Ujumbe maalumu kwa mheshimiwa Tundu Lissu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Nilipata taarifa za kupigwa kwako risasi muda mfupi tu baada ya tukio kupitia kwa mmoja wa watu ninaowaamini sana! Ingawa ulikuwa ni mchana lakini mwili wangu ulitetemeka sana! Mungu anajua nilichokifanya muda ule. Baadaye niliandika katika ukurasa wangu kuomba Mungu akuponye. Mungu amejibu maombi ya wengi na sasa umepona jambo ambalo linafaa kuitwa muujiza wa Mungu. Jambo lililokutokea linatosha kabisa kwa mtu kama alikuwa hamjui Mungu basi huo ndio unakuwa mwanzo wa kuutafuta uso wa Mungu.

Usiku wa leo ninao ujumbe kwako. Unapoendelea na harakati zako za siasa, huna budi kusamehe na kumuomba Mungu akuondolee chuki na uchungu moyoni mwako dhidi ya mtu au kikundi cho chote unachoweza kufikiri au kuhisi kuwa kilikuwa nyuma ya tukio la kushambuliwa kwako. Jambo hili sio jepesi hata kidogo bali unahitaji kumuomba Mungu akupe neema hiyo na ujasiri huo. Uchungu ukiruhusiwa kukaa katika kifua chako inaweza kuwa ni vigumu kwa mbingu kukupa nafasi kubwa zaidi baadaye! Ndiyo, mbingu zitaruhusuje mtu mwenye uchungu au chuki kushika madaraka makubwa? Kwa sababu akiruhusiwa ataweza kuyatumia kulipa kisasi jambo ambalo Mungu hataki kwa sababu kisasi ni cha kwake yeye Mungu.

Nelson Mandela alipokuwa tayari kusamehe ndipo Mungu akaruhusu atawale. Kwa mtazamo wangu, ukuu wa Nelson Mandela haupo katika mateso aliyopata na muda aliokaa gerezani pamoja na harakati zake. Bali ukuu wa Mandela ulitokana na kitendo cha yeye kusamehe waliomtesa miaka mingi. Nelson Mandela wakati mwingine alifikia hata hatua ya kumpa nafasi aliyekuwa mtesi wake mkuu kukaimu Urais wakati yeye hayupo.

Ninasoma, ninasikia na wakati mwingine ninaona yanayoendelea. Siyo siri, baadhi ya watu wananena mambo magumu na mabaya dhidi ya watu wanaowadhania walikuwa nyuma ya tukio lako. Ninaogopa kuwa 'huruma' za watu wa aina hii ukizisikiliza sana zitaweza kuujaza moyo wako uchungu badala ya rehema. Ninakusihi katika Jina la Yesu usikubali moyo wako ujazwe au ujae chuki.

Ukuu wa Jenerali Obasanjo na hata heshima aliyokuja kuipata baadaye ulitokana na unyenyekevu alioupata akiwa gerezani. Katika mazingira ambayo hayakutegemewa, baada ya Jenerali Abacha kufariki ghafla, Mungu alimuondoa 'mrithi halali' Abiola ili kuhakikisha tu Obasanjo anatawala. Siandiki ujumbe huu kama mtabiri, hapana. Na wala siandiki ujumbe huu kwa lengo la kukuandaa au kutokukuandaa kwa nafasi za uongozi, la hasha. Ninaandika ujumbe huu ili kuiandaa roho yako na nafsi yako kumruhusu Mungu aliyekuokoa kutoka katika bonde la uvuli wa mauti ili akuelekeze vizuri yakupasayo kufanya.

Ni dhahiri kuwa nafsi iliyoumizwa na inayoruhusu uchungu kifuani haiwezi kusikia ipasavyo sauti ya Mungu.
Kwa kuwa wewe ni mwanasiasa, utakuwa pia umemsoma Mahtma Gandhi yule kiongozi mashuhuri wa India aliyeiruhusu Biblia iongoze harakati zake ingawa yeye mwenyewe hakuwa Mkristo.

