelele mbele zake.

Corona hii inatuangamiza sababu ya kiburi chenu,wamisri walipigwa mapigo saba bila kosa sababu ya ukahidi Wa farao.
 
Mkuu umezungumza Jambo la heri sana Mungu ndiye mwamuzi wa mwisho. Ubarikiwe sana nahamini Mungu atatuvusha salama kwa kipindi iki tunachopitia
 
Malipo ni hapa hapa Duniani.Yupo wapi Ben saanane?
Nani alimmiminia Lissu risasi?

Uovu katika kuja,kupoteza,kudhulumu mali za watu,kudhulumu haki za watu,uchafuzi wa uchaguzi.Haya yote yana malipo na watanzania wapo wanasubiri pigo takatifu atakalopata mtu fulani.

Tupo tutafika tu

Hakuna pigo takatifu wala nini! Wewe ni msafi sana? Tulia acha kulalamika mkuu.
With no any valid proof
 
Mkuu umezungumza Jambo la heri sana Mungu ndiye mwamuzi wa mwisho. Ubarikiwe sana nahamini Mungu atatuvusha salama kwa kipindi iki tunachopitia

Amina Ndugu yangu.
Nina ushuhuda mkubwa sana na Mungu maishani mwangu hivyo nachoongea nakijua mkuu. Mungu wetu hashindwi
 
Nawashauri kabla ya kufunga na kuomba tubuni dhambi zenu hadharani kwa kuvaa magunia,maana damu za kina mwangosi,mawazo, zinawalilia,vinginevyo maombi yenu ni kelele mbele zake.

Corona hii inatuangamiza sababu ya kiburi chenu,wamisri walipigwa mapigo saba bila kosa sababu ya ukahidi Wa farao.

Soma hapa mithali 29: 18
 
Naombea na huyu Rais uliyempelekea ujumbe huu na yeye Upepo huu usimwache kabisa!!
 
Biblia hiyohiyo inasema kwamba kila MTU atavuna alichopanda.

Mi ninunue barakoa kwa gharama zangu afu MTU tu from no where aje anizuie kuvaa kwenye kikao chake kisa yeye hajavaa.

Vaa Barakoa, zingatia kanuni za afya na mpe Mungu nafasi ya kwanza.
 
Back
Top Bottom