The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Kwa muda sasa tumeshuhudia posts katika mitandao mbalimbali, baadhi (na pengine nyingi zaidi) zikisifia na nyingine zikipinga au kukosoa utendaji kazi wa Rais wetu na serikali anayoiongoza. Binafsi sina shida na wanaopongeza na wakati huohuo wakatoa mapendekezo ya kuboresha au kudumisha mazuri yanayofanyika. Pia sioni tabu kuona mtu kimsingi, akikosoa lakini akitoa pongezi panapostahili na kushauri namna nzuri ya kutatua matatizo.
Hawa watu wa makundi haya mawili nawaita wazalendo na wakweli japo wametofautiana mitazamo.
Kwa wanaosahau matamanio, utashi na ubinafsi wao kwa japo saa moja katika siku na kupima yanayofanyika chini ya serikali ya awamu ya tano watakiri wazi kwamba Tanzania ya leo ina ndoto ya jumla kama taifa. Siyo aibu kuwaza kwamba kuna siku mtu utaona sifa kuitwa mtanzania mbele ya mataifa mengine.
Safari bado ni ndefu sana lakini sote kwa pamoja (kama taifa) tukiweza kutofautisha matakwa yetu binafsi na mahitaji yetu kitaifa, Tanzania itapiga hatua kubwa ndani ya muda mfupi kuliko tunavyoweza kutarajia. Katika hili Mungu na atusaidie.
Tatizo langu kubwa ni hawa wenzetu walioamua kukosoa tuuuu! Yaani kwa kurahisisha (katika maoni yao) hakuna jema lolote lililofanywa na serikali hii ya sasa. Akifukuzwa kazi mtu kwa tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe au kushindwa kutekeleza majukumu basi utasikia "huo ni udikteta". Akihamishwa mtumishi sehemu ya kazi basi CCM ni ile ile na tusitarajie jipya. Guys! Hawa ni watu wanaona, wanaweza kusoma na kuandika lakini haya ndiyo maoni yao. Kazi bado pevu!
Rais Magufuli siyo malaika! Serikali yake si ya mitume. They are just people try to make their nation better by using all the blessings they have. Inawezekana (na ni lazima) kuna sehemu kasoro ndogo ndogo zitajitokeza.
Kusafisha hii nchi (kwa wale msioijua vizuri) ni vita kubwa kuliko ya kupambana na nchi jirani kijeshi hivyo, msitarajie mteremko katika hili ! Pasipo kuficha, kila raia aliyezoea mteremko; tajiri kwa maskini, mke kwa mume, vijana kwa wazee na makundi yote ya watu, lazima tujiandae kupitia maumivu ya aina fulani wakati tunajiweka sawa kuwa wachapakazi na kuneemeka kutokana na juhudi halisi na maarifa badala ya connections (technical know who).
Wewe unayekosoa kila kitu pasipo kutazama mazuri wala kushauri nini kifanyike ujumbe wako upo katika maswali yafuatayo:-
1. Unaridhika na nchi ilivyokuwa inaongozwa kabla ya ujio wa awamu ya tano?
2. Kama huridhiki na utendaji wa serikali ulitarajia mabadiliko yafanyike kwa njia ipi?.
3. Unadhani katika wote walioomba kuwa Rais wa Jamhuri nani angeongoza vizuri zaidi kuliko Mh. Magufuli?.
4. Kama yupo mtu wa aina hiyo (3) yeye angefanya nini kuisaidia nchi kutumia vizuri raslimali zake kutafuta maendeleo pasipo kupitia yanayofanyika sasa?
5. Unaamini unakosoa kila jambo linalofanywa na serikali hii kwa haki au roho bado inauma kwa kuwa matokeo ya uchaguzi uliopita hayakuenda upande uliotaka?
TAFAKARI KWA KINA
Watanzania wazalendo tafakarini sana faida na hasara za aina ya uongozi wa Mh. Magufuli kabla hamjalaumu. Kila utendaji una faida na hasara zake.
I tell you people kuwe na kasoro ama la, Mh. Magufuli ni the best and only genuine leader we have right now!
Mlinganishe na yeyote unayemjua hapa nchini halafu niambie kwa sifa za huyo mtu angeweza lipi kuisaidia nchi! Membe? Lowassa? Migiro?
Thanks for reading!