Ujumbe kwa Waziri Mkuu Pinda

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Ujumbe kwa Waziri Mkuu Pinda

Mheshimiwa, katika Mkutano uliopita wa Bunge uliomba miezi mitatu kuyafanyia kazi maazimio ya Bunge kuhusu Richmond/Dowans. Sasa miezi minne imepita, naomba katika hotuba yako ya kesho ya kuhitimisha ujibu pia masuala yaliyomo kwenye makala niliyoiambatanisha.

JJ
 
Attachments

  • HATMA YA RICHMOND.doc
    45.5 KB · Views: 172
John,

Thank you! We are committed to seeing an accountable conclusion to this.

Kama hawezi Uwaziri mkuu aachie ngazi na yeye. Hakuna kuendelea kufukia kichwa kwenye mchanga. Wameturudisha nyuma zaidi ya miaka 50!
 
He is a damn freak.Mtoto wa mafisadi.
 
Kwa jinsi nilivyoona mjadala unavyopendelea hapa Dodoma, sidhani kama Pinda atajumuisha hayo katika majibu yake kesho. Nadhani anatakiwa kuitoa ripoti hiyo pekee kama taarifa ya serikali jambo ambalo kwa mujibu wa kanuni za Bunge, haliwezi kufanyika wakati wa hotuba ya bejeti kwa sababu ripiti hiyo si sehemu ya bajeto yake. Lakini tusubiri tuone
 
John,

Ungeirusha ripoti yako kwa magazeti basi may be wangesaidia kumfikishia waziri.
 
pinda atapindisha kuhusu richmond/dowans. atasema kikao hichi cha bunge si nafasi ya kutoa majibu hayo.
 
Ujumbe kwa Waziri Mkuu Pinda

Mheshimiwa, katika Mkutano uliopita wa Bunge uliomba miezi mitatu kuyafanyia kazi maazimio ya Bunge kuhusu Richmond/Dowans. Sasa miezi minne imepita, naomba katika hotuba yako ya kesho ya kuhitimisha ujibu pia masuala yaliyomo kwenye makala niliyoiambatanisha.

JJ

Mizengo Pinda (MP) kama alivypewa nick na mwana JF mmoja atapitia kwenye mtihani wake wa kwanza karibuni ... labda kesho... au siku nyingine yoyote akiamua.

Natumaini kuwa sasa wale wasiomjua na wasiojua kwa nini alipewa hiyo nafasi wataelewa kinachoendelea.
 
Hapa naona hakuan majibuya kina wala nini.
kilichopo ni kutupumbaza kuwa wanayafanyia uchunguzi na maamuzi yatatolewa wakikaribia uchaguzi wa 2010.
kama unavyoona wamesha anza kuwasafisha wahusika.na wengine kwa akili zao za mgando basi wanajifanya ''ooh ni wabunge wote wanauchungu nazo ila tofauti ni jinsi ya kuzidai tu,na si kupayuka na mbwembwe kibao.''
ila wakae wakijua kuwa their days are numbered!!
 
Huu ujumbe umeenda kwa waziri mkuu au ni maoni yako kwa wana JF???

Mr. Zero

Najua watu wa OW na UWT huwa wanapita hapa sana tu. Hivyo naamini ujumbe utamfikia kama wakipenda. Ujumbe huo ni mwangwi wa sauti ya wananchi. Hata katika Kongamano la wanaUbungo la Mei 24 maoni kadhaa ya umma yalichukua mwelekeo huo. Sasa Pinda ni vyema akafahamu kwamba Vox Populi, Vox Dei. Kama hatajibu kesho, basi walau kesho atangaze ni lini katika kipindi hiki hiki cha bunge atawasilisha ripoti yake kwa kuwa miezi mitatu aliyoahidi imeshamalizika. Na umezidi mwezi mmoja tayari!

JJ
 
ala kumbe........... wenzenu bado wapo usingizini jamani hawajua kuwa adhana imeshapigwa sasa ngoja waje kukushuta wakati kumeshakuchwa na wajanja wameshawahi madala dala kuwahi kazini
 
Ujumbe kwa Waziri Mkuu Pinda

Mheshimiwa, katika Mkutano uliopita wa Bunge uliomba miezi mitatu kuyafanyia kazi maazimio ya Bunge kuhusu Richmond/Dowans. Sasa miezi minne imepita, naomba katika hotuba yako ya kesho ya kuhitimisha ujibu pia masuala yaliyomo kwenye makala niliyoiambatanisha.

JJ
Asante sana maana nimeshanga kwny hotuba ya Kayanza sikusikia neno RICHMOND kabisa
 
Ujumbe kwa Waziri Mkuu Pinda

Mheshimiwa, katika Mkutano uliopita wa Bunge uliomba miezi mitatu kuyafanyia kazi maazimio ya Bunge kuhusu Richmond/Dowans. Sasa miezi minne imepita, naomba katika hotuba yako ya kesho ya kuhitimisha ujibu pia masuala yaliyomo kwenye makala niliyoiambatanisha.

JJ

Kwani Mizengo Pinda hajitakii mema mpaka aingilie mambo hayo?.
Hili suala la Richmond bado ni bichi sana kwani kundi lililotupiwa lawama linajipanga kujibu mashambulizi ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu wote walioshiriki kuwaanika hadharani wahusika. Na kundi hili lina nguvu ya sunami, ndilo linaloendesha serikali kwa sasa pamoja na kutokuwa na Ofisi za serikali. Pinda analijua hilo hivyo sidhani kama atakuwa tayari kumwaga unga wake.

Kwa kifupi ni kwamba hakuna cha jawabu wala swali kutolewa katika hili suala.
 
Jamani alishasema anawaogopa mafisadi kwa kuwa wana hela nyingi na kwamba ukiwaendea harakaharaka wanaweza kukuchenjia au mmeshasahau
 
Back
Top Bottom