Ujumbe Maalum kwa Dkt. John Magufuli, Rais Mteule wa Tanzania

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Ndugu Rais, nakusalimu.

Awali ya yote ninakupongeza kwa dhati kabisa kwa kuchaguliwa kwako kwa kishindo kuingoza tena Tanzania kwa miaka mingine mitano. Ushindi huo sio bahati mbaya. Watanzania wameridhishwa na uongozi wako unaoacha alama.

Ndugu Rais, ninaomba niende moja kwa moja kwenye hoja yangu. Serikali hii utakayoiongoza kwa kipindi hiki cha miaka mitano itakuwa ni serikali yenye deni kubwa sana kwa watanzania. Kipindi cha kampeni uliomba watanzania wakuletee madiwani na wabunge wa CCM, nao wamekusikia

Ninaamini spika wa bunge atatoka CCM hivyo ninaomba akapatikane mtu ambaye atashirikiana vizuri na serikali katika kuendesha bunge ili kuhakikisha watanzania wanapata neema zaidi. Ikiwapendeza, Job Yustino Ndugai bado anafaa

Naomba pia uelekeze (Kama mwenyekiti wa CCM taifa) pati kokasi kuhakikisha inalishawishi bunge kupitia sheria mbalimbali zinazolalamikiwa ili zilete tija zaidi kwa watanzania. Mfano mmoja wapo ni sheria ya mafao ya wastaafu pamoja na fao la kujitoa kwa watumishi wa kazi za muda mfupi

Kasi yako kwenye maendeleo imeonekana kuanzia usambazaji wa umeme vijijini, maji, huduma za afya na elimu, kilimo, barabara na nidhanu serikalini. Umekuwa sauti ya wale wasio na sauti na kuwawezesha kuwa na sauti.

Pamoja na hayo, wapo baadhi ya viongozi ambao hawawajibiki ipasavyo, unakuta ni mpaka ufike wewe mwenyewe ndio unakuta viongozi wanawajibika.

Mheshimiwa Rais naomba sana hili ukaliangalie ili wateule wako wachape kazi zaidi na kutatua kero za wananchi na wewe ukifika usikutane na shida ndogondogo.

Naomba ikikupendeza, waelekeze wateule wako wahangaike usiku na mchana kubuni miradi, kupanua wigo wa vipato vya halmashauri, kudhibiti rushwa na kuhakikisha wanasimamia sera za serikali ili vijana waweze kujiajiri.

Kilimo, ufugaji na ujasiriamali vikipewa msukumo mkubwa zaidi katika ngazi za wilaya na halmashauri, Mheshimiwa Rais tutatoa ajira nyingi na Kukuza uchumi wa taifa letu.

Ninakutakia afya njema na kila lililo jema.

Amani Msumari
Tanga

Cc: Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
Katibu Mkuu - CCM
 
Labda kama ukimaanisha miezi 5. Kesho kutakuwa na maandamano nchi nzima ya kumkataa. Unakijua hilo?
Hakuna maandamano yoyote. Mkikatazwa jambo muwe mnaelewa ndugu zangu.

Huu sio muda wa kuandamana. Huu ni muda wa kufanya kazi kujenga nchi yetu kwa faida yetu na vizazi vyetu. Tumejifunza ya Burundi, Zimbabwe, Libya, Tunisia, Misri na kwingineko duniani.
 
Hakuna maandamano yoyote. Mkikatazwa jambo muwe mnaelewa ndugu zangu.

Huu sio muda wa kuandamana. Huu ni muda wa kufanya kazi kujenga nchi yetu kwa faida yetu na vizazi vyetu. Tumejifunza ya Burundi, Zimbabwe, Libya, Tunisia, Misri na kwingineko duniani.
Inabidi tuchapane ndipo tutaheahimiana.
 
Being sexless is natural but being senseless is intentional
Vipi kuiba na kupora haki za watu iko upande gani?

Hulka za watanzania tunazifahamu, hakika huyu mwenye kuyafanya haya hana utanzania. Tunamtaka arudi nchini kwake atuachie nchi yetu.
 
Back
Top Bottom