Ujumbe kwa wajumbe wa NEC (CCM): Golden chance never come twice. Muitumie vizuri siku ya kesho

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,885
Wote mnajua kuwa baada ya kumchagua mama kuwa mwenyekiti wa chama hapo kesho anakwenda kufanya uteuzi mkubwa wa kihistoria. Anakwenda kuteua wakuu wa wilaya, maDED, wakuu wa mikoa n.k

Karibia wateule wote wa hizo nafasi huwa wanatoka CCM hasa NEC. Jukumu lako wewe mjumbe unayetaka uteuzi ni kujipitisha pitisha angalau mama akuone kuwa na wewe upo.

Pia ukipata nafasi ya kusalimiana naye hakikisha unakuwa mnyenyekevu huku ukimuangalia usoni kwa macho ya huruma.

Pia kama atafanya kosa la kuwakaribisha futari hiyo ndio itakuwa nafasi sahihi ya kusalimiana naye.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
View attachment 1767401
 
Ndio umewafundisha hayo matope, bora Katiba Mpya ipatikane hizo nafasi zinazofanya watoto wa kiume wafundishwe kulegeza macho ili wapate teuzi ziondolewe.
 
1619690157899.png
 
Ndio umewafundisha hayo matope, bora Katiba Mpya ipatikane hizo nafasi zinazofanya watoto wa kiume wafundishwe kulegeza macho ili wapate teuzi ziondolewe.
Ha ha ha mkuu hizi mbinu zinafanya kazi ndani ya CCM pekee dunia nzima
 
Siyo tena uwezo wa mtu kuongoza bali ni kujipitisha na kujipendekezana ndizo sifa za kuwa DED ama DC!? Mnaitakia mema kweli Tanzania!?
 
Jerry Muro alimtukana Mbowe an Lema akala shavu la uDC.

2015 Makonda alimtukana Lowasa akapewa ukuu wa wilaya Kinondoni.

CCM hawana formula wala vetting ya kupata viongozi.
Kama Chadema wangekuwa wanafanya veting vizuri na ya uhakika, unafikiri viongozi wote wa juu kabisa Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Wakuu bara na Visiwani, wangekuwa vilaza kama ilivyo sasa, pamoja na Mgombea Makamu wa Rais kasoro Katibu wa Mambo ya Nje John Mrema?.

Midomo ipunguze kusema mambo Yale Yale yakiwa tofauti kwa CCM na kinyume chake ikiwa CHADEMA.

Na siku zote mjinga huwa salama akikaa na mjinga.
 
Dr. Mashinji alikuwa kilaza mbona anawalia hela zenu hadi leo?

Dr.Slaa alikuwa kilaza mbona mkamuhonga mijihela na ubalozi juu?

Waitara, Katambi, Silinde sio mawaziri mliowanunua kwa dau kubwa na uwaziri juu?

Unamfahamu waziri Pauline Gekul? Yaani CCM mnaongozwA na CHADEMA bila kujua. Vilaza kweli nyie.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom