Ujumbe muhimu sana kwa wenye tatizo lolote la ngozi

J

JAMII BORA

Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
73
Points
125
J

JAMII BORA

Member
Joined Apr 18, 2017
73 125
Kama wewe una tatizo lolote la ngozi ambalo umekuwa unahangaika kwa muda mrefu na tatizo hilo bila ya kupata utatuzi wa uhakika basi naomba unisikilize kwa makini kabisa kwani huenda taarifa ifuatayo ikawa taarifa muhimu kuliko taarifa yoyote katika maisha yako.

Baada ya kuwasaidia zaidi ya wagonjwa 300 wa magonjwa tofauti ya ngozi, nimekuja kugundua kuwa chanzo cha tatizo la magonjwa ya ngozi sio kuvaa nguo chafu au kutokuoga kama madaktari wengi wanavyodai bali ni jambo ambalo ukilifahamu utaweza kuondokana na tatizo hilo mara moja bila ya kupaka dawa kila siku.

Ndani ya taarifa hii fupi nitazungumzia chanzo cha tatizo lako na jambo kubwa la kuzingatia kuweza kutatua tatizo hilo na jambo gani la kufanya mara moja kuweza kutokomeza tatizo hilo sugu moja kwa moja”

Ili kuweza kukabiliana na tatizo lolote la ngozi yako, lazima ujue ngozi yako ni kundi gani. Kuna aina nne za ngozi kama ifuatavyo:


1.Ngozi ya kawaida(normal skin)

Hii ni ngozi ambayo ina mafuta na unyevu wa kawaida kwa ajili ya ustawi mzuri wa ngozi,hivyo huwa ni ngozi isiyo na mikunjo ya aina yeyote na huonekana vizuri. Pia ni ngozi ambayo ni vigumu kuwa na chunusi na matatizo mengine ambayo yanapatikana katika aina nyingine za ngozi. Kwa hiyo ni ngozi inayohitaji matunzo ya kawaida kama vile, kuisafisha na kuipatia unyevu wa kawaida kabisa(moisture).

2.Ngozi kavu(dry skin)
Ni ngozi ambayo ni rahisi kujikunja(wrinkles) na hivyo kuzeeka haraka na hii hutokana na kiasi kidogo cha mafuta kinachotengenezwa katika mwili. Hii ni ngozi ambayo haiendani na mazingira ya baridi kwani huwa kavu sana. Hii ni ngozi ambayo inahitaji unyevu(moisture) kwa wingi,kwa hiyo ni vyema kutumia vipodozi ambavyo vina unyevu mwingi mchana na usiku unapolala ili kuzuia mikunjo(wrinkles) na muonekano wa kuzeka kwa ngozi.

3.Ngozi yenye mafuta(oil skin)
Hii ni aina ya ngozi yenye mafuta mengi na hivyo kupelekea mtu kung’aa na hivyo kukosa mvuto. Pia ni ngozi ambayo ina uwezo wa kushika uchafu kama vumbi kutoka kwenye mazingira na hivyo kuonekana ni chafu.
Pia ni ngozi ambayo ni rahisi kuwa na chunusi kutokana na hayo mafuta pamoja na sababu zingine,hivyo inahitaji matunzo mazuri na ya kila siku ili kupunguza au kuondoa matatizo yanayoambatana na aina hii ya ngozi. Watu wenye ngozi ya aina hii wanatakiwa wawe na mtindo mzuri wa kimaisha ikiwa ni pamoja na vyakula wanavyokula,hali ya usafi na kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yao, ambapo vitu vyote vikifanyika kwa usahihi vitafanya ngozi iwe ni nzuri na yenye mvuto.
Kitu kizuri kwa watu wenye ngozi yenye mafuta ni kwamba ngozi zao hazipati mikunjo(wrinkles) na hivyo ngozi zao hazizeeki mapema.

4.Ngozi ya mchanganyiko(combination skin)
Hii ni ngozi ambayo ina sehemu ambazo zina mafuta na sehemu nyingine ambazo ni kavu, hivyo ni mchanganyiko wa ngozi yenye mafuta na ngozi kavu au ngozi ya kawaida.
Mara nyingi sehemu za uso kama vile paji la uso,kwenye pua na kwenye kidevu kunakuwa na mafuta mengi, wakati sehemu za shavuni na maeneo yote kuzunguka mdomo na macho huwa ni kavu.
Hapa unatakiwa utunze hizo sehemu za ngozi kutokana na aina yake,kama hiyo sehemu ina mafuta, tunza kama ngozi yenye mafuta,pia tumia njia za kutunza ngozi kavu sehemu ambapo kuna ngozi kavu.


Kama umefaidika na taarifa hii na utapenda kuonana na mimi ana kwa ana au kunipigia simu kwa ajili ya ushauri wa BURE KABISA kupata muongozo wa kutatua tatizo lako piga simu namba 0713-039 875

Ofa hii ya kupata ushauri wa BURE ni kwa watu wachache tu wa mwanzo.

Ili usipitwe na hiyo OFA hakikisha unafanya booking sasa hivi kwa kutuma meseji au kupiga 0746-945583.(Booking tu)
 
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
2,901
Points
2,000
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
2,901 2,000
Asante Kwa taarifa
 
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Messages
2,353
Points
2,000
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2018
2,353 2,000
Shukran mkuu, je unajua ugonjwa wa Vitiligo ? Ninao huo ugonjwa though hapo juu nipo namba 3
 
J

JAMII BORA

Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
73
Points
125
J

JAMII BORA

Member
Joined Apr 18, 2017
73 125
Shukran mkuu, je unajua ugonjwa wa Vitiligo ? Ninao huo ugonjwa though hapo juu nipo namba 3
Naujua, ni hali ya mabakamabaka kwnye ngozikama mtu aloungua. Tiba namba moja ni kujikubali, so far haijafahamika tiba kwa haraka.Pia waone dermatology pale MNH a KCMC
 

Forum statistics

Threads 1,342,677
Members 514,746
Posts 32,759,569
Top