Ninajua kuwa ujumbe huu unaweza usipendwe na baadhi ya watu hasa wale waliojaa uchungu mioyoni mwao kwa kuwa unalenga kukutaka usamehe. Lakini ni wajibu wangu kama Askofu kukutaka hivyo. Watu hao watakaposoma ujumbe huu nao watasaidika. Ni dhahiri kuwa Mungu akitaka ufike sehemu utafika na akitaka usifike sehemu hautafika.

Kuna uhuru katika kusamehe! Kuna baraka katika kusamehe (Zaburi 32). Kuna ushawishi katika kusamehe! Kuna ulinzi na usalama katika kusamehe kwani mtu anayetangaza msamaha huwasababisha hata adui zake waweke silaha zao chini. Kinyume chake, mtu asiyesamehe anawafanya adui zake wajihami zaidi na hapo ndipo mapambano yanakuwa mazito kuliko ya awali.

Ninakutia moyo upate nafasi ya kuisoma Sala ya Bwana kwa tafakuri nzito. Mungu akikujalia neema na utayari kuchukua hatua ya kutangaza msamaha hadharani atakuongoza na atakuinulia watumishi wa Mungu watakaoandaa ibada kwa ajili hiyo au kukutia moyo kwa namna ambayo Mungu atakuongoza. Unaweza kutumia tukio lililokupata kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu kwa njia ya kutangaza msamaha.

Utukufu uwe kwa Mungu awapae wakuu uwezo wa kutawala; awakwezaye wanyenyekevu na awashushaye wenye kiburi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) & Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Kama alikuwa anajiuliza ataanzaje kurudi na kusamehe lakini zaidi sana kutuomba msamaha Watanzania kwa maana hakututendea haki, umempa ufunguo. kama ana akili autumie sasa tena bila kuchelewa.
 
Baba Askofu, unasamehe Kwa tukio baya kama lile ukitegemea adui (kama Ndugai ) ataweka silaha chini, lakini sasa yeye anawageukia watoto wako awaue Kwa njaa(kuzuia mshahara na posho) baada ya kuona hutaki kumsujudia. Jee unafanyaje? Unacheka na kumshangilia?
Mungu wetu asingeitwa Bwana wa majeshi kama anaweza kuruhusu unyonge wa kiasi hicho.
Mwacheni Lissu akasirike ili nasi tukasirike naye na watesi wajue tumekasirika na tuna chuki nao.
Hata Maandiko yanaonyesha Mungu kuna mapambano aliyabariki na akasema "wapigeni na muwauwe wote" Kwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lisu kifupi atulie ajiuguze aache siasa kabisa asubiri apone.Hotuba ya Mwenyekiti Wake Mbowe Kwa vyombo vya habari leo nadhani atakuwa kaielewa vizuri Kama ana akili kama hana auilize mkewe amweleweshe.Mimi binafsi Mbowe nimemwelewa vizuri Sana kuhusiana na issue ya Lisu.Mbowe is intelligent.For the fist time I admit.
 
kutangaza msamaha hadharani

Maigizo? Unataka na yeye Lissu aendeleze maigizo kama yale ya kwenda kanisani na kujikusanyia viongozi wa kidini aonekane kuwa mcha Mungu ndio uwe ushuhuda kwako?

Ni wapi ulipomwona Lissu akionyesha uchungu na kulipiza kisasi? Unajuaje kuwa hayo yaliyofanyika kwake na yanayoendelea kufanyiwa yeye alishayachukua na kuyakabidhi kwa Muumba wake anayemwamini yeye? Kwa nini unaweka shurti ya yeye aje akueleze wewe yaliyo moyoni mwake ndio uamini?

Huu ni mwendelezo wa unafiki tunaouona kila mahali nyakati hizi!
 
Lisu kifupi atulie ajiuguze aache siasa kabisa asubiri apone.Hotuba ya Mwenyekiti Wake vyombo vya habari nadhani atakuwa kaielewa vizuri Kama ana akili kama Hana auilize mkewe amweleweshe.Mimi binafsi Mbowe nimemwelewa vizuri Sana kuhusiana na issue ya Lisu.Mbowe is intelligent.For the fist time I admit.
Msaga sumu. Kilangila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipata taarifa za kupigwa kwako risasi muda mfupi tu baada ya tukio kupitia kwa mmoja wa watu ninaowaamini sana! Ingawa ulikuwa ni mchana lakini mwili wangu ulitetemeka sana! Mungu anajua nilichokifanya muda ule. Baadaye niliandika katika ukurasa wangu kuomba Mungu akuponye. Mungu amejibu maombi ya wengi na sasa umepona jambo ambalo linafaa kuitwa muujiza wa Mungu. Jambo lililokutokea linatosha kabisa kwa mtu kama alikuwa hamjui Mungu basi huo ndio unakuwa mwanzo wa kuutafuta uso wa Mungu.

Usiku wa leo ninao ujumbe kwako. Unapoendelea na harakati zako za siasa, huna budi kusamehe na kumuomba Mungu akuondolee chuki na uchungu moyoni mwako dhidi ya mtu au kikundi cho chote unachoweza kufikiri au kuhisi kuwa kilikuwa nyuma ya tukio la kushambuliwa kwako. Jambo hili sio jepesi hata kidogo bali unahitaji kumuomba Mungu akupe neema hiyo na ujasiri huo. Uchungu ukiruhusiwa kukaa katika kifua chako inaweza kuwa ni vigumu kwa mbingu kukupa nafasi kubwa zaidi baadaye! Ndiyo, mbingu zitaruhusuje mtu mwenye uchungu au chuki kushika madaraka makubwa? Kwa sababu akiruhusiwa ataweza kuyatumia kulipa kisasi jambo ambalo Mungu hataki kwa sababu kisasi ni cha kwake yeye Mungu.

Nelson Mandela alipokuwa tayari kusamehe ndipo Mungu akaruhusu atawale. Kwa mtazamo wangu, ukuu wa Nelson Mandela haupo katika mateso aliyopata na muda aliokaa gerezani pamoja na harakati zake. Bali ukuu wa Mandela ulitokana na kitendo cha yeye kusamehe waliomtesa miaka mingi. Nelson Mandela wakati mwingine alifikia hata hatua ya kumpa nafasi aliyekuwa mtesi wake mkuu kukaimu Urais wakati yeye hayupo.

Ninasoma, ninasikia na wakati mwingine ninaona yanayoendelea. Siyo siri, baadhi ya watu wananena mambo magumu na mabaya dhidi ya watu wanaowadhania walikuwa nyuma ya tukio lako. Ninaogopa kuwa 'huruma' za watu wa aina hii ukizisikiliza sana zitaweza kuujaza moyo wako uchungu badala ya rehema. Ninakusihi katika Jina la Yesu usikubali moyo wako ujazwe au ujae chuki.

Ukuu wa Jenerali Obasanjo na hata heshima aliyokuja kuipata baadaye ulitokana na unyenyekevu alioupata akiwa gerezani. Katika mazingira ambayo hayakutegemewa, baada ya Jenerali Abacha kufariki ghafla, Mungu alimuondoa 'mrithi halali' Abiola ili kuhakikisha tu Obasanjo anatawala. Siandiki ujumbe huu kama mtabiri, hapana. Na wala siandiki ujumbe huu kwa lengo la kukuandaa au kutokukuandaa kwa nafasi za uongozi, la hasha. Ninaandika ujumbe huu ili kuiandaa roho yako na nafsi yako kumruhusu Mungu aliyekuokoa kutoka katika bonde la uvuli wa mauti ili akuelekeze vizuri yakupasayo kufanya.

Ni dhahiri kuwa nafsi iliyoumizwa na inayoruhusu uchungu kifuani haiwezi kusikia ipasavyo sauti ya Mungu.
Kwa kuwa wewe ni mwanasiasa, utakuwa pia umemsoma Mahtma Gandhi yule kiongozi mashuhuri wa India aliyeiruhusu Biblia iongoze harakati zake ingawa yeye mwenyewe hakuwa Mkristo.

Ninajua kuwa ujumbe huu unaweza usipendwe na baadhi ya watu hasa wale waliojaa uchungu mioyoni mwao kwa kuwa unalenga kukutaka usamehe. Lakini ni wajibu wangu kama Askofu kukutaka hivyo. Watu hao watakaposoma ujumbe huu nao watasaidika. Ni dhahiri kuwa Mungu akitaka ufike sehemu utafika na akitaka usifike sehemu hautafika.

Kuna uhuru katika kusamehe! Kuna baraka katika kusamehe (Zaburi 32). Kuna ushawishi katika kusamehe! Kuna ulinzi na usalama katika kusamehe kwani mtu anayetangaza msamaha huwasababisha hata adui zake waweke silaha zao chini. Kinyume chake, mtu asiyesamehe anawafanya adui zake wajihami zaidi na hapo ndipo mapambano yanakuwa mazito kuliko ya awali.

Ninakutia moyo upate nafasi ya kuisoma Sala ya Bwana kwa tafakuri nzito. Mungu akikujalia neema na utayari kuchukua hatua ya kutangaza msamaha hadharani atakuongoza na atakuinulia watumishi wa Mungu watakaoandaa ibada kwa ajili hiyo au kukutia moyo kwa namna ambayo Mungu atakuongoza. Unaweza kutumia tukio lililokupata kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu kwa njia ya kutangaza msamaha.

Utukufu uwe kwa Mungu awapae wakuu uwezo wa kutawala; awakwezaye wanyenyekevu na awashushaye wenye kiburi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) & Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

MHESHIMIWA Askofu, japo sijawahi kufahamu imani ya wa Monrovian wanaamini kitu gani hasa?

Lakini mpaka sasa, Umenena UJUMBE WA MUNGU kabisa Huu na umekuja wakati Mubashara sana.

Barikiwa sana
 
CCM na serikali yake hawana ubinadam, fikiria wamekataa kulipa matibabu ya Lissu, Wamegoma uchunguzi kufanyika, Kila kukicha makada wa ccm wana mshambulia mtu aliyemiminiwa risasi 16 mwilini mwake, wanamshambulia mtu aliyeingia chumba cha upasuaji mara 23 na akatoka salama, Wanapanga kumvua ubunge, na sasa wamekataa kumlipa mshahara wake, kwa kweli katika hili Askofu rudi kaisome biblia upya.
 
Huyu mtumishi gani anaangalia upande mmoja tu wa Lissu! je ana ushauri gani kwa watesi wa Lissu ambao inaelekea bado wamedhamiria kabisa kumuuua Lissu na familia yake yote?! nasaha za kufumbia macho uovu dhahiri hazina maana hata kidogo; akanywe mvinyo akalale, Lissu ni mtu mzima ataamua njia sahihi ya kusonga mbele.
 
CCM na serikali yake hawana ubinadam, fikiria wamekataa kulipa matibabu ya Lissu, Wamegoma uchunguzi kufanyika, Kila kukicha makada wa ccm wana mshambulia mtu aliyemiminiwa risasi 16 mwilini mwake, wanamshambulia mtu aliyeingia chumba cha upasuaji mara 23 na akatoka salama, Wanapanga kumvua ubunge, na sasa wamekataa kumlipa mshahara wake, kwa kweli katika hili Askofu rudi kaisome biblia upya.
Kisasi ni Juu ya Mungu tu. Mheshimiwa Askofu Yupo Sahihi 100%.
Samehe 7×70

Tundu Lisu atakua amechagua Fungu jema zaidi, kwakua atakua amewasamehe watesi wake zaidi.

Hayo makaratasi yake ya sheria, aweke pembeni kwa muda, aperuzi Bibilia. Amsome hata Daudi na Mfalme Sauli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom